Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,549
Ndugu wanajukwaa nami kama wakili msomi ninaomba ku-share nanyi kwa uzoefu wangu wa kesi mbali mbali nilizowahi kuzisimamia huko Tz na mifano ya rejea katika kufundisha kwangu somo sheria huku ugenini. Kiufupi kumfunga mtu kwa tukio ambalo hajalifanya ni ngumu sana hata kama umemkamata na nyenzo za kufanya tukio. Mbaya zaidi kama hana records zozote za kufanya matukio ya namna hiyo, hapa hamna kesi zaidi ya ubishani wa kisheria na uelewa wake.
Huwezi kunikuta nimesimama na Mtoto wako wa kike ukasema kuwa nilikuwa nataka kumbaka hata kama yeye amepiga kelele na akakiri kuwa nimembaka. Hapa ni lazima kwanza twende hospitali muda huo huo na daktari aandike muda aliobakwa mtoto na aoneshe kuwa kuna mbegu za kiume zimebakia kule sehemu za siri. Lakini tu huwezi kusema eti nilidhamiria kumbaka mtoto wako wakati sijambaka, ushahidi wa dhamira utathibitishwa na nani nisipokiri mimi mhusika?
Huwezi kusema fulani alidhamiria kulipua vituo vya mafuta wakati hajalipua na hakuna ushahidi wa dhamira hiyo, mbaya zaidi hujamkuta na vilipuzi. Ngumu sana na haiingii akilini kusema kuwa fulani alipanga kumpulizia fulani spray ya sumu wakati hajapuliza na wala hiyo Spray hana unaishia kusema alipanga kwenda kununua Spray hiyo, alinunua? Huwezi kusema watu walipanga kukata miti na kuiweka barabarani kisha kuitisha maandamano wakati hawakufanya tukio hilo,hata kama ungewakuta na mapanga lakini hawajakata miti, ulijuaje kama dhamira yao ni kukata miti?
Ingekua tukio limefanyika una uthibitisho upo wa tukio lenyewe kufanyika halafu akashukiwa mtu kisha akachunguzwa na kumkuta na nyenzo za kufanyia tukio kama ushahidi, hapa ni rahisi sana kumtia hatiani. Ndiyo maana imekuwa rahisi sana kwa Sabaya kufungwa maana alifanya matukio na ushahidi kuwa alikuwa anavamia maduka ya watu upo mpaka kwenye CCTV Cameras zinaonyesha. Watu wakisema kesi ya Mbowe na Sabaya ni tofauti ni kwenye matukio yenyewe.
Kwahiyo kwenye kesi hii ya Mbowe ni ubishani tu wa kisheria na kuonyesha nani ni fundi sana wa kuhoji maswali na nani fundi sana wa kubadili dhana au uongo kuwa kweli. Sioni misingi ya haki ya kimahakama kwenye hili. Labda iamuliwe kwa amri tu.