Maoni ya mtumishi wa Mungu mwl. Mwakasege kuhusu miaka 50 ya uhuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni ya mtumishi wa Mungu mwl. Mwakasege kuhusu miaka 50 ya uhuru

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mchemsho, Sep 9, 2011.

 1. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Leo nipata Neema ya kudhuria semina ya mwalimu Christopher Mwakasege inayoendelea viwanja vya biafra kinondoni jijini Dsm, kipekee ilikuwa semina yenye Baraka na inayoashiria mwanzo Mpya wa Maisha ya Kiroho na Mahusiano Bwana Mungu. Kichwa cha somo ni namna ya kuombea maisha yako ya baadae ili yawe mazuri. Ninachotaka ku-share nanyi ni sehemu ndogo ya hotuba yake juu ya baraka ambazo mtu anaweza kupata au taifa. Akatoa mfano kuwa mwaka 2001 alitembelewa na wageni wazungu kutoka ulaya ambapo walimwelezea furaha yao kwamba nchi zao zimekubali kuongeza misaada kwa tanzania katika sekta tofauti ikiwemo afya na elimu, Wazungu hao huku wakitegemea kwamba mwalimu Mwakasege angefurahi na kuwashukuru, badala yake aliwacharukia na kuonyesha kukerwa kwake na hiyo misaada ya wazungu, aliwauliza ,hivi mnafahamu kama nchi hii imepata uhuru zaidi ya miaka 40, ni sawa kuendelea kuitwa taifa changa?? Akaendelea kusema hivi ni nani ambae anazaa mtoto anafikisha miaka zaidi ya 40 na bado akaendelea kumhudumia?? Kama yupo basi lazima aitwe kwenye vikao vya familia na ahojiwe shida nini..akahoji kwanini kipimo cha umri kiwe na maana katika social perspective lakini isilete maana kwenye umri wa nchi?? Mwisho akawaambia wale wageni wazungu waliokuwa ofisin kwake kuwa kama wanazipenda nchi masikini wangezipeleka huko wao wanapochota mali ili na waafrika wakachote wao wenyewe ili wasiwe watu wakukaa tu na kusubiri misaada. MBARIKIWE NYOTE.
   
 2. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,231
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  hii kali, aje humu jf tulonge naye...anaweza akawa na mchango mkubwa sana...
   
 3. howard

  howard Senior Member

  #3
  Sep 9, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Imekaa vizuri hii argument ya mtumishi
   
 4. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,219
  Trophy Points: 280
  Kwani mali zinachotwa wapi?NI AFRICA of coz,sasa wazungu wakawaonyeshe wakati kwenu ndo zapatikana?
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,251
  Trophy Points: 280
  Nendeni mkutanoni Biafra, mtajifunza mengi sana
   
 6. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu, nilikuwepo pia tangu J3, uwa sipendi kukosa semina za huyu Mwalimu anapokuwa Dar au nikimkuta mji wowote, alinigusa sana alipozungumzia topic hiyo ni kama alikuwa anatuma ujumbe kwa wahusika kuwa Tanzania ni mtu mzima sasa tena anaelekea uzeeni hivyo si sahihi kuendelea kuwa tegemezi la misaada toka kwa wakoloni mamboleo.
   
 7. K

  Kalila JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2011
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli mwalimu menigusa sana na masomo yake tanzania ina miaka 50 now inabidi ijitegemee yenyewe mwalimu mwakasege anafundisha maisha pia amenigusa aliposema kuwa tusibishane kuhusu dini ztu bali wote tuhimizane kumtolea mungu sadaka na pia hata kama ni mlutheran unaweza kuwasaidia makanisa mengine kama ukiguswa lakini sio mitume na manabiii wanahubiri juu ya makanisa yao tu
   
 8. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,219
  Trophy Points: 280
  Mwaka jana kuhusu MZALIWA WA KWANZA nilihudhuria.This time nimekosa,hope mwakani nitahudhuria.Endeleeni kutujuza
   
 9. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nilikuwepo nimemsikia akashangaa pia watu wanaobishania mungu anasema kama unataka mungu wako aonekane toa sadaka !kuhusu swala la nchi inamiaka hamsini lakini bado omba omba kila mtu alisikitika!ukifikiria mku wa nchi anasema asipoomba nje uchumi hauendi!
   
Loading...