Maoni ya Viongozi wa Upinzani baada ya TAKUKURU kutupilia mbali tuhuma za rushwa za RC Mnyeti! Yapo ya Lema na Nassari

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
“Niliwapa takukuru kila aina ya ushahidi walioutaka”
niliwapa takukuru mpaka moja ya kifaa nilichotumia kurekodi baadhi ya vikao vya ununuzi na ushawishi wa rushwa.
Na wakasema wana teknolojia ya hali ya juu ku-retrieve kazi zote, muda na wakati ambapo video hizo zilichukuliwa, bila kukosea. Teknolojia ambayo mimi pia ninayo.
Cha ajabu hawajaona UHALISIA au UONGO uliopo kwenye ushahidi, badala yake wameona siasa.
Ni kweli ilikuwa lazima waone siasa kwa sababu hata ununuzi wenyewe ulikuwa ni rushwa ya ki-mfumo (systemic corruption ).
Na aina hii ya rushwa ni mbaya sana kama itaachwa ikasambaa kwenye mfumo mzima wa Siasa za nchi.

Mb Joshua Nassari
Jimbo la Arumeru Mashariki

18-12-2017
--
Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche (CHADEMA) amedai kwamba Serikali ya CCM haijawahi kupingana na rushwa kwani rushwa zote zinazofanyika zimeasisiwa na Chama Cha Mapinduzi

Heche amefunguka hayo baada ya TAKUKURU kutupilia mbali ushahidi wa 'video clip' iliyowasilishwa ofisini kwao na Wabunge wa CHADEMA, Joshua Nassari wa Arumeru Mashariki pamoja na Godbless Lema wa Arusha Mjini uliokuwa ukidaiwa kuonyesha madiwani wakipokea rushwa kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wa Arumeru.

Rejea hapa; TAKUKURU yautupilia mbali ushahidi ulioletwa na Nassari na Lema wa madiwani kuhongwa

Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa twitter John Heche ameandika kuwa;

"Serikali ya ccm haijawahi kupiga vita rushwa na haiwezi kwasababu rushwa zote katika nchi hii zimeasisiwa na zinatokana na ccm, kinachofanyika sasa ni vita dhidi ya watu wasiotakiwa na mfumo, ndio maana hata Escrow waliokamatwa ni wawili lakini bunge lilitaja wengi" .

Takukuru jana walisema kwamba sababu za kutupilia mbali ushahidi wa Wabunge hao ni kutokana na kuharibu ushahidi kwa kuingiza siasa.

heche.PNG

Naye Mbunge wa Arusha Mjini kwa kutumia mtatandao huo huo wa kijamii wa twitter ameandika kuwa;

"Kuna vitu ambayo Mume hawezi kumfanyia au kumsaidia mke wake hata kama anampenda kwa dhati sana ,kwa mfano kubeba mimba. Ndivyo ambavyo ni dhahiri kwa Takukuru kuhusu suala la Madiwani walionunuliwa."

Pia ameongeza kuwa "Nitaongea na vyombo vya habari kesho"

lema.PNG

Joshua Nassari nae kupitia Ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook ameandika haya:

“Niliwapa takukuru kila aina ya ushahidi walioutaka”
niliwapa takukuru mpaka moja ya kifaa nilichotumia kurekodi baadhi ya vikao vya ununuzi na ushawishi wa rushwa. Na wakasema wana teknolojia ya hali ya juu ku-retrieve kazi zote, muda na wakati ambapo video hizo zilichukuliwa, bila kukosea. Teknolojia ambayo mimi pia ninayo.
Cha ajabu hawajaona UHALISIA au UONGO uliopo kwenye ushahidi, badala yake wameona siasa. ni kweli ilikuwa lazima waone siasa kwa sababu hata ununuzi wenyewe ulikuwa ni rushwa ya ki-mfumo (systemic corruption ). Na aina hii ya rushwa ni mbaya sana kama itaachwa ikasambaa kwenye mfumo mzima wa Siasa za nchi.

nassari.PNG
 
Kitendo cha Takukuru tena Makao makuu chini ya Mkuu wao Mlowola wamediriki kutoa sababu za kitoto hivi kuhalalisha rushwa? Eti siasa iliingizwa kwani kwanini Takukuru walimkata Sadifa wakati pesa alizotoa sadifa zilihusu jambo la kisiasa?Mara nyingine kuliko kudhalilika hivi bora kukaa kimya...Eti ndio huyu alisema alitaka kuwa Padre???
 
Takukuru Mungu anawaona eti. Mnatudanganya mchana kweupee. Tulijua tu kesi ya nyani unapeleka kwa tumbiri. Eti nyani kala mahindi
 
Anaandika Mbunge wa Jimbo Arumeru Mashariki Joshua Nassari.
“Niliwapa takukuru kila aina ya ushahidi walioutaka”
niliwapa takukuru mpaka moja ya kifaa nilichotumia kurekodi baadhi ya vikao vya ununuzi na ushawishi wa rushwa. Na wakasema wana teknolojia ya hali ya juu ku-retrieve kazi zote, muda na wakati ambapo video hizo zilichukuliwa, bila kukosea. Teknolojia ambayo mimi pia ninayo.
Cha ajabu hawajaona UHALISIA au UONGO uliopo kwenye ushahidi, badala yake wameona siasa. ni kweli ilikuwa lazima waone siasa kwa sababu hata ununuzi wenyewe ulikuwa ni rushwa ya ki-mfumo (systemic corruption ). Na aina hii ya rushwa ni mbaya sana kama itaachwa ikasambaa kwenye mfumo mzima wa Siasa za nchi.
FB_IMG_1513600618962.jpg
 
Kuna mtu alietegemea kesi kweli? Kwan wao hawana akili? Ulitaka watumbuliw kama yule waziri kijana?
 
Back
Top Bottom