Maoni ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu Katiba mpya yawe chachu kwa Taasisi nyingine

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,491
40,999
Sote hivi karibuni tumeshuhudia msajili wa vyama vya siasa, Jaji Mutungi, kwa kupitia Kamati yake iliyoiunda, akiwakilisha maoni ya taasisi anayoiongoza, kuhusiana na katiba mpya.

Nasema ni maoni ya taasisi yake, kwa sababu sote tunajua kuwa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, siyo taasisi inayojishughulisha na masuala ya katiba, bali inatakiwa kufanya kazi kwa mujibu wa katiba. Hata hivyo, kama ilivyo kwa wananchi wote na taasisi zote, ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ni mdau wa katiba. Hivyo ofisi ya msajili wa vyama vya siasa inayo haki kuwasilisha maoni yake. Na maoni hayo ni maoni tu, hayamfungi yeyote kulazimika kukubaliana nayo.

Sasa, maadamu Rais Samia ameonekana kufungua milango, na kuwa tayari kupokea maoni ya wadau mbalimbali kuhusiana na upatikanaji wa katiba mpya, basi tukio lile la Rais kukabidhiwa maoni ya ofisi ya msajili wa vyama vya siada liwe ni hamasisho kubwa la taasisi nyingine mbalimbali, jazo kuwasilisha maoni yao kwa Rais. Na ofisi ya Rais inaweza kuweka utaratibu wa kuratibu maoni mbalimbali ili tuingie kwenye mchakato wa kupata katiba mpya, mara moja.

Napenda kuzihamasisha taasisi mbalimbali kuwasilisha maoni yao juu ya namna ya kukamilisha utaratibu wa kupata katiba mpya. Kumbukeni katiba ni yetu sote, hakuna mwenye haki zaidi kuliko mwingine. Watakaohusika hili wafanye kazi ya kuratibu tu, lakini maamuzi ni lazima, yawe ya kwetu sisi wananchi. Taasisi zifuatazo, ingieni kazini mara moja, Rais amefungua mlango:

Asasi za kirai
Vya vya siasa
Madhehebu ya dini
Vyama vya kitaaluma
Vyama vya wakulima na wafugaji
Vyama vya wafanyakazi
Vyama vya wanazuoni
Vya vya waajiri
Vikundi vya ujasiriamali
N.k. n.k.

Tunamwomba Rais, kama alivyofurahia na kuwa tayari kupokea maoni ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, afanye hivyo hivyo na kwa taasisi nyingine zitaxomfikishia maoni yao kuhusu umaliziaji wa upatikanaji Katiba Mpya..

Muda wa Katiba Mpya ni sasa. Watanzania tuungane katika hili kwaajili ya maslahi yetu ya sasa na ya vizazi vingi vijavyo. Kusiwepo wa kutufanyia hila au ujanjaujanza. Tunataka katiba mpya. Siyo ombi, bali ni lazima, kwa maana ni azimio la Watanzania kupitia Kamati ya Mheshimiwa Jaji Sinde Warioba, mtanzania ambaye uzalendo, umahiri na weledi waje, siyo wa kutiliwa mashaka hata kidogo.
 
Back
Top Bottom