Status
Not open for further replies.
Swali ni je,akitoka madarakani hilo genge litadhibitiwaje?
Binafsi nilitokea kukichukia Chama changu Cha Mapinduzi yaani CCM tangia nikiwa sekondari. Chuki zangu dhidi ya CCM sikupandikizwa na mtu bali uelewa na upeo wangu mkubwa wa masuala ya kitaifa.

Nakumbuka nikiwa kidato cha kwanza mpaka namaliza kidato cha Sita nilikuwa na ndoto ya kuwa Rais wa Tanzania siku moja.. najua wengi mnacheka ila nilikuwa serious kabisa, na bado nina ndoto ingawa inafifia ila ya Mungu mengi wenda akaiamsha upya.

Mwaka 2015, binafsi nilikuwa mpinzani mkubwa wa MAGUFURI sababu kubwa ilikuwa nampinga MAGUFURI zi yeye bali kuwa mgombea wa CCM iliyokuwa imechakaa sana na hiaijiwezi tena... Hivyo niliamini MAGUFURI atakuwa kama Marais waliomtangulia ukimuondoa mwl. NYERERE.

Msiojua Tanzania vyema na uelewa wa siasa za Tanzania yetu hamuwezi kujua kuwa tulikuwa tunatawaliwa KIFALME. Namanisha tabaka la watu/familia fulani zilijidhatiti kuhakikisha wanatutawala milele. Ila kwa kuwa MUNGU SI ATHUMANI WALA YOHANA siyo nilichokuwa nakiwaza kinafanywa na MH. RAIS MAGUFURI kwa asilimia kama 95% hivi, licha ya dosari ndogo dogo yeye si malaika.

Hivi Karibuni kulitokea udukuaji wa mawasiliano ya baadhi ya MAKADA WA CCM sitapenda kuzungumzia uhalali wa kudukua mawasiliano ya mtu, wanaojinasibu kuwa wao ndiyo CCM ASILIA, nisikitike kusema kuwa hili ni GENGE moja hatari kabisa lenye malengo mahususi ya kuitawala Tanzania kwa msingi ya koo na urafiki wa kifamilia.

Kama umefuatilia maongezi ya mzee YUSUFU MAKAMBA, JANUARY MAKAMBA NA NAPE NAUYE utakuwa ulionote kitu gani hawa jamaa wanapanga, moja kwanza no dhahiri kuwa wao waliamini Wana Hati na haki miliki ya kudumu na kuitawala Tanzania. Mzee MAKAMBA anasikika akimwelekeza NAPE kuwa baba yake NAPE mzee NAUYE na KINGUNGE NGOMBARE MWIRU eti hajawajatambuliwa mchango wao kwa kepewa majina ya mitaa. Hapo ndipo utajua kuwa kuna koo za kiutawala nchii hii.

Pia ndugu, KAMILIUS MEMBE ukimsikiliza hoja zake utagundua kauli zake anakerwa na kitendo cha MH. Rais MAGUFURI kuteuwa watu pasipo kujali hizo koo za kiutawala na hasa kitendo cha kuzibomoa hizo koo tawala.

Kimsingi naomba kumshukru na kumpongeza MH. Rais MAGUFURI kwa jinsi anavyofanya teuzi zake bila kujali hizi koo tawala. Enzi za NYUMA ilikuwa fhahiri kujua nani anaandaliwa kuwa Rais kitu ambacho ni ujinga kwa taifa la watu wapenda demokrasia ingawa Ina ukakadi bado.

Wapinzani niwashauri kitu, kwasasa hamna MTU MBADALA WA QUALITY ya MAGUFURI kusema mkampanishe, ata CCM hawana huyu MEMBE anashida na urais wala shida wala hashira na shida za watanzania. Mkenge wanaouvaa Wapinzani ni kuacha kuzima nyumba yao inayoungua na kujiunga na koo tawala eti lumpinga MAGUFURI.

Movie nyingine inayochezwa na Wapinzani ni UKANDA na UKABILA, hili nimeliona kanda ya kaskazini hasa ARUSHA na Kilimanjaro turufu ya kumpinga MAGUFURI Iliyobakia ni kupandiza UKABILA na UKANDA hii dhambi ya upanguzi inayofanywa na Wapinzani itawatafuna na imeisha anza uwezi amini Upinzani unakufa slowly kaskazini.

Mimi huwa ni mtafiti mzuri sana, vita dhidi ya MAGUFURI inaongozwa na wachaga ila mjue hizi cheap politics huwa hazidumu ni kama upepo zinapita fasta.

Kitendo cha MH. Rais MAGUFURI kuligeuka hili kunditawala/Kootawala Namuona shujaa na jasiri kabisa.

Nimalize na HEKIMA YA MZEE DR. SLAA" Vijana tunavyotaka mageuzi lazima tu tafakari juu ya AINA YA MAGEUZI TUNAYOTAKA na NJIA SAHIHIHI ZA KUYATAFUTA/KUYAPATA.

ViVa MAGUFURI...2020.
 
Endelea na ndoto yako usijirudishe nyuma.. jiongeze kimaarifa na kifikra utafika.

Magufuli 2020 hiyo haina ubishi.. oyeeeeee
Asante mkuu, ukweli bado ninayo hiyo ndiyo ingawa kimkakati Kuna sehemu nilikosea ila Mungu mkubwa naendelea vyema tuombe uzima..
 
Uchapakazi sio alternative ya kufminya haki demokrasia na uhuru wa habari.., unaweza ukachapa kazi na bado usiminye demokrasia.., labda niulize features za makufuli ambazo unazikubali ni zipi na ambazo hazifai ni zipi na je zote ni package lazima ziende pamoja ?

Kwa yote mazuri aliyofanya kuna mabaya mengi, na kibaya zaidi hayo mabaya yalikuwa hayana ulazima..
 
Tulitaka Rais dicteta tumempata,watu wanalalamika tena wanataka bora yule waliemwita dhaifu arudi kama kungekuwa na uwezekano. Watanzania hatujui tunataka nini.
IMO yaani akitoka huyu aje dictator mwingine zaidi Ya Huyu ili tuendelee kuwa sawa.
Ndio uwezo wako wa kufikiri ulipoishia hapo!?
 
Tulitaka Rais dicteta tumempata,watu wanalalamika tena wanataka bora yule waliemwita dhaifu arudi kama kungekuwa na uwezekano. Watanzania hatujui tunataka nini.
IMO yaani akitoka huyu aje dictator mwingine zaidi Ya Huyu ili tuendelee kuwa sawa.
Kwa hiyo kumbe magufuli ni dictator ?

Mimi kama team lumumba napinga hili sio dictator jamaa kwani sifa za dikteta ni zipi we unazozijua

Mi siamini kami ni dikteta hebu tupe sifa za u dictator hapa
 
Tulitaka Rais dicteta tumempata,watu wanalalamika tena wanataka bora yule waliemwita dhaifu arudi kama kungekuwa na uwezekano. Watanzania hatujui tunataka nini.
IMO yaani akitoka huyu aje dictator mwingine zaidi Ya Huyu ili tuendelee kuwa sawa.
Nyani Ngabu anasema miafrika ndivyo iivyo.

Mimi nasema miafrika haiendi bila ya viboko.
 
Ateyekuja baada ya Magufuli ni mtihani ambao majibu yake tutayapata muda ukifika. Mungu atupe afya.
 
Kapenda jina na hiyo profile picture. Anadhani sura yako ndiyo hiyo. Hajui kuwa huyo ni actress wa Marekani.
Hahahahahah,nimefuatilia yeye opinion yake ni ipi kutokana na thread hapo juu?Sijaona. Yaani kaja moja kwa moja kuniuliza kama huo ndo mwisho wangu wa kufikiri. Nilitegemea ningemsoma hapo juu yeye fikra zake kuhusu maada zilikuwa ni zipi? Nakuta hola.
 
Tulitaka Rais dicteta tumempata,watu wanalalamika tena wanataka bora yule waliemwita dhaifu arudi kama kungekuwa na uwezekano. Watanzania hatujui tunataka nini.
IMO yaani akitoka huyu aje dictator mwingine zaidi Ya Huyu ili tuendelee kuwa sawa.
Mlimtaka wewe na nani?
 
Tulitaka Rais dicteta tumempata,watu wanalalamika tena wanataka bora yule waliemwita dhaifu arudi kama kungekuwa na uwezekano. Watanzania hatujui tunataka nini.
IMO yaani akitoka huyu aje dictator mwingine zaidi Ya Huyu ili tuendelee kuwa sawa.
Binadamu unaishi mara moja tu. Kwanini uishi maisha yasiyokuwa na amabi ? Huku unafikiri wasiyojulikana na huna uhakika Kesha utakuwa mzima siyo kwa rehema ya Mungu la, wanaweza kuwa wanataka kumshoot Lisu mwingine risasi ikakupata wewe. Kumbuka hiyo risasi haichagui uwe wa kusifu na kuabudu au siyo.
Hatukuzoea kuona polisi wanarusha risasi bila mipangilio kama awamu hii. Tulikuwa tunasikia South Africa wakati wa apartheid tunawashangaa wanaishije.
Mungu mwenye huruma tusamehe makosa yetu uturudishie amani tuliyoizoea
 
Status
Not open for further replies.
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom