Maoni ya Joel Kimbisa juu ya Dr. W. Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni ya Joel Kimbisa juu ya Dr. W. Slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nsololi, Sep 1, 2010.

 1. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2010
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Joel Kimbisa
  2010-09-01


  Mtanzania yeyote Mzalendo wa kweli, mwenye akili timamu, asiye na mtindio wa ubongo, wala mtumwa wa hila chafu, wala udumavu wa kiakili, tena asiye na utando wa buibui wala tongotongo za ufisadi machoni, wala asiye mzembe wa kufikiri, anaalikwa asome kwa uangalifu na azingatie makala hii na awashirikishe ndugu, jamaa na marafiki zake popote pale walipo..

  Dr Slaa yes we can! Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo.
  Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.

  Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupungzwa kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!

  Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendeleee kuwa watumwa ni nini?

  Ni Dr. Slaa anayeongelea treni ya umeme kwenda Kigoma, Dodoma, Tabora, na Mwanza. Waulize mpango wao ccm kama si kuwapa wahindi wanaoleta mabehewa ambayo mababu zetu walitumia wakati wa ukoloni. Sasa wahindi wanabaki kutudanganya na bajaji wakati vyuma chakavu vya reli sasa vinatumika kujenga vyoo. Hawa hawatutakii mema. Hawana tofauti na akina Carl Peters.

  Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu ya maisha yao. Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..

  Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi 350.000 achana na CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao.

  Ni Dr.Slaa anayeweza kusimamia mashirika ya umma kuleta tija achana na CCM wanaofyonza michango yetu kule, kwani haya mashirika yameshindwa nini kuwajengea nyumba wanachama wake? Mbona kwingine yameweza? Ni Dr.Slaa anayeweza kuongoza nchi bila woga, kwa utawala wa kweli wa sheria bila kuwaonea watu wala bila kulipiza visasi.

  Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi? Naomba niwape heko ITV kwa kuturejeshe kwenye hotuba za mwalimu. Katika hotuba yake moja alisema waziri mmoja kule uingereza aliandikwa kidogo tu gazetini juu ya kashfa, yule waziri alijiuzulu na waziri mkuu hata hakumjibu bali aliteua mtu mwingine.

  CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!

  Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Si tumeona mnazi mmoja alivyowataja mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekaa chini? we must be serious! Hivi kweli dunia ya leo watu wanavuliwa nguo njiani kwenda Mwanza, Shinyanaga, Tabora, Kigoma, Mbeya, Lindi na Mtwara kwa sababu ya usafiri wa malori?

  Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu??

  Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi? Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?

  Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito, maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini tuko maskini wa kutupwa! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania.

  Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi, inawezakana na nafasi ni hii tuitumie.

  Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi wote na atuwekee katiba sawa. Huo ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi. CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio waendelee kututawala na kutunyonya.

  Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi. Peleke ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Peleka ujumbe huu haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela..
   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Hivi 2005 Kikwete aliahidi nini vile? Tukumbushane
   
 3. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Aliahidi maisha bora kwa kila mtanzania
   
 4. Safina

  Safina JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2010
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 498
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kitu kinachonichosha sana katika hizi siasa chafu za nchi yetu ni kwamba, ukipita barabarani kila mtu anamsema Dr. Slaa, Dr. Slaa, lakini cha kushangaza mwisho wa siku ccm wataibuka washindi, hivi hii imekaaje zaidi jamani? ningekuwa na uwezo wa kumulika kila mahali siku ya uchaguzi hili niweze kujua kama kweli ccm huwa inashinda kwa haki au ni changa la macho, kwa sababu mimi mwenzenu sielewi kabisa yaani niko karibu na kuchanganyikiwa kuhusu haya mambo yanayoendelea hapa Tanzania, kura yangu ya urais ni Dk. Slaa na ubunge ni Lema.
   
 5. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  la msingi ni kuhakikisha kila anayestahili kupiga kura akapige siku hiyo bila kukosa
   
 6. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Chadema wakaze sana buti kwenye kulinda masanduku ya kura mwaka huu kama wanataka kieleweke.
   
 7. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Sasa kama mahitaji yote anayohitaji binadamu bila kusahau maeneo ya burudani na starehe kama vinapatikana unataka Raisi afanye nini? Iliyobaki ni kila mmoja kufanya kazi kwa bidii sehemu aliyo kama ni mwajiriwa au mkulima ili kuweza kumudu kugharamia hayo maisha bora. Usilale ungoje SOSEJI, Sukari na Mikate iletwe mlangoni kwako ndiposa uyaone hayo maisha bora
   
 8. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mleta mada asante kwa kutukumbusha. Cha msingi ni kuhamasisha wapiga kura wafanye kweli, hebu anza na ndugu zako na marafiki wabadilishe mawazo yao. Then nasisitiza tena kuwa Chadema wekeni mawakala ambao hawahongeki, i.e ombeni hata ikiwezekana watu wajitolee ambao si rahisi kuhongeka. Naamini hamtakosa, kila mgombea ajizatiti kabisa kuhakikisha wakala ni mpingo usioliwa na mchwa!! Nafikiri mnanielewa.
   
 9. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  keleuwii!!

  ukisoma hapa utafikiri slaa kesha shinda uchaguzi. hapa moshi nasikia wale wafanyibishara wanazunguka na picha za ccm kwenye magari yao, mioyo yao ni chadema. kuna mmoja kanionyesha kadi ya ccm aliyokatiwa na ccm akiwa hayupo kabisa moshi. sasa uzi ni ule ule kikwete na ccm wapumzike,

  tufunge, tusali na kusonga mbele ccm byeeeeeeeeee
   
 10. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Asante mkuu. Nimeshatuma ujumbe huu kwa e mail kwa contacts wangu wote waliopo kwente e mail na kuwaomba wasambaze ujumbe huo ikiwezekana kwa e mail, sms au hata kwa mdomo. Ujumbe huu lazima umfikie kila Mtanzania, hauna matusi wala kbehi bali ukweli mtupu.
   
 11. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tumekupata mkuu na upo sawa
  Dr. Slaa ni shujaa
   
 12. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #12
  Sep 1, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mimi na familia yangu tumeanza mfungo rasmi wa kumuomba Mungu atupe kiongozi bora atakayeonyesha njia ya ukombozi wa taifa letu kutoka kwenye makucha ya mafisadi wanaohamisha utajiri wetu na kutuacha masikini sisi na vizazi vyetu vijavyo. Naamini Mungu atasikia kilio chetu na kutuletea mkombozi wa kweli.
   
 13. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2010
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kusema kweli Dr. Slaa anatajwa vema kila mtaa. Unajua, mwaka 1995 CCM chini ya Mkapa ilishinda kwa sababu upinzani ulikuwa haufahamiki. Na watu wengi walikuwa wanajua CCM ndicho chama tu pekee hasa vijijini. Mwaka 2000, Mkapa alishinda kwa sababu kusema kweli alifanya mazuri kipindi cha kwanza cha uongozi wake. Mwaka 2005, watu walitegemea mengi kutoka kwa JK ndio mana akashinda tena kwa kishindo. Mwaka 2010 tumegundua janja ya hawa CCM. Kwa hiyo, upinzani hasa ukikaa sawa mwaka huu unaweza ukashinda. Ila kusema kweli nilitamani Dr. Harison Mwakyembe angekuwa upande wa upinzani. Unajua mwelekeo wa upinzani Tanzania ni mzuri sasa. Kitendo cha Zitto Kabwe kushinda Kigoma vijijini, inaonyesha dhahiri kuwa upinzani unapata kueleweka hata vijijini.
   
 14. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Message sent

  Watanzania amkeni
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Sep 1, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,183
  Trophy Points: 280
  Political fanaticism without substantive input. Huu si muda wa propaganda and political farts, ni muda wa facts.

  Tunajua CCM imeoza, tuambie tena, bila kutumia propaganda zitakazo kulenga hisia zaidi ya akili, Dr. Slaa ana uwezo gani kimsingi? Hiyo piece hapo juu imejaa more holes than Swiss cheese.

  Nyerere alichukia ufisadi kwa vitendo? Nyerere siye huyu aliyekuwa anahamisha mafisadi kutoka sehemu moja kuwapeleka nyingine hata baada ya kupewa ushahidi tosha? Nyerere alifavor free education Chuo Kikuu? Hivi umeisikiliza hotuba ya Mei Mosi Mbeya 1995 kuhusu his views on that?

  Na hapo ni mwanzo tu, ukiendelea unakutana na utumbo kama huo paragraph after paragraph. Mpinzani wa kweli Tanzania ni yule anayeweza kupinga hata siasa za Nyerere. Ukishaingia katika hero worship ya Nyerere tu upinzani wako unatiliwa shaka kwa kuwa superficial.

  The piece, I am afraid, is long on rhetoric and short on facts. A mile wide and not even an inch deep.
   
 16. m

  mozze Senior Member

  #16
  Sep 2, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ingewezekana waraka huu uchapishwe na kusambazwa. Kila mmoja anayetamani kuona mabadilikoa autoe chapa huu waraka (angalau 50copies) na kuwagawia watu wasio na access ya computers, huko vijijini na sehemu nyingine. Ni wajibu wetu kama kweli tunataka mageuzi badala ya kumwachia Dr. Slaa mwenyewe au chama chake. Tuchue wajibu huu...kwa kuanzia mimi ntaprinti 20 pages leo!
   
 17. MKANDYA

  MKANDYA Senior Member

  #17
  Sep 2, 2010
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ahsante sana mtoa mada; hii itasaidia ikiwekwa kama vipeperushi isambazwe nchi nzima,kwani itachochea hamasa ya wapiga kura.
   
 18. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #18
  Sep 2, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  Alihahidi na mengine nafikiri hayakumbuki soma kwenye viambatanisho hiki.
   

  Attached Files:

 19. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #19
  Sep 2, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Amaaaa! Kwani tayari Kabwe keshashinda hata kabla ya uchaguzi? Bila kupingwa au?
   
 20. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #20
  Sep 2, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Watnzania mkimchagua kikwete, mtakuwa mmetia saini ya kuizika Tanzania Rasmi!
  Kutaka kujua wananchi wa Tanzania walivyochoshwa na system hii na wanakwenda kwenye kampeni za CCM kwa kuhongwa hebu cheki gazeti la mwananchi picha ya mbele kudadadeki....!
  Miaka mitano mingine ya CCM, kutakuwa na nchi tena?
   
Loading...