Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,479
- 30,144
Rais Mahufuli, tumeamua kuandika waraka huu ili tukuoredheshee mambo kadhaa.ambayo sisi wapiga kura wako tunakulilia.
1. Double Standard: Hii serikali yako imekuwa ya double standard ya hali ya juu ambayo haijawahi kuwepo katika serikali za nyuma.
Nitatoa baadhi ya mifano ifuatayo;-
Umetangaza kuwa wale watumishi wote ambao watakuwa wamefoji vyeti hutakuwa na huruma nao, kwa maana hiyo utawafukuza kazi.
Ni kweli maelfu ya wafanyakazi umewafukuza kazi bila huruma, lakini ilipofika wananchi wako tukakueleza kuwa Mkuu wako wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda ni miongoni ya watu waliofoji vyeti na jina lake halisi Mkuu huyo wa Mkoa ni Daudi Bashite, tukashangaa kuona unatwambia kuwa huyo Mkuu wa Mkoa hata kama hajui kusoma A wewe hujali ili mradi tu anakukamatia wauza madawa ya kulevya!
Hilo limetushangaza sana sisi wananchi wako kwa kuwa wapo baadhi ya wafanyakazluliowatimua kazi ambao ni wachapa kazi lakini hiyo "excuse" hijaizingatia na badala yake umewatimua kazi!
2. Dharau kwa wapiga kura wako:
Tumekusikia wakati wa ufunguzi wa barabara za juu pale Ubungo ukisema kuwa wewe huwa husikilizi kelele za wapiga kura wako, kwa kuwa ni wewe mwenyewe ndiyo ulienda Dodoma kuchukua fomu ya Urais na hukushauriwa na mtu yeyote yule!
3.Umekuwa ukisema kuwa katika serikaki yako hutakuwa na mdhaha hata kidogo juu ya watoaji na wapokeaji rushwa.
Tunakumbuka tukio la Aru Meru ambalo ulionyeshwa "video clip" ya Mkuu wako wa wilaya, Alexander Mnyeti akiwapa rushwa madiwani wa Chadema wa jimbo hilo. Badala ya kumweka "benchi" mteule wako huyo ili apishe uchunguzi, ndiyo kwanza ukampandisha cheo na kuwa RC wa Manyara!
Kwa kweli vitendo hivyo vimetukatisha tamaa sisi wapiga kura wako kiasi ambacho tumegundua kuwa kuna baadhi ya wateule wako ambao ni "vipenzi" vyako vikubwa na hata sisi wananchi tutakuja na ushahidi wa wazi kabisa wa wateule hao, kwako ni untoachables!
Kwa kuwa tunajua kuwa huko siku za nyuma ulimtumbua Waziri Nape Nnauye kwa "kosa" tu la kuunda Tume ya kuchunguza tukio la uvamizi wa Clouds Media, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, akiwa na askari wenye silaha za moto.
4. Kumekuwa na kelele nyingi sana za kukuomba kutokana na matukio ya mfululizo ya watu kupotea, kuuawa na kupotea, basi baadhi ya wateule wako, akiwemo Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba na IGP Simon Sirro wajiuzulu au uwatimue kazi ili kupisha uchunguzi wa matukio mengi mno ya mauaji wa wananchi wasio na hatia. Lakini kwa Bahati mbaya sana, umeweka "pamba" masikioni na kutotaka kabisa kutusikiza kilio chetu sisi wapiga kura wako!
Mungu ibariki Tanzania