Status
Not open for further replies.
Umekielewa ulichosoma ila ni ubishi tu "Askari akiua jambazi apandishwe cheo", huyo askari hajaua jambazi Bali kaua askari mwenzake, utata uko WAP?
 
Mh Rais. Pole kwa majukumu ya kulijenga Taifa, aidha nakupongeza kwa kazi nzuri unazozifanya. Suala langu ni la Kichama (CCM) Mh Rais wewe ndiwe mwenyekiti wa chama Tawala CCM, nakuomba kwa dhati kabisa Mbunge aitwaye DEODORUS BUBERWA KAMALA(CCM) Jimbo LA Nkenge huko Missenyi Kagera, siku mkifika kwenye hatua ya kuchuja wagombea Ubunge tafadhali huyu MTU ASIRUDISHWE TENA! Ki ufupi huyu jamaa hafai na hana msaada wowote. Huyu mbunge anakihujumu chama na anakuhujumu wewe Mh Rais kwa kuto watumikia wananchi. Huyu mtu hana muda na walio mpigia kura, sana sana mkimsumbua kumuleza kero zenu yeye anasema kuwa "KURA ALIZINUNUA KWA PESA YAKE" Mh hata kama alifanya hivyo kweli lakini amejisahau sana. Sitaweza kuzungumza mengi juu yake ila naomba nyie viongozi mfuatilieni kwa ukaribu huyu jamaa mtajionea mengi huko jimboni kwake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningepata walau nafasi ya kukutana na mheshimiwa Rais wa JMT ningempongeza kwa kuwateuwa vijana wengi kwenye nafasi mbalimbali. Hata hivyo ningemshauri vilevile awateue vijana wengi kwenye Bodi ya mashirika mbalimbali ya umma. Wakuu wengi wa mashirika mengi wamekuwa wakiwadanya wazee wengi ambao hawana hulka ya kusoma makabrasha hivyo kusababisha matatizo lukuki kwenye mashirika husika. Hapa napendekeza wapewa nafasi watu wenye nguvu na wanaoweza kufuatilia utendaji wa kila siku wa mashirika husika.
 
Mh Rais aka Daddy wa Taifaaa
Poleh na Hongera
Mi ishu yangu ni familia zinavunjikaaa.. mme wangu kahamishiwa Dodoma na Makazi ni ya kuwinda sanaa
Kuhamia Dodoma ni jambo jema la kitaifa ila nashauri lisipelekwe haraka sana watu wanaumia walau Serikali muinvest makazi,Ofisi zao,shule,hospital nk kwanza
Pia Wapatieni japo nyumba tupate pa kufikia
 
Hapo vip!!

Katika hawamu hii, hawajafanikiwa kuleta na kufanya mpango wa maendeleo inayogusa nchi nzima bali ni hizi program ndogo zinazogusa ukanda fulani, mfano ununuzi wa ndege inamsadiaje mtu wa nachingweya mtwara, au treni ya umeme kutoka dar kwenda mwanza inamsadiaje mtu wa Oldadai -Arusha.

Mfano kipindi cha Kikwete ulianzishwa mpango wa shule za Kata Tanzania nzima na niwazi huu mpango imewagusa na kuwasaidia watanzania wengi katika kila kona ya Nchi.

Pili Kikwete alifanya mpango wa kujenga barabara za lami Nchi nzima na mpango huu imemgusa na kuwasaidia watanzania wote.

Mimi tokea uingie madarakani bado sijaona mpango uliokuja nao Kwa lengo la kuwasaidia watanzania au kuibadisha Tanzania Kwa ujumla, hizi Sijui treni za umeme na ununuzi wa ndege ni projects ndogo ndogo sana.

Hivi washauri wa rais Kwa nini msimshauri vizuri katika eneo la uchumi , mkaacha kumuogopa, Kwanini yeye ni Mungu bhana.

Hivi viprojects vidogo vidogo anavyofanya ni za level za mawaziri na wabunge.
We unataka wenzio wafukuzwe kazi
 
Hakuna kipindi Serikali imefanya vizuri kwenye Sekta ya Afya Kama msimu huu wa Magufuli.

Mpaka WHO wametoa riport ya kuridhika na Hali ujue si mchezo.

Bajeti ya Afya imeongezeka Mara Tano zaidi ya ilivyokuwa kipindi Cha wawamu ya nne.

Hakika tuko pazuri.
Hilo halina ubishi.
 
Kinacho takiwa ni uchapaji kazi ndio TANZANIA ya sasa inavyo taka anae fanya kazi anaonekana na apewe nafasi ya kazi ...kwa nafasi yake
 
Kilio changu kwenye elimu mtoto anamaliza shule haajiliki hapo paboreshe .walimu waongezwe kukidhi mahitaji ya watoto .madarasa yasimamiwe yawe ya kutoshereza watoto manake mwaka hadi mwaka watoto wanaongezeka
FB_IMG_15468691200679801.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza niseme japo ulikuwa vizuri na siku ile NEC wanakupitisha nilikesha nikiangalia na nilifurahi sana atleast maana nilijua wewe ni mchapakazi licha ya kasoro ndogo ndogo.

Ulipoanza kuongoza nilikusifu humu na kukutetea na nakumbuka sana mwanzoni wanachama wengi wa CCM wale mafisadi walikuogopa maana ulikuwa huna mawaziri na unavamia kila ofisi kurekebisha mambo.

Lakini kadri muda unavyoenda mafisadi ndani ya chama wamejua kukuchezea akili sasa wanakusifu ili tu usiwatumbue.

Rais unawezaje kusifiwa na watu waliokuwa wanawaponda wakina Zitto na Tundu Lissu kipindi wanaleta hoja za madini na wewe ukiwa waziri uliwaona walivyotetea kwa juhudi?

Unawajua wote waliosema fedha za Escrow sio zetu. Je bado unawaamini kuliko waliosema ni zetu?

Unawaaminije waliopitisha kikokotoo kibovu bungeni halafu leo wanafanya maandamano ya kukusifu kukifuta?

Rais naona unakosea target, wapinzani sio target ya msingi kwa sasa. Target wanachama wako wa CCM maana wengi ndo mafisadi na wanafiki huku ukiwatumia wapinzani kukufichulia maovu.

Kuwa makini na watu kama akina Makonda wanaokuonyesha upinzani ndo watukutu ili kukutoa kwenye target.

Naamini kama unataka kuijenga Tanzania bora simamia misimamo yako huku ukifanyia kazi mawazo ya wapinzani kwenye background.

Mimi kuna vitu nakupinga kama airport Chato na wanafunzi wenye mimba. Lakini mambo kama reli, Stiegler Mh. fufua hata zote na ukiitisha harambee nitatoa mchango.

Mwisho mh. hebu kiangalie kizazi cha vijana wa sasa wengi hawanauelewa wa mambo kazi ni udaku mitandaoni na uhuni uhuni hebu kaa na waziri husika tuangalie, pia wabane wasanii maana wengi ni vichwa maji wanaoharibu vijana.

Kwa sasa ni hayo tu.

Tupige Kazi. Tukila Bata
 
Hakika kazi anayofanya Raisi MAGUFULI kwa taifa la TANZANIA inastahili pongezi nyingi sana,kitendo cha kuthububutu kununua ndege ili kuifufua Air Tanzania ilivyokuwa imekufa kwa kweli watanzania tuliihitaji Air Tanzania kuliko mnavyoweza kufikiri maana nakuna namna nzuri zaidi ya kuitangaza nchi kimataifa zaidi ya hiyo kuipeperusha bendera na jina la Tanzania kwenye anga za kimafaifa na kwenye ardhi za mataifa kupitia Airport zao,dada za kuwa na ndege yenye kupepeeusha bendera ya taifa ni kubwa kuliko unavyoweza kufikiri,kuna utalii kuna Biashara hata ya bidhaa za viwandani kuna mazao ya kilimo madini na kadhalika.hapa nina.maana kama nakuna anayekuamini kwa kukufahamu ama hata kukusikia hivi vitu utabaki navyo na wala hutafaidi kuwa navyo ila badala yake hata jifani yako mwenye chombo cha kupeperusha bendera ya nchi yake lakini akakosa hizi vitu anaweza kuvitumia hata kimojawapo kwa ajili ya kujinufaisha kibiashara kama walivyotumia mlima kilimanjaro wakichora mlima ambao upo Tanzania kwenye ndege zao.

Hapa nimetaja faida ambazo taifa litapata kwa upande mmoja tu kutoka nje bado zipo faida fursa lukuki zitazopatikana ndani kwa ndani kama ajira na hata watanzania wa ndani kurahisishiwa usafiri kutoka eneo moja la mkoa flani kufikia mkoa mwingine kibiashara ama ktk kazi za kiofisi.
Kilichobaki hapa ni bodi ya Atc nao wafanye ya kwao sasa wawe wabunifu wa biashara gani hizo ndege zifanye kwa faida ili shirika liwepo na lizidi kustawi maana kama ni mtaji ni tayari wameshapewa ndege za kutosha kabisa kwa kuanzia wasije wakamchosha tena Rais MAGUFULI awape mtaji na aanze tena kufikiri kazi ama route zipi waende kwa faida kwa hapa sasa nawashauri watanzania ambao wanapenda kulalamika na kulaumu wabadilike waende kwenye uhalisia ya kwamba Raisi MAGUFULI aliyethubutu kununua ndege apewe heshima na sifa zake halafu tuwageukie waendeshaji wa shirika Atc kusubiria ama kuwalaumu ama pia kuwashukukuru hii sasa itategemea mafanikio ama anguko lifakalotokana na namna gani watakavyoendesha biashara hii.

Pia kwa juhudi alizochukua Raisi kukutana na wadau wa madini na hata madhehebu ya dini yupo sawa kabisa kwa sababu huko ataibua changamoto na kero nyingi ambazo ingekuwa ni vigumu kumfikia

ninaona tunaelekea kuzuri sana maana hata namna ambayo walifunguka wafanyabiashara ya madini ni kwamba watanzania uzalendo unaanza kuimarika tena naamini Rais ameyapata mengi kwao na ambayo ataenda kuyafanyia kazi ili nchi izidi kustawi kwa faida ya wote
Kwa upande wa dini pia Rais atakuwa aliyapata mengi mazuri sana pia ila kunalo hilo la kuwepo sehemu za ibada kwenye maofisi ya serikali na maeneo wengine muhimu

Hilo naomba litizamwe kwa umakini kidogo lisije likatuvuruga maana madhehebu yaliyopo Tanzania ni mengi kwa hiyo hatuwezi kuyapatia yote mahali pa ibada sehemu za ibada wajitafutie wao wenyewe kwa sababu pia taifa letu halina dini ndo maana unaweza kuona madhehebu yaliyopo ni mengi sana sidhani kama tutakuwa na pasa za kutosha kumjengea kila mmoja kwa dhehebu lake chumba cha kusalia airport na ukishajenga viwili hapo ni kwamba ujiandae kwa malalamiko ya wengine nao wakidai kutengwa. Hivyo hili nashauri serikali isijiingize

Nilimsikia mama mchungaji mmoja wakidai sehemu za kujisaidia wawapo safarini kwenye usafiri wa mabasi,
Kwa namna nzuri pengine kwenye barabara kuu serikali ingetenga maeneo ambayo utakuwa yanatofautiana baada ya pengine kilomita mia ama mia na hamsini serikali inaandaa eneo kandoni mwa barabara inaweka parking pale panakuwepo na vyoo na pengine mgahawa ama grocery store ndogo kwa ajili maji soda take away na kuwepo na sheria kwamba hizo sehemu ni lazima gari ya abiria iingie ili watu waweze kuji-refresh lakini pia magari mengine yaruhusiwe kupaki malori na hata gari ndogo wakipenda ama wakihitaji ila kuwepo na muda wa kupaki pale kwamba hairuhusiwi kupaki kwa zaidi ya dakika ishirini ama hata nusu saa lakini kupaki ni bure ila grocery zitakazokuwepo zitalipa kodi ambayo itasaidia kulipa wafanyakazi watakaokuwepo eneo hilo kwa ajili ya usafi na kutunza mazingira
 
Status
Not open for further replies.
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom