Maoni ya kiongozi wa juu wa CCM Zanzibar kuh: Katiba mpya !!

Mzenji73

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
341
91
"Kila nikiyaangalia haya maoni kwa kweli sioni tofauti yake na tunachokipigania sisi wana UAMSHO!! hapa nasema alhamdulillah! je upo umuhimu wa muungano wa tanganyika na zanzibar hapo?, si na tujiunge tu na east african community? ndio pale tunaposema "TUACHIWEE TUPUMUEEE !!, maoni haya yanatoka kwa mtu mzito toka CCM- Zanzibar"
I. Nchi kamili inayoweza kujiamulia.mambo yake yote ni lazima ikidhi mambo manne yafuatayo:

1)Watu
2)Mipaka ya Nchi husika
3)Serikali ya kuendesha mambo ya Nchi husika
4)UWEZO WA KUJIAMULIA NA KUINGIA MIKATABA NA NCHI HUSIKA KWA NCHI NYENGINE BILA IDHINI KUTOKA NCHI NYENGINE.

II.NCHI YA ZANZIBAR inayo sifa ya mambo matatu hapo juu na kulikosa la nne UWEZO WA KUJIAMULIA MAMBO YAKE YENYEWE...ndio TUNAKOSA UWEZO WA:

i)Kuwa na kiti UN
ii)Kuwa na Mabalozi
iii)Kushirikiana na nchi nyengine kipeke yetu kama Nchi ya Zanzibar
iv)Kwa ujumla Nchi ya Zanzibar inakosa SELF DETERMINATION

III. TANGANYIKA HAIPO WALA HAWANA HATA SIFA MOJA KATI YA YALE MANNE YA MSINGI NA INAFAIDIKA NA KUBEBWA NA KUTEKELEZEWA NA Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania hivyo MANUFAA YOTE YANAKWENDA TANGANYIKA!!!

IV.MUUNGANO huu ni wa NCHI MBILI ZILIZOKUWA HURU!!!

a)Tanganganyika
b)Jamhuri ya Watu wa Zanzibar

V.PENDEKEZO

i)Kila Nchi IWEZE kuwa na SELF DETERMINATION.
ii)Iingie katika mikataba yake na ushirikiano na nchi nyengine.
iii)Iwe na Balozi zake.
iv)Iwe na kiti chake UN,AU,EA na kadhalika.
v)Tanganyika irejeshewe: a)Mipaka yake. b)Bunge lake c)Watu wake.

VI.Hivyo tuwe:

i)Serikali ziwe mbili ya Tanganyika na Zanzibar!!!
ii)Kila moja ishughulikie mambo yake yote!!!
iii)Kwa pamoja tutazame MAMBO YA USHIRIKIANO ILI TUWE NA 'MUUNGANO WA USHIRIKIANO'
iv)Hili litawekwa wazi katiba MIKATABA AU TREATY ambayo itasainiwa na Nchi ZOTE MBILI.
v)Tutatizama yale mambo tu ya ushirikiano na hayo LAZIMA KILA NCHI IYAKUBALI NA IYARIDHIE!!!
vi)Kama Nchi haikuridhia,basi sio LAZIMA KUINGIA katika mkataba hu.
vii)Mifano hii ipo Duniani kote kama mifano ifuatayo:

A.European Union
Kila nchi ina uhuru wake kamili,kwa mfano UK,FRANCE,GERMANY,BEGIUM,SPAIN,GREECE,HOLLAND,ITALY na kadhalika.
Kila Nchi inapokataa na kutoridhia protokoli fulani,hailazimiki wala hailazimishwi:
Mfano Euro na Pound Sterling ambapo UK haikukubalika na kuridhiwa.
Shenghen Viza na matumizi ya Nchi chache tu katika jumuia.

B.African Union

Nchi zote zote za Africa zimeungana,lakini kila Nchi ina uhuru wake kama vile:

Mambo ya Nje
Sarafu
Kiti UN
Balozi nchi nyengine
Utaratibu wa Viza
Na kadhalika

C.East Africa
Kenya
Uganda
Tanzania
Burundi
Ruanda
Protokoli zake pia ni kama Muungano kwengineko.

HIVYO TUNAPENDEKEZA UWEPO MUUNGANO WA NCHI MBILI!!!

1)Kuwa na Serikali mbili ambazo kila Serikali INAJITEGEMEA WENYEWE!!!

2)Kwa maana hiyo Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kila moja itakuwa na yale mambo manne ya msingi:
i)Mipaka yake
ii)Watu wake
iii)Serikali yake
iv)Uwezo wake wa kuingia mikataba kushirikiana na Mataifa ya nje,kuwa na Balozi zake,kuwa na viti vyake UN,AU,EA na kadhalika.

3)Kuwe na Muungano wa Shirikisho (Mungano wa Mkataba) kwa mambo ambayo nchi mbili hizo (Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar) zitaridhia na kukubaliana!!!
 
Huyu "kiongozi wa juu' ni nani? Kama ana nia njema na kama si mnafiki na anaweza kusimamia maneno yake basi ajitokeze. Tatizo la viongozi wenu Zanzibar chini chini wanadai kupinga muungano ila kwenye vikao vya maamuzi ndani ya chama na serikali wao siku zote kimya. Sasa huyu anaogopa nini kujitokeza wasi wasi kama siyo unafiki?
 
Heshima kwa mh.Lisu,

Huyu jamaa kapasua jibu na katupa maelezo safi kuhusu ulaghai wa CCM kuhusu muungano.

Me naomba Watanganyika umefika wakati tudai Tanganyika yetu, kwa kweli najisikia aibu sana kuwasikia Wazenji wakijifaharisha na Uzanzibari wao, hayo utayaona zaidi ukiwa huko Zenji utatamani urudi kwenu haraka sana maana yanaudhi maneno yao.

i. Kwanini sisi Watanganyika hatujikusanyi ktk Taasisi zetu tukawashajihisha na kuwaelimisha wazalendo kuitafuta Tanganyika???

ii. Kwanini cku zote tuwe nyuma nyuma ktk suala uasili wa Taifa letu la Tanganyika??? Mkataa kwao ni mtumwa!!!

Nawasilisha.
 
wakuu wekeni HISTORIA ya kudai Tanzanyika sawa, msimsahau MTIKILA,

Mtikila kufungua kesi ya kudai Tanganyika

na Ramadhani Siwayombe, Arusha

amka2.gif
MWENYEKITI wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, anakusudia kufungua kesi mpya katika Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika iliyoko Arusha, kudai serikali ya Tanganyika.
Mchungaji Mtikila aliyasema hayo jana mjini hapa, mara baada ya kuahirishwa kwa kesi aliyoifungua katika mahakama hiyo kudai uwepo wa mgombea binafsi.
Mtikila alisema kuwa kutokana na imani kubwa aliyonayo kwa mahakama hiyo, ana imani haki aliyokua akiitafuta kwa muda mrefu sasa iko mbioni kupatikana.
Alifafanua kuwa katika kufungua kesi hiyo ya kudai Tanganyika, kuna wanasheria kutoka Nigeria wako tayari kuja kusimamia katika kesi hiyo ambayo alidai itakuwa ni ukombozi kwa Watanganyika wote.
Aidha alisema kuwa wakati yeye anakusudia kufungua kesi hiyo tayari ana taarifa za kuwepo kwa baadhi ya Wazanzibari wanakusudia kufungua kesi katika mahakama hiyo kupinga muungano.
Awali katika mahakama hiyo, kesi iliyoanza kusikilizwa juzi na mahakama hiyo juu ya hoja ya mgombea binafsi iliyofunguliwa na Mtikila pamoja na kituo cha msaada wa sheria na haki za binadamu mara baada ya kusikilizwa hoja za pande zote mbili iliahishwa.
Kesi hiyo inayosikilizwa na majaji tisa kati ya 10 wa mahakama hiyo iliahirishwa hadi baada ya siku 90 ambapo itakuja kutolewa hukumu kutokana na pande zote mbili kukamilisha ushahidi wao.
Katika kuwasilisha maelezo ya mwisho na kujibu maswali yaliyotolewa na majaji wa mahakama hiyo, upande wa Mtikila uliiomba mahakama hiyo itamke kuwa na haki kuwepo na mgombea binafsi katika chaguzi zote za kisiasa hapa nchini.
Aidha kupitia kwa wanasheria James Jesse, Clement Mashamba, Donald Deye na Profesa Lajovi waliiomba mahakama hiyo pia iiamuru serikali ya Tanzania kulipa gharama zote za kesi hiyo.
Jaji Elsien Thompson alimuuliza Mtikila ni kwa nini anataka kuwepo kwa mgombea binafsi wakati yeye tayari ana chama chake kinachomuwezesha kupata fursa ya kugombea.
Kupitia mawakili wake, Mtikila alijibu kuwa kutokana na kuwepo na taratibu ngumu za uidhinishwaji wa vyama kuruhusiwa kusimamisha wagombea, imepelekea mteja wao kushindwa kupata haki hiyo.

Huyu "kiongozi wa juu' ni nani? Kama ana nia njema na kama si mnafiki na anaweza kusimamia maneno yake basi ajitokeze. Tatizo la viongozi wenu Zanzibar chini chini wanadai kupinga muungano ila kwenye vikao vya maamuzi ndani ya chama na serikali wao siku zote kimya. Sasa huyu anaogopa nini kujitokeza wasi wasi kama siyo unafiki?

"huyu hajajificha, kayasema haya hadharani/ kadamnasi, ila mimi si sehemu yangu kumtaja, nafikiri kwa msimamo alionao sasa ipo siku atayasema hadharani, si wanasubiri tume ije mbele yao?"
 
"huyu hajajificha, kayasema haya hadharani/ kadamnasi, ila mimi si sehemu yangu kumtaja, nafikiri kwa msimamo alionao sasa ipo siku atayasema hadharani, si wanasubiri tume ije mbele yao?"

Sasa kama kayasema hadharani unaogopa nini kumtaja? Ndio nidhamu ya woga na unafiki wenyewe huo.
 
Heshima kwa mh.Lisu,

Huyu jamaa kapasua jibu na katupa maelezo safi kuhusu ulaghai wa CCM kuhusu muungano.

Me naomba Watanganyika umefika wakati tudai Tanganyika yetu, kwa kweli najisikia aibu sana kuwasikia Wazenji wakijifaharisha na Uzanzibari wao, hayo utayaona zaidi ukiwa huko Zenji utatamani urudi kwenu haraka sana maana yanaudhi maneno yao.

i. Kwanini sisi Watanganyika hatujikusanyi ktk Taasisi zetu tukawashajihisha na kuwaelimisha wazalendo kuitafuta Tanganyika???

ii. Kwanini cku zote tuwe nyuma nyuma ktk suala uasili wa Taifa letu la Tanganyika??? Mkataa kwao ni mtumwa!!!

Nawasilisha.

"kwa nini ujisikie aibu kwa waZanzibari kujifaharisha na nchi yao!? je huwa waona aibu piya kuona waKenya wanajifaharisha na nchi yao? ni ukweli usiopingika sisi huku wala hatujifaharishi na uTanzania, hii haimaanishi kuwa nawachukia waTanganyika laa! nawapenda sana! ni ndugu/jamaa na marafiki zangu, kama walivyo waKenya pia. Ila huku Zanzibar tokea 'day one' ya huu wenye kuitwa muungano, hatukuwa tayari kupoteza nchi yetu katika ramani ya dunia, (iliwe na tanganyika). nyinyi waTanganyika wengi wenu munaona hivi vilio vimeanza leo, laa vipo tokea 'day one' ya wenye kuitwa muungano. historia yathibitisha hayo. Ela sasa wakati unfika wa kuachiliwa twende kwa amani, na udugu/ujamaa na urafiki wetu wa kijamii utaendelea kuwepo tu, hata kama wengine hawapendi hili, wao wanaona kujirejeshea sisi jamhuri yetu kama uhasama. Uzalendo mtamu bana! namshukuru Allah kunijaaliya kuwa mwana wa Zanzibar na namuomba anijaalie niishuhudie Zanzibar yetu pale itakapokuwa DOLA KAMILI pale ambapo ...

1. Rais wa Zanzibar atakapotambulika kimataifa

2. Nitakapokuwa na urai/passport yangu ya Zanzibar

3. Nitakapoiona sarafu na benki kuu ya Zanzibar

4. Nitakapokishuhudia kiti cha Znz kinarudi UN
!
 
Sasa kama kayasema hadharani unaogopa nini kumtaja? Ndio nidhamu ya woga na unafiki wenyewe huo.

"kila jambo na wakati wake, hili ndio linalotufanikishia lengo letu waZanzibari, unafiki, papara/jazba ni vitu vingine na subra, busara na hekma ni vitu vyengine, "
 
"kila jambo na wakati wake, hili ndio linalotufanikishia lengo letu waZanzibari, unafiki, papara/jazba ni vitu vingine na subra, busara na hekma ni vitu vyengine, "

Mkuu Mzenji73 kutaja jina sio papara, wewe mwenyewe umesema aliyasema hadharani which means alitaka ifahamike kuwa yeye flani kasema hivo, sasa wewe mtoa taarifa unavyokataa kutoa jina unaonekana wa ajabu mkuu, for sure, unbelievable.:confused2:
 
Last edited by a moderator:
Muungano wa Ushirikiano maana yake ni nini??

Kweli wewe ni Muamsho Dhaifu!
 
... lakini haopa kuna tatizo moja kubwa ambalo wazanzibari kwenye ngani za chini hamjaliona ikiwa tutakwenda kwenye serikali mbili kwanza ijulikane kuwa tanganyika ndio ibebe deni la Tanzania maana wao ndio waliokopoa, vni vizuri hiyo package ikaja responsibilities za tanganyika na madeni yao walionunulia rada.
 
timbilimu,mabumba ni nani?. Hizi ndizo kejeli ambazo hazisaidii kitu. mzenji73 ameleta changa moto na aliyoyaleta yametoka kwa kigogo wa CCM. Hofu nikuwa huu pengine ndio msimamo wa CCM zanzibar katika kikao chao cha siri kilicho fanyika juzi. Sasa basi fununu kama hizi huwa ni siri likisubiriwa tamko. Na tamko litajitokeza aidha kupitia baraza la wawakilishi au msemaji mkuu wa chama.
Changamoto iliopo ni kuwa wazanzibari hawataki tena kuwa kwenye muungano. Kama ni RADAR, hayo ni matatizo ya Mkapa. Sisi hakutushauri alipokwenda kununua radar. Na pesa ziliporudishwa zimetumiwa kwenye ukarabati wa mashule ya tanganyika. Hakuna hata shule moja zanzibar imenufaika na pesa hizo. Pili, katika kipindi kilichopita inasemekana munatudai. Tumeomba muwakilishe deni lenu. Kama munakumbuka palikuwa na deni la umeme, $50m. Pesa kidogo kulinganisha na uchumi wa taifa letu. Nimependekeza pachaguliwe kamati husika kufuatilia suala hili la kuvunja muungano kusudi limalizike kwa salama. Kama munatudai, tutawalipa na kama tunawadai mutatulipa. Sisi hatuna noma kuwalipa sabau tunajijua mulicho nacho chetu.
 
Wengine hujitia wenyewe changa machoni. Huyu jamaa kichwa.
 
"huyu hajajificha, kayasema haya hadharani/ kadamnasi, ila mimi si sehemu yangu kumtaja, nafikiri kwa msimamo alionao sasa ipo siku atayasema hadharani, si wanasubiri tume ije mbele yao?"
Usiwe mwoga, kama ni Shein tutakuwa na mgogoro, kama ni Hamad Sherrif yule pro-arab hatushangai sana.
 
Back
Top Bottom