Maoni ya Mh. Mbowe juu ya tatizo la umeme; Je, yana mashiko? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni ya Mh. Mbowe juu ya tatizo la umeme; Je, yana mashiko?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tuko, Jul 19, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Jul 19, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Mh Mbowe alitoa maoni yake akichangia bajeti (iliyopigwa chini) ya miundombinu kuwa "kwa sasa serikali peke yake haiwezi kutafuta mbinu za kuinasua nchi na janga la umeme, na akashauri iundwe task force itakayoshirikisha wadau mbalimbali kama serikali yenyewe, bunge na sekta binafsi kufanya kazi hiyo"
  Mh Mbowe anatoa sababu nyingi kama za ku-share lakini kubwa akisisitiza kuwa kwa kuwa serikali (wizara na Tanesco) ndio wamesababisha tatizo hili kwa uzembe wao, ufisadi wao, ubinafsi wao, uwezo wao mdogo na hivyo wao kwa sasa hawataweza kuwa na uwezo wa kutatua suala hilo peke yao.
  Mh Mbowe alifikia kutumia neno kuwa serikali haina 'legitimacy' ya kutatua tatizo la umeme, neno ambalo lilimkasirisha Mh Lukuvi na kutoa taarifa ya kukanusha.
  Serikali kwa upande wake imekuwa ikisisitiza kuwa inayo mipango na uwezo wa kutatua tatizo la umeme, na Mh Pinda alitumia dk kadhaa kuanisha 'mikakati kabambe' ya serikali kuinusuru nchi na janga la giza. Hata hivyo Mh Mbowe ameendelea kusimamia na kusisitiza msimamo wa serikali kuunda task force.

  Je, who is more correct?
  Kuundwa kwa task force kunaweza kuinasua nchi?\
  Je serikali itaweza kutekeleza yenyewe mikakati yake na kuiondoa nchi gizani?
  Na je, serikali itaeleza yapi mapya zaidi ya yaliyoelezwa kwenye bajeti ya Ngeleja, na kwenye hotuba ya Pinda ya kuiahirisha bajeti hiyo?

  Yetu "meso"
   
 2. nditolo

  nditolo JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 1,335
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Yesu alikuja kwa wenye dhambi ili awaokoe, lakini walimpiga na kumuadhibu hukumu ya kifo. CCM hawana mikakati yoyote inayotekelezeka labda mbingu ishuke, ushauri unaotolewa na viongozi wa upinzani haufanyiwi kazi ndio maaana hatufanikiwi.
   
 3. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,689
  Trophy Points: 280
  Nimeshindwa kumaizia baada ya kusoma mistari miwili ya mwanzo. Bajeti ya Miundombinu imepigwa chini lini mkuu?
   
 4. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #4
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Nilimaanisha kuwa ilichoeleza hakikukubaliwa na wabunge na wakaamua ikafanyiwe marekebisho kwanza. Back to topic sir...
   
Loading...