Maoni ya Zitto juu ya katazo la Rais Magufuli kuhusu kusafirisha mchanga

Massivve

JF-Expert Member
Jun 4, 2015
274
368
Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo ametoa maoni yake juu ya katazo la Rais Magufuli kutotaka mchanga usafirishwe nje ya nchi huku akidai Raia mwema wameuliza maoni yake juu ya zuio hilo.

Zitto ametoa maoni yake haya kupitia mtandao wake wa kijamii:

RaiaMwema waliniuliza maoni yangu kuhusu zuio la kupeleka nje mchanga wa madini. Haya Ndio majibu yangu ambayo yamenukuliwa na Toleo la Leo la gazeti Hilo, Toleo namba 500 la 8/3/2017.

“Kuweka zuio la kusafirisha mchanga wa dhahabu ni uamuzi sahihi uliofanywa bila kuzingatia kwanza uwezo wa ndani wa kuchenjua ( refinery).

Kumekuwa na maneno kuwa hatuna uwezo wa kuchenjua hapa nchini, haya ni mawazo ya kilofa na kasumba ya hatuwezi. Unahitaji tani 150,000 za mchanga kwa mwaka kuweza kuwa na kinu cha kuchenjua chenye manufaa ( economies of scale) lakini sisi tunazalisha tani 40,000 Hivi. Pia tunahitaji umeme zaidi ya 1500MW kwa mwaka ambazo kwa sasa hatuna. Tunachoweza kufanya ni kwanza kutazama potential ya hii region ya kuzalisha Hizo copper concentrates ili kuingia mikataba na nchi jirani ziweze kuleta mchanga wao hapa na sisi tuwe kituo cha uchenjuaji kwenye region.

Pili tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye uzalishaji wa umeme ili kufikia mahitaji hayo. Sasa mjadala hapa ni kwanini tunazuia kabla ya kujenga huo uwezo? Inawezekana zuio alilotoa Rais Ndio litaweza kuanzisha mjadala wa majawabu hayo kwani ni mjadala wa miaka mingi Sana. Kuna nyakati vijana wa Kahama walikuwa wanayapiga mawe magari yaliyobeba mchanga kwa hasira. Sisi wanasiasa tulikuwa tunaibua jambo hili Kila mwaka kupinga mchanga kusafirishwa. Kwahiyo AMRI ya Rais iwe ni kuleta mjadala kisha tukubaliane mkakati wa kuhakikisha jawabu la kudumu linapatikana.

Lakini pia wataalamu wanaweza kukaa na kubuni teknolojia yenye uwezo wa kufanya uchenjuaji kwa kiwango cha mchanga tunachozalisha nchini. Haiwezekani dunia nzima ikawa na teknolojia moja tu ya tani 150,000 la hasha.

Ushauri wangu ni kwamba Serikali ikae na sekta ya madini ili kupata jawabu la kudumu na kuweka commitment ya muda maalumu kuendelea kusafirisha mchanga na baada ya muda huo mchanga huo uchenjuliwe nchini kwetu na kuzalisha ajira na kuongeza uwezo wetu wa kuzalisha. Hii sio Zero-Sum game ( Kama sio kusafirisha basi hakuna lingine). Hapana. Mjadala unaweza kuleta jawabu lenye faida kwa nchi”
 
Niliombwa kutoa maoni yangu kuhusu mgombea wa uraisi 2020 toka upande wa wapinzani. Nilimjibu yule muhusika kuwa Zitto anafaa sana kama atapunguza au kuacha umimi. Nikasema jamaa anakili nyingi na anajua uongozi na juu ya yote anasoma sana mambo yanavyoendelea duniani na historia za viongozi/uongozi huko tulikotoka.
 
Tatizo la Jepesi ni unafiki na ubinafsi! Kwa sifa hizi ni rahisi sana kwa Jepesi kusaliti kwa kutumiwa na sirikali!
 
Ameongea facts tupu.. Hii nchi yetu sote, tuijenge.
Fact hapo aliyoongea ni hipi? Shida ya nchi hii ukishakuwa mwanasiasa basi kila kitu unajua,
Swali la kujiuliza je Tanzania kuna Migodi mingapi? Na migodi mingapi ndio inapeleka mchanga nje? Je (Barrick) Acacia ina migodi mingapi Tanzania?, kwa nini Wachukue mchanga wa Bulyanhulu waupeleke Japani ili hali wana mgodi wa jirani hapo Buzwagi?

Sayansi haitaki shortcut na wala sio Siasa
 
ametumia maneno mengiii
ila in summary ni kwamba kwa Sasa hatuna uwezo huo
hatuweziii
 
Yaani hii ni bongo tu maskini anafanya maamuzi na kushauri uwekezaji mzuri na faida kwa wawekezaji wenye mitaji.

Kama hutoi pesa utapataje uchungu na thamani katika maamuzi unayofanya? Kuwa raisi au mwanasiasa haitoshi kuwa na uchungu.
 
Kama nimemuelewa mpaka sasa hakuna mwenye jibu sahihi ya kwamba tufanye nini. Inabidi jambo hili lifanyiwe kazi. Hata hilo la wengine kuleta mchanga wao kwetu nalo ni jambo la kutafakari (sisi hatutaki wetu uende hukooo, sasa ni incentive gani tutawapa wao ili walete wao hapa?). Je hiyo technology tunaweza kupata (naogopa kusema kutengeneza) inayotufaa? Nafikiri kwa sasa hakuna mwenye majibu zaidi ya kusema acha mchanga wetu ulundikane tu. Na hapa tunajadili technical feasibility. Economic feasibility ni habari nyingine. Kazi ipo.
 
Fact hapo aliyoongea ni hipi? Shida ya nchi hii ukishakuwa mwanasiasa basi kila kitu unajua,
Swali la kujiuliza je Tanzania kuna Migodi mingapi? Na migodi mingapi ndio inapeleka mchanga nje? Je (Barrick) Acacia ina migodi mingapi Tanzania?, kwa nini Wachukue mchanga wa Bulyanhulu waupeleke Japani ili hali wana mgodi wa jirani hapo Buzwagi?

Sayansi haitaki shortcut na wala sio Siasa
tupe figure Acha porojo
40000 tones per year
wewe utafiti wako wakisayansi unasemaje
 
Niliombwa kutoa maoni yangu kuhusu mgombea wa uraisi 2020 toka upande wa wapinzani. Nilimjibu yule muhusika kuwa Zitto anafaa sana kama atapunguza au kuacha umimi. Nikasema jamaa anakili nyingi na anajua uongozi na juu ya yote anasoma sana mambo yanavyoendelea duniani na historia za viongozi/uongozi huko tulikotoka.
That's right, jamaa akiacha umimi ni atafaa sana. Namuelewa sana Zitto, ana akili na anajua, sema namuonaga kama yupo a little bit selfish
 
Porojo gani nilizoongea?, 40,000 tonnes per year ndio ina maana gani? Acha kukaririshwa
Unapokosea ndo hapo ndugu!! Hii industry ni wachache sana ndio wanaifahamu!! Zitto katoa takwimu zake na kwahiyo ni rahisi mtu kumuamini!! Lakini kama unaona Zitto amedanganya; wewe ulitakiwa kueleza ukweli wenyewe! Hivyo ndivyo mijadala inavyotakiwa!!!

Sasa ikiwa unaishia kusema huo ni uongo mtupu lakini ukweli hujauweka; unachoongea kinaonekana hakina nguvu!!!!
 
Niliombwa kutoa maoni yangu kuhusu mgombea wa uraisi 2020 toka upande wa wapinzani. Nilimjibu yule muhusika kuwa Zitto anafaa sana kama atapunguza au kuacha umimi. Nikasema jamaa anakili nyingi na anajua uongozi na juu ya yote anasoma sana mambo yanavyoendelea duniani na historia za viongozi/uongozi huko tulikotoka.
Ana u mimi kama nani hapa kwetu?
 
Fact hapo aliyoongea ni hipi? Shida ya nchi hii ukishakuwa mwanasiasa basi kila kitu unajua,
Swali la kujiuliza je Tanzania kuna Migodi mingapi? Na migodi mingapi ndio inapeleka mchanga nje? Je (Barrick) Acacia ina migodi mingapi Tanzania?, kwa nini Wachukue mchanga wa Bulyanhulu waupeleke Japani ili hali wana mgodi wa jirani hapo Buzwagi?

Sayansi haitaki shortcut na wala sio Siasa
Iko hivi. Mgodi wa buly ni mgodi wa shaba kwa zaidi ya asilimia 49. Yaani shaba ni nyingi kuliko dhahabu. Pia una madini kama mercury. Lead. Silver na platnum kwa kiwango kidogo.

Migodi mingine ya Accacia ni ya dhahabu kwa zaidi ya asilimia 90. Hivyo kama kuna shaba ni haina faida.

Kila mgodi wa Accacia una mitambo ya kuchenjua dhahabu. Hivyo mchanga wenye dhahabu haupelekwi nje.

Technologia ya kuchenjua shaba ndiyo hiyo umeona wameongelea hapo juu. Pale Buly mtambo unachenjua asilimia kama 90 ya dhahabu na mabaki yanakuwa ni shaba zaidi ya asilimia 90 na madini mengine nilotaja hapo juu pamoja na mabaki ya dhahabu. Huo ndio MCHANGA unaopelekwa Japani.
 
Unapokosea ndo hapo ndugu!! Hii industry ni wachache sana ndio wanaifahamu!! Zitto katoa takwimu zake na kwahiyo ni rahisi mtu kumuamini!! Lakini kama unaona Zitto amedanganya; wewe ulitakiwa kueleza ukweli wenyewe! Hivyo ndivyo mijadala inavyotakiwa!!!

Sasa ikiwa unaishia kusema huo ni uongo mtupu lakini ukweli hujauweka; unachoongea kinaonekana hakina nguvu!!!!

Kaka hiyo kitu nimeiongea hapo juu lakini kuna watu wanawamini zaidi wanasiasa kuliko uhalisia
Kwenye Maswala ya Migoni hatuangalii tonnage (quantity) pekeyake, bali tunaangalia na Quality ya unachokichimba, dhahabu ya sehemu moja haifanani na ya sehemu nyingine unaweza kukuta dhahabu imechanganyika na Copper, Silver nk
Kwa Tanzania ni mgodi mmoja tu (Bulyanhulu Gold Mine) ndio unaosafirisha mchanga kwenda nje (Japan) kwa ajili ya processing, Barrick then Sasa Acacia walikuwa na migodi minne mikubwa Tanzania, Bulyanhulu, Tulawaka, NorthMara na Buzwagi, lakini katika migodi yote hiyo ni mmoja tu ndio mchanga wake ulikuwa unasafirishwa kwenda nje WHY?
Kwa nini hawakuchukua mchanga wa Bulya na kuupeleka Buzwagi ama Northmara ama Tulawaka? Process ya kutenganisha dhahabu ya Bulya ni tofauti na migodi yote iliyopo Tanzania, na gharama za kufunga mashine za kuchakata aina hiyo ya Dhahabu ni kubwa na inahitaji Umeme mkubwa sana ambao kwa Tanzania hatukuwa nao na wala hatunao mpaka sasa, na hata Duniani ni nchi chache sana zenye hiyo mitambo ikiwemo Japan, so ilikuwa ni Rahisi sana kuchakata mchanga huo Japan kuliko kufunga hiyo mitambo Tz na hao Barrick then walilieza hilo na likaeleweka na wataalam wetu na mkataba ukasainiwa

Huo Mchanga ukichakatwa kokote kule wala hakuna shida kama Tanzania itaweka watu wake wa kusimamia hilo zoezi, yaani mchanga unapofikishwa kwenye hizo refinery kuna kuwa na Watanzania wanaofanya control same kama wanavyofanya hapa Tanzania na mwisho wa siku watajua dhahabu ni kiasi gani na Byproducts (Silver, Copper) ni kiasi gani

So issue ya mchanga kwenda nje sio issue ya Quantity bali Quality (Metallurgical factors)

Cc: young solicitor haya kariri kaka
 
Unapokosea ndo hapo ndugu!! Hii industry ni wachache sana ndio wanaifahamu!! Zitto katoa takwimu zake na kwahiyo ni rahisi mtu kumuamini!! Lakini kama unaona Zitto amedanganya; wewe ulitakiwa kueleza ukweli wenyewe! Hivyo ndivyo mijadala inavyotakiwa!!!

Sasa ikiwa unaishia kusema huo ni uongo mtupu lakini ukweli hujauweka; unachoongea kinaonekana hakina nguvu!!!!
Well stated! Kuna watu wengine wanafanya mpaka jamii forum inazaraulika. Zitto katoa lkile alichokifanyia kazi, unaposema siyo sahihi sema kipi ni sahihi. Siyo vema kupinga kila kitu wakati huna facts na hicho kitu.
Tujifunze kujadili mada kuliko kumjadili mtu, tuache kuangalia nani kasema tuangalie nini kimesemwa.
Kuna watu utazani wanalipwa kwa ku criticise kila kinachosemwa na Zitto.
HONGERA ZITTO KWA HIZI FIKRA, STILL MIJADARA INAHITAJIKA TO BE ADDRESSED AT THIS ISSUE.
 
Back
Top Bottom