Maoni ya katiba: ‘Walimu wanaopewa mimba na wanafunzi kushitakiwa’

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
BAADHI ya wanafunzi wa sekondari wilayani Mpanda na Mlele mkoani Katavi wamejitokeza mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kupendekeza Katiba ijayo ibane walimu wa kike ambao wanapewa ujauzito na wanafunzi wao.

Pia wanafunzi hao walipendekeza wanafunzi wanapopeana mimba, mvulana na msichana, wote wachukuliwe hatua za kisheria kwa kushitakiwa na si msichana kufukuzwa shule tu wakati mvulana anashitakiwa na baadaye kufungwa.
Wanafunzi hao pia walipendekeza mabadiliko ya mitaala ili kumpunguzia masomo mwanafunzi wa sekondari na wakapendekeza lugha ya Kiswahili iwe ya kufundishia kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne.
Sabath Katabi ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika Sekondari ya Kasokola wilayani Mulele, alisema maisha ya shule yana wanafunzi na walimu na mwalimu wa kiume anapompa mimba mwanafunzi wake, anafukuzwa shule na kushitakiwa.
"Naomba Katiba mpya pia iseme kuwa mwalimu wa kike anayepewa mimba na mwanafunzi wake pia afukuzwe kazi na ashitakiwe, kwani naye atakuwa amefanya kosa kufanya mapenzi na mwanafunzi wake," alisema Katabi.
Mwanafunzi huyo alisema hajawahi kuona walimu wa kike wanaofanya mapenzi na wanafunzi wao wakichuliwa hatua, jambo ambalo alisema ni ubaguzi mkubwa wa kisheria kwa kuwaonea walimu wanaume ambao wanajikuta kwenye uhusiano na wanafunzi wao, kwa sababu ya kujaribiwa na wanafunzi hao.
Mikisedeki Nyambwago ambaye ni mwanafunzi wa Sekondari ya Milala alitaka wanafunzi wa kike ambao wanapachikwa mimba na wanafunzi wavulana nao wachukuliwe hatua za kisheria, kwa kushitakiwa ili wawe waoga wa kufanya mapenzi wakiwa shuleni.
"Sheria inabagua, mvulana akifanya mapenzi na msichana, mvulana anafukuzwa shule na kushitakiwa, lakini msichana anafukuzwa shule na hashitakiwi, kwa nini wakati wote hawa wamefanya kosa la jinai?"
Alihoji mwanafunzi huyo. Nasri Lubeba mwanafunzi wa kidato cha tatu wa Sekondari Milala, alipendekeza Katiba itamke kuwa mwanafunzi wa kike anayepata ujauzito, akishajifungua apewe fursa ya kurudi shuleni ili aendelee na masomo.


CHANZO:GUMZO LA JIJI
 
mmekosa ya kuweka kwenye katiba? Badala ya kuzungumzia mhimili wa nchi mnaongelea mambo ya kupeana mimba si mlishaambiwa ni viherehere vyenu?
 
Back
Top Bottom