Maoni ya Director General wa WHO kuhusu lockdown kwa nchi masikini kama Tanzania

carcinoma

JF-Expert Member
Mar 5, 2017
5,059
13,718
Habari za mida hii wakuu.
Kufuatana na janga hili la ugonjwa wa COVID 19 unaosababishwa na kirusi cha corona,
Kumekuwa na mjadala kuhusu lockdown ya nchi nzima ambapo baadhi ya watu wanamtaka Rais wa nchi aidhinishe total lockdown.
Na wengine wakitaka hali iwe hivi hivi ilivyo.

Ninadeclear interest kwamba mimi ni mmoja wa watu ambao hawaungi mkono jambo la total lockdown sababu ikiwa ni kwamba nchi kama yetu ambapo kipato cha watu wengi kinategemea kufanya kazi kula siku ndio wapate ridhiki zao.. sasa ukifanya total lockdown kuna watu watu watakufa kwa njaa.

DG wa WHO amesema ili kufanya lockdown inabidi upime uzito wa athari za watu kukaa ndani na kutoka nje..

Chini hapa ni screenshot ya press ya DG wa WHO ambapo ameongelea kuhusu lockdown kwa developing countries
Screenshot_20200413-205224.png
Screenshot_20200413-205048.png


Nini maoni yako..

#carcinoma01
 
Lockdown is the best way of controlling Corona. Lakini kwa hapa kwetu total lockdown ni shida kwa kweli kwa sababu ya umaskini na hata serikali siamino kama itaweda kumudu kulisha familia zote maskini zikiwa lockdown all in all tuombe mungu balaa hili liishe

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa.. pia na busara za polisi wetu nina mashaka nazo sana.. unaweza kukuta baada ya week moja watu waliokufa kisa polisi sababu ya lockdown ni wengi zaidi wa waliouawa na corona
 
Lockdown hats mimi siungi mkono ila kwa hali inavyokwenda na uzembe wa watanzania tutajilock tu wenyewe ntaona hakuna watu waoga kama watanzania au binadamu kwa ujumbe
Kweli itafikia kipindi watu watapungua mtaani wenyewe.. lakini baadhi ya watu watafuta msosi wa kila siku lazima wataonekana mtaani tu.
 
carcinoma,
Dunia nzima HAKUNA. Narudia tena HAKUNA anaependa LOCKDOWN.

Ila wamelazimishwa na HALI ILIVYO TETE.

Hata hapa kwetu huu UBISHI wa kuanza kujadiliana kuhusu kuwepo na LOCKDOWN au ISIWEPO ni MBWEMBWE tu za UZIMA kwa kuwa ZAGA haijachanganyia.

Siku wakianza kukata MOTO watu 2000 kwa siku huku NEW CASES zikiwa 3000 kwa siku. Hapo hakutakuwa na MJADALA TENA wala MABISHANO.

Hata Trump anatamani watu warudi kazini hata sasa ila ndio hivyo HALI TETE, Hairuhusu. Tena alitamani wamarekani warudi kazini kabla ya PASAKA ila imeshindikana, amebaki tu kuwa MOTIVATIONALA SPEAKER Twitter maana mafanikio yake yote ya miaka 4 ( JOBS +STOCKS MARKET ) yameliwa na COVID-19.

Refer: Trump, despite virus warnings, wants US back at work by April 12
 
Mkaruka,

Hivi mkuu mfano wale jamaa daywaka anaeamka asubuhi hana kitu.anaingia kariakoo anapiga mishe akipata elf 3 ndio anakula ..hizi wale watu wanaweza kukaa hata siku 5 ndani? Hata kama ukiweka vifari nje??
 
Hivi mkuu mfano wale jamaa daywaka anaeamka asubuhi hana kitu.anaingia kariakoo anapiga mishe akipata elf 3 ndio anakula ..hizi wale watu wanaweza kukaa hata siku 5 ndani? Hata kama ukiweka vifari nje??
Mkuu hali ikiwa tete, unafikiri kutakuwa na mabishano tena. Kwanza hata ukienda kariakoo huko utamkuta nani wa kumuuzia mzee ?

Mpaka sa sa walimu wa dayworker, makonda, wapiga debe , watu wengi wa stationery ni kama hawana kazi mzee.

Hali imekuwa ngumu sana.

Ingawa hakuna LOCKDOWN lakini ukiangalia ni kama watu wamepungua sana barabarani, unadhani ni kwanini ?
 
Tanzania ilivyo kataa lockdown nchi zingine zilisema sisi WAKAIDI, leo hii wameona nani alikuwa sahihi.

Sehemu ambazo watanzania wanakutana na kuchanganyika na raia wengi wa mataifa ya mbali ni Zanzibar, Dar, Kilimanjaro, Arusha na Mwanza. Ni rahisi kudhibiti hayo maeneo na kuhakikisha raia wengine wanajikinga kwa kuwa wasafi, kuvaa mask na kuzuia mikusanyiko.
 
Tanzania ilivyo kataa lockdown nchi zingine zilisema sisi WAKAIDI, leo hii wameona nani alikuwa sahihi.

Sehemu ambazo watanzania wanakutana na kuchanganyika na raia wengi wa mataifa ya mbali ni Zanzibar, Dar, Kilimanjaro, Arusha na Mwanza. Ni rahisi kudhibiti hayo maeneo na kuhakikisha raia wengine wanajikinga kwa kuwa wasafi, kuvaa mask na kuzuia mikusanyiko.
Kweli kabisa.
 
Uzuri wa hilo gonjwa huwa haliangalii nani ni nani. Linaua wote, rais, waziri, mlalahoi nk.

Viongozi ni zaidi kwa vile wana umri mkubwa, na wengine wana vibetri kwenye moyo.

Hivi punde watajua umuhimu wa lockdown, mara yatakapowafika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uhai ni bora zaidi Kwa maslahi ya maendeleo ya nchi lockdown ni muhimu Kwa nchi yetu hakùna atakae kufa njaa Kwa mwezi mmoja hata miwili na hapo gojwa litayeyuka lenyewe maisha yataendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chanjo nyingi sana za ugonjwa huu zinafanyiwa majaribio.. Hopefully mpaka kufikia June kinga itakuwa imepatikana.. Tuzidi kujikinga tuu kwa kufuata muongozo kutoka wizara ya afya pamoja na wataalamu wa afya.. Asubuhi ya leo Nimesoma sehemu flani wanasema Kuna chanjo zaidi ya 70 zimeshatengenezwa na 3 Kati ya hizo zimeanza kufanyiwa majaribio kwa binadamu.. Hivyo tumuombe mwenyezi mungu awape nguvu na mwangaza wataalamu wote wanaohangaika usiku na mchana kutafuta hii chanjo ili dunia irejee kwenye Hali yake ya kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom