Maoni ya John Mnyika juu ya Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni ya John Mnyika juu ya Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ukweli2, Jul 30, 2012.

 1. u

  ukweli2 Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.Maoni yangu kama Waziri Kivuli wa Nishati na Madini na mbunge:
  JOHN MNYIKA: Kufuatia uamuzi wa Spika wa Bunge jana jumamosi tarehe 28 Julai 2012 kukubali kuvunja Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini nimetakiwa kutoa maoni yangu kuhusu uamuzi husika kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini

  [h=2]Sunday, July 29, 2012[/h][h=3]Kufuatia uamuzi wa Spika wa Bunge jana jumamosi tarehe 28 Julai 2012 kukubali kuvunja Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini nimetakiwa kutoa maoni yangu kuhusu uamuzi husika kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini na mbunge:[/h]

  Kwa maoni yangu uamuzi huo ni sahihi lakini umechelewa na pekee hauwezi kurejesha heshima ya bunge kwa ukamilifu wala hautaweza kushughulikia uzembe na udhaifu ulioko kwenye bunge na kwenye serikali ikiwa hautaambana na hatua nyingine za ziada na za haraka.Kwa upande mwingine, uamuzi huo umedhihirisha nilichokisema kwa nyakati mbalimbali kuhusu uzembe wa kibunge pamoja na udhaifu wa serikali.

  Ukiondoa tuhuma za wabunge wanaodaiwa kupokea rushwa ama kuwa na maslahi ya kifedha kwenye wizara, taasisi au mashirika wanayoyasimamia kwenye kamati mbalimbali, heshima ya bunge imeathiriwa vile vile na maamuzi mathalani uamuzi wa kuchaguliwa kwa mtuhumiwa wa ufisadi wa Rada Mbunge Andrew Chenge kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi.

  Hivyo hatua zaidi zichukuliwe ikiwa ni pamoja na kuvunja na kamati zenye wajumbe waliotuhumiwa na pia kufanya mabadiliko makubwa kwenye wajumbe wa kamati mbalimbali za kudumu za bunge ili kupunguza maslahi ya kifedha ama tuhuma za rushwa miongoni mwa wajumbe wa kamati. Aidha Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imalize kazi yake kwa dharura ili majina ya wahusika yatajwe ndani ya bunge na bunge lijadili kupitisha maazimio ya hatua za ziada za kuchukuliwa na vyombo huru vya kiuchunguzi na hatimaye watakaothibitika kuvunja sheria wafikishwe mahakamani. Pamoja na hatua hizo, Kamati za Vyama nazo zichukue hatua kwa wabunge wake watakaotajwa ili kudumisha misingi ya uadilifu na uwajibikaji kwa maslahi ya umma.
  Hata baada ya hatua hizo, izingatiwe kuwa Bunge litaweza kujinasua kwenye uzembe ikiwa litatimiza kikamilifu wajibu wake wa kuisimamia serikali kwa mujibu wa ibara ya 63 kuondoa udhaifu wa serikali kwenye sekta ya nishati na sekta nyingine muhimu za taifa kwa kuhakikisha maazimio yote ya bunge yanatekelezwa kwa ukamilifu na kwa haraka kama nilivyoeleza kwenye maoni ya kambi rasmi ya upinzani bungeni tarehe 15 Julai 2011 na tarehe 27 Julai 2012.

  Nilisema bungeni kwamba “Naamini iwapo maazimio ya Bunge juu ya Mkataba baina ya TANESCO na Kampuni ya Richmond Development Company LLC yangetekelezwa yote na kwa wakati toka mwaka 2008, maazimio ya bunge juu ya uendeshaji wa sekta ndogo ya gesi asili ya mwaka 2011 yangezingatiwa yote na kwa haraka, maazimio kuhusu uhalali wa utaratibu wa Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti bungeni ya mwaka 2011 yangechukuliwa kwa uzito unaostahili; taifa lingeepushwa kurudia mijadala ile ile kuhusu Wizara hii hii mara kwa mara”.

  Mathalani, Waziri wa Nishati na Madini ameeleza bungeni tarehe 28 Julai 2012 kuwa wapo wabunge wanaotuhumiwa kufanya biashara zenye kulihujumu Shirika la Umeme (TANESCO) na Spika wa Bunge akahitimisha kuwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge itachunguza tuhuma husika na pia kwamba inakusudiwa kutungwa kwa Kanuni za Maadili (Code of Conduct) ili kudhibiti hali hiyo.

  Hata hivyo, Serikali na Uongozi wa Bunge kwa pamoja wamesahau kuwa mwaka 2008 baada ya Kashfa ya Richmond iliazimiwa katika Azimio Na. 11, kwamba “Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Mwaka 1995 (The Public Leadership Code of Ethics Act), ifanyiwe marekebisho makubwa ili kudhibiti utaratibu unaoonekana wa kawaida sasa wa Viongozi Waandamizi wenye dhamana ya kisiasa kuendelea na biashara zao binafsi wakiwa madarakani, jambo ambalo lina mgongano wa kimaslahi. Serikali ianze rasmi maandalizi ya majadiliano ya kina kuhusu suala hili ndani na nje ya Bunge kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali.”

  Bunge lilitaarifiwa Februari 2010 kuhusu utekelezaji wa Serikali kwamba kikundi kazi (Task Force) kiliundwa ambacho kiliandaa waraka wenye mapendekezo ya kurekebisha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, (Sura 398) ambao ulikuwa katika ngazi ya kujadiliwa na Kamati ya Makatibu Wakuu (IMTC). Aidha, Bunge lilielezwa kuwa serikali ilitarajia kuwasilisha muswada husika katika mkutano wa kumi na tisa wa Bunge la tisa. Muswada huo haukupitishwa katika Bunge la tisa kama ilivyoshauriwa na kamati na mpaka kutokana na uzembe na udhaifu azimio hilo halijatekelezwa na tuhuma nyingine zimeendelea kuibuka.

  Aidha, kumetolewa madai ya baadhi ya wabunge kupokea ama kudai rushwa suala ambalo nalo Spika wa Bunge ametoa uamuzi kuwa litashughulikiwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge. Lakini Serikali na Uongozi wa Bunge kwa pamoja wamesahau kwamba hii si mara ya kwanza kwa tuhuma za namna hiyo kutolewa juu ya baadhi ya wabunge wa kamati mbalimbali za bunge.

  Hata hivyo, kwa sababu ya kutochukua hatua kwa haraka na kwa ukamilifu tuhuma kama hizo zitaendelea kujirudia hata baada ya kuvunjwa kwa kamati ya bunge ya nishati na madini. Izingatiwe kwamba madai ya rushwa kutolewa kwa wabunge yaliwahi kujitokeza kuhusu Kamati ya Nishati na Madini na binafsi nilitoa ushuhuda kwa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mwaka 2011, na nikatoa ushuhuda tena kwa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza uhalali wa utaratibu wa Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti bungeni mwaka 2011 kuwa yamekuwepo matukio ya kushawishi wabunge kwa rushwa hata hivyo hatua hazikuchukuliwa ama kuvunja kamati zilizotajwa au kuwachukulia hatua wahusika.

  Suala hili likatajwa tena na Mbunge wa Kigoma Kaskazini David Kafulila kuhusu Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa na likatajwa tena na Kiongozi wa Upinzani Freeman Mbowe na Mbunge wa Kyela Dr Harrison Mwakyembe kuhusu uchaguzi wa Afrika Mashariki lakini hatua hazikuchukuliwa kuchunguza wabunge husika na kuchukua hatua. Iwapo maazimio kuhusu uhalali wa utaratibu wa Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti bungeni ya mwaka 2011 (Maarufu kama Sakata la Jairo), yangetekelezwa na wahusika wangechukuliwa hatua ingejenga nidhamu pia kwa watendaji wa wizara na mashirika ya umma kuhusu rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma yenye kulenga kuwaathiri wabunge kwa rushwa na maslahi mengine ya kifedha.

  Katika hali inayoonyeha kwamba Serikali bado haioni uharaka na ulazima wa kuchukua hatua, wakati bunge lilipokaa kama kamati tarehe 28 Julai 2012 kupitisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini nilitaka ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Nishati na Madini kuhusu utekelezaji wa maazimio hayo ambayo mpaka sasa hakuna taarifa ya utekelezaji iliyowasilishwa bungeni toka yapitishwe mwezi Novemba mwaka 2011; lakini Waziri akajibu tu kwamba hawezi kufanyia kazi taarifa za magazetini, bila kujali kwamba nilichouliza hakihusu taarifa za magazetini bali maazimio ya bunge baada ya kazi iliyofanywa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na ikarudiwa tena na Kamati Teule ya Bunge ambayo ilihoji wahusika na kupata pia vielelezo.

  Kwa hiyo, ni muhimu Serikali na Uongozi wa Bunge ukarejea kwenye Hotuba niliyowasilisha bungeni na kuchukua hatua kwa usimamizi wa Rais, Waziri Mkuu na Spika wa Bunge juu ya masuala yote niliyoyaeleza. Pamoja na kutaja ushawishi uliokuwa ukifanywa kwa wabunge kuhusu suala la ununuzi wa mafuta ya IPTL, na ufisadi ndani ya TANESCO nilieleza pia masuala mengine makubwa kwenye nishati na madini yenye kuhusu mabilioni ya shilingi kwenye mikataba mikubwa ya umeme, madini, mafuta na gesi asili pamoja na hatua za mabadiliko ya kimfumo zinazopaswa kuchukuliwa.

  Nimetoa maoni hayaleo jumapili tarehe 29 Julai 2012:


  John Mnyika (Mb)


  Waziri Kivuli wa Nishati na Madini

  nawakilisha!!!
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  funguka jembe.
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Tamko kabambe kabisa
   
 4. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Laiti wahusika wangechukua hadhari au kujifunza chochote. Kwa nijuavyo, bunge letu halina tofauti na serikali yake wala chama. Wengi wa wabunge wetu wanawakilisha matumbo yao. Spika mwenyewe alipachikwa pale na mafisadi ukiachia mbali naibu wake ambaye juzi alitoa kituko kuwa yeye ni chimbuchimbu asiyejua hata idadi ya watoto aliozalisha. Rais kaingia kwa pesa ya EPA unategemea nini.
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  It is bound to happen over and over again, unless we; the people decides to put a stop to this. Its like dating your ex, you know all his/her moves and what to expect next.
   
 6. k

  kijiichake JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ee Mungu nalia mbele yako, Taifa langu Tanzania kila kukuchapo leo afadhali na jana. Taifa langu hii limekuwa kiwanja cha mpira wa wahuni hakuna jipya humu nimiendelezo ya kutufilisi. Ifike wakatati Ee Mungu wetu ututete na kuwalipizia kisasi wale wanaofanya ufedhuli huu. Uyafute majina yao katika vitabu vyako vya rehema na kuyaandika majina yao, katika vitabu vya hukumu ya jehanum wasione raha wao wala watoto wao. Uwalipizie mara elfu matendo yao maovu juu ya Taifa hii. Tumelia hawakuona huruma, tumeteta hawakusikia wala kututizama, Taifa limevamiwa na viwavi jeshi, kila kitu kinatafunwa, hakuna vinavyo sazwa hata kwa ajili ya vizazi vijavyo, Ee Mungu tukomboe macho yetu tunayaelekeza kwako.
   
 7. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Jembe asilia hili.
   
 8. l

  lovagirl22 New Member

  #8
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna jipya humu nimiendelezo ya kutufilisi. Ifike wakatati Ee Mungu wetu ututete na kuwalipizia kisasi wale wanaofanya ufedhuli huu. Uyafute majina yao katika vitabu vyako vya rehema na kuyaandika majina yao, katika vitabu vya hukumu ya jehanum wasione raha wao wala watoto wao. Uwalipizie mara elfu matendo yao maovu juu ya Taifa hii. Tumelia hawakuona huruma, tumeteta hawakusikia wala kututizama, Taifa limevamiwa na viwavi jeshi, kila kitu kinatafunwa, hakuna vinavyo sazwa hata kwa ajili ya vizazi vijavyo, Ee Mungu tukomboe macho yetu tunayaelekeza kwako.
   
 9. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Bwana Mdogo Mnyika umeshasema uamuzi wa Bi kiroboto ni sahihi na hiyo inatosha haina haja ya kueleza sana. Chadema sisi ni wepesi wa kuchanganua na kupambanua mambo. Yuko wapi January Makamba? kelele zake kumbe alikuwa anamuwinda Msukuma wa sengerema
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  mbunge wangu umefunguka sawia kabisa, mambo mengi yamepita hakuna hatua zimechukuliwa!
   
 11. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mnyika umetoa maoni ambayo ni too general, be specific please !
   
 12. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tusaidie sisi pamoja na Mnyika, kipi ambacho ulitaka aseme hajasema au kipi amesema hukutaka aseme?
   
 13. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #13
  Jul 30, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  QUOTE=Mpungati;4337911]Mnyika umetoa maoni ambayo ni too general, be specific please ![/QUOTE] Mkuu ni kweli wewe Punga!
   
 14. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Ahsante jembe langu Mnyika.

  HONGERA KATIBU MKUU WA MTARAJIWA WA CHAMA BAADA YA DR. SLAA.

  Peoples............................!
   
 15. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #15
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Suluhisho ni wabunge kuacha kuomba na kuchukua Rushwa. Wajitakase na kujitoharisha, vinginevyo utukufu wa Bunge uko mashakani.
   
 16. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #16
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,636
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Mwongozo,Mkuu ili kuweka kumbukumbu zetu vizuri ktk hansard za JF juu ya maoni husika, tafadhali sahihisha hapo kwenye rangi nyekundu.
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Anarukia hoja, alikuwa asisema mwanzo yote hayo?

  Huu ndio uzembe wa chadema wa hali ya juu, wenzao wakishafanya kweli wao ndio wanawahi kurukia hoja. Acheni mchezo wa kitoto huo. Na mijitu eti inashangilia.
   
 18. A

  Asa79 JF-Expert Member

  #18
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 591
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bora umefunguka mapema kwani vijana walidhani nawewe ni mnufaika umewasaliti watz km mnafiki zitto....
  Go jembe mungu naona kaamua kuwafunulia watz uozo wote
   
 19. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #19
  Jul 30, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180

  Du! Kweli wewe ni CHADEMA mzuri! Kwa hiyo January Makamba alikuwa CHADEMA au siyo, alikuwa mahiri wa kuchanganua na kupambanua mambo lakini leo yuko wapi (ndiyo kawaida ya CHADEMA si ndiyo?),

  Watu watakushangaa hapa kama wewe ulikuwa hujui mawindo hayo, ingawa pia aliyekuwa akiwindwa naye alistahili kuwindwa, maana hakuwa msafi!
   
 20. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mkubwa wa kunishangaa hapa hayupo. January alijisingizia kwamba anapigana na ufisadi na akajifanya yuko imara kumbe ni kibaka tu. CCM ni kizazi cha joka wanarithishana sumu tu. Ni utwana tu kwenye system yenu. Chama cha wanafamilia. unakuta mama mtoto baba wajukuu wote wana wadhifa ndani ya magamba.
   
Loading...