Wadau, mimi niko nje ya nchi katika taasisi fulani ya elimu. Taarifa hizi zimeshasambaa sana kwenye vyombo vya habari vya kimataifa. Sasa tunaulizwa sana na wenzetu kuwa inakuwaje wafanyakazi zaidi ya elfu kumi wawe na vyeti feki. Kwa maoni yao ni kwamba, credibility yetu nje ya nchi imeshuka sana.Tutegemee kunyanyapaliwa sana kwa watanzania watakaoomba kuja kusoma nje ya nchi. Wamesema hata Nigeria inayoaminika kwa ujanjaujanja hatujaifikia kabisa kwa rekodi hii. Wewe una maoni gani? Tujadili.