Status
Not open for further replies.
Namshauri tu akipigwa chini mwaka huu aachie nchi kwa amani na katu asiote kutaka kuongeza muda wa urais, patacimbika na yeye atachimbika
 
Mhe Rais pole na majukumu ya kulijenga taifa letu.Binafsi imani yetu ni kubwa kwako, watanzania wengi wanafuraha kwa upendo wako na ujasiri wako,usioyumba.

Mhe Rais tunaomba ufanye maamuzi magumu ya kupunguza ya kodi ya magari ili watu wengi waingize magari. Magari yakiwa mengi maana yake tutanunua mafuta, tutalipa kodi ya barabara hii itatuwezesha kujenga uchumi wetu bila kukopa kopa.

TRA wamebaki hawana ubunifu.Ulithubutu kodi ya nyumba kupunguzwa ,ulibuni vitambulisho
 
Mimi kinachonishangaza kama Serikali inataka Wananchi wake wasiagize magari makukuu ilichotakiwa ni kuyaongezea kodi kubwa kisha magari mapya yapunguziwe kodi ili Wananchi wamudu lakini TRA inalitoza kodi gari la zamani mara 2 ya bei ya kununulia na ukiagiza la la miaka 2018 nalo kodi yake ni Balaa

Sent using Jamii Forums mobile app
ubunifu hawana TRA
 
Mhe Rais pole na majukumu ya kulijenga taifa letu.Binafsi imani yetu ni kubwa kwako, watanzania wengi wanafuraha kwa upendo wako na ujasiri wako,usioyumba.

Mhe Rais tunaomba ufanye maamuzi magumu ya kupunguza ya kodi ya magari ili watu wengi waingize magari. Magari yakiwa mengi maana yake tutanunua mafuta, tutalipa kodi ya barabara hii itatuwezesha kujenga uchumi wetu bila kukopa kopa.

TRA wamebaki hawana ubunifu.Ulithubutu kodi ya nyumba kupunguzwa ,ulibuni vitambulisho
Jukumu hilo ni la BUNGE wao ndio hutunga SHERIA hizo.. yeye anaweza kushauri tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasalaam
Heshima yako mheshimiwa Sana.
Maneno haya ninayoyaandika hapa ungenipa nafasi hata ya Ana kwa Ana ningekwambia tu, Tena Bila woga.
Ndugu mheshimiwa Rais, naomba nikupongeze Kwanza kwa kazi kubwa unayoifanya, hakika si kazi ndogo inahitajika kuthaminiwa na kuheshimiwa
Ndg Rais, Nina mambo machache ambayo ningependa uyasikie kutoka kwangu

1. Fanikisha miradi uliyoanzisha ndani ya kipindi chako
Ndg Rais, nasisitiza Hilo ulifanyie kazi, tumeshuhudia mara zote miradi mingi inayoanzishwa na kiongozi alieko madarakani asipoyafanikisha kwa kiwango Cha 100% ndo kwisha habari yake. Serikali inaingia kwenye gharama kubwa na mikopo kibao alafu mwisho wa siku miradi hiyo huachwa tu.
Nikupe mfano wa miradi iliyoanzishwa wakati wa Jakaya Kikwete ambayo we huna habari nayo, hususani kwenye Elimu.
(a) Vyumba vya madarasa hasa kwa shule za kata
(b) Maabara za sayansi.

Shule nyingi za sekondari hasa kwa shule za kata zina Hali mbaya, wanafunzi hawatoshi madarasani, walimu hawana ofisi, hakuna madawati, hakuna matundu ya kutosha ya vyoo kwa wanafunzi na walimu, hakuna miundombinu ya maji, hakuna umeme nk

Pia suala la Maabara za sayansi, kwa shule nyingi haya majengo yalianza kujengwa na kufikia hatua ambayo hayawezi kutumika kwa shughuli lengwa, lakini pia gharama nyingi zimetumika na mwisho wa siku yanabaki kuwa magofu tu. Miradi hii umeitupa, Kama Kuna unayoifanyia kazi Basi ni kwa uchache mno, tofauti na nguvu unayotumia kwenye miradi unayoianzisha

2. Boresha maslahi ya watumishi
Hili Jambo ni kilio kikubwa Cha wafanyakazi wa umma Ila naona kabisa Kuna Kila dalili za kufumba macho Kama huoni.
Labda nikukumbushe kwann watumishi wanaomba kuboresha mishahara yao;

i. Tangu umeingia madarakani hujaongeza mishahara hata kwa Senti kumi, yaani miaka zaidi ya minne sasa watu wako pale pale, sasa tukija kwenye uhalisia maisha mitaani yamepanda, Bei ya mchele 2014 sio bei ya mchele huo 2020, sukari imepanda, unga umepanda Bei nk. Sasa Kama mishahara ulokuwa unatosha wakati sukari kg 1 ni Tsh 1200, Leo unatosha vipi wakati kg 1 ya sukari ni 3000?
ii. Taarifa unazowaaminisha wananchi kuwa unaelekeza nguvu kwenye kufufua reli, SGR, hazina msaada mbele ya dhiki. Kujengwa nyumba ya familia hakutafanya watoto nyumbani wasile.
iii. Malimbikizo mnayosema mnayalipa sio kweli, Kuna watumishi wanadai miaka nenda Rudi, ila hakuna kinachoeleweka.
iv. Siku hizi muda wa kupanda madaraja haueleweki, zamani ni miaka mitatu Ila sasa hivi Kuna watu wapo zaidi ya miaka mitano na hawajapanda.
v. Watumishi walipanda madaraja hawabadilishwi mishahara kwa wakati nk.

3. Punguzeni mikwara na vitisho
Hili nalizungumza hususani kwa watumishi wa umma. Nafurahi umerudisha nidhamu ya kazi Ila Kuna mikwara kibao ambayo mengine sasa inafikia hatua ya kuwaondoa watumishi moyo wa kufanya kazi

4. Kuwa balance.
Siku hizi Kila kitu kinaanzishiwa Chato. Hilo sitaki kuliongelea Sana inajulikana.

5. Uhuru wa habari
Ruhusu waandishi wa habari wayaseme na kuandika madudu yaliyopo ili ujue pa kuanzia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
M
Mhe Rais pole na majukumu ya kulijenga taifa letu.Binafsi imani yetu ni kubwa kwako, watanzania wengi wanafuraha kwa upendo wako na ujasiri wako,usioyumba.

Mhe Rais tunaomba ufanye maamuzi magumu ya kupunguza ya kodi ya magari ili watu wengi waingize magari. Magari yakiwa mengi maana yake tutanunua mafuta, tutalipa kodi ya barabara hii itatuwezesha kujenga uchumi wetu bila kukopa kopa.

TRA wamebaki hawana ubunifu.Ulithubutu kodi ya nyumba kupunguzwa ,ulibuni vitambulisho
Mheshimiwa tunaomba siyo magari yote lakini kodi ishushwe ya magari mapya kuanzia mwaka 1-7 hii itasaidia kulinda mazingira yetu.
 
Fact, kitu alichotuaminisha mzungu kuwa sisi si chochote bila wao wakati wao ndio sio chochote bila sisi
Huku africa tumshukuru Mungu saana tuna kila Kitu Na Hao usa Na wenzao hawezi chochote bila sisi africa wamefika walipofika kupitia sisi africa ni tajiri ukiifahamu historian wala hutawasifia wala kuwapongeza mabeberu tujitahidi kuchapa Kazi .

Sent from my iPhone using JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom