Status
Not open for further replies.
Huyu mama nimemkubali sana na sijui kwanini sikuwahi kumsikia kabla ya uchaguzi! Naunga mkono hoja ila natamani ateuliwe kuwa mbunge tuu na asipewe uwaziri maana ndani ya serikali ya ccm anaweza akaonekana tofauti kutokana na mfumo.

Humu jamiiforum kuna vichwa vizuri vingi tu hasa kwenye mambo ya uchumi. Magufuli tumia system yako kuwapata wakusaidie katika kuendesha nchi. These are a hidden resource!
 
Kichwa cha habari chahusika,

Napendekeza mishahara yao ipunguzwe kwa kuwaondolea mambo yafuatayo:

1. Transport allowances, hii ni zaidi ya million 8 ambayo ni posho kwaajili ya kutembelea jimbo, mafuta, nk
2. Mfuko wa jimbo

Hii ni kutokana na mlipuko ulioikumba dunia kwa sasa. Napendekeza hizo posho zikatwe ili zikasaidie hili janga. Hata kama Taifa halijakumbwa sana,na tatizo hili kwa sasa lkn yapo mataifa yanayotuzunguka ambayo kukaa kimya kwao haimaanishi kuwa hawana maambukizi. Nchi kama Zimbabwe zinahitaji msaada mkubwa.

Posho hizi pia zinaweza kukatwa hata kwa maofisa wengine wa juu ambao kimsingi kwa sasa hawasafiri na wako nyumbani wakitekeleza kauli ya "STAY HOME, STAY SAFE"

Ikumbukwe kuwa Tanzania is a DONOR COUNTRY
 
Kati ya wabunge na yeye
Nani ana matumizi ya ovyo ya pesa za umma. Nafurahi siku za karibuni sijasikia ule utoto wa kugawa gawa hela kama pipi akiwa kwenye pilika zake
Kugawa pesa sio utoto ni utu. Unachokipata unakula na wenzako.

Pia ni ishara ya unyenyekevu, kuondoa daraja kati ya wanaoongozwa na anayewaongoza.

Peter Tino ambaye hana kazi na umri unasogea anapopewa milioni tano zikamsaidie huo sio utoto ni ubinadamu.
 
Kugawa pesa sio utoto ni utu. Unachokipata unakula na wenzako.

Pia ni ishara ya unyenyekevu, kuondoa daraja kati ya wanaoongozwa na anayewaongoza.

Peter Tino ambaye hana kazi na umri unasogea anapopewa milioni tano zikamsaidie huo sio utoto ni ubinadamu.
tssssk
 
First Born, Duhhh kweli nimekuelewa mkuu maisha yamekuwa magumu hata ile morali ya kazi hakuna.

Hapa kazi tuu ni kauli mbiu nzuri sana, lakini sasa ni kazigani pasipo kulaa?
Kula ni haki ya kitatiba ndo maana ukigoma kula unachukuliwa hatua
Sawa na mhalifu mwingine


Sent using Jamii Forums mobile app
 
NITANGULIE kuliweka hili vizuri. Rais Magufuli kama Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu, yeye ndiye mshua wa nchi. Ni mshua wetu.

Hapa namaanisha angekuwa baba yangu mzazi. Kama ndiye angekuwa marehemu Alhaj Swaleh Nyambo. Tuanzie hapo.

Najua mshua yupo busy kuihudumia nchi. Basi ningeomba naye kikao baada ya dinner. Tuongee. Nimpe yangu. Nisingesubiri Izzo Business aniimbie "Maloto Ongea na Mshua". Ningetimiza wajibu wangu kama mtoto.

Ningeanza kwa kumwambia mshua wangu, Rais Magufuli, atambue kuwa ulinzi bora wa kiongozi baada ya kutoka madarakani ni kuongoza kwa haki.

Nitamkumbusha kuwa siku Rais Jakaya Kikwete alipomkabidhi ala ya Urais, ndio siku nafasi yake ya kutoa amri ilikoma. Hata yeye akikabidhi ala, atabaki raia wa kawaida. Sanasana ataitwa Rais mstaafu.

Sitaacha kumwambia mshua ajue kuwa Rais mstaafu ni hadhi historia tu. Mbali na kinga ya kutoshitakiwa, ulinzi mbuzi na malipo ya pensheni, hawezi kuagiza au kuzuia chochote kwenye nchi.

Ni heri kuwa mstaafu mwenye rekodi ya kutenda haki, kuliko kuwa mstaafu dhalimu. Wanadamu wana tabia hii; kama hawatolipa kisasi, basi watakusimanga. Vema kuchunga hili!

Kuna mstaafu aliyekuwa na nguvu nchi hii kuliko Mwalimu Nyerere? Mbona alikufa ameshashuhudia yote aliyoyaanzisha yameshabadilishwa? Azimio la Arusha liliuawa Zanzibar. Alifanya nini? Aliishia kulalamika tu.

Mashirika ya umma aliyoyaanzisha na hata kuyastawisha, yaliuzwa akiwa hajafumba macho. NBC ilimliza. Viwanda vilimtoa machozi. Si ni Baba wa Taifa? Lakini hakuwa na nguvu ya kuzuia chochote.

Nitamwambia mshua, Rais Magufuli, atimize wajibu wake, kwa wakati wake. Aufanye uongozi wa nchi kuwa sio matakwa ya mtu, bali taasisi. Tena taasisi imara.

Siku zote uongozi wa mtu mmoja hukoma pale anapoondoka madarakani. Uongozi wa taasisi huendelea hata baada ya kiongozi kuondoka na kufuata mwingine.

Ndoto za kiongozi mwenye kutawala kwa mawazo yake, huyeyuka mara kiongozi husika anapoondoka madarakani. Ndoto zilizochakatwa kitaasisi, huendelea kuishi hata kiongozi anapoondoka.

Ndoto za Mobutu Sese Seko kuufanya mji aliozaliwa wa Gbadolite kuwa wa kibiashara, akajenga uwanja wa ndege wa hadhi ya kimataifa, akashusha malls, supermarkets na ghasia nyingi, ziliyeyuka siku Laurent Kabila na Banyamulenge walipomuondoa madarakani.

Hata ndoto ya Valentine Strasser kuifanya Valentine's Day kuwa sikukuu ya kitaifa Sierra Leone, kwa vile jina lake ni Valentine, ilikoma ile siku naibu wake, Julius Bio alipoongoza uasi wa kijeshi kumpindua.

Sitaacha kumkumbusha mshua wangu kuwa madaraka yana ukomo wake, iwe kwa wito wa Mungu, Katiba au vyovyote. Hayupo wa kutawala milele.

Jambo ambalo ningemwambia kwa mkazo kabisa ni kuhusu chama chake. Vema atambue kuwa vyama ni kama kusanyiko la mafisi wanaotolea macho mzoga. Akili zao zote huwaza uongozi na fursa zitokanazo na uongozi.

Na kwa sababu watu kwenye chama huwaza uongozi na fursa, utakuta kiongozi mwenye mpini amezungukwa na watu ambao ni hodari kunyenyekea, kusema ndio na kusifia. Hutokea kiongozi kujisahau na kuvimba kichwa kwa kudhani watu ambao yupo nao wanamtii na ni waaminifu.

Nitamfahamisha mshua kuwa utii wa watu kwenye vyama huwa wa muda. Ni utii wa mpito. Utii wa kinafiki. Wanamwonesha unyenyekevu kwa sababu ndiye mwenye mpini. Siku mpini ukishikwa na mwingine, ni hapo rangi zao halisi huonekana.

Wengi wanaomnyenyekea leo ni walewale walioimba Dodoma "wana imani na Lowassa". Ni kwa sababu walijua ndiye Rais baada ya Jakaya. Ilipodhirihirika Lowassa hana chake tena, walimtosa. Wengine walimkashifu. Vyama ni kusanyiko la watolea macho uongozi na fursa zitokanazo na uongozi. Akili ikae mahali pake.

Wanaosema nchi imepata Rais jiwe na kumpamba kwa kila neno, ni hao hao walimkweza Jakaya kwa nafasi yake. Wanaosema zama za Maguli si zilizopita, ni haohao walimlamba miguu Jakaya kwa wakati wake. Hivyo, hata yeye akiondoka, atalambwa atakayempisha, halafu yeye si ajabu akazodolewa.

Hata Mwinyi alizodolewa alipoingia Mkapa. Kisha Mkapa alipewa kashfa nyingi alipoingia Jakaya. Mpaka Jakaya akasema mzee Mkapa aachwe apumzike.

Unapokuwa na ufahamu mzuri kuhusu vyama na wanavyama, ukiwa Rais hutapambana kuua vyama vingine ili chama chako kistawi na eti kitawale daima, bali utaongoza kwa haki.

Yalimkuta yapi Bakili Muluzi? Alikipigania chama chake cha UDF, Malawi. Aliposhindwa kubadili Katiba ili asalie madarakani, akapambana UDF iendelee kuongoza dola. Akamrithisha madaraka Bingu wa Mutharika.

Ile siku Muluzi anakabidhi ala ya Urais kwa Bingu, ndio mambo yaligeuka. Muluzi akajikuta anakula msoto, mara mashitaka. Waliokuwa wakimlamba miguu wote walimgeuka. Walihamia kumlamba Bingu.

Muluzi alipotaka kutumia nguvu yake ya chama, Bingu akahama, akaanzisha chama chake, DPP. Vigogo wengi wa UDF waliokuwa wanamlamba miguu Muluzi, walimfuata Bingu DPP.

Yalimkuta yapi Frederick Chiluba? Aliposhindwa kubadili Katiba asalie madarakani Zambia, alihakikisha chama chake, MMD kinashika dola. Na alipambana kumwachia uongozi aliyekuwa mtiifu sana kwake, Levy Mwanawasa.

Siku Chiluba alipomkabidhi Mwanawasa ala ya Urais, ndio siku alianza kula msoto. Akashitakiwa kwa ufisadi, mkewe akafungwa. Wale waliokuwa wakimshangilia zamani, walimshangilia Mwanawasa alipomshughulikia yeye.

Watu wa MMD walimshangilia Chiluba alipomfunga jela Baba wa Taifa la Zambia, Kenneth Kaunda. Kisha haohao wakamshangilia Mwanawasa alipomtoa jela Kaunda na kumpa hadhi ya Baba wa Taifa. Watu wa vyama si wa kuwaamini. Huenda na upepo.

Hayo ndio mambo kuhusu vyama na wanavyama, kama Rais Magufuli angekuwa mshua wangu, ningemwambia ajihadhari na wanaomsifu bila kumkosoa. Yeye si malaika, hawezi kuwa hafanyi makosa. Wanaomsifu bila kumkosoa ni wanafiki wa maisha.

Kuna aliyeipigania CCM kama Mwalimu Nyerere? Mbona mwaka 1995 aliitupa kadi yake ya uanachama na kusema chama hicho si mama yake mzazi?

Kisa tu alitaka jina la mzee John Malecela liondolewe katika wawania Urais. Alipogomewa, akawa hana ubavu zaidi ya kususa.

Ni Malecela kwa kutambua umuhimu wa Mwalimu, aliamua kujitoa, kisha hali ya hewa ikasafishwa. Ningemwambia mshua, kwamba kama Mwalimu Nyerere hakuwa na nguvu zaidi ya kuishia kususa, je yeye akishaondoka?

Huo ni mfano wa kumtaka aheshimu chama chake, lakini atambue nguvu zake kwenye chama ni za kupita. Aheshimu zaidi nchi na atawale kwa haki. Akiondoka, watu wakitaka kumuonea, wananchi watamtetea. Watamuombea.

Nisingeacha kumwambia mshua wangu kuhusu kutegemea jeshi. Lile linaitwa jeshi la wananchi. Duniani kote, wananchi wakishaingia barabarani kwa maelfu, ni hapo jeshi hufanya kazi yake ya kulinda watu.

Kama wanajeshi walivyomgeuka Hosni Mubarak, Misri, ndivyo jeshi lilivyomshinikiza Omar al Bashir kujiuzulu. Jeshi haliwezi kuua watu laki tano wakati lenyewe ni jeshi la watu.

Ulinzi bora zaidi ni kuwaongoza watu vizuri. Dunia haijabadilika kutoka Februari 1917, jeshi lilipowaacha Warusi wamwondoe madarakani Tsar Nicholas II.

Ningemwomba mshua, amtazame Tundu Lissu kwa jicho la haki, alishinikize jeshi la polisi liwasake waliomshambulia.

Kuna mambo ni mabaya na hukaribisha kisasi. Nani anajua kesho? Vipi Tundu Lissu akiwa Rais baada ya mshua?

Fernando Marcos hakudhani angeshindwa uchaguzi kwa nguvu alizokuwa nazo. Hata Robert Guei aliona hakuwepo wa kumtoa. Laurent Gbagbo kadhalika. Walishindwa kwa kura na wananchi waliwatoa.

Ni visasi vya kisiasa vilivyosababisha Guei apigwe risasi hadharani akiwa na mkewe pamoja na watoto wake. Ndicho pia kilimtokea Nicholas II na familia yao.

Ningemwambia mshua kuwa katika uongozi wake aache alama ya haki na huruma hata kwa wapinzani wake. Lissu ni hasimu wake, lakini waliomshambulia ni wanyama. Washughulikiwe.

Ningemkumbusha mshua kuhusu Ben Saanane, Simon Kanguye na Azory Gwanda. Wanahitaji sana sauti yake. Polisi wawatafute na majibu yatoke. Wamekwenda wapi? Mwanafunzi Akwilina Akwilini haki itendeke.

Siasa zina tabia za ajabu. Vijana pendwa wa Rais Magufuli, Paul Makonda au Hamis Kigwangalla, ndio mmoja wao anaweza kumgeuka na kumsumbua endapo atamkabidhi ala ya Urais. Unaweza kustaajabu mwema wa Magufuli akawa Freeman Mbowe au Zitto Kabwe. Siasa hazibetiwi. Odds zake ni tata sana.

Hali ya maisha ilivyo, ningemwambia mshua, Rais Magufuli, kwamba ni vigumu kuiona njaa ukiwa Ikulu, hivyo ni vizuri kuwasikiliza wanaolia maisha magumu mitaani. Siri ya mtungi anaijua kata.

Sema nini? Mungu anajua ampe nani amnyime yupi. Unadhani Rais Magufuli angekuwa mshua wangu ningekuwa na mawazo yote hayo? Sijui angeshanitimua?

Ningekuwa na kashkashi nyingi za kula bata. Mara niwe wakala wa Mbwana Samatta. Halafu ningemshinikiza Diamond atimue mameneja wote ili WCB niimeneji mimi. Hapohapo ningemsimamia Ali Kiba. Ningekuwa na matukio mpaka Miraji Kikwete angenishangaa.

Unadhani Rais Magufuli alivyomkali angeniacha nimchafulie jina ? Angenishanipa kibano.

Vitabu vyangu vitatu; JEHANAMU VIP, ALIMOND na KIKWETE LOWASSA vinatoka mwezi huu. Stay alert.

Ndimi Luqman MALOTO
 
Kila zama na kitabu chake at the ni lzm daladala litasimama kituoni abiria watashuka watapanda wengine.
 
Kwanza naunga mikono juhudi za Mh Rais wetu John Maguli. Yapo mengi mazuri alofanya tangu aingie madarakani, kwa mfano swala la miundombinu, ufisadi, nishati na madini amesimamia kwa weledi mkubwa.Nampongeza sana kwa hilo.
Rai yangu kwa Mh Rais ni juu ya hili janga la CORONAVIRUS (COVID19).
Ninamwomba Mh Rais aiagize wizara ya afya pamoja na mamlaka husika, kununua mashime za kutosha kupima WATANZANIA wote, ili kupata takwimu sahihi za maambukizi na pia kuweza kujua walioambukizwa na ambao hawajaambukizwa ili wale wenye maambukizi watengwe ili wasiendelee kuambuliza wengine.
Pia kuongeza vifaa tiba na kinga ili kupungunguza maambukizi na vifo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninamshuku Mungu kwa uzima aliotupa kwa neema yake, natambua pia hata katika wakati huu ambao dunia inapambana kutafuta ufumbuzi juu ya covid19, Mungu angaliko anajua mahitaji yetu na uwezo wa kutusaidia ungaliko kwake.

Mh. Rais nikupongeze kwa uamuzi uliobora wa kumtafuta Mungu aliyeziumba mbingu na ardhi, kama sehemu ya ufumbuzi kwa changamoto hii ya Covid-19 katika taifa letu.

Ukirejea katika Biblia, utaona chanzo cha matatizo yaliyokuwa yakisababisha watu kuangamia kwa tauni ilikuwa ni kukithiri kwa DHAMBI.

Hivyo watu wamekuwa wakiangamia maelfu kwa maelfu ndani ya muda mfupi tu, ukisoma biblia utaona! Hata sasa covid19 haijafikia changamoto iliyotokea wakati wa Daudi mfalme, ambapo watu 70,000 walikufa ndani ya masaa tu. 2 Samuel 24:15 -16

Tunaona toba ya mfalme na dhabihu/SADAKA aliyotoa mbele za Mungu, ikaiponya nchi ya Israel.

Kuna mawazo mengi unayopewa, na ushauri mwingi pia, ila uamuzi wa toba, ndio uliobora zaidi, hata maelfu wakikubeza, usiteteleke.

Imeandikwa wanaomkimbilia Bwana hawata AIBIKA. Mungu akujaalie kutoaibika.

Mungu ayasikie maombi yetu, aisikie toba yetu, atusamehe maovu yetu na kuiponya nchi yetu.

Mungu akujaalie kuwa MSHINDI mwisho wa KADHIA hii, wanaotamani UAIBIKE waone UKISONGA katika USHINDI MKUU.

Mungu awalinde watanzania wenzangu, Mungu aubariki UTAWALA wako. Ukawe na mwisho mzuri.

Mimi ni mtanzania nisiye mfuasi wa chama chochote cha siasa. Naipenda nchi yangu.

Amani kwako na Watanzania wenzangu.

Ni mimi kijana Mtanzania.

Mtingi1.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom