Maoni ya Zitto Kabwe kuhusu azimio la Arusha

BAKOI

JF-Expert Member
Jan 31, 2016
1,211
2,328
" tukipata msaada hutangaza; tukipata mkopo hutangaza; [ ...... ] tukiahidiwa msaada, mkopo au kiwanda kipya hutangaza. Japo tukianza mazungumzo tu na nchi au shirika la kigeni juu ya msaada, mkopo au kiwanda hutangaza japo hatuna hakika ya matokeo ya mazungumzo hayo". - Azimio la Arusha 1967.

Miaka 50 baadaye Hali ni hiyo hiyo. Kila Rais wetu akikutana na Rais wa nchi nyengine au hata Balozi tu inatoka Taarifa kwa vyombo vya habari Tanzania imeahidiwa misaada. Reli kwa mfano, tumeomba na ' kukubaliwa' Uchina. Tumeomba India. Tumeomba Uturuki. Sasa tumesaini mkataba wa ujenzi hakuna hela ya china wala India. Tumetangaza mkataba wa USD 1.2bn wakati kwenye Bajeti tuna USD 450m tu. Tukiendelea kutenga Bajeti kiwango hiki hiki kila mwaka itatuchukua Bajeti 3 kufikisha Reli mpya Morogoro.
Huu ni mfano mmoja tu wa uhalisia wa kuishi kinyume na maono ya Azimio la Arusha. Kwanini tunatangaza maombi ya misaada kana kwamba tumepewa misaada hiyo tayari? Kwanini kila mgeni anayetutembelea sisi tunaomba tu? China Reli na tumekosa. India Reli na mengine wamenyuti. Uturuki Reli na kampuni yao tumeipa biashara tayari. Hata Morocco tumewaomba misikiti na viwanja vya mpira. Miaka 50 mwelekeo wa nchi umebadilika kana kwamba nchi hii haijawahi kuwa na Azimio la Arusha.

Tumekuwa omba omba na kutangaza kuomba omba bila aibu. Azimio lilionya Februari 5, 1967.

Je una nukuu yako ya Azimio la Arusha? Ilete hapa tuijadili na kulinganisha na Hali ya sasa.
 
Back
Top Bottom