Maoni yako Katika Hii barua ya kazi

Udochi

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
782
1,056
Heshima yenu wakuu.

Elimu yangu ni diploma ya ualimu,
Ninafanya kazi ya kufundisha katika shule ya binafsi kwa miezi kadhaa,
Ingawa idadi ya wanafunzi ni Kubwa na vipindi kuwa vingi sana, malipo yameongezeka kidogo tu zaidi ya yale ya serikalini.
Leo nimepewa barua ya mkataba wa miaka miwili, lakini pia nina lengo la kwenda kujionea hali itakavyokuwa kwenye ajira za serikalini zitakapotoka.

Wakuu ni vizuri kuusaini huu mkataba?
Na nisipousaini watanivumilia mpaka miezi miwili mbele?
 
Ni vizur kuangalia unataka nini, kama mipango yako ni kufundisha serikalin subili ajira zitoke, kama ni private sign mkataba uendelee kupiga kazi. Ila kama haujafanya maamuz waambie wakupe muda wa ili ufanye maamuzi. Usiwe mwoga kuongea na hao wakuu wa shule, kuwa huru hilo ni suala linalohusu future yako so usikurupuke. Fanya analysis ya possibilities zote mbili private na government, kabla ya kufanya maamuz ya mwisho
 
Ajira za ualimu kuna uwezekano zikatoka juma lijalo kwa kauli ya serikali so kuwa mvumilivu
 
Mpaka sasa hajachagua kama anataka kusuka au kunyoa. Angekuwa kachagua au anataka apewe abc's za nini ni nni na wapi ni wapi kazi hii nyepesi sana. Komaa kwanza ujue exactly unataka nni hapa jukwaani ndo uje uombe ushauri
 
Back
Top Bottom