Status
Not open for further replies.
Mimi kama Mtumishi,

Kwa Muheshimiwa Rais John Pombe Magufuli, haya ndiyo niliyofunuliwa na nikuombe unitegee sikio.

Ulitangazie Taifa zima kuwa katika hali ya maombi ya nchi nzima na Maombi haya yawe ya wiki moja na ya watu wote wenye mapenzi mema na nchi yao na yawe ya kufunga walau saa 12 kila siku na kilele chake iwe siku ya tarehe 5 Novemba 2016 mwaka mmoja baada ya kuapishwa kwako kitaifa yafanyike Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Pengine utaniuliza ni Mungu yupi tutakuwa tunamuomba watu wote hawa? Jibu ni Mungu wetu wa Taifa letu, Mungu wa Watanzania wote, tunayemuimba katika wimbo wetu wa Taifa…Mungu Ibariki Tanzania….. Ili Mungu huyu atubariki lazima Mh Rais kila mmoja wetu tumpe nafasi ndani ya mioyo yetu, tumuombe kwa nguvu zetu zote.

Maombi yetu yawe haya (Prayer Points)….Pengine na wewe utapenda kuongezea …ruksa.

1) Kumshukuru Mungu wetu kwa yote aliyotuwezesha kwa huu mwaka mzima 2016, siyo siri Mh Rais sasa hivi heshima ya Mtanzania inaonekana, tunaheshimiana maofisini, mitaani, nikupe mfano tu mmoja nilikuwa nikishughurikia transfer ya hati yangu kwa miaka 5 sasa kila nikienda naambiwa uje baada ya wiki 3 mpaka nilikata tamaa. Nimeenda mwezi wa sita mwaka huu kwanza nilipofika nilipewa kiti na wahudumu wale wale na kusikilizwa haraka sana. Na kila aliyekuwa akipita ananiuliza “Mzee umesikilizwa” na siku hiyo hiyo hati ilipelekwa kwa kamishna na kusainiwa na nikaondoka nayo, heshima ipo sasa hivi. Tumshukuru huyu Mungu aliyekutia nguvu Mh. Rais.

2) Maeneo mengi katika nchi yetu yanaingia katika msimu wa kilimo, hivyo tumuombe Mungu wetu alete mvua ya kustawisha mazao yetu kwa wingi zaidi ili tuweze kuuza nje ya nchi bidhaa za mazao nakupata kipato kikubwa kwa maendeleo ya wananchi wako wa Tanzania. Mungu huyu ninaimani atafanya na bila kuchelewa. Kilimo wanategemea watanzania wote.

3) Hofu ya Mungu huyu wetu, itufunike Watanzania wote ili dhuruma, rushwa, vurugu, mateso, wizi, yatoweke katika jamii yetu, watu waishi kwa amani na nchi yetu iwe kisiwa cha amani kweli kweli. Mh Rais watu wako wakiwa wacha Mungu ndipo itakuwa rahisi sana kuwaogoza na kufikia malengo ya maendeleo uliyoyaweka kwa watu wako. Najua unania njema na ya dhati kwa watu wako.

4) Kutokee wawekezaji ndani na nje ya nchi walio na nia njema wanaojali maendeleo ya watu wako ili tuifikie adhma yako ya kuwa Tanzania ya viwanda. Kila kijiji kiwe na kiwanda cha kuyaongezea thamani mazao yanayopatikana na kuuza kwa faida katika sako la ndani na nje ya nchi.

5) Mungu aibue vipaji katikati ya watu wako, Watanzania wenye kufikiria na kubuni mipango ya kuendeleza taifa lao. Vijana shupavu wenye mapenzi mema na nchi yao waonekane na kulitumikia taifa lao kwa moyo safi.

6) Tukemee unyonge ndani ya watu wako, wasijione kuwa hawawezi kila kitu na kuanza kulialia tu, bali Mungu huyu atujaze ujasiri wa kuwa tunaweza maana tunaye Yeye atutiaye nguvu na yuko upande wetu tutaibuka washindi katika mambo yote. Mh Rais siyo utani tukimuweka Mungu wetu juu yetu uchumi utakua kwa Zaidi ya 100% kila mwaka. Amini haya Mh. Rais

7) Mihimili yote yaani Bunge, Mahakama na Serikali zifanye kazi kwa ufanisi mkubwa na kwa hofu ya Mungu zikilenga kuleta maendeleo ya watu wako

8) Vyama vote vya siasa vihubiri maendeleo, upendo na amani kwa Watanzania wote, Mungu awafunulie wanasiasa wote kuona katika jicho la Kitaifa Zaidi, tujiviunie Utanzania wetu.

9) Jeshi letu ambalo mimi binafsi huwa nalimani sana nalo lipewe mbinu mpya za kuweza kupambana na maadui wetu wa sasa yaaani Ujinga, Maradhi na Umaskini. Hawa ndiyo maadui wetu kwa sasa Mh. Amiri Jeshi Mkuu, Mungu awape mbinu za kisasa kupambana nao hawa.

Nakuandikia mafunuo haya Mh Rais nikijua kuwa wewe ni Jemedari wetu, kiongozi wetu, uliye mstali wa mbele katika vita. Na naamini ukiwaongoza watu wako katika kumulilia huyu Mungu wetu hatakawia kushuka na kutuletea majawabu ya yale tumemuomba, napengine siku ya kilele hicho ambacho kitafanyika uwanja wa taifa akashuka kwa mfano wa mvua,, amini haya Mh. Rais.

Hatuwezi kubarikiwa kwa kuimba tu Mungu ibariki Tanzania bila ya kumtengea siku maalumu ya kuzungumza naye kumueleza shida zetu zinazotukabili. Nilazima tumtambue Mungu wetu na tuweke utaratibu wa kumshukuru na kumuomba walau mara mbili kwa mwaka kama taifa.

Ukisimama katika haya Mh. Rais nchi itaendelea kwa kasi ya ajabu mno mtu wa Mungu. Lakini ni lazima ukubali kuuwatesekea watu wako na pengine ukubali kuitwa mwendawazimu,,haya ndiyo mambo ya Mungu. Taifa lazima lijengwe kupitia hofu ya Mungu ili tuendelee.

Watangazie Watanzania wote, viongozi wa dini zote juu ya maombi ya wiki nzima na kilele chake iwe siku ya tarehe 5/11/2016 uwanja wa Taifa, kitaifa, na kila mkoa utaadhimisha katika viwanja vya mkoa husika na ikikupendeza hata vijijini.

Haya ndiyo niliyofunuliwa mimi kama mtumishi kwa Taifa lako, Uongozi wako, na watu wako yaani Watanzania.

Ahsante sana kwa kunitegea sikio.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
f926fbaf691f53accc27f0378d76026b.jpg
 

Attachments

  • 1476911974942.png
    1476911974942.png
    27.1 KB · Views: 42
10) Mungu ampe Mh Rais moyo wa kukubali kwamba kakosea na kujirekebisha siyo aibu bali ni utumishi tukuka.

11) Mungu amjalie Mh Rais atangaze ajira mpya na apate fedha za kuwalipa na aache visingizio kwamba ni watumishi hewa ndo wanakwamisha.

12) Mungu ampe Rais washauri wazuri watakaomuambia UKWELI juu ya hali halisi na njia za kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

13) Mungu amjalie Rais moyo wa kutimiza ahadi yake ya kuwapatia wanafunzi hasa watoto wa Kimaskini mikopo kama alivyoahidi katika sera zake 2015.
 
Hili janga linaloendelea sasa la mikopo ya elimu ya juu ndilo linamtoa Rais midomoni mwetu kama mpigania haki kwa wanyonge ilihali vijana anatutesa kuanzia ajira hadi kusoma kwetu.
 
Kama mtu anakaa na kuandika haya ule utafiti uko sahihi kabisa. Bora nikose transfer ya hati, Ila nipate chakula na nisiwe na msongo wa mawazo ya kazi. Leo hii unaenda kazini na hujui kama utarudi ukiwa na ajira yako, kila mwenye kacheo anamtishia alie chini yake.
 
Haya kuna waziri huko kasema kila mwanafunzi awe na miti mitatu .. La sivyo hapati cheti chake
 
Sjawahi kaa kufkiria kumuombea malaika au tajiri wakt nina uhitaji na wapo maskini wenye uhitaji...
Nsomba hta kwenye liturugia ile kipengele ya kuombea taifa na rais kiondolew wafanyie marwkebisho haiwezekan Mungu huyo tunae muomba asituskie jiulize tunakosea wapi.. Mungu alisema omben mtapewa tafteni mtapTa lakin kwa hali iliopo sasa na kadri kila jpl sala znafanyika

Viongoz wetu wakae waseme na Mungu kumbuka imani pasipo matendo ni kazi bure pia matendo bila upendo pia ni bure

Tuliachiwa amri iliyo kuu ni upendo
Mpende jirani yakp kama nafsi yako na hii ndio amri kuu..
Sasa kama malaika wakiish kama mashetani
Ukimdharau mpinzani na kuto heshimiana hyo amri inakuwa haitekelezeki sasa eew endlea omba ukimaliza ulete mrejesho
Pia maombi hyalazmishwi wala kupangiwa
 
Sometimes nafikiria labda aliingia kwa bahati mbaya vile ..this is realy an omen kwa taifa hili,ajue tuu at this age ni wachache ambao wanaweza wakapumbazika na cheap politics wanazoleta kwenye mambo muhimu yanayogusa maisha ya watanzania directly!!
 
Siwezi muombea huyo jamaa hata siku moja milele! Aende zake na ww na maombi yako mtakutana na jamaa zako huko huko, kwangu never ever ever nimuombee kwa lipi? Yaani mpaka nimehisi kichefuchefu!
 
Wewe ni mnafiki kama wale viongozi wa dini wamatamasha ya kuombea amani.Sijasikia kiongozi wa dini anaombea HAKI itendeke tz kila siku maombi ya kinafiki amani amani hiyo amani bila haki utaipata?
 
Gambo hawezi kutenguliwa uteuzi kwa sababu ya propaganda za bavicha.

Gambo amefanya makubwa Arusha kuliko hii singeli isiyo na maana yoyote tunayojaribu kuimbiwa na chadema.

Gambo alipofika tu Arusha alifumua uozo wote wa chadema ikiwemo madiwani wa chadema kujilipa posho za kifisadi, aliwaamrisha hela zote wazirejeshe na akaamru zikalipe madeni ya walimu..


Kwa mazuri haya, chadema mtasubili Sana uteuzi wa Gambo kutenguliwa.
 
10) Mungu ampe Mh Rais moyo wa kukubali kwamba kakosea na kujirekebisha siyo aibu bali ni utumishi tukuka.

11) Mungu amjalie Mh Rais atangaze ajira mpya na apate fedha za kuwalipa na aache visingizio kwamba ni watumishi hewa ndo wanakwamisha.

12) Mungu ampe Rais washauri wazuri watakaomuambia UKWELI juu ya hali halisi na njia za kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

13) Mungu amjalie Rais moyo wa kutimiza ahadi yake ya kuwapatia wanafunzi hasa watoto wa Kimaskini mikopo kama alivyoahidi katika sera zake 2015.
14) MUNGU amkumbushe pia ule uhakiki wa vyeti vya fomfooo usiishie kwa walimu na madakitali manesi n.k.. APITIE PIA VYETI VYA WAJEDA WOOOTE wale waliotumia FEKI awapige chini waingie kitaani kama sie.
 
Gambo hawezi kutenguliwa uteuzi kwa sababu ya propaganda za bavicha.

Gambo amefanya makubwa Arusha kuliko hii singeli isiyo na maana yoyote tunayojaribu kuimbiwa na chadema.

Gambo alipofika tu Arusha alifumua uozo wote wa chadema ikiwemo madiwani wa chadema kujilipa posho za kifisadi, aliwaamrisha hela zote wazirejeshe na akaamru zikalipe madeni ya walimu..


Kwa mazuri haya, chadema mtasubili Sana uteuzi wa Gambo kutenguliwa.
ACHA UZOBA WEYEEE MAMA!! hizo posho zilikuwa zinatumiwa na mburula sisiem tangu wameshikilia hizo kata.. asa leo wamepigwa chini ndio mnajifanya eti mnapunguza matumizi... ...mbaffffff kapunguzeni matumizi kwa waume zenyu
 
ACHA UZOBA WEYEEE MAMA!! hizo posho zilikuwa zinatumiwa na mburula sisiem tangu wameshikilia hizo kata.. asa leo wamepigwa chini ndio mnajifanya eti mnapunguza matumizi... ...mbaffffff kapunguzeni matumizi kwa waume zenyu
Chadema ni watetezi wa wanyonge walitakiwa wazikatae hizo posho.

Cha ajabu wakaendelea kuzitafuna kwa spidi kubwa,!!
Kumbe na chadema ni mafisadi tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom