Status
Not open for further replies.
mtu ateuliwe kutokana na kuwajibika na kusimamia vizuri majukumu yake na si kujitangaza. kuna wakuu wa wilaya wengi wanafanya kazi nzuri sana ila kwa kuwa wapo mbali na vyombo vya habari , basi hatusikii wanayofanya. hata mimi mwenyewe naweza kujitangaza au nikatumia watu wanitangaze ili niteuliwe ningali najua kabisa sina dhamira ya kuwatumikia wananchi kwa dhati ila kukitumikia cheo.
Utaacha lini wivu?
 
sio kwamba hazi-attract media ila hawana mambo ya kuita vyombo vya habari katika kila tukio.ukimuangalia jokate ni mtu wa media sana, gondwe alikuwa mfanyakazi wa ITV na hali kadhalika huyo mwengine ni media kwa sana. unaweza kuta wanayoyafanya wenzao walifanya muda ila hawakupata media coverage kama wanavyopata wao na kuonekana wao ndio waanzilishi
Ukipata nafasi tumia ukikosa jutia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Historia za hao vijana ni kwamba wamekulia shida na wanajua shida ipoje. Kiufupi maisha yao yamewafundisha kwamba ili uendelee ni lazima uwe na nidhamu na kazi. Maneno maneno hayampi mtu kitu, na debe tupu hotoa mlio mkubwa.

Mfano, Gondwe katokea mbali sana kimaisha.
 
Kuna Eng mmoja kama sikosei mkuu wa mkoa wa Geita ambaye ameanzisha masoko ya madini bila kuwa na maspika naye yuko njema.
 
Nikupe pole kwa Majukumu uliyonayo. Pia Shikamoo! Ni kaushauri kadogo tu asubuhi ya leo ningependa kupendekeza. Unao Vijana watatu ambao Mimi Binafsi nawaona Kama watu ambao ulipatia kuwateu kukusaidia. Nakuomba uwape majuku makubwa zaidi, kwa kiwango walichokionesha, wanastahili kukusaidia katika Majukumu makubwa zaidi. Vijana Hawa watatu Ni:
1. Anthony Mtaka (RC-SIMIYU), kwakweli Ni mtu anaejiamini, mbunifu, mtu wa kutafuta fursa za kimaendeleo kwa ajili ya Wananchi wa Mkoa wake. Atatufaa zaidi hata tusio wa Mkoa wake.
2. Jokate Mwegelo, Young and Ambitious, ameonesha alivyo mbunifu, ameamua kufanya kazi tofauti na wengine ambao kazi Yao Ni kukuimbia nyimbo za kukusifu na kukuabudu.
3. Godwin Gondwe. Amekuwa msaada Mkubwa Sana kwa Wananchi wa Handeni. Amehamasisha kilimo Cha mihogo, shughuli za Maendeleo na Mambo mengi ambayo Ni positive.

Ni hao TU muheshimiwa, na nakuhakikishia, HAWATOKUANGUSHA. Ila kaombi kengine kadoooogo, pale Hai huna Mkuu wa Wilaya, una MUHUNI NA KILAZA(sijui walikupa vigezo gani umteue?).

Sent using Jamii Forums mobile app

Natamani hata wewe uliyetoa ushauri huu, apate fursa ya kukufahamu. Nahisi kama anaweza akakupatia angalau zawadi ya kukushika mkono tu kama aliyompa yule mheshimiwa wa TRA, japo yeye amepata na cheo pia. Wazalendo huwa hawatupani, wanafahamiana.
 
PLEASE be honest umemsahau mtu mmoja muhimu sana anajituma kwelikweli ila tu hamuoni juhudi zake huyu si mwingine bali ni PAUL MAKONDA mkkuu wa mkoa wa DSM
 
Natamani hata wewe uliyetoa ushauri huu, apate fursa ya kukufahamu. Nahisi kama anaweza akakupatia angalau zawadi ya kukushika mkono tu kama aliyompa yule mheshimiwa wa TRA, japo yeye amepata na cheo pia. Wazalendo huwa hawatupani, wanafahamiana.
Nashukuru. Ila mi nimewiwa tu Kama Mtanzania, nimeona nami nimsaidie kwa Maoni kidogo. Tuijenge nchi yetu sote. Huku nilipo nahudumia pia Wananchi Kama sehemu ya kuisaidia Serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru. Ila mi nimewiwa tu Kama Mtanzania, nimeona nami nimsaidie kwa Maoni kidogo. Tuijenge nchi yetu sote. Huku nilipo nahudumia pia Wananchi Kama sehemu ya kuisaidia Serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mungu (Allah) wa Ibrahim, Isaka na Yakobo awe pamoja na wewe daima. Hiyo Allah nimeweka kwenye mabano ni kwa ajili ya ku-take care kama wewe ni Muislam!
 
Bila kumshau mhe.Eng Evarist Ndikolo RC Pwani
Ana bahati ya kuwa karibu na Dar na kwa kuwa maeneo ya uwekezaji dar hayapo ,wawekezaji wengi sana wameona mkoa wa pwani kuwa ndio kimbilio la uwekazji kwa ajili ya soko la wakazi wa dar.
 
Status
Not open for further replies.
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom