Maoni ya Mh. Zitto Kabwe juu ya kuondoa mgawo wa umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni ya Mh. Zitto Kabwe juu ya kuondoa mgawo wa umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nice 2, Aug 14, 2011.

 1. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mpango mzuri, Fikra pungufu kidogo

  Zitto Kabwe

  Taifa zima lilikuwa linasubiri siku ya tarehe 13 Agosti 2011 ili kufahamu ni jambo lipi jipya Waziri wa Nishati na Madini atakuja nalo kuhusu kumaliza tatizo la mgawo wa Umeme nchini. Tangu mwaka 2006, Tanzania imekuwa ikipata tatizo hili kwa wastani wa kila mwaka isipokuwa mwaka 2007 na 2008 kipindi ambacho Shirika la Umeme nchini TANESCO lilikuwa linanunua umeme kutoka mitambo ya Kampuni za Aggreko na Dowans. Mwaka 2009 adha ya mgawo ilikuwa kubwa sana, ikaendelea mwaka 2010 na baadaye mwaka 2011. Mamlaka ya Mapato nchini walikadiria kupoteza zaidi ya shilingi 840 bilioni kama kodi kutokana na mgawo wa mwaka 2011 peke yake. Hakuna hesabu zilizowekwa wazi kuhusu mgawo wa mwaka 2009 na ule wa mwaka 2010. Pia wachumi wa Tanzania hawajaweza kutueleza katika kila mgawo unaotokea nchini ni kwa kiwango gani ukuaji wa Pato la Taifa unaathirika. Kwa mfano, ukuaji wa sekta ndogo ya Umeme ukiporomoka kwa nukta moja, ukuaji wa uchumi unaathirika kwa kiwango gani. Taarifa kama hizi zinaweza kusaidia sana watunga sera kuweza kujua umuhimu wa sekta ndogo ya Umeme katika juhudi za kukuza uchumi na kuondoa umasikini nchini.

  Mwaka 2011 ulianza kwa Kamati za Bunge za Nishati na Madini na ile ya Mashirika ya Umma kuweka kipaumbele katika uzalishaji wa Nishati ya Umeme. Kamati ya Mashirika ya Umma ilijikita katika kuhakikisha Uzalishaji wa Umeme wa uhakika kutoka katika vyanzo vya Makaa ya Mawe (Mchuchuma, Ngaka na Kiwira).

  Kamati ya Nishati na Madini Ilijikita katika kuhakikisha Wizara inasimamia vya kutosha sekta ndogo ya Umeme na kumaliza kabisa tatizo la Mgawo wa Umeme katika muda wa mfupi, wa kati na mrefu. Kutofanikiwa kwa juhudi hizi na hasa kutoonekana kwa Bajeti ya kutosha ya Sekta hii kulifanya Bunge likatae kupitisha Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini.

  Hatimaye Serikali ilileta Mpango wa Dharura ulioitwa Mkakati wa kuondoa Mgawo wa Umeme na kuimarisha Sekta ndogo ya Umeme. Mkakati huu ni wa miezi 16, kuanzia Agosti 2011 mpaka Disemba 2012. Mkakati huu utakagharimu jumla ya Shilingi 1.2trilioni. Fedha nyingi sana lakini kwa matumizi muhimu sana ya kulihami Taifa. Kimsingi hii ni ‘stimulus package’ kwa Sekta ya Umeme!

  Mkakati huu utaingiza jumla ya 882MW za Umeme katika gridi ya Taifa ifikapo mwezi Disemba mwaka 2012. Katika hizi 572MW zitaingia katika Gridi mwezi Disemba 2011. Jumla ya 422MW zitatokana na Mashine za kuzalisha Umeme za kukodisha kutoka Kampuni mbalimbali binafsi (37MW Symbion, 80MW IPTL, 100MW Aggreco, 205MW Symbion II ). Mradi pekee ambao tunaweza kusema ni wa ndani ni ule wa 150MW ambao utamilikiwa na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

  Shirika la NSSF liliomba Serikalini kuingia katika uzalishaji wa Umeme toka mwaka 2010 kufuatia maelekezo ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma. Juhudi zake zilikuwa zinagonga mwamba kutoka kwa watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini kwa sababu ambazo hazijaelezwa waziwazi. Kwa hatua ya sasa iliyo kwenye Mkakati, Tanzania italipa Kampuni binafsi za nje zaidi ya Shilingi 523 Bilioni kutokana na kununua Umeme kutoka katika mitambo yao. Ingewezekana kabisa NSSF wangeombwa kuwekeza zaidi na hata kuwaomba Mashirika mengine kama PSPF kuwekeza na kupunguza kulipa fedha za kigeni kwa kampuni za nje.

  Serikali itatoa dhamana (guarantee) kuiwezesha TANESCO kuchukua mkopo wa 408 bilioni tshs kutoka katika Mabenki ya ndani. Sekta Fedha nchini itabidi iandae ‘syndicated’ mkopo mwingine kwa TANESCO zaidi ya ule wa mwanzo wa mwaka 2007 wa tshs 300 bilioni ambazo ninaamini unalipwa bila ya mashaka. Hivi Serikali isingeweza kuuza Bond ya thamani hiyo? Wataalamu wa fedha wataweza kulijuza Taifa njia bora zaidi ya kupata fedha hizi. Hata hivyo Sekta ya Fedha ni moja ya sekta zitakazo faidi Mkakati huu, ikiwemo Sekta ndogo ya Mafuta (kwa kuuza mafuta ya kuendesha mitambo). Sekta ndogo ya Usafiri pia nayo itafaidika kwa kusafirisha mafuta kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda kwenye mikoa ambayo Mitambo ya kuzalisha umeme itawekwa kama Tanga, Dodoma, Mwanza na Arusha.

  Ifikapo Mwezi Disemba 2012 Tanzania itakuwa imeongeza 310MW za Umeme ambazo zote zitakuwa zinamilikiwa na Shirika la Umeme au 150MW kati ya hizo Shirika la NSSF. Kwa maana hii ni kwamba katika jumla ya Uzalishaji wa Umeme wa 882MW* tunaotarajia kuongeza katika Gridi ya Taifa, utakaobakia nchini baada ya Mashine za kukodi kuondoka ni 460MW peke yake. Tutatumia* tshs 1.2tr kuingiza katika Gridi wa umeme wa kudumu wa 460MW tu. Hii inatokana na ukweli kwamba baada ya Disemba 2012 jumla ya 422MW zitakuwa zimeondoka kwenye Gridi baada ya mikataba ya kukodisha kumalizika.

  Jambo moja zuri* ni kwamba Serikali imefikiri kimkakati kwamba tuwe hatuna mitambo ya kukodi ifikapo Disemba 2012 (kwa maana ya symbion na Aggreco). Huku ni kufikiri vizuri, kwamba Serikali itakuwa* imejenga uwezo wa Taifa kupitia TANESCO na NSSF kuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wake. Imefanya ‘sequencing’ kwamba itatumia umeme wa kukodi wakati inajenga uwezo wa kununua mitambo yake yenyewe. Wakati Mikataba ya kukodi inakwisha, ndani ya miezi 16 Serikali kupitia TANESCO na NSSF itakuwa inazalisha 460MW. Hatua ya kupongeza.

  Hata hivyo, Serikali na wananchi wanapaswa kujiuliza katika hiki kipindi cha mpito jambo gani litakuwa linafanyika? Ifikapo Disemba mwaka 2012 kutakuwa na mahitaji zaidi ya Umeme kwa ziada ya 200MW au zaidi. Hii inatokana na ukweli kwamba mahitaji ya umeme yaliyopo hivi sasa ni ‘suppressed’ licha ya ukuaji wa asilimia 15 kila mwaka. Vile vile inatarajiwa *kuwa kuwepo kwa umeme kutaongeza uzalishaji ambao utaongeza mahitaji zaidi. Hapa Serikali ilifikia ukomo wa kufikiri (ilichoka). Kunapaswa kuwa na kazi inayofanyika ambayo inafikiri zaidi ya 2012 (Thinking Beyond Dec 2012). Kunahitajika mradi wa angalau 200MW kuanza kutekelezwa kati ya sasa na Disemba 2012 ili mitambo ya kukodisha ikiondoka kuwepo na uwezo wa angalau 600MW. Hapa ndipo Mradi wa Kiwira I unaingia.

  Mkakati wa Serikali kwa KIWIRA una makosa ya kifikra. Serikali inataka kukopa Uchina ili kujenga Kiwira. Mchakato wa mkopo utachukua zaidi ya miaka 2. Taifa haliwezi kusubiri. Serikali iharakishe utwaaji wa Hisa za Kampuni ya TanPower Resources na kukabidhi hisa hizo kwa Shirika la Umma. Shirika litangaze Zabuni kupata ‘strategic investor’ kwa utaratibu wa PPP ambao utazingatia kwamba mara baada ya Mwekezaji kujilipa gharama zake na faida kidogo umiliki uwe sawa kwa sawa (50/50).

  Licha ya Mkakati kuendeshwa na zaidi na fedha za mikopo kutoka katika Mabenki, bado umepangwa vizuri mpaka 2012. Hata hivyo, Mkakati wa kuondoa mgawo wa Umeme na kuimarisha sekta ndogo ya Umeme nchini haukufikiriwa vya kutosha (inadequate thinking) na hasa kwa mbele ya 2012. Bado kuna fursa ya kuboresha. Kamati za Bunge za Nishati na Madini na Mashirika ya Umma zinapaswa kufuatilia kwa karibu sana utekelezaji wa Mkakati huu. Source:http://zittokabwe.wordpress.com/2011/08/13/kuondoa-mgawo-wa-umeme-tanzania/
   
 2. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ngoja niisome nitarudi baadaye kidogo
   
 3. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,028
  Likes Received: 7,422
  Trophy Points: 280
  Here comes again Zitto Kabwe na style yake ya kuimba table na kuhubiri asiyoyaamini...
   
 4. 2

  2015 Senior Member

  #4
  Aug 14, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huyu nae siku hizi anaaminika nusu nusu, Kwanza kilichofanya akose arusha alhamis ilikuwa ni kitu gani?
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  uzalishaji wa umeme nchi utaendelea kuwa ni wa kusuasua tu...........hivi kuna sababu zipi uzalishaji wa umeme kwa gesi ya siongosongo kufanyika Dar badala ya Songosongo? hivi umeme wa dizeli kwa nini ufanyike Dom na Arusha wakati bandari ya upakuaji iko Dar kama siyo kuongeza gharama za uzalishaji? Nchi hii inaendeshwa na waendawazimu na usitegemee hata huo umeme kuwepo kwa viwango vinavyoongelewa..........gharama za uzalishaji ni zaidi ya bilioni 500 lakini matarajio ya mapato ni chini ya 20% ya hizo!!!!!!!!!!

  something is deeply wrong with this country's leadership.......................................bajeti ya nishati imekwisha kuvuruga bajeti za wizara zote na lakini hata wabunge hilo hawalioni hata kidogo ya kuwa itabidi warudie kuzipambanua kiupa jambo ambalo halitafanyika hadi disemba kwenye mini bajeti ambayo ndiyo bajeti ya kiutekelezaji hii.........is just mere politics going on to hoodwink the lazy and the poor...........unfortunately they are the majority..........
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  stupid boy......kabwe....ha.....kheri ukope kulikoni kuingizwa mkenge na scrupulous strategic investors ambao kesho wanakurudia uwadhamni mikopo yao ambayo inakuja kwa bei kubwa................................anachofanya mjinga Zitto ni kuikabidhi nchi hii kwa walanguzi..........................tumeona mengi kuanzia UDA, NBC, NBM, mashirika kadha wa kadha ya umma...........................................ttcl, n.k kuwa no serious strategic investor will come and invest in this country that is run by IDIO-ts............................and bimbos.....................................too
   
 7. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Huuu umeme wa mafungu mafungu sana sana ni kuwaongezea umasikini ha gharama watumiaji. Tanzania haiwzi kuwa kivutio cha wakwekezaji kwa uweezaji wa umeme wa Vimegawati vya mafungu.

  Miaka si minggi tutasikia mtu kuwa na generator binafsi ni nafuu kuliko kuuganishiwa umeme wa TANESCO. wakati seriali itajisifia kuwa kuna umeme wa kutosha hakuna mgao huku watu wakiendelea kutumia mkaaa kukata mistu sabbau gharama za umeme ni juu na vyanzo vyeneywe vya mapato hakuna....
   
 8. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nimefuatilia tweets zao asubuhi, Zitto kabwe, January na mtu anayetumia Jforums! Wana mipango ambayo haitekelezeki!
   
 9. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2011
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  <br />
  <br />

  Zitto Kabwe! I hate politics lakini if poeple were thinking like you, act like you labda ningependa siasa. Hotuba zako nyingi percentagewise umeweka utaifa mbele. Alafu you think strategically sio kama wale washikaji wa contemporary politics. Keep it up! At least in your life you will either be a president or PM. of URT and not less... Tuombe Mungu. Ila nakuomba uachane na kuwa sifa za cku mbili hazilipi... Fanya vi2 vya muda mrefu. Strategic things. Siasa za Ufisadi ni za muda tu
   
 10. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Anything personal? Arusha na kuondoa mgawo wa umeme wapi na wapi! Kwa style hii ili nchi yetu iendelee bado kazi ipo
   
 11. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #11
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,028
  Likes Received: 7,422
  Trophy Points: 280
  .
  Sikuzote wana malengo ya kuwapeleka wenzao mkenge iwapo watafuata ushauri wao.... Ukiwapa majukumu ndiyo kabisa utaharibu kila kitu kwani hakuna watakalo weza kusimamia, kuongea ni ni hulka na matendo ni uwezo..
   
 12. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kwanza serikali haijui poject planning na resource allocation. mambo ya project na resource allation kama za finance na fedha za nishati yamekakaaa kisiasa tu.

  Kwa nini Nasema hivyo?

  Tazama kwenye website ya Tanseco anagalia miradi ya kusambaza umeme wilayani. Inatumia shilingi ngapi? Je umeme huo unaosambazwa upo. Kwa nini wanza pesa na resouces zinaztumika sasa au toka mwaka jana kusambaza mgao wilayani.( (Sorry mimi siiti hi miradi ama ya kuesambaza umeme ni kusambaza mgao)zisngeelekezwa kwenye kuzalisha huo umeme.

  Matokeo yake bungeni wanajisfu kwa miradi ya kusambaza umeme wilayani kumbe ukweli ni kusambaza mgao.  Hii nchi imefika na inatendeka kudidiamia sbabau wanasiasa hawataki kuwahsirkissha wasomi na wataalmu wa fani kabla ya kufanya maamuzi.

  Ukiangalia hata kwenye bajeti ya mwaka huu ya Nishati sitashangaa kuna wilaya za wahemshimiwa wachache zina bajeti ya kusambaziwa mgao
  .
  teh teh teh
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Aug 14, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mheshimiwa Zitto ni mtu safi na anajua sana kutazama vitu kwa picha kubwa lakini ana tatizo moja kubwa sana. Anaamini baadhi ya WATU kwa kila kitu..anaamini sana maandishi na ahadi za chama bila kujiuliza haya maneno yanasemwa na NANI...Ndivyo tunavyoishi mjini yaani ule ujanja wa kuwashtukia Watanzania ktk hulka na matendo yao Zitto hana ujanja huo..

  Kwa nini naseam hivi.. Zitto kaeleza kila kitu vizuri sana na kuweka mashaka vizuri sana lakini alichoshindwa kuona ni kwamba hayo mashirika yoote yanayokuja wekeza nchini are here to stay! hakuna habari wala ukweli kwamba ifikapo Desemba 2012 mashirika hayo yataondoka..Yataondoka vipi wakati mahitaji yetu ya Umeme ni zaidi ya hizo Megawatts? na wala hakuna mpango madhubuti wa NSSF wala TANESCO kuzalisha umeme kufidia hizo zitakazo ondoka ifikapo Dec 2012 acha mbali mahitaji kamili na ongezeko la mahijtaji ya Umeme nchini kufikia 2012.

  Mashirika hayo yataendelea kuwepo na hizo sijui Tanesco na NSSF watapewa chao maadam wanaoumiza vichwa ni wananchi..Tuliambiwa na Mwinyi kuwa Mitumba imeletwa kwa sababu ya dharura na ukosefu wa nguo..Leo hii miaka 20 imepita Mitumba bado ipo tena ndio kwanza imekuwa na nguvu ya soko kuliko hata nguo Mpya. Daladala hivyo hivyo na Mwaka 2007 JK alipoingia madarakani alitwambia kuwepo kwa Richmond, Aggreko na mashirika haya ilikuwa dharura na kwamba kufikia 2009/10 yangeondoka (mkataba wa miaka miwili), Tanzania tungekuwa tayari tunajiweza na hatuna tena tatizo la Umeme.. Yako wapi?..

  Hizi habari za TANESCO au serikali kukopa fedha Benki za ndani kwa ajili ya kujiendesha ni bad economy! yaani ni ujinga usiokuwa na kifani sijawahi kusikia serikali au shirika la Umma linakopa fedha benki za ndani... Kaama nchi imepoteza credibility na tumeshuka credit value yetu kiasi kwamba hatuwezi kukopeshwa na benki za dunia au financial institution zinazotoza interest chini ya 4 leo tukakope benki za ndani zenye interest ya juu kufikia asilimia 20 hadi 30... Basi nchi yetu imekwisha! kilichobakia tukatafute sanda na jeneza tuache kabisa kujadili habari za Kiwira, Mchuchuma na kadhalika.

  Mheshimiwa Zitto, mara zote usipende sana kuamini hawa jamaa zetu kwa sababu hakuna lolote la maana isipokuwa ni kamba tupu kwa kwenda mbele. Hizo trillion 1.2 Ni mtaji mkubwa sana kwa Mafisadi na nakuhakikishia kwamba Tatizo la Umeme nchini ndio kwanza limeanza. Hatuwezi kuiita hii 1.2 tr kama stimulus package wakati hai stimulate kitu chochote kilichokuwa ndani ya uzalishaji uliopo isipokuwa kutegemea miradi mipya.

  Infact nachoona hapa ni mashirika ya nje kuwezeshwa kuwekeza nchini na sijaona jinsi gani hizo 1.2 trillioni zitatumika kama stimulus halafu iwe sababu ya kupitisha bajeti ya wizara haraka haraka mara tu baada ya ongezeko hili. Ongezeko la fedha sio dawa ya matatizo yetu bali mipango yenye dhamira ya kuondoa tatizo ndiyo tunaitazama gharama yake..Hii yote ni changa la macho na nasikitika mh. Zitto anashindwa kuliona.
  Na mwisho tusisahau kwamba mahala popote penye scarcity - don't count out Corruption!
   
 14. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #14
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Mkandara inaonekana unakaa sana nje ya nchi.

  siku nyingine kabla hujajibu hebu muulize mwanakijij akufeed data kabla hujaa ndika

  Unandishi wako utafkiri bado uko standard 6
   
 15. Cassava

  Cassava JF-Expert Member

  #15
  Aug 14, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 282
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mkakati wa kuondokana na mgao wa umeme ni mzuri,tatizo ni pale wazili anapoomba TANESCO waombe ridhaa ya kupandisha gharama za umeme ili kufanikisha hatua hizo. Kwa kupandisha gharama za umeme, walala hoi ndo tunapoumia. Hata wale wasiotumia umeme lazima waumie kwa kuwa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa kwa nguvu ya umeme lazima zipae juu. Ikiwemo na gharama za internet cafe. HApo ndo ninapoona ile hoja ya posho mbalimbali zinazotolewa kwa baadhi ya kadhia zifutwe ili kufidia baadhi ya michakato ya kuzalisha umeme.

  Hata hivyo kuhusu posho imeshatoka.
   
 16. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Serikali hii tuliyonayo inatia aibu sijaona hata mradi wake ambao ni endelevu mingi huishia kufa. Hata hii ya kukodi umeme wa dharula ni usidi mwingine "stimulus package" ya umeme kama ilivyokuwa kwa package ya kilimo ililiwa tu na hao akina Simon Agency (UDA) na wenzake
   
 17. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #17
  Aug 14, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mimi naishangaa serikali yetu NSSF waliomba wapewe kiwira na kwamba wangezalisha 400mw hadi kufikia December mwaka huu lakini kwasababu mradi huo haukuwa na maslahi kwa mafisadi umebaki kuwa hadithi, badala yake wamepewa mradi wa dharura ambao una maslahi kwa mafisadi. Mimi nasema watanzania tupiganie katiba mpya ambayo itaweka bayana hatua za kuwabana mafisadi ili kuondokana na kansa ya ufisadi inayolitafuna Taifa letu
   
 18. Mageuzi

  Mageuzi Member

  #18
  Aug 14, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zitto amepoteza credibility

  mimi binafsi sina Imani Naye,namuona ni Oportunist ,sijui wenzangu.Bora tu angerudi CCM au akampokee yule babu Mrema wa TLP.

  Swala la Umeme Tanzania lipo wazi, Songas wanaozalisha Gas,wapewe Jukumu la kuzalisha umeme pia, lakini ukichunguza ni Vigumu Sana kupata EPA/10 percent kutoka songas ,matokeo yake vijikampuni vya mkononi vimeingizwa kuzalisha na kusambaza gas,

  Zitto analijua hili mbona halizungumziii


   
 19. k

  kayumba JF-Expert Member

  #19
  Aug 14, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tatizo letu hapa Tz ni kuwa na viongozi na wanasiasa wenye upeo mdogo sana. Sijui ni kwanini serikali na washauri wake wote wanaona njia ya kuondoa mgao ni kuwekeza kwenye miradi midogo midogo ya 400MW? Kwa mtindo huu, hata Rais atakaye ingia baada ya JK tatizo lake la kwanza litakuwa umeme!!! Ni kipofu tu asiyeweza kuona hili.

  Nini kinaitajika kufanywa?

  Kwa sababu taifa limepata tatizo la umeme kwa miaka 20 sasa, basi tutekeleze miradi mikubwa itakayokidhi mahitaji yetu ya miaka mingi ijayo. Miradi ya kuzalisha kama megawati 4000! Yes i mean 4000MW. Ukiangalia hizo pesa tunazotumia kwenye dhalura kila mwaka zinatutosha kutekeleza miradi mikubwa kama hiyo. Nasikitika kusikia tutatumia 1.2trion na mwisho wa siku tutapata 450MW. Kizazi kijacho kitatulaani kwa maamuzi mengi ya sasa!

  TAFAKARI!
   
 20. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #20
  Aug 14, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  siku zote mawazo yao (CCM) yanaleta matumaini tatizo ni utekelezaji wa kinacho pangwa hapa ndipo naona Mh. Zitto amejisahau kuwa yeye ni mpinzani na sababu ya kuwa mpinzani. Sioni sababu yake Kuwaamini sana hawa mawaziri wa Mega watt (MW)

  pia suala la TANESCO kupandisha bei za umeme kwa kisingizio kuwa itawahusu watumiaji wakubwa pekee si kweli kwani wananchi wa kawaida ndiyo watao beba gharama za uzalishaji baada ya kupandishiwa bei ya bidhaa " Upinzani uwe makini kutetea wananchi dhidi ya serikali hii na ha Mh ZITTO''
   
Loading...