CripWalkin' Nephew
Member
- Apr 2, 2012
- 75
- 159
Baada ya kuangalia mechi za Young Africans vs. Al Ahly ya Misri na Azam vs. Esperance ya Tunisia, nimegundua mambo kadhaa. Kwanza, imedhihirisha kiwango kidogo cha soka ya ligi yetu. Ukiangalia bila ya unazi, Al Ahly na Esperance walicheza kwa uelewano mkubwa zaidi, wakipeleka mashambulizi mbele zaidi. Pasi zao zilikuwa zinaenda mbele sio kupasiana nyuma na pembeni. Walishambulia zaidi na kucheza kwa madhumuni zaidi ya Young Africans na Azam. Walicheza mchezo wa kasi zaidi.
Pili, miili ya wachezaji wetu wengi ni midogo sana. Hawana miili ya kumudu mikikimikiki ya kucheza kwa muda mrefu. Najua kuna wachezaji kadhaa maarufu duniani wana maumbile madogo lakini wana kiwango cha juu sana (mfano Lionel Messi, David Silva, etc), lakini wengi wao wanafanya mazoezi ya kutosha na kufuata maadili ya michezo kama kula chakula sahihi, muda wa kupumzika, kuangalia mikanda ya michezo na kujifunza zaidi, etc. Waarabu walituzidi na kasi ya mchezo wao.
Tatu, kwa hakika kutolewa kwa timu zetu kumeonyesha jinsi ligi yetu ilivyo dhaifu. Huwezi kuwa unashindana na timu za kiarabu ambazo ziko kwenye kiwango cha juu kama ligi yetu ni dhaifu. Young Africans na Azam walijiandaa na mashindano ya Afrika kwa kiwango kikubwa kwa kucheza mechi za ligi yetu. Nimeangalia mechi nyingi za ligi ya VPL na kwa kweli viwango vya timu nyingi ni vya chini sana. Ligi haina ushindani. Ushindi dhidi ya Prisons au Mwadui au Kagera Sugar au Majimaji au Toto Africans hautaweza kukusaidia kupambana na miamba ya soka Afrika. Tutakuwa tunajifurahisha tu kwa kuchukua ubingwa wa VPL halafu kutolewa mapema kwenye mashindano ya Afrika. Angalia timu ambazo Young Africans itapangwa nazo kwenye kombe la shirikisho baada ya kutolewa na Al Ahly. Karibu zote ni za waarabu. Hio inakuonyesha kwamba wako katika viwango tofauti sana na sisi. Kama viongozi wa TFF wanagunduliwa kujihusisha na upangaji wa matokeo, itasaidiaje vipi kukuza soka Tanzania?
Uwekezaji kwenye michezo unahitajika sana ili kukuza viwango vyetu sio tu kwenye soka bali kwenye michezo yote. Nchi nyingi zinazofanikiwa kwenye michezo, nyingi zao zimewekeza raslimali nyingi. Kufanikiwa sio kwa kubahatisha. Ama sivyo tutaendelea kujipa moyo na kusema tutajipanga mwakani.
My two cents.