Maoni ya Wakili: Kumfunga mtu kwa kitu ambacho hakifanyi ni gumu sana, labda kwa amri

Hardbody

JF-Expert Member
Jan 25, 2017
2,651
2,000
Uliyoyasema yote kwa tz hii yanawezekana kabisa mkuu. Kuna inavyotakiwa kuwa na ilivyo mkuu
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
8,864
2,000
Inawezekana lengo sio kumfunga bali kumuondoa uraiani muda mrefu kadri iwezekanavyo.
Ndio kifungo chenyewe hicho, hata asipokutwa na hatia kwa muda aliokaa gedezani ni sawa na kutumikia kifungo cha muda mfupi.

Hii kesi inaonesha kuna haja ya kufanyia reforms sheria zetu ili kuwapa haki watuhumiwa wanaoshikiliwa kwa makosa yasiyo na dhamana, kama wakithibitika hawana hatia mzigo wa lawama (fidia) waubebe jamhuri.
 

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
309
1,000
Ndugu kwa upande wangu mimi nakubali umefafanua vyema sana na niseme tu wanasheria ni watu wagumu sana kuwaelewa maana mara nyingi sana mnagusa mahala kwa kutumia weledi mkubwa kuepusha madhara kwa wengine, basi itoshe kusema Mungu awape hekima na busara viongozi wetu wasione vyama vya upinzani kuwa ni dhambi na niwatu wakushinda mahakamani na selo tu.
Asante sana Bwashee, tutaendelea kutumia taaluma zetu kuusema ukweli. Hatukuona kunyamazia uongo
 

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
309
1,000
Kwa Tanzania kesi za aina hiyo huanfikiwa hukumu Ikulu na jaji kwa vile ni mteule wa Rais kazi yake ni kudurufu yaliyo andikwa tuu. Tanzania kwa sasa hamna mahakama wala bunge.
Ni kujitafutia laana za bure kwa mwenyezi Mungu. Kama wewe ni Jaji halafu ukatumia nafasi yako kuumiza wengine wakati ukweli unaujua, pasina shaka wewe adhabu ya Mungu iko juu yako .Siyo kila mtu anaweza kua jaji
 

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,199
2,000
Serikali chini ya Chama changu CCM hii kesi isimamiwe kwa haki ya Mungu. Kama itajulikana inalitia taifa hasara basi wahusika wawajibishwe. Huu ushahidi unatupa wasi wasi na kuwachanganya mawakili Jamhuri
 

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
7,429
2,000
Ni kujitafutia laana za bure kwa mwenyezi Mungu. Kama wewe ni Jaji halafu ukatumia nafasi yako kuumiza wengine wakati ukweli unaujua, pasina shaka wewe adhabu ya Mungu iko juu yako .Siyo kila mtu anaweza kua jaji
Ina tia ikakasi sana. Yaani uki wasikiliza mashahidi ya Jamhuri kwenye kesi ya Mbowe na wenzake, kama kweli ni Jaji anae simamia sheria, hii kesi ingekuwa imesha futwa. Yuko wapi Jaji Nyalali, yuko wapi Jaji Kipenka? Yuko wapi Jaji Kisanga? Mungu wa Mbinguni awape pumziko jema wale walio itendea mahakama haki. Hawa majaji wa tumboni Mungu awaandalie adhabu iliyo kuu.
 

Langlang

Member
Jul 29, 2021
53
125
Kwa Tanzania kesi za aina hiyo huanfikiwa hukumu Ikulu na jaji kwa vile ni mteule wa Rais kazi yake ni kudurufu yaliyo andikwa tuu. Tanzania kwa sasa hamna mahakama wala bunge.
Hapo ndo umuhimu wa katiba mpya ulipo. Spika anajitahidi asimuudhi Mkt wake, Jaji Mkuu ateuliwe na Mkt wa chama chake, na maviongozi chungu nzima wa Mahakama watoke hukohuko... dah!
Mifano alotoa Prof ni rahisi kufundishia hata level ya chini kuhusu umuhimu wa ukweli ktk kutoa ushahidi.
Taratiibu naona wakimkomaza Mbowe ktk kudai haki za wanaoitwa kwa kejeli "wanyonge". Nionavyo mm, kesi hii itaongeza ladha ktk kuimarisha upinzani. Bila kujitambua wanaujenga upinzani, ni suala la muda - tuwe wastahimilivu, tutaona mengi na huenda kuna watakaojutia haya yanayoendelea. Mungu ni Mkuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom