Status
Not open for further replies.
Mkuu usifosi tufanane wote, kila mtu ana wajibu kuwa na uhuru wake ili mradi asivunje sheria.

eg. wewe kama unatumia choo cha kukaa, acha sisi wengine tutumie cha kuchuchumaa
 
Iwapo unapenda vijana na taifa lao Basi huna budi kupiga marufuku kamari zote nchini kwani ni ukoloni hata Kama wanatulipa Kodi wanazoa fedha nyingi sana.pia pombe hasa kali hizi portable spirit hazina tofauti na viroba ni janga linaloua vijana wengi piga marufukuu.kisha ukemee uasherati wowote kuanzia biashara ya umalaya ya kuuza mwili peleka Askari maeneo Kama kambi ya fisi,sudani,mwananyamala n.k wakasafishe maeneo Yale Kisha tangaza nchi nzima biashara hio ikome pia anzisha kampeni ya kitaifa kuwakataza na kuwaonya watu kuangalia picha za porno (x) katika mitandao.mimi nakuja kusema na kuitetea kweli na ntakuja kukwambia mengine mengi.
Badala ya kushughurikia mambo ya muhimu, uchumi kuwa hivi, gharama za maisha kuwa juu, mnakimbilia vitu vya kipuuzi!!kuna mambo mengine huwa yanapungua yenyewe tu endapo hali ya uchumi ikiwa nzuri, ila sio kuisha kabisa, na kuisha haiwezekani, hata atumie JWTZ.
 
Mlevi akinywa serikali inaingiza kodi, mkamaria akibet serikali inaingiza kodi, malaya akinunua condom na kulipia lodge serikali inaingiza kodi.

Labda kama unataka haya mambo yaondolewe irudishwe kodi ya kichwa ufuate mpaka pale ghetto kwako TRA waje kuchukua chao sawa. Ila unge suggest na alternative ingependeza, labda rais akataze pombe alafu aongeze kodi kwenye kahawa na chai. 😁
 
Kumuunga mkono rais, si suala la matakwa ya mtu ni suala la kikatiba na kisheria. kwa hiyo wote tunamuunga mkono ndio maana tunatekeleza maagizo yake yote kwa utimilifu.

Wasiwasi wetu ni kununua ndege hali ya kuwa barabara zetu zinazounganisha wilaya ni mbaya mno, kutokuajiri, kuwanyima watoto wetu mikopo, kutumia fedha za dawa kununua wapinzani? kupotea kwa watu nk, nk.

Bado tunamuunga mkono, tutamlinda, tutamtunza lakini na yeye afikirie haya malalamiko.
Kumbuka kipind cha rais kikwete kila mpinzan alisema nchi kubwa haina hata Airbus moja ina kandege kamoja ten kadogo mhhh jmn Leo hii ndege zipo za kutosha maneno ten onhoo lami mbovuuu hahahahaaaaaaaaa This is Tanzania hahahaaaaa naipenda nchi yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mhe: Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Popote ulipo amani ya bwana iwe.

Kwa heshima na taadhima ninaomba kutumia fursa hii kukushauri kuhusiana na watumishi hewa na watumishi waliokuwa na vyeti feki (makanjanja). Nikianza na watumishi hewa (non existed workers) hawa hawatakiwi kujadiliwa sana kwa sababu hawapo ni majina tu yalioingizwa kwenye system na wajanja wachache ili kujipatia fedha.Janan nimekusikia vyema ukizindua mpango wa TASSAF na ulizungumzia kaya hewa.Hii inaonyesha jinsi gani wajanja wachache wanazitumia ofisi zao katika mambo yasiokubalika.

Niliwahi sikia pia kuna wanja wachache wanaotumia mpango wa kusitishwa kwa uhamisho watumishi kujinufaisha kwa kuwasaidia watumishi kuhama kutoka kwenye mazingira wasioyapenda na hivyo kupelekea upungufu watumishi katika sehemu hizo.Nashauri kuundwa kwa mifumo ya taasisi imara itakayo zuia watu wachche kujinufaisha na mambo hayo.

Sehemu ya pili nitajikita kwenye watumishi waliokumbwa na sakata la vyeti feki hawa wengi wao wamejiendeleza naaamanisha wamesahihisha makosa yao kama mtu alikutwa na chet kisichostahili cha form four au form six amefsnya mitihani yake na amefaulu na kuna wengine walikumbwa navyeti feki vya chuo pia wamesoma na kupata vyeti upya hivyo kwa heshima na taadhima tunakuomba mhe: raisi uwarudishe kazini
 
Hapa tutakutana kujadili na kuunga juhudi utendaji kazi wa Mhe Rais wetu pamoja na Serikali yake

Hii ni special kwaajili ya matukio yote yanayo Muhusu Mh. wetu Rais Magufuli
Kupeana habari n.k

Haya Team JPM Tukae humo

20200223_230034.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom