mchemsho
JF-Expert Member
- Jun 8, 2011
- 3,212
- 867
Leo nipata Neema ya kudhuria semina ya mwalimu Christopher Mwakasege inayoendelea viwanja vya biafra kinondoni jijini Dsm, kipekee ilikuwa semina yenye Baraka na inayoashiria mwanzo Mpya wa Maisha ya Kiroho na Mahusiano Bwana Mungu. Kichwa cha somo ni namna ya kuombea maisha yako ya baadae ili yawe mazuri. Ninachotaka ku-share nanyi ni sehemu ndogo ya hotuba yake juu ya baraka ambazo mtu anaweza kupata au taifa. Akatoa mfano kuwa mwaka 2001 alitembelewa na wageni wazungu kutoka ulaya ambapo walimwelezea furaha yao kwamba nchi zao zimekubali kuongeza misaada kwa tanzania katika sekta tofauti ikiwemo afya na elimu, Wazungu hao huku wakitegemea kwamba mwalimu Mwakasege angefurahi na kuwashukuru, badala yake aliwacharukia na kuonyesha kukerwa kwake na hiyo misaada ya wazungu, aliwauliza ,hivi mnafahamu kama nchi hii imepata uhuru zaidi ya miaka 40, ni sawa kuendelea kuitwa taifa changa?? Akaendelea kusema hivi ni nani ambae anazaa mtoto anafikisha miaka zaidi ya 40 na bado akaendelea kumhudumia?? Kama yupo basi lazima aitwe kwenye vikao vya familia na ahojiwe shida nini..akahoji kwanini kipimo cha umri kiwe na maana katika social perspective lakini isilete maana kwenye umri wa nchi?? Mwisho akawaambia wale wageni wazungu waliokuwa ofisin kwake kuwa kama wanazipenda nchi masikini wangezipeleka huko wao wanapochota mali ili na waafrika wakachote wao wenyewe ili wasiwe watu wakukaa tu na kusubiri misaada. MBARIKIWE NYOTE.