Status
Not open for further replies.
... ni kweli nchi ilikuwa kwenye hamasa kubwa sana by then; hamasa ikaanza kushuka taratibu kadiri siku zilivyokwenda na kufikia kiwango cha chini kabisa siku Tundu Lissu alipopigwa risasi. Kwa hakika siku ile tuliingia "enzi mpya".
 
... ni kweli nchi ilikuwa kwenye hamasa kubwa sana by then; hamasa ikaanza kushuka taratibu kadiri siku zilivyokwenda na kufikia kiwango cha chini kabisa siku Tundu Lissu alipopigwa risasi. Kwa hakika siku ile tuliingia "enzi mpya".
Yes na siku alivyotekwa mo na baada ya hapo wananchi walielewa shoo yote wameisha muelewa mkubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka ile vibe ya JPM miezi mitatu ya mwanzo wa utawala wake, I swear that was the best moment,nchi ilihamasika,watu wakaanza hadi kudai risiti wakinunua bidhaa,msisimuko ukarudi kwamba we are heading somewhere as a country.
Najua wengi sasa hivi wamepoteza matumaini ya maisha, Rais akiongea inaonekana kama anadanganya tu,kwa kweli sijui ni kina nani walimshauri baadhi ya maamuzi anayofanya ila ninachoweza kumuambia ni:Mr President get back to what matters,embu fanya yanayosaidia maisha ya watu wa kawaida wewe huwa unawaita wanyonge
Kuna wasaidizi wako wanakusifia tu na kukupamba kinafiki kama huamini angalia video zako mtandaoni ukiwa unahutubia au wakiwa wanakusalimia kuna unyenyekevu wa kinafiki uliopitiliza,wapuuze jamani WNAKUPOTEZA.
Unajuwa, wengi wa watendaji walioko chini hutekeleza amri, maagizo au directives zake… ILA ZIKIBUMA NDO MNAKUJAGA NA MAELEZO KAMA HAYA....

TRA walisababisha maduka kufungwa… Lindi, Mtwara etc...
Korosho wote tunajuwa nini kimetokea na wapi tulipo na wangapi wamekufa kisa korosho…
Sukari tulinunu hadi Tshs 5,000/- kwa kilo
Etc....

Yaani akichemsha, lawama zinashushwa.. ANAKUWA SIYO YEYE ALIYESABABISHA.... Wakati wote tunajuwa kuwa ANA UTAALAMU MKUBWA WA KUTENGENEZA TATIZO, THEN ANARUDI KIVINGINE KAMA MKOMBOZI ("Yesu" wetu) kuja kuleta suluhisho… MFANO ISHU YA MIFUKO Y HIFADHI YA JAMII (NSSF, PPF, PSPF etc)... Mwishoooni eti turudi kama zamani, Korosho, mwishoooni eti nimewasamehe ila msirudie..!!!!
 
Baba Magu watu hawakuelewi kwamba ukitengeneza miundombinu umeendeleza sector zote, wewe maliza reli umeme wa rufiji na umeme wa gesi uwe sawa, waone Tanzania itakavyokimbiza kimaendeleo. waache walopoke, tulikuomba kwa Mungu atupe Rais mkali atakayesimamia rasilimali za waTz nashangaa unaanza kupoa, hata ukifika 2020 huna hata mmoja uliyeanza naye sawa tu.,sisi hatutaki himaya ya watu bali kazi. na maendeleo sisi watu wa magharibi tunajua jinsi tulivyotelekezwa kimaendeleo wakidhani area yetu siyo economic viable sasa wataona. si rami ya Tabora mpanda inajengwa, si Mpanda- kigoma inajengwa kigoma Nyakanazi, umeme wa Rusumo si karibu utawaka mie na kwambia Magu watatusikilizia, naomba tu Mungu akupe uhai na akuongeze ukali kidogo.
 
Napenda kumshauri Mh: kwa taarifa anazopata asizifanyie kazi mpaka azipatie ufumbuzi wa kina,
Kwa mfano: vijana walojenga mererani ni wachache sana walochaguliwa kujiunga na jeshi la POLISI na wengine ni vijana tu wakawaida ambao hawajashiriki katika ujenzi ila walikua vikosini wakishughurika na kazi mbali mbali ndo walobahatika na kujiunga na jeshi hilo. Aya na kwa tarifa ya vijana walojenga Ukuta mererani kua wamejiunga katika RTS na wamemaliza hiyo tarifa haina ukweli kwa kua hakuna vijana waliofanya usairi wa TPDF tangu Op Magufuri iingie vikosini, na Mafunzo ya RTS yalokua yakiendelea juu ya Ops KIKWETE na MUUNGANO vijana hawa walikua bado wako kwenye ujenzi asa hiyo tarifa ya vijana hawa wamejiunga na mafunzo na wamemaliza inatokea wapi? kwa mantiki hiyo sasa ni kwamba hakuna kundi la vijana walokwenda kufanya mafunzo hayo bali baadhi wapo vikosini ukiondoa wachache walopata nafasi ya kujiunga na Jeshi la Polisi, wanasubiri Neema yako, swara la vijana wa JKT vijana hawa wamefanya kazi nzuri katika Taifa na sifa zimevuka hata mipaka ya Nchi, hakika inapendeza, ila tatizo lina kuja pale mpeleka ripoti ya jumla kuhusu idadi ya vijana na hata washiriki wa matukio mbalimbali, vijana hawa wapo katika makundi (operations) OPs na wote wanafanya kazi kwa kutegemeana yaani sio ikitokea kazi, vijana wote waende katika kazi hiyo bali watachaguliwa wachache kwenda kushiriki kazi hiyo nao ndo wataowakilisha vijana wengine walobaki vikosini kwa ajiri ya kazi mbalimbali, hivyo sasa kama kinachofanyika kua watakao pata nafasi ya upendeleo ni wale wanaoshiriki majukumu mbalimbali ya kitaifa na wote wakaenda, Je? Shughuri za Ulinzi na kazi mbalimbali za vikosini nani atafanya
Namuomba mh: ajaribu kuweka usawa kwa vijana wote yani afanyae kazi za ujenzi mbali mbali (kitaifa) ni sawa na yule aliye kikosini afanyae kazi mbali mbali za ulinzi na hata ujenzi( ujasiliamali) na zitokapo Fursa wate wahusishwe asiweke mipaka (matabaka). Akhasante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tujiulize kama wewe ungekuwa Raisi leo ungefanya nini kama nchi ilivyo leo. Mimi ningefanya hivi kwa uzoefu wangu na nina Imani kabisa nchi ingebadilika na maendeleo ya kiuchumi yangeonekana. Hivi vitu nitavitaja kwa umuhimu kwamba ninaanza na nini. Hivyo namba hapo chini ni kama hatua moja moja



  • Kwa kutumia ofisi ya CAG na kampuni za consulting za kimataifa kama (Deloitte, Ernst & Young (EY), KPMG and Pricewaterhouse) wafanye uchunguzi kwenye idara zote za serikali na watoe report ya kuongeza ufanisi mfano kuunganisha idara, kuongeza technologia na kuangalia idadi ya wafanyakazi. Lengo ni kupunguza gharama, kuongeza ufanisi na kutoa maelezo ya kila mfanyakazi anatakiwa kufanya nini na malengo yake ni yapi. Hivyo kila mtu kuanzia katibu mkuu anakuwa na malengo ya mwaka. Hii itasaidia kila mtu kuamka na kuafanya kazi bila mpangilio maalumu na kuongeza ufanisi kazini. Vilevile nitajua serikali ikoje kwa urahisi na mapungufu. Kwenye hili hakuna siasa.
  • Nitatoa uhuru kwa vyombo vya habari na wanasiasa wawe na uwezo wa kufanya mikutano wakati wowote bila kujali. Maendeleo hayajali maneno. Lakini demokrasia inaleta maendeleo. Kutakuwa na demokrasia ya ukweli
  • Mfumo wa shule kuanzia msingi mpaka form six kubadilika. Nitabadilisha mfumo wa sasa wa elimu wote. Lengo kubwa ikiwa kushindanisha watoto wetu hasa kwenye technologia. Hivyo nitahimiza technoologia iweze kutumiaka zaidi kwenye mashule na tutaongeza walimu wa technologia ngazi zote. Vilevile nitaomba misaada kutoka kwa waziri mkuu wa India, US na kwenye foundation kama Bill gate foundation kuweza kusaidia kuweka technologia kwenye madarasa. Lakini sio hilo tu nitaomba watuwekee utaratibu ili wahitimu wetu waweze kujifunza software mbalimbali ili waweze kufanya kazi kimataifa hata wakiwa Tanzania. Vilevile nitaongea na kampuni za software mbalimbali kama SAP ya German, Oracle na Cisco za USA kutusaidia kwenye hili. Kuna vitu virahisi sana mfano simu nyingi ni computer tayari ina maana kukiwa na data free basi unaweza kutafuta simu za bei rahisi zigawe kwa kila mtoto na kuweka vitabu, lecture za vyuo na kuunganisha n ahata na vyuo na shule mbalimbali duniani. Mtoto wa Tanzania anaweza kufanya homework yake akaipiga picha na mwalimu wa kujitolea ambaye yuko India anaweza kusahihisha hii inawezekana kama tunafikiria vizuri. Haya ni mambo ya kuongeza tu haina maana tusiwe na walimu lakini ni mfano tu.
  • Nitawekeza kwenye kilimo. Tukasome sera za kilimo kwanza na tufanye kama sera ilivyo
  • Mapendekezo ya kubadilisha katiba hasa kwenye mambo ya kiuchumi. Nita ruhusu watu zaidi kuja Tanzania wenye vipaji kwenye technologia, diaspora wa Tanzania na NGO za maendeleo. Mimi siamini kama tuna matatizo ya kuwa wengi au tutapoteza mashamba yetu nchi yetu ni kubwa na tunahitaji watu productive. Mimi mwenyewe niko nchi ya watu kwa sasa!. Sera za kijinga za uraia nitazitoa kwa manufaa makubwa ya nchi mfano mzuri ni katiba ya Kenya. Tofauti ni kwamba kwenye katiba hii hakutakuwa na kuongeza ukubwa wa serikali kama ilivyo Kenya. Nitabadilisha mfumo wa Ardhi ili iongeze uwekezaji lakini kutakuwa na sehemu maalumu ambazo huta ruhusu uwekezaji ni za makazi tu.
  • Bodi maalumu za ushauri. Kutakuwa na bodi za ushauri kila wizara. Hizi board ni za wasomi mbali mbali na watu wenye nia nzuri na Tanzania wanashauri kwenye sera. Hakuna kulipwa ukiwa mwana bodi wala posho ni kujitolea. Diaspora wa watu wanje wenye nia nzuri wanakaribishwa.
  • Mahakama nitaiacha huru na kuwapa watakalo kuongeza ufanisi.
  • Tutatoa elimu ya Afya kwa vijana hasa chini ya miaka 30 ya mazoezi na lishe na itaingiza kwenye elimu yetu
  • Tutakuwa na Parks za kupumzikia, kukimbia, kutembea ,kucheza watoto, na kuendesha baiskeli na kila wilaya ni lazima iwe na sehemu za wazi za hivi.
  • Nitakuwa nahutubia Taifa kila mwezi
  • Nitakuwa nafanya debate na kupokea maswali kutoka kwa wananchi kila miezi mitatu. Debate wapinzania wanaruhusiwa na itakuwa kwenye TV kwenye chuo kimojawapo live. Debate za maendeleo tu.
  • Nitaanzisha mfumo wa mobile Hospital. Yaani hospitali za magari ziende kila kijiji na Dr wa meno, kisukari, watoto nk kupunguza watu kusubiri kuzidiwan na kuja hospitali za rufaa ambazo ni chache. Yaani hii itakuwa kama kinga.
  • Ningewapa bank kuu kazi ya kuhakikisha lengo lao ni pamoja na kuongeza ajira kama ilivyo USA. Hii itasaidia Bank kuweka sera za kusaidia biashara ndogondogo ambazo ndiyo waajiri
Nitatoa mengine baadae nipe yako
 
ningekuwa rais...

1. ningejenga shule nyingi sana za bweni kwa watoto wa kike ili kuweza kidhibiti matukio yote yanayoambana na kufanyiwa vitendo viovu pindi wanaporudi na kwenda shule.

2. ardhi ya tanzania ni kubwa sana, ningeanzisha plantations nyingi kwa ajili ya kuongeza malighafi za uzalishaji viwandani.

3. wafungwa wangefanya kazi usiku na mchana , kuzalisha zana bora na za kisasa za kilimo ambazo zingeuzwa kwa bei nafuu na hivyo kuongeza ufanisi katika kilimo.

4. ningeanzisha science centers and technology centers nyingi ambazo zingekuwa zinafanyakazi ya kuwatayarisha wanasayansi wakubwa wa teknolojia toka wakiwa wadogo sana. Centers hizo zingekuwa zinachukua watoto wenye uwezo mkubwa sana wa kiakili na kama ukionekana una uwezo mdogo unaondoka

5. Ningeifungua Tanzania kwa mataifa mengine waifahamu na kushirikiana na nchi zote katika masuala muhimu yote yahusiyo maendeleo, uchumi, siasa, elimu n.k.

6.madaraja ya ufaulu shuleni na vyuoni yangekuwa makubwa sana , kiasi kwamba kufaulu ingehitaji kusoma sana na mitihani ingekuwa migumu sana kwa kila hatua.

7. mfanyakazi( mwalimu, daktari, n.k.) angeongezewa mshahara au kupandishwa cheo kulingana na uwezo wako wa kuzalisha na ubora wa unachozalisha. mwalimu anayefaulisha vizuri atapata zaidi.

8. kwa shule ambazo changamoto ni nyingi za upatikanaji wa nyenzo za kujifunzia na kufundishia, ma-RC na ma-DC wahakikishe wanazitatua mara moja.

9.ningeanzisha maktaba kubwa kila tarafa ambayo itakuwa na vitabu vingi na vya kujitosheleza na hivyo wanafunzi kwa utaratibu maalumu utakaowekwa wataenda kujisomea na kuazima vitabu serikali ikiangalia utaratibu wa kujenga maktaba mashuleni.

10.CAG angekuwa na mamlaka ya kupeleka kesi mahakamani kama ataona inafaa kuwa hivyo ili kupunguza na kudhibiti mianya ya wizi na ubadhirifu wa mali za umma
 
Ningewateua vipanga tusaidiane kazi na wala kamwe nisingepingana na professional says wala kuishi kama MUNGU MTU kila kitu unajua wewe
 
Hii nchi ni yetu sote, kila mmoja ana dhamana ya kuijenga kwa namna inavyopasa, kuanzia raia wa kawaida hadi raia wa kwanza (Rais Magufuli).

Hebu tuzungumze na Rais Magufuli kwenye hii thread kama Rais na kama raia mwenzetu ambaye naye siku si nyingi tutakuwa naye uraiani. Tumkosoe, tumshauri na tumpongeze popote inapobidi.

Karibuni sana!
 
Namkumbusha maadui zake sio upinzani akae awatafakari wanaomzunguka huko chamani. Ndio wale wale waliokuwa wanapiga hela kipindi cha JK. Wapinzani ndio wamefanya ATCL kuhamishiwa ikulu? Tafakari
 
Hii nchi ni yetu sote, kila mmoja ana dhamana ya kuijenga kwa namna inavyopasa, kuanzia raia wa kawaida hadi raia wa kwanza (Rais Magufuli).

Hebu tuzungumze na Rais Magufuli kwenye hii thread kama Rais na kama raia mwenzetu ambaye naye siku si nyingi tutakuwa naye uraiani. Tumkosoe, tumshauri na tumpongeze popote inapobidi.

Karibuni sana!
wazo zuri ila thread kama hii nadhani ipo tayari humu
 
Mimi namshauri tu kama inawezekana 2020 asigombee tena, huenda akaja kuharibu zaidi yale mema aliyokwishafanya
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom