mpimamstaafu
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 4,445
- 4,704
Hakuna haja kwani kujenga fly over haimgusi mwananchi? Aendelee kujenga maendeleo ya VituHapo vip!!
Katika hawamu hii, hawajafanikiwa kuleta na kufanya mpango wa maendeleo inayogusa nchi nzima bali ni hizi program ndogo zinazogusa ukanda fulani, mfano ununuzi wa ndege inamsadiaje mtu wa nachingweya mtwara, au treni ya umeme kutoka dar kwenda mwanza inamsadiaje mtu wa Oldadai -Arusha.
Mfano kipindi cha Kikwete ulianzishwa mpango wa shule za Kata Tanzania nzima na niwazi huu mpango imewagusa na kuwasaidia watanzania wengi katika kila kona ya Nchi.
Pili Kikwete alifanya mpango wa kujenga barabara za lami Nchi nzima na mpango huu imemgusa na kuwasaidia watanzania wote.
Mimi tokea uingie madarakani bado sijaona mpango uliokuja nao Kwa lengo la kuwasaidia watanzania au kuibadisha Tanzania Kwa ujumla, hizi Sijui treni za umeme na ununuzi wa ndege ni projects ndogo ndogo sana.
Hivi washauri wa rais Kwa nini msimshauri vizuri katika eneo la uchumi , mkaacha kumuogopa, Kwanini yeye ni Mungu bhana.
Hivi viprojects vidogo vidogo anavyofanya ni za level za mawaziri na wabunge.