Status
Not open for further replies.
Kwenu,

Ni jambo la msingi kwa serikali kuhakikisha huduma za maji ,umeme na afya(zahanati/hospitali) zinapatikana kwa uhakika. Huduma hizi ni kichocheo cha maendeleo kuanzia ngazi ya kaya.

Inasikitisha kuona wananchi wanavyoshukuru mbele ya kamera kwa kuwekewa umeme kana kwamba ni hisani.
Kuna wakati wananchi mkoa wa Manyara walinyimwa umeme wa REA kwa kudai fidia ya mazao yao ambaoyo yangeng'olewa ili kupitisha nguzo. Waliambiwa hakuna fedha ya fidia. Wakitaka fidia wasahau umeme.

Huduma za jamii ni wajibu wa serikali, si hisani. Ni mrejesho wa kodi tunazolipa.
 
Hili suala la mwekezaji wa Mlimani city ni baadhi tu ya machache yanayotia dosari chuo chetu hiki kikongwe nchini, ni vizuri pia ukafanyika uchunguzi kuhusu matumizi na mapato ya hiki chuo. Wafanyakazi wengi wa hichi chuo hawana motisha kabisa ya kufanya kazi hapo, ubora wa chuo unapungua kila kukicha, wataalam vijana wanaonekana hawana kabisa hamu au motisha ya kuwa hapo chuoni. Kuna haja ya Kuinyoosha UDSM irudi kwenye heshima yake iliyopotea siku nyingi.
 
Rais anafanya vizuri sana. Kasoro moja tu ni kuzuia baadhi ya haki za kikatiba kwa wananchi kitu ambacho ni kibaya sana kwa kiongozi. Ni vizuri aheshimu na kuilinda katiba kama alivyoapa. Akumbuke kuwa kuvunja mwiko huwa kunaendana na matokeo au mapokeo hasi au laana. Vile vile kuvunja kiapo nako huwa kunaendana na matoke hasi. Otherwise he is doing good
 
Paaaap naudondosha ukweli mchungu,
Amini nawaambia huwezi kua master wa kila kitu ktk dunia hii ndio maana alie unda gari sie alie unda ndege.
Kwake jamaa yule muda huu mdogo uliobaki chagua kimoja kati ya hivi;-
1- Weka maji nchi nzima
2-Jenga barabara nchi nzima
3- Boresha elimu
4- Boresha afya
5- Jenga reli
6- Jenga viwanda
7- Yafanye maisha kua rahisi ili ajae achague moja kati ya hayo sita aishie zake.
Kwenu nyinyi jamaa panguseni vumbi muanze upya miluzi mingi humpoteza mbwa.



Nasikia konyagi imeshuka bei ni 3,500
 
Ngoja waje wakutukane manake humu kuna nzi wakijani wameajiliwa kwa ajili yamatusi tu nakukashifu vitu ambavyo havimpi sifa boss wao...

ndagha kyala
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom