Maoni: Wazee wote nchi nzima waanze kulipwa pension umri kuanzia miaka 55

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
948
1,092
Habari Tanzania !

Naomba kuuliza; Je, ni lini sasa tutatunga sheria na kufanya maamuzi ya kuwalipa wazee wote kuanzia umri miaka 55 pension ya uzee mpaka umauti wao? Ili iwe utamaduni na mfumo wetu rasmi wa maisha Tanzania.

Sababu kuu: Hawa wazee kwa umri wao wamechangia sana pato la taifa, wamechochea maendeleo makubwa haya tuliyonayo na tunayoendelea kuyapata(kadri umri unavyozidi kuongezeka; ndivyo ulipaji wako wa kodi unaongezeka) kwa kulipa kodi kuu (indirect taxes) kwa njia mbalimbali. Pia kwa kupitia umri huo uwezo wao wa kiutendaji na uzalishaji kwa ujumla ni mdogo sana.

NB

Tuwalinde wazee wa taifa maana wao ndio tunu kuu ya taifa. Wazee ndio chanzo cha amani, heshima na hekima kuu itawaliwayo na busara safi.

Karibu.
 
Labda tujadili kuwaweka kwenye Bima ya Afya tena iwe ni kuanzia miaka 60..
 
Pole kwa umri wako kosonga mbele na kukaribia 55 na haujajipanga. Miaka 55 uanze kulipwa
Tumia akili yako vizuri
 
Hata nchi tajiri hawalipi kwa umri huo, acha uvivu kapige kazi mpaka 70 yrs ndio uanze kulalamika
1. Utaacha lini kujidharau kifikra?

2. Nchi ikiamua namna bora ya ketengeneza mfumo wake wa maisha nani anazuia?

3. Acha kupenda ukoloni mambo leo?

Mwisho

Mawazo uliyonayo ni utumwa kabisa na ushamba hapa duniani.
 
Pole kwa umri wako kosonga mbele na kukaribia 55 na haujajipanga. Miaka 55 uanze kulipwa
Tumia akili yako vizuri
Wewe ndio hujitambui na huenda akili yako iko kwenye shida.

Nakushangaa sana kukuona namna ulivyokuwa kipofu. Huo umri niliotaja ndio umri sahihi (wazee) kwa mujibu wa sheria zetu.

Mbona kuna mifumo yakufanana yenye lengo la kukuza na kuboresha maisha ya Tanzania mfano TASAF. Sasa kinashindikana kipi kuanzisha Pension kwa wazee wetu wote kwa umri tajwa.
 
Labda tujadili kuwaweka kwenye Bima ya Afya tena iwe ni kuanzia miaka 60..
Brother sio bima tu yaani walipwe kabisa mafao ya kulitumia taifa la Tanzania.

Pawepo kabisa na taasisi ya kuhudumia wazee kwa mambo yote kwa kujiwekea sheria na utamaduni wa milele kwa wazee.
 
matibabu kwao bure ni mtihani ulioshindikana.!

hiyo pension itawezekanaje?
Usihofu, hapa ni platform nzuri. Hili wazo litawezekana sana endapo mamlaka na serikali wakiamua sasa kwa kuchukua hatua.

Wazee wote wapewe haki ndani ya Taifa la Tanzania popote walipo aidha kijijini au mjini. Yaani walipwe mafao yao ya kulitumikia taifa iwe ni lazima na uwe ndio utamaduni wetu milele.
 
Lisu akiwa rais itawezekana kweupe

but,kwa hawa fisiemu ni never
 
Kwa nature ya watanzania tutaongeza kundi la watu wavivu na wasio wachapakazi

Jitu linakaa kizembe zembe linasubiri lifikishe 55 lianze kulipwa hiyo haiwezekani, walau ungeongelea kuanzia miaka 70

Mimi mzee wangu ana miaka 76 na ana mtoto wake (mdogo wetu) ana miaka 9 sasa mtu kama huyu alipokua kwenye 55 kumuita mzee si ni sawa na kumtukana.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Tujifunze kutunza wazee. Huo ni wajibu wa serikali na mamlaka zake zote na sio familia ambazo wazee watokazo.

Ndio maana napendekeza wazee wote kuwa wanastahili kutunzwa na Jamuhuri kwa njia zote. Nchi hii ndio wao wameifanya kupata maenendeleo tuliyonayo.

Kwa kupitia wazo hili litachochea vijana wa sasa kufanya kazi kwa bidii bila hofu ya uzee sababu serikali itawahudumia kwa pension na bima uzeeni kwa miaka tajwa.
 
Nakuunga mkono mkuu. Miaka 55 ni umri wa kufikiria kuoa mke wa mwisho wa kukuchangamsha na siyo kuwaza kulipwa na serikali
 
Tujifunze kutunza wazee. Huo ni wajibu wa serikali na mamlaka zake zote na sio familia ambazo wazee watokazo.

Ndio maana napendekeza wazee wote kuwa wanastahili kutunzwa na Jamuhuri kwa njia zote. Nchi hii ndio wao wameifanya kupata maenendeleo tuliyonayo.

Kwa kupitia wazo hili litachochea vijana wa sasa kufanya kazi kwa bidii bila hofu ya uzee sababu serikali itawahudumia kwa pension na bima uzeeni kwa miaka tajwa.
Naungana na wewe mkuu ila sio wazee wa miaka 55 huyo bado ananguvu za kujihudumia walau hata ungesema 65 ungeeleweka hoja yako.
 
Habari Tanzania !

Naomba kuuliza; Je, ni lini sasa tutatunga sheria na kufanya maamuzi ya kuwalipa wazee wote kuanzia umri miaka 55 pension ya uzee mpaka umauti wao? Ili iwe utamaduni na mfumo wetu rasmi wa maisha Tanzania.

Sababu kuu: Hawa wazee kwa umri wao wamechangia sana pato la taifa, wamechochea maendeleo makubwa haya tuliyonayo na tunayoendelea kuyapata(kadri umri unavyozidi kuongezeka; ndivyo ulipaji wako wa kodi unaongezeka) kwa kulipa kodi kuu (indirect taxes) kwa njia mbalimbali. Pia kwa kupitia umri huo uwezo wao wa kiutendaji na uzalishaji kwa ujumla ni mdogo sana.

NB

Tuwalinde wazee wa taifa maana wao ndio tunu kuu ya taifa. Wazee ndio chanzo cha amani, heshima na hekima kuu itawaliwayo na busara safi.

Karibu.
Safi Sana mkuu bonge la wazo ingawa Kuna bwege mmoja mvivu wakufkl anajalbu kukupnga eti ata nchi zilzo endelea wanaainzia70.Anasahau life span yetu nindogo kulko hao wenzetu.kwangu mm napendekeza walau kuanzia60.Afu me pia nlitaman Sana watoto chini yamiaka7 na wazee,wajawazito wangepewa bima yaafya yabule.Kulingana naidadi yawazee mi sizani Kama hili linashndkana lakn Hawa viongozi wetu nihewa wao mawazo Kama Aya hawana.wanawaza tu kununua ndege nakujenga flying over wakati wanachi wao wanateseka
 
Habari Tanzania !

Naomba kuuliza; Je, ni lini sasa tutatunga sheria na kufanya maamuzi ya kuwalipa wazee wote kuanzia umri miaka 55 pension ya uzee mpaka umauti wao? Ili iwe utamaduni na mfumo wetu rasmi wa maisha Tanzania.

Sababu kuu: Hawa wazee kwa umri wao wamechangia sana pato la taifa, wamechochea maendeleo makubwa haya tuliyonayo na tunayoendelea kuyapata(kadri umri unavyozidi kuongezeka; ndivyo ulipaji wako wa kodi unaongezeka) kwa kulipa kodi kuu (indirect taxes) kwa njia mbalimbali. Pia kwa kupitia umri huo uwezo wao wa kiutendaji na uzalishaji kwa ujumla ni mdogo sana.

NB

Tuwalinde wazee wa taifa maana wao ndio tunu kuu ya taifa. Wazee ndio chanzo cha amani, heshima na hekima kuu itawaliwayo na busara safi.

Karibu.
Lakini kwa kikokotoo kipi?
 
Lakini kwa kikokotoo kipi?
Haahaa hii haina uhusiano na utumishi brother inahusisha wazee wote waliojiajiri na walioajiriwa; kwa ufupi watu wote wenye umri huo 55 Jamuhuri tuanze kuwalea kwa upendo.

Yaani nchi nzima wazee wa kuanzia umri huo wawe registered kwenye mfumo wa pension na bima tuwalee wazee aisee.
 
Back
Top Bottom