Maoni ya Wapinzania/UKAWA kuhusu Bajeti 2016/17

Sophist

Platinum Member
Mar 26, 2009
4,486
3,407
Leo asubuhi katika kipindi cha Kumekucha, ITV alikuwepo Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo akijadili msimamo na mtazamo wa UKAWA kuhusiana ya Bajeti. Kubenea alijadili mtazamo wa UKAWA kuhusiana na kikao cha kesho cha Bunge la JMT litakapopokea majibu ya Serikali na kisha kukaa kama Kamati kupitisha ua kukataa bejeti husika.

Binafsi nimemsikiliza kwa makini na kisha kuwa na reservation juu ya namna ambavyo Upinzani Bungeni umejiruhusu kwenda chini kiasi hicho.

Naibu Spika Tulia ameonekana kuwa significant variable kwenye mipango na hoja za UKAWA kuhusiana na Bajeti ya 2016/17.

Total thinking ya Kubenea/UKAWA ni kuwa Bajeti mipango yote ya serikali itakwama. Kubenea ametoa ushahidi wa takwimu za Benki ya Dunia kuthibitisha madai yake kuwa mapapo ya ndani hayatazidi shilingi trilioni 12. Kwamba TRA itashindwa kukusanya kodi za pango na property tax. Kwamba mipango ya wali ya kuandaa mazingira ya kisera-uchumi kwa ajili ya kuanzisha viwanda itashindwa. Kubenea ametabiri viwanda vya juice tu kuwa ndivyo vinaweza kuanzishwa chini ya bajeti ya serikali 2016/17.

Huo ndio upinzani/UKAWA na hayo ndio mawazo yao kwenye bajeti ambayo, kwa imani yao, wangependa kuchangia kuiboresha iwapo Tulia Ackson asingeongoza Bunge kesho.

Akili ni nywele kila mtu ana zake. Toa mchango wako pia.
 
Hujamwelewa kuhusu viwanda, cha kukusaidia tu,soma bajeti ya wizara ya viwanda na bishara, ndio utaelewa alikuwa anamaanisha nini
 
Huu ni upunguwani wa hali ya juu. Kama kongea hivyo basi nimemdharau sana Kubenea. Utasemaje eti mapato ya ndani hayatazidi trilioni 12 wakati kwa mwaka huu pekee ni zaidi ya trilioni 17? Upuuzi mwingine mdanganyane huko huko Ufipa
 
Hapo ndipo UKAWA wanapokosea. Hivi unamtuma kweli kihiyo Kubenea kuwa msemaji kwenye masuala asiyo na uelewa nayo!
 
Huu ni upunguwani wa hali ya juu. Kama kongea hivyo basi nimemdharau sana Kubenea. Utasemaje eti mapato ya ndani hayatazidi trilioni 12 wakati kwa mwaka huu pekee ni zaidi ya trilioni 17? Upuuzi mwingine mdanganyane huko huko Ufipa
lete budget ya wizara viwanda na biashara kwa mwaka huu wa fedha
 
Hivi viwanda..
Vitabakia kua fantasy ya hii serkali na wapiga vielegele wake..
 
Hujamwelewa kuhusu viwanda, cha kukusaidia tu,soma bajeti ya wizara ya viwanda na bishara, ndio utaelewa alikuwa anamaanisha nini
Ninafahamu kuwa mwaka 2016/17 Wizara ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji imekadiria katika bajeti yake kutumia kiasi cha fedha kisichozidi shilingi bilioni 81.8; 41.8 (51 %mishahara na o/c):40 (49% maendeleo). Nafahamu pia kuwa hii siyo bajeti ya kuanzisha viwanda ila kuandaa mazingira ki-sera (uchumi) kwa ajili ya kurahisisha na kuhudumia uwekezaji katika viwanda. Aidha, ninajua kuwa serikali ata-mobilise local and foreign private and public sectors kuwekeza katika viwanda (hususan manufacturing industry). Sasa unaweza kuendeleza hoja yako.
 
Sijamsikia Kubenea hoja zake kuhusu bajeti ya 2016/17. Kwa machache yaliyojadiliwa humu, hakika tunahitaji kuwa makini katika kutetea au kupinga hoja.

Niseme tu, kitendo cha Wabunge wa upinzani kususia mijadala ya bajeti na kusemea nje ya Bunge siyo tu ni unafiki bali ni utoto. Na mtoto akililia wembe mpe.
 
Back
Top Bottom