Maoni yangu binafsi kuhusu ACT Wazalendo kuingia SUK

Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mungu mwingi wa rehema na mwenye kurehemu kwa neema ya uhai na afya njema.

Pili niwashukuru wananchi wenzangu wa Zanzibar kwa subira kubwa baada mazito kupita kwenye nchi yetu. Pia nichukuwe fursa hii kutoa pole kwa ndugu na jamaa walodhulumiwa roho zao na wale ambao ni majeruhi mpaka hivi sasa.

Nikiwa mpenzi na mfuasi wa Act - Wazalendo, ningependa kuweka wazi msimamo wangu wa kuto kukubaliana na viongozi wa chama "ikiwa" watafanya maamuzi ya kuingia kwenye Serikali kwa kile kinachoitwa Maridhiano.

Mimi nimekuwa nikiamini kinachoitwa Maridhiano huwa hakina maana kama kinavyotamkwa, bali huwa ni kuridhiwa kwa CCM baada yote waliyo yafanya.

Kwa nini CCM wanataka kuridhiwa wakati wao chama chao kimeunganishwa na mifumo ya dola? Taasisi nyeti kama TISS, Jeshi la Polisi nk. Vyombo hivi vyote nimekuwa vikifanya kazi kubwa kuhakikisha CCM inabaki madarakani kwa gharama yoyote ile.

Pamoja na nguvu hii ya taasisi nyeti za mfumo wa kiutawala wa Serikali kukisaidia chama chao bado kuna kitu muhimu CCM wamekikosa miaka yote, nacho ni kukubalika kwenye jamii, wananchi walio wengi Zanzibar wameikataa CCM na wamekuwa na msimamo huwo daima.

Kwanini Wazanzibari kila siku wamekuwa wakiikataa CCM? Kwa sababu wanaamini kuzorota kwa maisha ya Zanzibar katika kila sekta kunatokana na CCM kwa kutaka kutimiza lengo lao la kuwa na Serikali moja na chama kimoja (yaani kupotezwa kwa Zanzibar na kutambulike kwa Tanzania).

Jambo hili Wazanzibari hawajawahi kulikubali hata mara moja na ndio maana ajenda kubwa ya Wazanzibari ni kuwa na mamlaka kamili ya nchi yao jambo ambalo wamelikosa kwa CCM (sio kwamba wamelikosa tu CCM wao wanaamini Zanzibar kutawaliwa na Tanganyika ndio mafanikio yao) na hapa ndio upinzani mkubwa wanaoupata CCM kutoka kwa Wazanzibari.

Hapa ndipo Wazanzibari wengi wamekuwa wakiikataa CCM kila uchaguzi mkuu. Hakuna kitu muhimu katika maisha ya binaadamu kama uhuru wa taifa lake ambao utampelekea yeye binafsi kuwa huru pia.

Wananchi ambao wamekuwa wakiteswa na kuuliwa na dola kwa kuilinda CCM ising'oke madarakani huwafika hayo kwa malengo ya kuipigania Zanzibar sio CUF wala Act Wazalendo, haya ni majukwaa tu ya kufanyia harakati zetu.

Kama Wazanzibari walivyoipata talaka 3 CUF wanaweza kufanya hivyo kwa Act Wazalendo pia.
Niliarifiwa kwamba Maalim Seif Sharif Hamad aliitwa kuonana na Dkt. Hussein Mwinyi, lengo Kuu la kuitwa huko ni kumtaka aingie Serikalini.

Nasikia Maalim Seif akatoa masharti yake kwa niaba ya chama ikiwa yatatekelezwa ndio wao wataingiya Serikalini.

a) Uamsho waachiwe huru.

b) Walioshikwa wakati wa chaguzi wote waachiwe huru.

c) Iundwe tume ya uchunguzi dhidi ya ukatili wa mauji na mateso yale kisha wahusika wachukuliwe hatua.

d) Kuundwe Tume (huru) mpya ya uchaguzi Zanzibar.

e) Kutiliana saini mkataba wa kufanya mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia uandikishaji, kampeni mpaka uchaguzi wenyewe kwa misingi ya uwazi, haki, uhuru na uadilifu ili kuepusha machafuko mengine huko mbele.

Ikiwa hayo niliyo yaeleza hapo ni kweli Maalim Seif kayapeleka kwa Dk. Hussein Mwinyi, basi muda upo katika siku 90 nadhani hata siku 20 bado hazijatimia tunaweza kuona ukweli wake na uwongo uko wapi.

Narejea Ikiwa hayo ni kweli na yatatekelezwa mimi nitaungana na Maalim Seif na viongozi wote Act Wazalendo kuingia katika Serikali, kinyume na hapo siwezi kuwazuia kuingia katika Serikali lakini napenda nieleweke kwa uwazi kabisa kwamba sitokuwa pamoja nao katika hili.

Kwa kuzingatia roho za ndugu zetu, vilema vya maisha athari za ndani ya mioyo kwa kubakwa na kuporwa mali kwa baadhi ya wenzetu.

Hii miezi miwili na ushei ilobakia tunaweza kuona kama kweli wana nia thabit kutaka kuwa waadilifu au wanataka waridhiwe kisha baada ya miaka 5 mengine wafanya mauaji mengine.

Naomba nirudi kwenye nukta yangu.

1. Iliyokuwa CUF ilikuwa na wawakilishi zaidi ya 20 wa kuchaguliwa majimboni, hii haijawahi kuwa kikwazo kwa CCM kupitisha yale wanayoyataka kwenye BLW.

2. Makamo wa Kwanza + Wizara mbili + Wawakilishi 5 wa kuteuliwa hawaendi kubadilisha chochote zaidi kukalia damu ambayo ripoti ya chama imesema wazi kuwa haikubaliani na uharamu wa uchaguzi ule ikafika mbali mpaka kutaja idadi ya vifo na majeruhi na kutaka uchunguzi ufanyike na pia kuitishwe kwa uchaguzi mwengine.

3. Pengine chama kinahofia vipi kitajiendesha ikiwa kitakosa ruzuku (sina hakika na hili) ikiwa nipo sahihi Act wanapaswa kuitumia fursa hii kukaa na wahanga ambao ni wananchi na wananchi ndio jamii.

Kwa hiyo, wao kama chama watakuwa na mtaji wa kuongoza jamii na kuiwacha CCM kuongoza dola pasipokuwa na support ya wananchi. Nimewahi kujadiliana na baadhi ya watu kuhusu hili, katika nilojadiliana hayo tumekubaliana tuanzishe utaratibu wa kukichangia chama kila mwezi kulingana na uwezo wetu.

4. Kwa zaidi ya muongo mmoja CCM wamekuwa wakimsema Maalim Seif kuwa ni mtu ambae wao wanamtumia anawapiganisha Wazanzibari kisha yeye hurudi kukaa nao meza moja. Sikuwahi kaumini upuuzi huu lakini naamini binaadamu hatupo sawa wapo ambao waliamini na ikiwa Act Wazalendo wataingia GNU bila ya hayo masharti yao kutimizwa naamini sehemu kubwa kwenye jamii itaanza kuyajengea imani maneno yale.

5. Kwanini nimemtaja Maalim Seif binafsi hapo kwenye nukta no, 4? Yes, kwa sababu Maalim Seif yeye binafsi bila chama bila chochote ni taasisi yenye nguvu na yenye kukubalika.

6. Mimi naamini CCM ni vigumu kukubaliana na lolote lenye kuonesha kuleta haki na uadilifu (Mfano kuwe na haki kwenye vitambulisho vya Mzanzibari, kuwe na haki kwenye uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura) ambalo litadhoofisha chama chao. Ndio maana ni CCM wachache sana walikubaliana kuundwa kwa mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. CCM wengi waliamini mwisho wa zama zao ni pale ilipoundwa Tume ya uchaguzi yenye makamishna kutoka CCM na CUF, matukio haya mpaka leo Dk. Amani Karume anaendelea kutukanwa na CCM.

7. Najizungunzia mimi binafsi namna ninavyo pokea malalamiko kutoka kwa wananchi wenzangu ninao wajua na nisio wajua, kupitia haya majukwaa ya mitandao ya kijamii kuanzia hapa Facebook, Twitter, Instagram na WhatsApp nimepokea maoni mengi sana na sehemu kubwa ya maoni hayo wameonesha hisia zao kuwa hawataki Act - Wazalendo waingie kwenye Serikali kwenda kukaa pamoja na watu ambao wanaamini ni wauaji.

Siwezi kuyachukulia malalamiko ya wananchi ambao wananifikia mimi kuwa ndio eneo la nchi nzima la, lakini angalau napata mwanga kuona jamii ikoje mpaka muda huu.

Kwa kumalizia naomba nitoe fursa kwa wafatuliaji wa ukurasa huu watoe maoni yao kwa njia za busara bila ya lugha chafu wao wanahisi nini kifanyike katika kadhia hii?

Je, ACT Wazalendo wanapaswa kuingia kwenye Serikali au wasiingie? Kama waingie wangependa nini kifanyike kwanza ndipo waingie, au kama wasiingie nini kifanyike baada ya hapo?

Ahsanteni.

Mleta uzi huu ameongea mengi ila kwa ufupi amejaa unafiki,choyo na mawazo mafupi yasiyo na tija yoyote.
Kwanza suala la mamlaka kamili ya Zanzibar halipo na anapaswa kulisahau!
Zanzibar na Tanganyika zilisha- surrender sovereignty zao kwa Tanzania.Ni total union and no turning back kama ilivyo United States of America.
Pili suala la ACT - Wazalendo kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar siyo suala la hisani bali ni suala la Katiba.ACT- Wazalendo imefikisha the required threshold hiyo ikisusa kwa sababu yoyote itajuta baadaye!
 
Image may contain: text that says 'ZANZIBAR PEMBA SLAND UNGUJA ISLAND க''ZANZIBAR PEMBA SLAND UNGUJA ISLAND க'
Ni vizuri akashiriki na kuwa sehemu ya social , economic development ya ZnZ, na mabadiliko mengine , kama ya Miundo Mbinu, na hatuwezi jua suala la mabadiliko ya kimfumo wa kisiasa nayo ikafanyika, naye akawa sehemu ya jambo hilo na la Mwisho ingawa si dogo ni hili la

"Due to significant gas reserves off Zanzibar’s coast, there is a special dissatisfaction that the union also has overall responsibility for the natural resources." Toka kwenye web site ya Denmark government??

Na ninakumbuka hivi karibuni JPM alisema Mafuta na Gas ni ya We ZnZ kama yatakuwa kwenye eneo la kiuchumi la ZnZ maana kuna sehemu ya Maji tuna share upande wa kushoto wa visiwa hivyo na upande wa kulia baada ya 200 nautical miles of the coast ya Tanzania Bara
 
Mleta uzi huu ameongea mengi ila kwa ufupi amejaa unafiki,choyo na mawazo mafupi yasiyo na tija yoyote.
Kwanza suala la mamlaka kamili ya Zanzibar halipo na anapaswa kulisahau!
Zanzibar na Tanganyika zilisha- surrender sovereignty zao kwa Tanzania.Ni total union and no turning back kama ilivyo United States of America.
Pili suala la ACT - Wazalendo kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar siyo suala la hisani bali ni suala la Katiba.ACT- Wazalendo imefikisha the required threshold hiyo ikisusa kwa sababu yoyote itajuta baadaye!
Haya ni maoni yangu binafsi , katika muendelezo wa kutoa maoni yetu hii yote ni katika kuelimishana juu ya suala la ushirika katika serikali ya Umoja wa kitaifa,Napenda kusema tena kua najaribu kuweka hapa mawazo ya kila mmoja wetu kimtazamo wake juu ya suala hili wajibu wetu kusoma na kuelewa vizuri hoja za watu mbali mbali ili na wewe uweze kutoa maoni yako. NINACHOKIOMBA NA KUSISITIZA KUCHANGIA BILA MATUSI WALA JAZBA toa maoni yako na wewe kimtazamo wako
 
Public interest ni kutanguliza mbele maslahi ya public vs maslahi ya chama kwa kujuiliza kwa kugomea chama kitafaidika na nini zaidi ya pride ya jeuri ya kugoma kuonyesha msimamo, then what?.
P
Pascal kila mara unaonyesha dharau sana kwetu wazanzibari Bro
We are minority community in this so called UNITED REPUBLIC
Tumepoteza ndugu zetu wengi kwa kuuawa na Hivi sasa kuna mamia wapo kizuizini wanateseka hapa Zanzibar hadi huko Tanganyika
Hubu fikiri ni Binadamu wa Aina gani anaweza kufanya mambo waliofanyiwa Akina Jussa na mzee Mazrui bila makosa
Bro be fair when you comment anything about us or just keep quiet we will appreciate than kutukebehi Hivi
Pls try to understand we are human being like others and we have feelings
Bro jaribuni kua waungwana japo kua uungwana sio asili yenu
 
Paskali Paskali chonde Chonde kudole na jicho
Ina maana mambo yaliotukuta wewe unaona ni pride na kiburi?
Hivi ingekua dozens za wasukuma wameuawa kikatili na wengine mpaka sasa wapo jela na wengi wamepata ulemavu wa maisha ungesema maneno hayo kwa dharau. Kebehi na kiburi hivyo?
Bro if you will be quite and do nothing for us,, nothing will go wrong for you
 
Yaan ACT wakikubali kuwaridhia ccm, ni mwisho wao
Tena sio Zanzibar hatahuku bara watakuwa wamekwisha kabisa namuhurumia zito ilezana ya usaliti itakuwa haina shaka tena vidonda vyote vilekwawatu huko Zanzibar alafu etimaridhiano hapo act kwisha kabisa
 
Public interest ni kutanguliza mbele maslahi ya public vs maslahi ya chama kwa kujuiliza kwa kugomea chama kitafaidika na nini zaidi ya pride ya jeuri ya kugoma kuonyesha msimamo, then what?.
P
Uuaji, ukatili na udhalimu waliofanyiwa wananchi wa Zanzibar na wanachama wa ACT Wazalendo je ulikuwa na maslahi gani kwa umma? (CCM na watawala sio umma)
 
Yanayoendelea mitandaoni.
vijimamboblog_20201121_1.jpg
 
Mleta uzi huu ameongea mengi ila kwa ufupi amejaa unafiki,choyo na mawazo mafupi yasiyo na tija yoyote.
Kwanza suala la mamlaka kamili ya Zanzibar halipo na anapaswa kulisahau!
Zanzibar na Tanganyika zilisha- surrender sovereignty zao kwa Tanzania.Ni total union and no turning back kama ilivyo United States of America.
Pili suala la ACT - Wazalendo kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar siyo suala la hisani bali ni suala la Katiba.ACT- Wazalendo imefikisha the required threshold hiyo ikisusa kwa sababu yoyote itajuta baadaye!
wee mpuuzi kama Tanganyika haipo kwanini munasherehekea UHURU wa TANGANYIKA?
 
Pascal kila mara unaonyesha dharau sana kwetu wazanzibari Bro
We are minority community in this so called UNITED REPUBLIC
Tumepoteza ndugu zetu wengi kwa kuuawa na Hivi sasa kuna mamia wapo kizuizini wanateseka hapa Zanzibar hadi huko Tanganyika
Hubu fikiri ni Binadamu wa Aina gani anaweza kufanya mambo waliofanyiwa Akina Jussa na mzee Mazrui bila makosa
Bro be fair when you comment anything about us or just keep quiet we will appreciate than kutukebehi Hivi
Pls try to understand we are human being like others and we have feelings
Bro jaribuni kua waungwana japo kua uungwana sio asili yenu
Mpuuze bro. Huyo jamaa ana vinasaba vya ki ccm, roho mbaya, ubinafsi, wizi, uchumia tumbo utesi hadi uuaji.
 
Naheshimu mawazo yako na maoni yangu, kwa maoni yangu, ACT isipojiunga GNU, huo utakuwa ni uamuzi wa kiendawazimu na viongozi wa ACT Wazalendo watakuwa ni insane!.
P
Empty set imefika hi hapa bila aibu kabisa .
 
Back
Top Bottom