Maoni ya Katiba Mpya yakusanywe upya, Rasimu ya Warioba ifanywe kuwa rejea tu

The lost

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
2,695
8,209
Nimetafakari sana juu ya watanzania waliotoa maoni ya ya kuundwa katiba mpya mwaka 2012 na ushirikishwaji wa makundi yote ya kijamii.

Kuanzia mwaka 2015 kuna ongezeko kubwa la wasomi na vijana waliohitimu elimu ya upili kuliko kipindi cha nyuma na wakati wa ukusanywaji wa maoni ya katiba ya Tume ya Warioba. Lakini pia mfumo wa maisha ya mtanzania yamebadirika sana, ajira kwa vijana, suala la afya ya jamii pamoja na umiliki wa ardhi.

Yote haya yamekuja katika kipindi ambacho hakukuwa na ushirikishwaji wa kutosha wa wananchi juu ya mchakato mzima wa kisiasa, kiuchumi na suala zima la madaraka ya viongozi wa serikali za mitaa na mipaka yao kwa viongozi wa serikali kuu na watumishi wa umma.

Ongezeko la vijana wasomi pia limetufumbua macho juu ya mfumo wa elimu yetu kufanywa suala la ndani ya katiba ili iweze kujulikana wapi na nani anapaswa kubadiri mfumo na utaratibu wa utoaji wa elimu.

Kulingana na mtazamo huu, nilikuwa naonelea serikali ikusanye upya maoni ya katiba mpya na ushiriki uhusishe Watanzania wote.
 
Hata chai hunanywa unawaza katiba mbona mnakuwa misukule


USSR
 
Back
Top Bottom