Maoni Yangu Baada ya Kuangalia Mechi za Young Africans na Azam Kwenye Mashindano ya Afrika

Apr 2, 2012
75
159
Baada ya kuangalia mechi za Young Africans vs. Al Ahly ya Misri na Azam vs. Esperance ya Tunisia, nimegundua mambo kadhaa. Kwanza, imedhihirisha kiwango kidogo cha soka ya ligi yetu. Ukiangalia bila ya unazi, Al Ahly na Esperance walicheza kwa uelewano mkubwa zaidi, wakipeleka mashambulizi mbele zaidi. Pasi zao zilikuwa zinaenda mbele sio kupasiana nyuma na pembeni. Walishambulia zaidi na kucheza kwa madhumuni zaidi ya Young Africans na Azam. Walicheza mchezo wa kasi zaidi.
Pili, miili ya wachezaji wetu wengi ni midogo sana. Hawana miili ya kumudu mikikimikiki ya kucheza kwa muda mrefu. Najua kuna wachezaji kadhaa maarufu duniani wana maumbile madogo lakini wana kiwango cha juu sana (mfano Lionel Messi, David Silva, etc), lakini wengi wao wanafanya mazoezi ya kutosha na kufuata maadili ya michezo kama kula chakula sahihi, muda wa kupumzika, kuangalia mikanda ya michezo na kujifunza zaidi, etc. Waarabu walituzidi na kasi ya mchezo wao.
Tatu, kwa hakika kutolewa kwa timu zetu kumeonyesha jinsi ligi yetu ilivyo dhaifu. Huwezi kuwa unashindana na timu za kiarabu ambazo ziko kwenye kiwango cha juu kama ligi yetu ni dhaifu. Young Africans na Azam walijiandaa na mashindano ya Afrika kwa kiwango kikubwa kwa kucheza mechi za ligi yetu. Nimeangalia mechi nyingi za ligi ya VPL na kwa kweli viwango vya timu nyingi ni vya chini sana. Ligi haina ushindani. Ushindi dhidi ya Prisons au Mwadui au Kagera Sugar au Majimaji au Toto Africans hautaweza kukusaidia kupambana na miamba ya soka Afrika. Tutakuwa tunajifurahisha tu kwa kuchukua ubingwa wa VPL halafu kutolewa mapema kwenye mashindano ya Afrika. Angalia timu ambazo Young Africans itapangwa nazo kwenye kombe la shirikisho baada ya kutolewa na Al Ahly. Karibu zote ni za waarabu. Hio inakuonyesha kwamba wako katika viwango tofauti sana na sisi. Kama viongozi wa TFF wanagunduliwa kujihusisha na upangaji wa matokeo, itasaidiaje vipi kukuza soka Tanzania?
Uwekezaji kwenye michezo unahitajika sana ili kukuza viwango vyetu sio tu kwenye soka bali kwenye michezo yote. Nchi nyingi zinazofanikiwa kwenye michezo, nyingi zao zimewekeza raslimali nyingi. Kufanikiwa sio kwa kubahatisha. Ama sivyo tutaendelea kujipa moyo na kusema tutajipanga mwakani.
My two cents.
 
Naomba nitofautiane na wewe kidogo kwenye baadhi ya mambo:
(1) Kama ni kweli kwamba kiwango cha ligi yetu ni dhaifu ndio kisa timu mbili hizo zimefungwa, basi ilikuwa pia ukubali kwamba timu mbili hizo na/au wachezaji wake na/au benchi lao la ufundi ama vyote kwa pamoja ni nzuri mno. Wote wametolewa kwa mabao 3-2, ambayo ni sawa na aliyotolewa Barca na Atletico, PSG na Man C na Wolfsburg na Real Madrid. Kama Madrid alizidiwa mechi ya ugenini, naye akamzidi Wolfsburg kwa bao moja nyumbani. Ni kwa sababu Bundesliga ni dhaifu kuliko La Liga? Au La Liga (Barca) ni dhaifu kuliko La Liga (Atletico)? Au EPL kuliko Ligue 1? Sidhani.
......... Samahani, nitaendelea baadaye.
 
Mkuu nenda kasomee ukocha. Unajua kuchambua mpira
 
Nimekuelewa ulichosema. Lakini kwa maoni yangu kulinganisha matokeo ya ligi za mabingwa wa Ulaya na nilichozungumzia nafikiri itakuwa sio sawa. Viwango vya timu za Ulaya ulizozitaja vinakaribiana au vinalingana zaidi kuliko kati ya Al Ahly na Young Africans. Tofauti ya viwango kati ya Man City na PSG au Barca na Atletico Madrid ni ndogo zaidi kuliko ya Al Ahly na Young Africans au Azam na Esperance. Ukiwa unaingia kwenye mashindano na timu ambazo zina viwango vya juu zaidi kuliko wewe, ni muhimu na jambo muhimu uipe kipaumbele kujiandaa na timu ambazo ziko katika kiwangu karibu au zaidi na timu unayoshindana nayo. Ukiwa unajiandaa kwa kucheza na Mtibwa Sugar/Ndanda/Mwadui/Mbeya City/Stand United etc. utakuwa unajidanganya mwenyewe kwa kuwa utazishinda hizo timu dhaifu ambazo hazina kiwango cha kujipima nao. Ndio maana ninaamini mpaka kiwango cha timu za ligi ya VPL kitakapopanda na kuwa na timu kabambe kama tano za ushindani, tutaendelea kuwa wasindikizaji kila mwaka kwenye mashindano ya Afrika.
My 2 cents.
 
Azam wameshindwa kwa kukosa uzaoefu tu
ila sio kiwango

Yanga walizidiwa na 'home advantage' tu kwa al ahly
The Boss, naomba uangalie huu mjadala kwenye mtizamo tofauti kidogo. Kwa mfano, ili uwe na matokeo mazuri darasani, unatakiwa ujipime na wanafunzi wanaofanya vyema zaidi darasani. Ukijipima na wanafunzi walio katika kiwango chako, utajiona unafanya vizuri sana wakati moyoni unajijua hauko kwenye kiwango cha kushindana na wanaofanya vizuri zaidi.
Kwa kusema kwamba Young Africans walizidiwa na home advantage na Al Ahly ni kuzidi kuipa nguvu maoni yangu. Kwa maana hiyo inaonyesha kwamba Young Africans kama timu haikujua umuhimu wa kushinda uwanjani kwake. Al Ahly walikuja Tanzania kutafuta suluhu na wakaipata. Wakaenda kwao na wakashinda. Sina imani kwamba hata tungeanza kucheza Misri kwanza kuwa tungeweza kufuzu. Mfano mwingine, wakati Tanzania inafanya vizuri kwenye riadha (Enzi za akina Juma Ikangaa na Gidamis Shahanga) ushindani ulikuwa mkubwa sana kati ya wanariadha wa humuhumu nchini na pia kati ya Tanzania na majirani zetu hususani Kenya na Ethiopia. Hii ilichangia kupata wanariadha bora. Ninavyoamini, jipime na walio juu yako sio walio katika kiwango chako. Hii inakupa motisha zaidi kufikia kiwango chao.
 
Naomba nitofautiane na wewe kidogo kwenye baadhi ya mambo:
(1) Kama ni kweli kwamba kiwango cha ligi yetu ni dhaifu ndio kisa timu mbili hizo zimefungwa, basi ilikuwa pia ukubali kwamba timu mbili hizo na/au wachezaji wake na/au benchi lao la ufundi ama vyote kwa pamoja ni nzuri mno. Wote wametolewa kwa mabao 3-2, ambayo ni sawa na aliyotolewa Barca na Atletico, PSG na Man C na Wolfsburg na Real Madrid. Kama Madrid alizidiwa mechi ya ugenini, naye akamzidi Wolfsburg kwa bao moja nyumbani. Ni kwa sababu Bundesliga ni dhaifu kuliko La Liga? Au La Liga (Barca) ni dhaifu kuliko La Liga (Atletico)? Au EPL kuliko Ligue 1? Sidhani.
......... Samahani, nitaendelea baadaye.
(1)......... Kwa hivyo Kama timu zetu kutoka ligi dhaifu zimetolewa kwa tofauti ya bao moja na timu za kwenye ligi ngumu, maana yake ni kwamba timu hizo ni nzuri mno. Ni sawa na kumtoa mwanafunzi wa Sekondari ya Kata ukamfanyisha mtihani na yule wa International school na wakapishana kwa tofauti ya daraja moja, yaani mmoja ana A na mwengine B.
(2) Tatizo kubwa nililoliona ni ukosefu wa ustadi (professionalism). Wachezaji wengi wasio professionals wanashindwa kuweka nadhari zao mpirani (concentration) kwa dakika zote za mchezo. Angalau Yanga walijaribu kwa dakika 94. Dakika moja tu waliyojisahau kidogo tu ikatosha kuwamaliza. Kufungwa goli la mapema kabisa, au mara tu baada ya kufungwa, au mara tu baada ya kufunga, au kuchelewa kujipanga mpira wa adhabu unapoanzwa harakaharaka, au muda mchache tu kabla ya kipindi cha kwanza ama cha pili kimalizika, zote hizo ni ishara za ukosefu wa umakini. Professionalism ni jinsi ya kuepukana na athari hizo na jinsi ya kutumia makosa ya aina hiyo yanapofanywa na wapinzani wako. Ndivyo ilivyowatokezea Yanga na Azam. Si swala la ligi gani timu i
(3) Ufanisi (efficiency) kwenye ufungaji. Kocha mzuri ni yule anayeiwezesha timu yake kutengeneza nafasi nyingi za kufunga. Timu nzuri ni ile inayozitumia nafasi za kufunga inszopata. Baina ya timu inayotengeneza nafasi kumi ikazitumia tatu na ile inayotengeneza tano ikatumia tatu, kura yangu iko kwenye hii ya pili. Bado timu zetu na wachezaji wetu hawajafikia ufanisi huo, la sivyo mechi yetu na Algeria ingemalizika kipindi cha kwanza cha mechi ya Dar. Ile ilikuwa na akina Samatta na Ulimwengu wanaochezea ligi na timu bora zaidi kuliko za hapa nyumbani. Lakini hawajafikia ufanisi huo. Algiers walitufunga kwa sababu walikuwa na ufanisi wa kutumia nafasi na ufanisi binafsi wa akina Mahrez wanaowazidi akina Samatta na Ulimwengu.
(4)
Nimekuelewa ulichosema. Lakini kwa maoni yangu kulinganisha matokeo ya ligi za mabingwa wa Ulaya na nilichozungumzia nafikiri itakuwa sio sawa. Viwango vya timu za Ulaya ulizozitaja vinakaribiana au vinalingana zaidi kuliko kati ya Al Ahly na Young Africans. Tofauti ya viwango kati ya Man City na PSG au Barca na Atletico Madrid ni ndogo zaidi kuliko ya Al Ahly na Young Africans au Azam na Esperance. Ukiwa unaingia kwenye mashindano na timu ambazo zina viwango vya juu zaidi kuliko wewe, ni muhimu na jambo muhimu uipe kipaumbele kujiandaa na timu ambazo ziko katika kiwangu karibu au zaidi na timu unayoshindana nayo. Ukiwa unajiandaa kwa kucheza na Mtibwa Sugar/Ndanda/Mwadui/Mbeya City/Stand United etc. utakuwa unajidanganya mwenyewe kwa kuwa utazishinda hizo timu dhaifu ambazo hazina kiwango cha kujipima nao. Ndio maana ninaamini mpaka kiwango cha timu za ligi ya VPL kitakapopanda na kuwa na timu kabambe kama tano za ushindani, tutaendelea kuwa wasindikizaji kila mwaka kwenye mashindano ya Afrika.
My 2 cents.
Dhana (hypothesis) yako hiyo inakosa mashiko kwa sababu tofauti ya viwango inapaswa kuonekana kwenye matokeo ya timu zenyewe. Kusema kwamba kusonga kwa 3-2 kwa Atletico, Real, Bayern na Man City ni kwa sababu ya kukaribiana viwango na Barca, Wolfsburg na PSG lakini tofauti hiyo hiyo ya 3-2 kwa Ahly na Esperence dhidi ya Yanga na Azam ni kutokana na tofauti kubwa ya viwango kunakuwa ni kichekesho kwa mwenye akili ya tafakuri. Angalia San Marino ama Iceland zinapocheza na timu nyengine za Ulaya. Matokeo Yao ni ishara ya tofauti za viwango. Lakini si matokeo ya 3-2 popote pale.
 
Baada ya kuangalia mechi za Young Africans vs. Al Ahly ya Misri na Azam vs. Esperance ya Tunisia, nimegundua mambo kadhaa. Kwanza, imedhihirisha kiwango kidogo cha soka ya ligi yetu. Ukiangalia bila ya unazi, Al Ahly na Esperance walicheza kwa uelewano mkubwa zaidi, wakipeleka mashambulizi mbele zaidi. Pasi zao zilikuwa zinaenda mbele sio kupasiana nyuma na pembeni. Walishambulia zaidi na kucheza kwa madhumuni zaidi ya Young Africans na Azam. Walicheza mchezo wa kasi zaidi.
Pili, miili ya wachezaji wetu wengi ni midogo sana. Hawana miili ya kumudu mikikimikiki ya kucheza kwa muda mrefu. Najua kuna wachezaji kadhaa maarufu duniani wana maumbile madogo lakini wana kiwango cha juu sana (mfano Lionel Messi, David Silva, etc), lakini wengi wao wanafanya mazoezi ya kutosha na kufuata maadili ya michezo kama kula chakula sahihi, muda wa kupumzika, kuangalia mikanda ya michezo na kujifunza zaidi, etc. Waarabu walituzidi na kasi ya mchezo wao.
Tatu, kwa hakika kutolewa kwa timu zetu kumeonyesha jinsi ligi yetu ilivyo dhaifu. Huwezi kuwa unashindana na timu za kiarabu ambazo ziko kwenye kiwango cha juu kama ligi yetu ni dhaifu. Young Africans na Azam walijiandaa na mashindano ya Afrika kwa kiwango kikubwa kwa kucheza mechi za ligi yetu. Nimeangalia mechi nyingi za ligi ya VPL na kwa kweli viwango vya timu nyingi ni vya chini sana. Ligi haina ushindani. Ushindi dhidi ya Prisons au Mwadui au Kagera Sugar au Majimaji au Toto Africans hautaweza kukusaidia kupambana na miamba ya soka Afrika. Tutakuwa tunajifurahisha tu kwa kuchukua ubingwa wa VPL halafu kutolewa mapema kwenye mashindano ya Afrika. Angalia timu ambazo Young Africans itapangwa nazo kwenye kombe la shirikisho baada ya kutolewa na Al Ahly. Karibu zote ni za waarabu. Hio inakuonyesha kwamba wako katika viwango tofauti sana na sisi. Kama viongozi wa TFF wanagunduliwa kujihusisha na upangaji wa matokeo, itasaidiaje vipi kukuza soka Tanzania?
Uwekezaji kwenye michezo unahitajika sana ili kukuza viwango vyetu sio tu kwenye soka bali kwenye michezo yote. Nchi nyingi zinazofanikiwa kwenye michezo, nyingi zao zimewekeza raslimali nyingi. Kufanikiwa sio kwa kubahatisha. Ama sivyo tutaendelea kujipa moyo na kusema tutajipanga mwakani.
My two cents.

True, tatizo la kwetu badala ya kutumia vipaji na formations za uhakika, sie bado tuna amini wale wazee wa Pemba waturahisishie mambo yetu ya jadi ili tupate ushindi. Ndiyo maana kuna kipindi wachezaji wa Yanga walionekana wamepotea kimbinu kila mmoja akimuangalia mwenzake anafanya nini huku waraab wakiwalisha tende kwa ujanja wao. Cha kushangaza wana Yanga wanasema walicheza mpira wa uhakika, how....I don't know when kila mmoja wetu aliyeona ile mechi alishangazwa na kiwango kile kwani muda mwingi sana Yanga walipotezana. My take: Safari za Pemba kabla ya mechi hazina tija, tunahitaji wachezaji wa kiukweli si wabeba ndumba uwanjani, si mliona jana?
 
Mara nyingi tumeona kwamba nchi zenye ligi zenye ushindani mkubwa zaidi ndio zinazotoa timu bora zaidi na vile vile ndio zinazotoa timu bora zaidi za taifa. Ukiangalia listi ya timu na timu za taifa zinazoongoza kwa kuchukua makombe mengi Afrika (CAF Champions League - Wikipedia, the free encyclopedia), karibu zote zinatoka magharibi na kaskazini mwa Afrika. Hio si kwa bahati. Wenzetu wamewekeza zaidi kwenye soka na wanakula faida ya uwekezaji wao (kupitia watu binafsi na pia serikali zao). Ni sawasawa na mzazi anayewekeza kwenye elimu ya mtoto wake (kwa kutumia fedha zake, muda wake, shule nzuri, etc) mara nyingi atakula matunda ya uwekezaji wake. Ni gharama kubwa kuwekeza kwenye michezo lakini ndio njia peke ya kuweza kupiga hatua na kuwa na mafanikio. Mafanikio hayatakuja bila uwekezaji.
 
True, tatizo la kwetu badala ya kutumia vipaji na formations za uhakika, sie bado tuna amini wale wazee wa Pemba waturahisishie mambo yetu ya jadi ili tupate ushindi. Ndiyo maana kuna kipindi wachezaji wa Yanga walionekana wamepotea kimbinu kila mmoja akimuangalia mwenzake anafanya nini huku waraab wakiwalisha tende kwa ujanja wao. Cha kushangaza wana Yanga wanasema walicheza mpira wa uhakika, how....I don't know when kila mmoja wetu aliyeona ile mechi alishangazwa na kiwango kile kwani muda mwingi sana Yanga walipotezana. My take: Safari za Pemba kabla ya mechi hazina tija, tunahitaji wachezaji wa kiukweli si wabeba ndumba uwanjani, si mliona jana?
jina lako na mawazo yako vinafanana.uwezo walioonyesha jana yanga ni wajuu sana.
 
Baada ya kuangalia mechi za Young Africans vs. Al Ahly ya Misri na Azam vs. Esperance ya Tunisia, nimegundua mambo kadhaa. Kwanza, imedhihirisha kiwango kidogo cha soka ya ligi yetu. Ukiangalia bila ya unazi, Al Ahly na Esperance walicheza kwa uelewano mkubwa zaidi, wakipeleka mashambulizi mbele zaidi. Pasi zao zilikuwa zinaenda mbele sio kupasiana nyuma na pembeni. Walishambulia zaidi na kucheza kwa madhumuni zaidi ya Young Africans na Azam. Walicheza mchezo wa kasi zaidi.
Pili, miili ya wachezaji wetu wengi ni midogo sana. Hawana miili ya kumudu mikikimikiki ya kucheza kwa muda mrefu. Najua kuna wachezaji kadhaa maarufu duniani wana maumbile madogo lakini wana kiwango cha juu sana (mfano Lionel Messi, David Silva, etc), lakini wengi wao wanafanya mazoezi ya kutosha na kufuata maadili ya michezo kama kula chakula sahihi, muda wa kupumzika, kuangalia mikanda ya michezo na kujifunza zaidi, etc. Waarabu walituzidi na kasi ya mchezo wao.
Tatu, kwa hakika kutolewa kwa timu zetu kumeonyesha jinsi ligi yetu ilivyo dhaifu. Huwezi kuwa unashindana na timu za kiarabu ambazo ziko kwenye kiwango cha juu kama ligi yetu ni dhaifu. Young Africans na Azam walijiandaa na mashindano ya Afrika kwa kiwango kikubwa kwa kucheza mechi za ligi yetu. Nimeangalia mechi nyingi za ligi ya VPL na kwa kweli viwango vya timu nyingi ni vya chini sana. Ligi haina ushindani. Ushindi dhidi ya Prisons au Mwadui au Kagera Sugar au Majimaji au Toto Africans hautaweza kukusaidia kupambana na miamba ya soka Afrika. Tutakuwa tunajifurahisha tu kwa kuchukua ubingwa wa VPL halafu kutolewa mapema kwenye mashindano ya Afrika. Angalia timu ambazo Young Africans itapangwa nazo kwenye kombe la shirikisho baada ya kutolewa na Al Ahly. Karibu zote ni za waarabu. Hio inakuonyesha kwamba wako katika viwango tofauti sana na sisi. Kama viongozi wa TFF wanagunduliwa kujihusisha na upangaji wa matokeo, itasaidiaje vipi kukuza soka Tanzania?
Uwekezaji kwenye michezo unahitajika sana ili kukuza viwango vyetu sio tu kwenye soka bali kwenye michezo yote. Nchi nyingi zinazofanikiwa kwenye michezo, nyingi zao zimewekeza raslimali nyingi. Kufanikiwa sio kwa kubahatisha. Ama sivyo tutaendelea kujipa moyo na kusema tutajipanga mwakani.
My two cents.
ile mechi ya yanga yaleyaliyotokea ni matokeo ya mechi tu.vp kuhusu matokeo ya tp mazembe na wahdad?nao congo ligi yao ni mbovu?
 
muhuwesichimalamyasi, kila mwaka ni timu moja tu inayochukua ubingwa wa soka Afrika. Inafikia kuchukua ubingwa kwa kuzifunga timu nyingine bora za Afrika. Tafadhali angalia ushiriki wao kwa ujumla kila mwaka wa timu ulizozitaja. Mara nyingi huwa zinafika mbali zaidi ukilinganisha na timu zetu. Ni mara chache zinatolewa katika hatua za awali au za chini. Kwa timu zetu, hadithi ni ileile kila mwaka. Hio ndio tofauti ya wenzetu na sisi.
 
Dr. Liki Abdallah anachambua mpira vizuri kuliko G. Neville

Kwangu mimi Dr. Leakey ni historian wa mambo ya soka ila sio mchambuzi wa mambo ya kiufundi. Half time badala ya kuongea mambo ya kiufundi kuhusu mchezo, yeye hukumbushia matukio ya zamani ghafla muda umeisha.
 
Kwa maoni yangu. Yanga ilijitahidi illa timu za misri miaka ya karibuni na hata timu yao ya taifa hazipo vizuri. Imesababishwa na hali ya kisisa katika taifa hilo. Wanaanza kujenga timu za taifa na vilabu. Kwa yanga ulikuwa ni wakati mzuri kuitoa timu lenye jina kubwa kwenye mashindano haya lakini haiko kiwango kizuri kama miaka ya nyuma. Tatizo kubwa ni concertration yaani tahadhari dakika mpaka ya mwisho zina tugharimu sana timu zetu. Tumbuke pia wachezaji wa ndani bado illa wakigeni walisaidia sana. Ili vilabu vyote vifanikiwe kwanza ni uongozi pili kuachana na uchawi halafu mechi za nyumbani tusiruhusu goli na tujitahidi kufunga zaidi ya goli 2-0. Tofauti na hapo tutabaki tulijitahidi neno sio zuri tuseme tumefanikisha. Na kumtoa Al Ahly haikuwa imetosha muhimu tutachukua kombe lini?????.
 
Back
Top Bottom