Status
Not open for further replies.
Namkumbuka sana GWAJIMA Bishop alisema huyu bwana mdogo atamtia hasara na aibu yako wapi? mwaka hata haujakatika kitu hichooo na bado... na ndimi kujaa kwa mdomo
 
ni rahisi Mh. ajiuzulu wadhifa wake,kuliko kufikiria kumfuta kazi Bashiite
 
Tuombee taifa, liwe na amani, afya, maendeleo na Baraka tele. hata kabla ya mussa kulikuwako na farao na filauni
 
Habari za muda huu kiongozi wangu? Shikamoo mzee wangu!

Mheshimiwa Rais, leo nakuja kwako kwa unyenyekevu mkubwa, najaribu kutumia hekima zangu, busara na weledi kujaribu kusema kwa lugha yetu ya kiswahili nawe, Rais wetu, kiongozi wetu MPENDWA!

Mheshimiwa Rais, Nani asiejua kwamba wewe ni kiboko yao? Kwamba umewashughulikia hata watu wa Chama chako, waliokupigania kwenye kampeni, walipozingua, haukuwatazama mara MBILI!

Tunaelezwa. Kwamba ni kweli, umewashughulikia ipasavyo wahujumu uchumi wa nchi yetu, mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma. Wanasema wakisikia jina lako wanazimia, MAFISADI wa RICHMOND, EPA na ESCROW!

Huko nje ya nchi, tunaelezwa kwamba wewe ndie yule "kiongozi ambaye alikuwa akisubiriwa kwa wakati wote, baada ya JK wa kwanza" sasa umekuja, wanakuita "Nyerere of our time" alisema PLO Lumumba!

Mheshimiwa Rais, hapa nyumbani, wasomi, maprofesa wa chuo kikuu kikongwe cha DSM wakaungana na kuweka kongamano, wakitaja na kulinganisha sifa zako na mzee wetu Nyerere, sifa kedekede zikamwagwa!

Mheshimiwa Rais, tunaelezwa, ingawa tunaona, umenunua mijindege mikubwa, hadi "MABEBERU" wameogopa, wametikisika, wametetemeka, wanajiuliza, "anatoa wapi pesa huyu kiumbe?" na umewatikisa kweli!

Haukuishia hapo, umekwenda mbali na kuangusha "mijidaraja ya kutisha" umejenga "mi-flaiova" na naona unatandika mkeka (reli ya SGR) kutoka DSM kwenda Morogoro, watapata taabu sana, tunaelezwa hivyo, wakosoaji wako..

Wanasema, mapato ya ndani yameimarika, ukusanyaji umepanda, uzalishaji umeongezeka, na wanakwenda mbali na kusema "ajira ni kedekede" na wanasema umeongeza bajeti ya Afya sasa.. Imeshiba!

Mheshimiwa Rais, wakulima wa korosho, umewapelekea "mijisenti" na umekwenda kukomboa korosho yao kutoka kwa 'Kangomba' na unasema utanunua mzigo wote, mambo ndio hayo, tupewe nini kingine sie, shikilia 'baba'

Wanasema, wanatueleza kwamba Umejenga mabweni, umejenga maktaba pale UDSM, na hiyo WAMEFANYA wawili pekee, Wewe na Mwalimu, na wasomi wale wanasafiri na kauli mbiu "NYERERE WA WAKATI WETU"

Sasa naona Machinga na mama ntilie wanatengenezewa vitambulisho. Safi. Naona na wanafunzi sasa wanasema mikopo ya elimu ya juu "kuchereee" nafikiri wanamaanisha, sasa wanapata pesa nyingi, vilio vyao sivisikii kwa sikio la kawaida!

Kule Kibiti tumewafukuza kabisa hawa "maharamia" ambao walitamani kuchafua taswira ya nchi yetu. Walikuonesha utovu wa nidhamu mheshimiwa Raisy, ukiwa Pwani ziarani, wakafanya TUKIO, loh! Hawafai hawa watu!

Mheshimiwa Rais, kama kweli haya yote ambayo yanaelezwa ni kweli, na yamefanyika hadharani, watu wanaona kwa macho yao, wanashuhudia, kwanini tunatumia nguvu kuwaaminisha na kuwataka WAONE?

Mheshimiwa Rais, kama kweli haya yamefanyika, una sababu gani ya kuzuia hawa "wapinzani wako kisiasa" kufanya siasa za majukwaani, ili wakifika huko wakose AGENDA ya kukuongelea na wapigwe mawe jukwaani?

Kama kweli tumewapa wananchi ajira, tumeimarisha uchumi wao, kuna sababu gani ya msingi sasa hata kuogopa hawa wanasiasa wasikutane na hao wananchi, ili wakazomewe huko mtaani?

Mheshimiwa Rais, kama ni kweli wewe ni "Nyerere wa wakati huu" ni kwanini unafikiri njia sahihi ya kuleta maendeleo kwa wananchi wako, ni kuzuia shughuli za. Kisiasa za vyama vilivyosajiliwa kisheria kufanya siasa?

Mheshimiwa Rais, umefanya yote hayo yanayotajwa, kwanini UOGOPE KUKOSOLEWA? kwanini wakosoaji wako wengi wanapata mashtaka ya uchochezi? Kwanini ni HARAMU sasa kuhoji ya msingi kuhusu utawala wako? Mifano ipo mingi sana!

Kama umewapa wananchi wako maendeleo, hawakudai kitu, kwanini hawa wapinzani wako unawazuia hata kufanya vikao na mikutano yao ya ndani? Polisi wako wanawakamata na kuwaweka mahabusu!

Mheshimiwa Rais, katika kelele za Maandamano YA UKUTA (2016) baadae yale ya Mange Kimambi (2018) imetunushiwa nguvu kubwa sana ya askari wako barabarani, gharama na. Muda ingawa ndio kazi yao..

Je, hawa watu wakiandamana na agenda zao mkononi, wakapewa ulinzi kuzuia uhalifu wa mali za raia, jioni ikawadia wakaenda kulala bila risasi au bomu kurushwa kwao, tunaamini tutaathirika eneo lipi kwa kiwango gani?

Mheshimiwa Rais, kuna wakati hata Kenya na Uganda walitamani kupata kiongozi kama wewe, Mwanzo katika utawala wako. Unafikiri kwanini sasa hawaimbi nyimbo zako? Hawataki tena 'sampuli yako' katika tawala zao? Umewahi kujipa muda kuuliza hilo mheshimiwa?

Umewapa wananchi wanachokitaka, watakupenda, hautatumia nguvu kuwashawishi wakupende! hakuna sababu ya kuwaeleza kwamba sasa wakuombee. Ili kuwa na hekima, ni wakati wa kuwatumikia, kwa busara na hekima za uongozi!

Mheshimiwa Rais, "dudu liumalo kwanini tulipe kidole?" unasema wapinzani wako wanatumiwa na MABEBERU kuharibu taswira ya nchi yetu, kama ni kweli, hawa ni wasaliti, lakini haujawahi kutueleza, HOW?

Sisi tunakopa pesa kwa hao WATU, wanachangia hadi pesa kwenye bajeti yetu, wanajenga miradi ya maendeleo, na baada ya hapo tunawaita IKULU na kuwapa jina la WAHISANI au MARAFIKI

Lakini what watu hawa wakitupa masharti kutokana UVUNJIFU wa masharti ya misaada na mikopo yao, tunawaita MABEBERU, kwanini sasa tusiache kabisa kushirikiana nao katika maeneo hayo, TUJIENDESHE, kama kweli sie tumekomaa? Miaka 57 SIO HABA!

Mheshimiwa Rais, kweli kabisa, inakera sana kuvaa "jezi nyingi" yaani hatueleweki sisi ni watu wa ITIKADI gani, hatujulikani kama sie ni mabepari au wajamaa, hatujui kama ni wahafidhina au waliberali, sehemu zote tupo!

Hii sasa ndio Chanzo cha kuanza kuletewa masharti ya USHOGA nchini kwetu, lazima tutambue kwamba, kumiliki ITIKADI na FALSAFA ya Taifa, na kuacha kuomba na kupokea kila kitu, kutapunguza hii misaada yenye masharti magumu.

Pia, lazima tutambue kwamba, nchi yetu haitambui USHOGA kama haki za binadamu iwa Sheria za ndani, isipokuwa imekubaliana na jumuiya za kimataifa kuheshimu haki za makundi hayo ya kijamii, na kuheshimu shughuli zao. Tumetia na saini kabisa.

Mheshimiwa Rais, kama ndivyo, kuna njia za kushughulika na matatizo ya namna hii katika Jamii yako, na sio kwa kutumia njia ambayo aliitumia yule kijana wako MPENDWA sana, kutoka MZIZIMA, ile ndio imetuletea hizi Kashi-Kashi zote hadi kuazimiwa!

Mheshimiwa Rais, siku zote 'chuki humchoma mtu anaeihifadhi', tujitahidi kuhubiri upendo, twende kanisani tumuombe Mungu wetu atupe hekima na busara, uvumilivu na upendo Kati yetu. Tusiishi kwa kuichukia nafsi ya mwingine..

Kama ambavyo uliweza kumsaidia Ruge Mutahaba kwa kumpa zaidi ya 45M na hata kuubeba ipasavyo msiba wa Erick Shigongo basi onesha hayo kwa Ndesamburo na hata Tundu Lissu. Ndio UKATOLIKI huo!

Pamoja na umoja na mshikamano wetu. Tutakuwa tunafanya kazi bure ikiwa tu hatuna AMANI ambayo inaletwa na UHURU watu, haki ya kujieleza ni muhimu, ingawa ina mipaka yake. Inapaswa kulindwa!

Mheshimiwa Rais, waruhus hawa watu wakupongeze, wakusifu na wakuimbie kwa nyimbo, vinanda, vinubi na vigelegele, lakini kamwe usiwazuie wakikukosoa wewe na uongozi wako. Uvumilivu unapimwa hapa!

Kiongozi atakosolewa, atajengwa na wanaoweza kumuonesha makosa yake, watu ambao hawatafuti TEUZI mbele yake, ndio wanaweza kumueleza ukweli, wasitendwe visivyo, sio wahaini! Ni wazalendo wa Taifa lako hili.

Yesu Kristo Pamoja na miujiza yote alidhihakiwa na kukosolewa na kuuwawa. Mtume Muhammad (S.A.W) alidhihakiwa na hata manabii wakubwa, Mussa na WENGINE walipata wakati mgumu kueneza injili, sembuse wewe Rais wangu? Waruhusu wakukosoe!

Mheshimiwa Rais, mimi yangu ni mengi sana, ujumbe wangu kwa mwaka 2018 ni huu, nakutakia Heri ya mwaka mpya, na hakika Christmas ni njema kwako, maana umemaliza mwaka mwingine pasi-na kwenda kwa "MABEBERU" TUNALINDA RASILIMALI ZETU, WASIZIPORE!

#MMM, Martin Maranja Masese
 
Wakuuuu niwe mkweli kabisaaa, huyu rais wa jamhuri Ya muungano wa Tanzania anafanya mambo ambayo ndio hitaji kuuu la kwangu Mimi hivyo naomba watumishi wake wa tiss mlioko humu mmpelekeee salam za Pekee kutoka kwangu binafsi na ninamhakikishia kuwa Niko nyuma yake na ninamuombea Kwa MUNGU ampe Afya njema na kumlinda ili aendelee na haya majukumu MAGUFULI HOYEEEEEEEE
 
Sawa mkuu, wamekusikia. Pia upokee na wenye maoni tofauti
Wakuuuu niwe mkweli kabisaaa, huyu rais wa jamhuri Ya muungano wa Tanzania anafanya mambo ambayo ndio hitaji kuuu la kwangu Mimi hivyo naomba watumishi wake wa tiss mlioko humu mmpelekeee salam za Pekee kutoka kwangu binafsi na ninamhakikishia kuwa Niko nyuma yake na ninamuombea Kwa MUNGU ampe Afya njema na kumlinda ili aendelee na haya majukumu MAGUFULI HOYEEEEEEEE
 
Hapo vip!!

Katika hawamu hii, hawajafanikiwa kuleta na kufanya mpango wa maendeleo inayogusa nchi nzima bali ni hizi program ndogo zinazogusa ukanda fulani, mfano ununuzi wa ndege inamsadiaje mtu wa nachingweya mtwara, au treni ya umeme kutoka dar kwenda mwanza inamsadiaje mtu wa Oldadai -Arusha.

Mfano kipindi cha Kikwete ulianzishwa mpango wa shule za Kata Tanzania nzima na niwazi huu mpango imewagusa na kuwasaidia watanzania wengi katika kila kona ya Nchi.

Pili Kikwete alifanya mpango wa kujenga barabara za lami Nchi nzima na mpango huu imemgusa na kuwasaidia watanzania wote.

Mimi tokea uingie madarakani bado sijaona mpango uliokuja nao Kwa lengo la kuwasaidia watanzania au kuibadisha Tanzania Kwa ujumla, hizi Sijui treni za umeme na ununuzi wa ndege ni projects ndogo ndogo sana.

Hivi washauri wa rais Kwa nini msimshauri vizuri katika eneo la uchumi , mkaacha kumuogopa, Kwanini yeye ni Mungu bhana.

Hivi viprojects vidogo vidogo anavyofanya ni za level za mawaziri na wabunge.
Heeeee mpaka nimeshangaa, Kodi ya shirika la Umma inaingia kwenye kapu Kuu la makusanyo ya Kodi sio Halmashauri. Yaani TRA ndo inakusanya direct.

Baada ya makusanyo hayo, matumizi yanapangwa nchi nzima bila kujali hii imetoka SRG au ATCL

So hata huko kwenu mtapata manufaa yanayoletwa na ukusanywaji wa Kodi
 
Maji ambalo ni hitaji muhimu kwa uhai wa binadamu ni issue Tanzania karibu yote. Wakati wa kiangazi wenye nguvu hupata rizki kwa kuchotea maji wale wasio na nguvu au wenye u shuleni wa maisha.

Pesa inayotumika kugharamia maji ingeweza kuboresha makazi na kudhibiti wadudu kama mbu, tungedhibiti malaria.

Ulizia pesa ya budget ma maji mwaka huu wa fedha iliyofika Wizara ya maji.
Biashara inayoongoza Duniani siku zote Ni biashara ya Dawa za Binadamu. Matajiri wakubwa Duniani Kama wakina Bill Gates ndo wameshikilia hizo biashara za dawa ulimwenguni.

Sasa ukitaka kumaliza malaria, uwe umeshaandaa ugonjwa mpya ili dawa ziendelee kununuliwa
 
Unaishi dunia gani mkuu,elimu bure pamoja na uboreshaji wa huduma za afya kwako sio maendeleo?
Hakuna kipindi Serikali imefanya vizuri kwenye Sekta ya Afya Kama msimu huu wa Magufuli.

Mpaka WHO wametoa riport ya kuridhika na Hali ujue si mchezo.

Bajeti ya Afya imeongezeka Mara Tano zaidi ya ilivyokuwa kipindi Cha wawamu ya nne.

Hakika tuko pazuri.
 
Kitufe cha like hakipo....nalazimika nikunukuu.

Ukumbi wa diamond jubilee ulikuwa kimya pale mama Mghwira aliposema tunataka katiba mpya kama kichocheo halali cha kuleta mabadiliko.

Hakika zile ndio siasa.......siasa mpya.....Huyu mama ametokea kupendwa ghafla.
great one
 
Nimewahi kufungua andiko mahala nikakuta tamko la mkuu kuwa askari akiua jambazi apongezwe na apandishwe cheo maana askari wetu hawajawahi kumuonea mtu,nalifikiria sana hilo andiko au tamko(kumbuka kauli ya mkuu ni sheria)sasa nasikia kuna askari kaua askari mwenzake pamoja na mke(mtalaka wake)hivi huyu si anastahili pongezi?kumbuka kauli ya mkuu,,,akiua jambazi,,sasa inakuaje yule askari akamatwe na kuwekwa ndani wakati mkuu kasema askari akiua jambazi apandishwe cheo?kumbuka kauli ya mkuu haikuhusisha chombo kingine kufikia maamuzi yale kuwa aliyeuwawa ni jambazi au la,ni suala la muuaji(askari)kutamka tu kuwa nimeua majambazi baaaas anapanda cheo,,,wajuzi niambieni kwa kauli ya mkuu huyo afande atakua na kosa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom