Status
Not open for further replies.
YAH: kichwa cha habari tajwa hapo juu☝
Wanasema samaki ana mengi na hata siri za kuteta ila......ndio tatizo.
Hebu turudi kwenye mada husika, hivi ikitokea siku ya leo ukakutana uso kwa uso na rais wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshiwa J.P Magufuli je ni swali lipi ungependa kumuuliza!? Au ni jambo lipi ungependa kumwambia!?
#Amoun.
Kwambe ajue hapa Duniani wote ni Wapitaje na Je analijua hilo?
 
Alipokuwa Mwalimu ni kipi kilimkera katika utumishi na baada ya kupata uraia namba moja ameweza kuondoa kero hiyo kwa waalimu na watumishi wa umma kwa ujumla??
 
Dah, kwanza ningemsifu kwa kazi na dhamira safi ya kulikomboa taifa letu Tanzania maana mengi yamefanywa tayari. Ila Ningemuambia yafuatayo 1. Afungue mipaka ya mazao hasa mahindi ili wakulima tunufaike tofauti na miaka 3 iliyopita hali imekuwa mbaya mahindi yametuozea 2. Tujenge viwanda mfano viwanda vya korosho, kiwanda cha pamba kutengeneza nguo na kuchakata parachichi Njombe maana wakulima wanapanda lkn hakuna kiwanda hata kimoja tumebaki kuongea kwenye majukwaa uhalisia we are very slow resulti g mazao ya kilimo kutokua na dhamani daima. 3. Watoe ajira kwa wataalamu wa ufugaji samaki ili watusaidie sisi wakulima tunapenda kufuga samaki Lkn tunakosa wataalamu.
 
Wengine kukutana na Magufuli tunaona mkosi, hata ukitulipa hela tutakataa, kwa nini unasema kukutana na Magufuli kutakuwa bahati?

Na kipi ambacho unafikiri unaweza kumuambia ambacho hakijui sasa hivi? Mtu msomi kasoma mpaka Ph.D, anajua mpaka boiling point ya silver kwa kichwa (hata kama Ph.D ya kuandikiwa hawezi kukosa kujua the basics), mtu ana nyota zote za serikali zimemzunguka na kumsujudia akitaka kujua lolote anajua, mtu anadukua simu za watu anavyotaka, leo wewe utamwambia nini ambacho hajui?

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anajihusisha na uanaharakati wa elimu Tanzania. Msomi kasoma mpaka Harvard.Kisha anajua mambo ya mtaani kupita maelezo.Mjanja kimtaa mtaa na kisomi somi.

Akawa anafanya kazi na NGOs. Akawa mstari wa mbele kuikosoa serikali na kuishauri. Kikwete akamuona huyu anasema sana, ngoja nimuingize serikalini aone mambo yanavyoenda.

Kikwete akampa formal appointment na access zote kwa rais, nafikiri alikuwa mshauri wa rais wa mambo ya elimu. Basi jamaa akawa anakaa na Kikwete anampa makabrasha yake na mipango ya kufanya elimu iwe bora.

Kila jamaa akitoa makabrasha akimpa Kikwete, Kikwete anamjibu hili? Hili tunalijua, tena tunayo ma kabrasha ya studies zilifanyika kwa miaka mingi sana, ukitaka habari zaidi nitakupa mtu wizarani akuoneshe.

Jamaa akija na jipya anaambiwa hili? hili tulishaliundia tume na majibu yako yote haya yapo kwenye ripoti ya tume, naweza kukupa namba ya simu ya profesa aliyeandika ripoti.

Mwishowe jamaa akagutuka, kumbe hawa watu wa serikali tatizo lao si kwamba hawana habari, kwa kweli wao wanajua mambo kuliko mimi. Tatizo ni siasa na machinery ya operation ya serikali, tatizo si kwamba hawajui mambo, wanajua kuliko tunavyofikiri, wana wasomi wengi sana, wamefanya studies nyingi sana. Tatizo si kwamba hawajui mambo.

Jamaa alivyoona hivyo hakukaa sana, alijitafutia kazi sekta ya watu binafsi kimataifa akasepa.

Sasa wewe leo unataka kumshauri Magufuli kipi ambacho hajakijua na hawezi kukijua akiwa na nia?
 
Unaonesha unauchungu na nchi hii unahitaji taifa lisonge mbele tunakupongeza kwa jitihada unazoendelea kuzichukua kuboresha miundombinu lakini kuna mambo madogo inabidi uyafanyie kazi ili wananchi waendelee kukuunga mkono juhudi zako kuna watu wanasema wanahitaji democrasia ni jambo zuri lakini kwa mawazo yangu mimi tanzania Tunahitaji rais mkweli na muwazi kama nyerere ambaye alikuwa anakubali kabisa kuna mambo amefanikiwa nakuna mengine amekosea kipindi cha uongozi wake tofaut na uongoz wa sasa kuna mambo mengi watu wanabolonga lakini wamekuwa wanataka sifa
 
YAH: kichwa cha habari tajwa hapo juu☝
Wanasema samaki ana mengi na hata siri za kuteta ila......ndio tatizo.
Hebu turudi kwenye mada husika, hivi ikitokea siku ya leo ukakutana uso kwa uso na rais wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshiwa J.P Magufuli je ni swali lipi ungependa kumuuliza!? Au ni jambo lipi ungependa kumwambia!?
#Amoun.
Ningemwambia Mzee tunakushukuru kwa yote , ila ninakuomba ujiuzulu tu , maana uongozi ni sawa na mbio za kupokezana vijiti
 
Kwanini haamini anachokifanya mpaka kushindwa kuhimili ukinzani au changamoto zaki mtazamo anazokutana nazo kwa mujibu wa sheria na uhalisia???
*"haamini" kwakua matumizi ya nguvu yanayofanya na vyombo vyake vya usimamizi na polisi.
YAH: kichwa cha habari tajwa hapo juu
Wanasema samaki ana mengi na hata siri za kuteta ila......ndio tatizo.
Hebu turudi kwenye mada husika, hivi ikitokea siku ya leo ukakutana uso kwa uso na rais wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshiwa J.P Magufuli je ni swali lipi ungependa kumuuliza!? Au ni jambo lipi ungependa kumwambia!?
#Amoun.
 
Mkuu, rais nijuavyo ndie husimamia system yote, na kibongobongo anamamlaka hakuna mfano wake, sasa kama anajua yote hayo anashindwaje kusema iwe na ikawa?
je kuna mtu mwingine mwenye mamlaka makubwa zaidi nyuma ya raisi ambaye humpangia kipi afanye na lipi aache?
Au mioyo yao ni migumu kama jiwe,
isiyitaka mabadiliko mapya?
Wengine kukutana na Magufuli tunaona mkosi, hata ukitulipa hela tutakataa, kwa nini unasema kukutana na Magufuli kutakuwa bahati?
Na kipi ambacho unafikiri unaweza kumuambia ambacho hakijui sasa hivi? Mtu msomi kasoma mpaka Ph.D (hata kama ya kuandikiwa hawezi kukosa kujua the basics), mtu ana nyota zote za serikali zimemzunguka na kumsujudia akitaka kujua lolote anajua, mtu anadukua simu za watu anavyotaka, leo wewe utamwambia nini ambacho hajui?
Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anajihusisha na uanaharakati wa elimu Tanzania. Msomi kasoma mpaka Harvard.Kisha anajua mambo ya mtaani kupita maelezo.Mjanja kimtaa mtaa na kisomi somi.
Akawa anafanya kazi na NGOs. Akawa mstari wa mbele kuikosoa serikali na kuishauri. Kikwete akamuona huyu anasema sana, ngoja nimuingize serikalini aone mambo yanavyoenda.
Kikwete akampa formal appointment na access zote kwa rais, nafikiri alikuwa mshauri wa rais wa mambo ya elimu. Basi jamaa akawa anakaa na Kikwete anampa makabrasha yake na mipango ya kufanya elimu iwe bora.
Kila jamaa akitoa makabrasha akimpa Kikwete, Kikwete anamjibu hili? Hili tunalijua, tena tunayo ma kabrasha ya studies zilifanyika kwa miaka mingi sana, ukitaka habari zaidi nitakupa mtu wizarani akuoneshe.
Jamaa akija na jipya anaambiwa hili? hili tulishaliundia tume na majibu yako yote haya yapo kwenye ripoti ya tume, naweza kukupa namba ya simu ya profesa aliyeandika ripoti.
Mwishowe jamaa akagutuka, kumbe hawa watu wa serikali tatizo lao si kwamba hawana habari, kwa kweli wao wanajua mambo kuliko mimi. Tatizo ni siasa na machinery ya operation ya serikali, tatizo si kwamba hawajui mambo, wanajua kuliko tunavyofikiri, wana wasomi wengi sana, wamefanya studies nyingi sana. Tatizo si kwamba hawajui mambo.
Jamaa alivyoona hivyo hakukaa sana, alijitafutia kazi sekta ya watu binafsi kimataifa akasepa.
Sasa wewe leo unataka kumshauri Magufuli kipi ambacho hajakijua na hawezi kukijua akiwa na nia?
 
Hata Mimi nitamuunga mkono kama 2020 ataamua kupumzika siasa na kuwaachia wengine kwa moyo mweupe.
Kazi aliyoifanya inatosha, miaka 20 ya Ubunge na 5 ya Urais inatosha kabisa kwa vile hii minne ya mwisho taifa nimegubikwa na kukosa furaha na kujaa woga kama tuko Afghanistan kumbe tuko nchi aliyoikuta na amani.
Hicho kitakuwa kitendo cha kishujaa sana na heshima kuliko kusubiri kina Membe waje wamgaragaze pale Dodoma kwa aibu.
 
YAH: kichwa cha habari tajwa hapo juu
Wanasema samaki ana mengi na hata siri za kuteta ila......ndio tatizo.
Hebu turudi kwenye mada husika, hivi ikitokea siku ya leo ukakutana uso kwa uso na rais wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshiwa J.P Magufuli je ni swali lipi ungependa kumuuliza!? Au ni jambo lipi ungependa kumwambia!?
#Amoun.

Mi ningemwomba anipe ka wilaya kamoja tu hapa nchini niwe DC nimsaidie kuhangaika na shida za wananchi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom