Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
prof mkenda.jpg

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda

Akizungumza na waandishi wa habari tarehe 9/5/2023, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 toleo la 2023 pamoja na Rasimu ya Mitaala Mipya ya Elimu ya Msingi, Sekondari na Vyo vya Ualimu zimekamilika, na sasa serikali imetoa rasimu hizo hadharani ili kupata maoni ya mwisho, na maoni hayo yawe yameshapokelewa kufikia tarehe 31/5/2023.

Akaongeza kuwa tarehe tarehe 10/5/2023 Wizara itafanya Semina na Wabunge kuwapitisha katika Rasimu hizo na tarehe 12/5/2023 mpaka 14/5/2023 kutakuwa na Kongamano Kubwa la Kitaifa la kujadili Rasimu hizo.

Rasimu hizo zinapatikanakatika Tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, lakini pia katika tovuti ya Idara ya Habari na Maelezo pamoja na tovuti ya Taasisi ya Elimu Tanzania.

Kwa maelezo zaidi unaweza kusoma kimbatisho hapo chini.

Screenshot 2023-05-10 at 12.05.40.png
Screenshot 2023-05-10 at 12.06.00.png
Screenshot 2023-05-10 at 12.06.18.png

Screenshot 2023-05-10 at 12.06.35.png

Screenshot 2023-05-10 at 12.07.50.png

Screenshot 2023-05-10 at 12.08.07.png
Screenshot 2023-05-10 at 12.08.17.png
 
Attachments

  • RASIMU_YA_MITAALA_YA_ELIMU_YA_AWALI,_MSINGI,_SEKONDARI_NA_UALIMU.pdf
    1.7 MB · Views: 31
  • SERA- Elimu na Mafunzo.pdf
    1.4 MB · Views: 26
Katika rasimu hizo, umri wa kuanza darasa la kwanza umepunguzwa, muda wa elimu ya lazima umeongezeka huku masomo mapya ya lugha, Tehama na stadi za maisha yakizingatiwa ili kuendana na mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kisayansi na kiteknolojia.

Mapendekezo ya rasimu hizo yalitolewa jana na wizara hiyo kwa umma kupitia Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda.

Inapendekezwa kuwa kwenye sera hiyo umri wa kuanza darasa la kwanza umepunguzwa kutoka miaka saba hadi sita, kama ilivyo katika nchi nyingi duniani huku muundo uliorekebishwa ukiruhusu mwanafunzi kukamilisha mzunguko wa masomo kwa muda mfupi zaidi.

Muundo katika mfumo rasmi wa elimu na mafunzo utakuwa 1+6+4+2/3+3+, kwa maana ya mwaka mmoja wa elimu ya awali, miaka sita ya elimu ya msingi, miaka minne ya elimu ya sekondari ngazi ya chini, miaka miwili ya elimu ya sekondari ngazi ya juu au miaka mitatu ya amali sanifu na miaka isiyopungua mitatu ya elimu ya juu.

Vilevile, elimu ya lazima itajumuisha elimu ya msingi na elimu ya sekondari ngazi ya chini na itatolewa kwa miaka 10. Lakini kila mtoto mwenye umri wa miaka sita na ambaye amepata au hakupata elimu ya awali kwa mujibu wa sheria, apatiwe elimu ya lazima itakayotolewa kwa muda wa miaka 10 ili kumwezesha mwanafunzi kumudu stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu, kuwa na ufahamu wa jumla na pia kupata umahiri ikiwamo maarifa na ujuzi kulingana na matakwa ya ngazi hiyo.

Pia, elimu ya awali itakuwa ya mwaka mmoja kwa watoto wenye umri wa miaka mitano kwa kuzingatia mahitaji yao, mazingira na hali halisi ya upatikanaji wa rasilimali nchini.

Serikali itaweka utaratibu wa kuhakikisha kuwa muda wa kukamilisha elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali unalenga mwanafunzi kupata ujuzi na maarifa stahiki kwa kuzingatia mfumo wa tuzo wa taifa huku elimu ya msingi na sekondari katika mfumo wa umma ikitolewa bila ada.

Kadhalika, sera hiyo inalenga kuweka mazingira wezeshi ya kuongeza ushiriki wa wasichana katika elimu ya amali na elimu ya juu hususan katika fani za sayansi, Hisabati na teknolojia.

Kuhusu matumizi ya lugha, serikali itahakikisha kuwa lugha za Kiswahili, Kiingereza na nyingine za kigeni zinafundishwa kwa ufasaha na ufanisi, lugha ya alama ya Tanzania na maandishi ya Breli zitatumika ngazi zote za elimu na mafunzo.

LUGHA YA KUFUNDISHIA

Lugha ya Taifa ya Kiswahili itatumika kufundishia katika elimu ya awali na elimu ya msingi, isipokuwa masomo ya lugha za kigeni na katika shule zitakazoomba kutumia lugha ya Kiingereza kufundishia.

Lugha ya Kiingereza itatumika kufundishia kuanzia ngazi ya sekondari ya chini, isipokuwa somo la Kiswahili, masomo ya lugha za kigeni na katika shule za sekondari na vyuo vitakavyoruhusiwa kutumia lugha ya Kiswahili kufundishia.

Lugha ya Taifa ya Kiswahili itatumika kufundishia somo la Historia ya Tanzania na Maadili ili kujenga na kuendeleza mila, desturi na utamaduni wa Mtanzania katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

YALIYOMO

Maeneo ya ujifunzaji yamejikita katika utamaduni, elimu ya imani, sanaa na michezo, lugha ya mawasiliano, rejea maeneo ya ujifunzaji, stadi za awali za maisha, afya na mazingira.

Mapendelezo ya mitaala kwa darasa la kwanza na la pili, masomo ni kusoma, kuandika, Demonstrate Mastery of Basic English Language Skills, Hesabu, kuthamini utamaduni, sanaa na michezo, kutunza afya na mazingira.

Masomo kwa darasa la tatu hadi la sita ni Kiswahili, English, Kifaransa, Kichina, Kiarabu, Hisabati, Historia ya Tanzania na Maadili, Elimu ya Dini, Sanaa na Michezo, Sayansi na Jiografia na Mazingira.

Kwa elimu ya sekondari hatua ya chini masomo ni Historia ya Tanzania na Maadili, Historia, Jiografia, English, Literature in English, Kiswahili, Kiarabu, Kichina, Kifaransa, Michezo, Baiolojia, Kemia, Fizikia, Kilimo, Hisabati, Additional Mathematics, Sayansi ya Kompyuta na Utunzaji wa Taarifa za Fedha (Book Keeping).

Pia masomo ya Elimu ya Biashara (Business Studies), Ushoni (Textiles and Garment Construction), Sanaa Sanifu (Fine Art), Muziki (Music), Sanaa za Maonesho (Theatre Arts), Maarifa ya Nyumbani (Home Management), Chakula na Lishe (Food and Nutrition), Elimu ya Dini ya Kikristo (Bible Knowledge), Elimu ya Dini ya Kiislamu na Fasihi ya Kiswahili.

Kwa upande wa umahiri mkuu na umahiri mahususi, elimu ya sekondari hatua ya juu ni Historia, Jiografia, Elimu ya Dini ya Kikristo (Divinity), Elimu ya Dini ya Kiislamu, Kiswahili, English, Kiarabu, Kifaransa, Kichina, Fizikia, Kemia, Baiolojia, Chakula na Lishe, Sayansi ya Kompyuta, Hisabati, Hisabati Tumizi (Basic Applied Mathematics).

Pia masomo ya Kilimo, Historia ya Tanzania na Maadili, Michezo, Sanaa Sanifu, Muziki, Sanaa za Maonesho, Ushoni, Mawasiliano ya Kitaaluma, Elimu ya Biashara, Uhasibu, Uchumi, Fasihi ya Kiswahili na Literature in English.

Kwa upande wa masomo, umahiri mkuu na umahiri mahususi-Stashahada ya Ualimu na Stashahada ya Ualimu (Elimu Maalum), Elimu ya Awali na Astashahada ya Elimu ya Ukufunzi wa Karakana/Maabara ni Misingi ya Kinadharia, Mbinu za Ufundishaji, Ualimu kwa Vitendo, Masomo ya Jumla, Lugha na Mawasiliano.

Akizungumza na waandishi jijini hapa, Prof. Mkenda alisema serikali imeamua kutoa rasimu hizo ili kupata maoni na mwisho wa kuyapokewa ni Mei 31, 2023. Baada ya hapo rasimu hizo zitapelekwa katika ngazi za uamuzi mwezi ujao.

Waziri Mkenda alisema kuwa leo wizara itafanya semina kwa wabunge kuwapitisha katika rasimu hizo na Mei 12 hadi 14 kutafanyika kongamano kubwa la kitaifa jijini Dodoma la kuzijadili.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, alisema kongamano hilo ni la kimataifa na wamewashirikisha Watanzania wanaoishi nje ya nchi ili kutoa maoni yao na uzoefu wao katika nchi wanazoishi.
 
Attachments

  • rasimu_ya_mitaala_ya_elimu_ya_awali_msingi_sekondari_na_ualimu.pdf
    1.7 MB · Views: 13
Elimu ya msingi hadi sekondari kuwepo soma la Madini, uvuvi , kama walivyoweka kilimo.
2. Rasimu ionyeshe combinations kwamasomo ya kidato cha tano na sita ili vyuo vikuu vianze kufuta kozi za hovyo walizonazo.
3. Somo la sayansi kwa elimu msingi ni somo jipya au lipo kwa sasa linafundishwa?
4. Somo la kiarabu na kifaransa yafutwe kwa elimu msingi.
 
Masomo ya dini yafundishwe kwenye nyumba za dini,huu upuuzi wakuingiza masomo ya dini kwenye mitaala ya elimu ni kupotezeana muda.

Sijaona somo la elimu kwa mlipa kodi

Sanaa ,michezo na utamaduni waanze kufundisha tangua awali

Muda wa masomo uwe sa3 asbh
 
Masomo machache yaliyopo tayari yamewalemea wanafunzi. Kuongeza masomo ya kipuuzi kama kichina, kifaransa, kiarabu, muziki na michezo ni kuwaongezea wanafunzi mzigo usiokuwa wa lazima na kusababisha ufaulu uendelee kushuka. Sijawahi kuona rasimu ya elimu ya ovyo kama hii tangu nchi hii ipate uhuru.
 
Masomo ya dini yafundishwe kwenye nyumba za dini,huu upuuzi wakuingiza masomo ya dini kwenye mitaala ya elimu ni kupotezeana muda.

Sijaona somo la elimu kwa mlipa kodi

Sanaa ,michezo na utamaduni waanze kufundisha tangua awali

Muda wa masomo uwe sa3 asbh
Unataka somo la elimu kwa mlipakodi hiyo elimu ya kuipata hiyo pesa ya kulipia kodi umeiona hapo?
 
View attachment 2616490
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda

Akizungumza na waandishi wa habari tarehe 9/5/2023, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 toleo la 2023 pamoja na Rasimu ya Mitaala Mipya ya Elimu ya Msingi, Sekondari na Vyo vya Ualimu zimekamilika, na sasa serikali imetoa rasimu hizo hadharani ili kupata maoni ya mwisho, na maoni hayo yawe yameshapokelewa kufikia tarehe 31/5/2023.

Akaongeza kuwa tarehe tarehe 10/5/2023 Wizara itafanya Semina na Wabunge kuwapitisha katika Rasimu hizo na tarehe 12/5/2023 mpaka 14/5/2023 kutakuwa na Kongamano Kubwa la Kitaifa la kujadili Rasimu hizo.

Rasimu hizo zinapatikanakatika Tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, lakini pia katika tovuti ya Idara ya Habari na Maelezo pamoja na tovuti ya Taasisi ya Elimu Tanzania.

Kwa maelezo zaidi unaweza kusoma kimbatisho hapo chini.

View attachment 2616524View attachment 2616525View attachment 2616527
View attachment 2616528
View attachment 2616529
View attachment 2616530View attachment 2616531
Hii tabia ya kung'ang'ania SoMo la historia Kwa ngazi zote ni useless na historia yenyewe ndio hiyo ya kina Manka Musa sijui wa Mali empires na upuuzi kama huo..

Badala ya kulazimisha historia all the way tuweke mda mwingi kwenye Masomo ya ujuzi..

Unaweka historia advance ya nini? Historia iishie form 4
 
Hapa cha msingi Ni masomo ya stad za kazi pamoja na kiingereza na hesabu. Yaan mtoto anamaliza la7 anasimamisha ghorofa, anajua shuguli yote ya kuchimba madini anajua Mambo ya medical kwa hio kuanzia Form one yeye anacheza na kombi yake tu mpaka anaingia chuo haya Mambo ya lundo la masomo yasio na maaana tuachane nayo tutafute professionalism mapema kwa mtoto kumuepusha kufanya vitu ambavyo hapendi matokeo yake alipewa position serikalini anaharibu kumbe sio sehem yake

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
View attachment 2616490
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda

Akizungumza na waandishi wa habari tarehe 9/5/2023, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 toleo la 2023 pamoja na Rasimu ya Mitaala Mipya ya Elimu ya Msingi, Sekondari na Vyo vya Ualimu zimekamilika, na sasa serikali imetoa rasimu hizo hadharani ili kupata maoni ya mwisho, na maoni hayo yawe yameshapokelewa kufikia tarehe 31/5/2023.

Akaongeza kuwa tarehe tarehe 10/5/2023 Wizara itafanya Semina na Wabunge kuwapitisha katika Rasimu hizo na tarehe 12/5/2023 mpaka 14/5/2023 kutakuwa na Kongamano Kubwa la Kitaifa la kujadili Rasimu hizo.

Rasimu hizo zinapatikanakatika Tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, lakini pia katika tovuti ya Idara ya Habari na Maelezo pamoja na tovuti ya Taasisi ya Elimu Tanzania.

Kwa maelezo zaidi unaweza kusoma kimbatisho hapo chini.

View attachment 2616524View attachment 2616525View attachment 2616527
View attachment 2616528
View attachment 2616529
View attachment 2616530View attachment 2616531
Haya
 
Back
Top Bottom