Maoni ya watu wa Kyela na Mbeya kwa ujumla kuhusu afya ya Dr Mwakyembe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni ya watu wa Kyela na Mbeya kwa ujumla kuhusu afya ya Dr Mwakyembe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hydrocephalus, Feb 22, 2012.

 1. H

  Hydrocephalus Member

  #1
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani, nimeguswa sana na hali aliyo nayo Mbunge wetu wa Kyela, Mh. Mwakyembe. Kusikitishwa huku hasa kunatokana na mazingira mazima yanayozunguka hali aliyonayo mbunge wetu huyu, ambaye zaidi ya ubunge bali ni mtanzania mzalendo ambaye siku zote ametetea si tu maslahi ya wana kyela bali maslahi ya uma kwa ujumla dhidi ya waporaji wakuu wa mali za nchi hii.

  Nimeanzisha uzi huu, ili wana kyela, tutoe mtazamo wetu wa ugonjwa wa mbunge wetu na jinsi serikali inavyolishughulikia suala hili. Na kisha tuweze kupata way forward ktk kujaribu kunusuru maisha ya mbunge wetu. Na pia tujiandae kama lolote linatokea ni kwa namna gani tutawaadhibu wale wote ambao mazingira na ushahidi mwingiene utaonesha kuwa wapo nyuma ya tatizo hili la mbunge wetu.

  Jamani huyu ni mbunge wetu, ni lazima tumuoneshe kuwa tunampenda na tunampigania kama ambavyo amekuwa akitupigania siku zote za yeye kuwa mbunge wetu.

  Tujowe awammweto, abando habha bhikolonda okotokinela. Tobaboneswe okote tokaja bando ba kokenelwa kwa namna hii.
   
 2. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,904
  Likes Received: 2,329
  Trophy Points: 280
  Inanikumbusha sakata la Aboud Jumbe Mwinyi na watu wa Kyela miaka ilee ya Mwalimu Nyerere
   
 3. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Wana Kyela waseme kama kweli bado wana imani na ccm inayotaka kumwua mbunge wao,watangaze rasmi kuachana na hayo majambazi wajiunge na wazalendo wenzao kukomboa taifa letu!
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Nyie Wanakyela mnampenda na Watanzania tunampenda lakini ccm haimpendi na ndo inamwangamiza, Mnachokatiwa ni kuiwajibisha ccm
   
 5. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mi hata sioni umuhimu wa ubunge wa huyu mnafiki. Kwa kweli wanakyela hawana cha kukukumbuka zaidi ya kukwonea huruma kibinadam. Umeshindwa kuturudishia maji yetu, mabomba yapo, umeshindwa kutawanya umeme vijijin, afya, shule, barabara da kwa kweli alipoachia kasyupa ndo had sasa. Tulikwambia ulipokuja kijijin kwetu uame ccm ukasema unaipenda sn. Mku najua we ni mbishi na mnafki sn ndo vinavokumaliza. Hatuna cha kumskitikia make kila kijiji anachoenda wanampiga mawe na vilevile analana za wazee akumbuke sku alipokusanya hela za kuludisha maji na kulala mbele nazo.
   
 6. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  tangazeni na kutohudhuria ibada ya kanisa ambalo el atakuja kuwarubuni na vidinari vichache kati ya nyingi walizotudhulumu. Ukisoma taarifa yake kwa jeshi la polisi mwaka jana kuna sehemu inamtaja fred kuhusika kwenye mpango wa kutaka kumuua.ukiunganisha dots atakuwa alitumwa na dingi yake. Hapo mtakuwa mmeonesha msimamo wa kupinga ufisadi.
   
 7. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Sioni ccm kushinda tena kyela.
  HUU NI MWISHO WA CCM KYELA.
   
 8. KirilOriginal

  KirilOriginal JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 1,920
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Mojawapo ya maeneo ambayo ni misukule ya ccm ni kusini, amkeni kataeni hili balaa ona sasa watu wenu mashujaa wanateketea na bado mnaichekelea ccm
   
 9. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,833
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Kwanza wewe Ndomyana hebu uwe na huruma, wabunge karibu wote ni staili hiyohiyo, hata wewe ndomyana ukipata ubunge utafanya hivyohivyo.

  Mhe Mwakyembe sasa hivi yuko katika kipindi kigumu, inaaminika kabisa kwa sisi great thinkers ugonjwa wake siyo god creation bali ni man made. Hivyo wahusika wa ugonjwa wake wameona mbali zaidi, siku chache zilizopita walipendekeza yaani NEC ya sisiemu ilishauliwa iiagize serikali yake kwamba pasipo kuvunja sheria wala katiba ifute chaguzi ndogo zisiwepo ila chama kitakacho poteza mbunge hicho hicho kipewe nafasi ya kuteuwa mbunge mwingine kwa utaratibu unaofaa. kwa sisi great thinkers tuliona utaratibu huu unalenga kukwepa sehemu ngumu kama huko Kyela kwa vyovyote likitokea la kutokea huko hakuendeki basi utumike utaratibu huo.

  Naomba kuwasilisha. ila Ndomyana umenibore kweli kweli.
   
 10. B

  BUBERWA D. JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  kwakweli hata mimi naungana na wewe kuonyesha masikitiko yangu kama binadamu. Ila anadhambi moja ya kuficha ukweli wa richmond. Ni wakati sasa atueleze ukweli wa riport ya richmond. Ashilikiane na mwenzake sitta wanao ukweli.
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Getwell soon Mwakyembe na uwasamehe waliokutenda maana mola atawapatiliza
   
 12. p

  panadol JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani tuchangie hoja vizuri,Mm huyu ni mbunge wangu,sioni sababu ya kuhusisha ugonjwa wa mbunge wangu Dr H Mwakyembe na CCM, yeye mwenyewe na wapiganaji wa Ufisadi wakina Sita hawajawahi kutuambia na kulitangazia taifa kuwa CCM ndiyo imemdhuru Dr H Mwakyembe waliomdhuru ni kikundi cha watu wachache ambao wao wanawaita mafisadi na wala si CCM jamani kama huna cha kuchangia kaa kimya usitake kupotosha watu kwa utashi wako wa kisiasa kyela ni jimbo la CCM damu damu kama wapinzani hamuamini njoeni tutawathibitishia kwa vitendo sisi huku huwa hatutaki mtu mwenye porojo!
   
 13. n

  nketi JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sisi wanakyela na wanambeya kwa ujumla hatutaki kuona kikaragosi chochote cha ccm huku kwetu. Ndio maana kila wakitia maguu na uongo wao tunawapopolea mawe. Wanambeya tunatangaza vita na ccm na wasije majimboni kwetu.
  Yaani kikwete lowasa na rostam mnaamua kumuua mwenzenu kwa kuwaanika kujianzishia kampuni hewa la richmond(richard from monduli)?
   
 14. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,928
  Likes Received: 1,461
  Trophy Points: 280
  Kwa vile ni Mbeya kwa ujumla wakati wa kujadili Mwandosya asisahaulike!CCM Is No longer in love with Mbeya jamani
   
 15. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Unamaanisha mkoa gani?Maana sijaona mkoa mwingine kama mbeya ambao unajua kudai haki
  na hauna unafiki.Watu wa mbeya wapo open.Hawataki kudanganywa,au kupewa ahadi hewa.
  Na kunako haki hawaogopi kuweka wazi kwa kiongozi yeyote yule.

  Ujumbe wa leo ni-Bye bye ccm mbeya.
   
 16. n

  nketi JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mirija ya ccm ni mingi sn ni mikubwa sn ni mirefu sn. Inafyonza raslimali za nchi km itakavyo. Serikali ya kifisadi kuanzia rais. Akijitokeza mpiganaji km mwakyembe dawa yake ni kumuua apotee ili ccm na wanaccm waendelee kutunyonya na kutufyonza. Wanambeya tunaandaa mirija binafsi ya kuifyonzelea mbali ccm
   
 17. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #17
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  nine ngwitika nkamu,.....Mwakyembe kama mbunge hajafanya lolote la maana kyela,..ila kama binadamu mwenzetu ni lazima tumuonee huruma....hivyo naunga mkono hoja zako mkuu,...nilikuwa huko/home mwaka jana....nilisononeka kuona mabomba yapo lakini maji hayatoki.
   
 18. only83

  only83 JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Too late..Mwambie atoke CCM,kujadili kwenu hakutakuwa na msaada kama hatatoka CCM,tena msije shangaa bado anaendelea kupewa sumu nyingine taratibu wakati ile ya kwanza bado haijatoka.
   
 19. m

  mlavie JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 298
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 60
  kwa heri CCM
   
 20. K

  KIMALIKE Member

  #20
  Feb 22, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani tumuombee uyu mtanzania mwenzetu kwani iyo sumu nasikia inaua taratibu,nimesikia watu wakisema mwakyembe saizi nikama mfa maji tu ambae aachi kutapatapa na izo juudi zake zakurudi india kwa matibabu ni bure, kwaiyo tumuombee jamani kwani akuna lisilo wezekana kwa mungu.
   
Loading...