Maoni ya katiba kupitia mtandao wa Internet - nafasi nzuri sana tusiache wandugu

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Jamani wananchi wote wenye uwezo wa kufikia na kutumia internet naomba tutoe maoni yetu kupitia mtandao wa tume ya katiba www.katiba.go.tz Ila sasa sijui watamjuaje kwa haraka kuwa mtoa maoni sio raia wa Tanzania. Ingekuwa vema wangeweka na sehemu ya namba ya mpiga kura na baadae ku-crosscheck kwenye daftari la kudumu la wapiga kura badala ya kutumia mi-IP addresses.
 
Nadhani kutoa maoni kupitia internet ni kupotezeana muda. Si wazanzibari wanasema wazi wazi wanataka kura ya maoni juu ya mustakbali wa muungano. Mbona mnawapiga mabomu basi?
 
Sio Jamhuri ya Zanzibar tu, Jamhuri zote zirudi na muungano wenye tija ndio tuuzungumzie. Jamhuri ya watu wa Zanzibar itakuwa salama pale Jamhuri ya Tanganika itakapohuishwa. Watu wa Zanzibar wanadhani kuwa wakiwa nje ya muungano ndio watafaidi sana ila ukweli ni kuwa nje ya muungano Zanzibar itaparaganyika na kuwa vipande viwili vya Unguja na Pemba. Sisi yetu macho tu. Na Wapemba watataka kubaki kwenye muungano kwa maslahi wanayoyaona. Mh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.
 
Back
Top Bottom