Status
Not open for further replies.
Nyota huwakilisha nguvu ya Taifa hivyo kuwa na nyota mbili ktk bendera ni kuwakilisha nguvu ya nchi Bara na visiwani.Pia tutatoa ajira kwa wabunifu kushauri ziwekwe pembe ipi,na ziwe za rangi ipi.

Mbili na mwisho,nitamuomba kama Rais na baba wa Watanzania apitie upya barua yangu niliyomtumia mwaka 2018 ikiwa tu watumishi wa Ikulu hawakuimisplace na kutomfikia,nilituma kwa njia ya EMS tokea Kahama,na Posta huwa na reference ya kilakilichotumwa ikiwemo tarehe na mtu aliyetuma.
Rangi ya Bluu imetokana na Rangi ya Bendera ya Zanzibar naona umekosa Kazi ya Kufanya ebu Tafuta Kazi ufanye,chukua haya Jembe ukalime
 
Nyota huwakilisha nguvu ya Taifa hivyo kuwa na nyota mbili ktk bendera ni kuwakilisha nguvu ya nchi Bara na visiwani.Pia tutatoa ajira kwa wabunifu kushauri ziwekwe pembe ipi,na ziwe za rangi ipi.

Mbili na mwisho,nitamuomba kama Rais na baba wa Watanzania apitie upya barua yangu niliyomtumia mwaka 2018 ikiwa tu watumishi wa Ikulu hawakuimisplace na kutomfikia,nilituma kwa njia ya EMS tokea Kahama,na Posta huwa na reference ya kilakilichotumwa ikiwemo tarehe na mtu aliyetuma.
Kwa nini huendi mahakamani, liwe shauri la kikatiba
 
Nyota huwakilisha nguvu ya Taifa hivyo kuwa na nyota mbili ktk bendera ni kuwakilisha nguvu ya nchi Bara na visiwani.Pia tutatoa ajira kwa wabunifu kushauri ziwekwe pembe ipi,na ziwe za rangi ipi.

Mbili na mwisho,nitamuomba kama Rais na baba wa Watanzania apitie upya barua yangu niliyomtumia mwaka 2018 ikiwa tu watumishi wa Ikulu hawakuimisplace na kutomfikia,nilituma kwa njia ya EMS tokea Kahama,na Posta huwa na reference ya kilakilichotumwa ikiwemo tarehe na mtu aliyetuma.
Don Nalimison a.k.a Deogratius Kisandu alianza Kama wewe. Mdogomdogo akajikuta anataka kumuoa Malia Obama, Mara akaanza kuandika kule Facebook kuwa ananyege, serikali isimpangie mwanamke wa kum..... Kufumba na kufumbua, jela miaka mitatu
 
Kwani ndugu unadhani kwanini kila nchi INA Bendera duniani!
Tuweke nyota nyingi nyingi ipendeze kama hii?
flag.jpg
 
Kipindi hiki cha Corona tukitumie vizuri. Tufunge breki tufanye tathmini sahihi ya tulikotoka, tulipo na tunakotaka kuelekea huku tukizingatia dunia inavyobadilishwa na hiki kirusi.
Mambo muhimu sana ya kuzingatia:
1. kuimarisha mifumo ya uongozi ya nchi nzima. Iundwe upya iliyopo inahatarisha maendeleo ya nchi. Kiongozi aliyeko madarakani anaweza kutuongoza tukapiga hatua kumi mbele, anayefuata akaturudisha hatua 7 nyuma. Hatutakaa tufike!
2. Utafiti makini wa ubora wa elimu inayotolewa mashuleni na kwenye vyuo ni muhimu sana ili elimu yetu iwe inaakisi maisha halisi ya mtanzania, mila na desturi zetu, mazingira ya mtanzania, afya ya mtanzania, mahitaji ya mtanzania, hali ya hewa ya nchi na raslimali tulizonazo.
3. Kuboresha zaidi tena zaidi au sana huduma za afya, taifa lisilo na afya haliwezi kusonga mbele. Kama mahospitali yataendelea kujaa wagonjwa kiasi ilivyo sasa korido zimejaa vitanda hiyo sio alama nzuri na huwezi kukataa kwamba sehemu kubwa ya nguvu kazi ya taifa iko hoi.
4. Tuheshimu na tuonyeshe hivyo wazi wazi, kwamba uti wa mgongo wa uchumi wetu ni kilimo, tuwekeze zaidi kwenye kilimo cha kisasa. Tusizalishe vile tunavyokula sisi tuu, bali hata wanavyokula zaidi mataifa mengine. Mkulima wa kitanzzania awe na mahusiano ya moja kwa moja na walaji wa mataifa mengine. Utafiti, Utafiti makini ufanyike.

Nawasilisha
 
Nampongeza Mheshimiwa Rais Magufuli kwa kazi nzuri mpaka sasa kwa kipindi cha miaka mitano sasa.

Kwa kweli mheshimiwa amejitahidi sana katika sehemu nyingi na nyanja mbalimbali. Kuanzia miundombinu mpaka raslimali watu na utendaji serikalini.

Ninaomba sana Mheshimiwa Rais, tupia jicho ubora wa elimu katika shule za serikali. Siku za nyuma kidogo shule hizi zilikuwa bora sana na kimbilio la wengi hasa wanyonge.

Shule kama Iliboru, Mzumbe, Azania, Tambaza, Tabora boys, Tosamaganga, Jangwani, Zanaki na nyinginezo. Shule hizi zilitoa elimu bora, kwa bei nafuu na kwa watanzania wote.

Hivi sasa shule hizi zipo taabani. Najua kuna waziri husika wa elimu, lakini mkuu ikiwezekana tilia mkazo eneo hili. Naamini hakuna jambo linashindikana. Kama ulivyofanya mageuzi ya miundombinu na usafirishaji au hata kule mambo ya hujuma za bwawa la mtera.

Hivi sasa katika elimu, kuna tabaka kubwa sana la elimu. Jambo hilo ambalo huko mbele lina adhari kubwa sana.

Wasaidizi wa Mheshimiwa tusaidieni kufikisha ombi hili kwa Rais wetu mpendwa, najua pengine kuna taratibu zipo tayari juu ya hili basi naomba nikumbushe kwa umuhimu wa kipekee.

Ahsante!
 
Ushauri kwa Mheshimiwa Mwenyekiti CCM Taifa pia akiwa Ndie Raid wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2015-2020 na 2020-2025 inayofuata

Kuusema ukweli asieziona juhudi zako na Uzalendo wako Akajinyongee makamasi .
Niombe kusema kero yangu moja nitamalizia maoni.

1-Chama Cha Mapinduzi ndicho kinachounda Selikali za Mitaa hadi Selikali kuu je huyu Mwenyekiti wa Selikali ya mtaa wa Igombe B alipata wapi ujasiri wa kuwaambia Viongozi wake wa Tawi CCM wavue sare za,CCM waziweke chini?

Alipata wapi udume wakusema ni marufuku kuvaliwa safe za CCM kwenye vikao vyake anavyoitisha?

-Vitendo na kauli hizi ni uhaini dhidi ya Chama Cha Mapinduzi nisawa na kutangaza mapinduzi ama uasi .

Hatua zilizo chukuliwa.

1-Secretariet ya Tawi niliielekeza ifanye kikao na wahusika iwahoji .

2-Bada ya kuwahoji iandae taarifa ya kikao na iwasilishwe kwenye kikao cha Kamati ya Siasa cha Tawi ambacho Mimi ndie Mwenyekiti na taarifa yao ikiwa watakutwa na hatia Secretariat ije na mapendekezo ya hatua gani zichukuliwe .

3-Secretariat ilifanya yote kwa umahili mkubwa naipongeza.

4-Kwa kuwa walikutwa na hatia kwa kukiri Mwenyekiti wa selikali ya mtaa akikiri alisema alifanya hivyo kutokana na ushauri aliopewa na kiongozi wa chadema kwa uchambuzi zaidi hili linamaanisha yuko tayali kufanya uhaini dhidi ya,CCM kwa maslahi ya chadema kibaya zaidi mtu huyu alikuwa Mwenyekiti wa Tawi CCM kwa miaka isiopungua 5 kabla ya kujihudhuru na kugombea umwenyekiti selikali ya mtaa.

5-Maamuzi ya Kamati ya siasa yasipo pinduliwa na marafiki zake walioko Kamati ya siasa kata
adhabu aliopewa nifunzo kwake na wengine wenye nia ya kufanya makosa yanayo weza kutafsiriwa kuwa ni uhaini.

Na aliewatukana viongozi wa CCM naye hakuachwa aliopewa adhabu pia.
Ninaomba kanuni za Chama Cha Mapinduzi na nyaraka zingine mhimu ziwe pia zinafika kwenye Matawi yetu .

Ushari kwako Rais
Urais ni taasisi na nimzigo anaejua uzito wa huo mzigo ni Rais mwenyewe.
Bada ya kipindi cha pili cha miaka 5 kufikia ukomo 2025 nikutakie Amani ya Bwana akulinde ukimaliza mda wako Ubaki kuwa Baba Mdogo wa Taifa letu kwa kuwa Baba mkubwa wa Taifa Mwl Julius K Nyerere aliisha tangulia mbere ya haki.

Ni AAJK
Mwanza
Ushauri wangu ajira, watu mwaka wa tano huu tunasugua bench.
 
Ushauri wangu kwa Dr Magufuli ni kwamba: Kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa muda mfupi inamtosha kumpitisha awamu ya pili,inapendeza,But afanye juu chini pia aboreshe Demokrasia nchini,ili ang'are zaidi,wala asiogope mchuano,cha maana ni aendelee kuchapia kazi.

Pia ninamshauri Mheshimiwa Dr Magufuli afuatilie jinsi Waekezaji wanavyo wagandamiza wananchi waliowaajiri,mfano katika kipindi hiki cha Corona wengi wametelekezwa na mikataba haifuatwi na toka enzi hizo wafanyakazi wa sekta binafsi ni yatima mpaka Leo hawana mtetezi.

Pia ninamshauri Dr Magufuli kabla ya kumaliza muda wake[awamu ya 2]ahakikishe ametuachia mfumo mzuri wa mazingira hasa plastic, sheria ndondogo zianzishwe kuzunguka kila nyumba kuanzia mjini mpaka vijijini,But muhimu sana afanye juu- chini kupata machine za ku-recycle ili itengezewe vitu vya kudumu kama madawati n.k.

Pia namshauri Dr Magufuli katika awamu yake pili aanzishe harambee kubwa ya kupanda miti,mfano 2019-20 ulikuwa mwaka mzuri wa kupanda miti,mvua zilikuwa za kutosha.Misitu ya kupandwa ni ile kipindi cha Dr/Mwalimu Nyerere,hivyo ninamuomba afanye ku-boost kwa nguvu zaidi.

Ninamshauri pia Mheshimiwa Magufuli kurusha satellite kwani itatusaidia sana. Japo ana mengi ambayo tungehitaji kutoka kwa Raisi kama huyu,but pia atuachie mwanzo mzuri wa matumizi ya nuclear kwani virutubisho tunavyo.

Pia nashauri mawasiliano ya Barbara na reli ziongezewe jitihada kwani ni muhimu kuwanyanyua wanyonge,infrastructure ya barabara ndiyo kilichowanyanyua nchi nyingi duniani,na pia nchi itafikiwa kirahisi na utalii kwani takriban kila mkoa/wilaya ktk TZ haikosi utalii.

La mwisho kwa Leo ni kwamba moto wa Rushwa na Ufisadi alioanza nao,uliofanya wanyonge na maskini kupumua,unaomfanya akumbukwe daima aongezee moto mkubwa zaidi na Nchi yetu kuwa mfano kuwa Taifa la Mungu, kwani rushwa ni adui wa haki.

Asante
 
Ushauri wangu kwa raisi na serikali Ni muhimu Serikali ikawa Msimamiami wa Sekta binafsi kiliko yenyewe kujiingiza kufanya biashara na kigeuka mshindani kibiashara

Mfano Clearing and Forwarding wanalalamika kwamba Ujio wa Tasac umechukua biashara zote kubwa na zenye pesa za ku clear freight.

Hata hili la TPDC kufungua Petrol gas station zake si sahihi katika uchumi wa kibepari.

Taasisi kama GPSA nayo inafanya Clearing ya mizigo yote ya serikali sasa hapa kutakuwa hakuna maana ya kuwepo sekta binafsi ya clearing and Forwarding.

Hii habari kila kazi za serikali kupewa Suma JKT haileti afya na mzunguko wa pesa kwa sekta binafsi. Kazi za Surveying zote wapewe Ardhi university huu ni Ujamaa na ujamaa duniani kote hata Soviet ulifeli vibaya sana kwa nguvu nyingi.

Ningependa wanasiasa wanpozungumza majukwaani waongelee suala la wages kwa ufasaha na sio percentage. Bila wages kipato kwa wananchi na mzinguko wa pesa kwa wananchi wa kawaida wasiokuwa waajiriwa wa serikali hatuwafikia.

Suala la kuanzishwa Taasisi nyingi halibani matumizi ya fedha za umma bali linanyonya wananchi mfano Tarura, Tanroad, Taesa, Latra, Tasac, ikiwezekana kama ilivyofanyika kwa mifuko ya pensheni hizi taasisi ziunganishwe ili gharama za kuendesha ofisi, masururu, mishahara, magari n.k zielekezwe kwenye miundombinu.


Tunahitaji miundombinu ya kusafirisha maji ya mvua. Hali ya dunia inazidi kubadilika mafuriko ni mambo inabidi tujiandae nayo sasa maeneo mengi ya makazi hayana mifereji mikubwa ya kutosha kusafirisha maji hili lingependeza lingeenda sambamba na ujenzi wa hizi barabara. Mfano eneo kama Mbweni linahitaji mifereji ya kitaalamu ya kupunguza mafuriko sasa hivi kuna ukarabati wa barabara kuu unaendelea lakini mifereji ni kituko bado.
 
Status
Not open for further replies.
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom