Jile79
JF-Expert Member
- May 28, 2009
- 17,668
- 13,237
Haijawahi kutokeaTuna Rais wa hovyohovyo mno
Haijawahi kutokeaTuna Rais wa hovyohovyo mno
Wewe kama ni Raiya wa Tanzania na si hawa wingine waliijipenyeza na kujivika Utz humu kwa nia ovu mbili moja ya kutambua fursa mbali mbali za kwetu. Ya pili kumanipulate na ku spin kila jema linaloongekewa au linalotreand kwa lengo la kuchafua nchi yetu na hasa Mkuu wa nchiAmani iwe nanyi wadau.
Natumaini mu wazima na mnaendelea vizuri na majukumu yenu Ni vizuri pia kabla ya yote nikatoa pole kwa watanzania wote walioguswa na tukio la kinyama dhidi ya kiongozi wa upinzani Bw Tundu Lissu.
Nikiwa sijaonekana kitambo sana kwenye jukwaa hili leo napenda kusema kuwa kwa yanayoendelea nchini Tanzania kwa sasa, imebidi niamue kujitokeza tu na labda niamue kutoa mchango wangu wa mawazo hata kama hayatasikilzwa lakini nikiwa na Imani kuwa haya mawazo kwa kuwa ni mazuri na yanajenga basi yatasikilizwa na kufanyiwa kazi.
Sipendi kwenda kwenye hili la Lissu ila kwa kuwa nia yangu ni ya kumsaidia Mh Raisi naona kwa hili la Lissu linaweza kupata utatuzi wake humuhumu.
Kwanza nianze na maana halisi ya wasaidizi wa Mh. Raisi ni kina nani hasa- Kama hamjui kwa Tanzania hawa wanaanzia na baraza la mawaziri ambalo kisheria na kikatiba ndicho chombo kilichopewa mamlaka ya kumshauri Mh. Raisi juu ya mambo yote ya nchi. Kwa hapa Tanzania washauri wengine ni mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na wasaidizi wengine wa Mh Raisi.Wengine ni viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Kwa nini leo nimeamua kuwaelezea hawa watu na kuongea na hawa watu????
Hawa ndo watu wa kumsaidia kumwambia ukweli Mh.Raisi, ukweli wa kiuchumi, ukweli wa kisiasa hata kijamii. Bila shaka kwa hali ilivyo sasa napenda kusema kuwa wasaidizi wa raisi hamfanyi wajibu wenu ipasavyo na inapoelekea nchi itaenda kuanguka chini ya raisi Magufuli. Naomba nielezee kwa mifano hili suala.
KIUCHUMI.
Pamoja na Mh Magufuli kuwa na nia njema kwa nchi hii kiuchumi napenda kusema kuwa mmekuwa mnapotosha vibaya sana Mh. Raisi kiuchumi kiasi kwamba nchi imekuwa ikipata matokeo hasi zaidi kiuchumi zaidi ya chanya.Swali langu kwenu ni kwa nini mmeshindwa kumshauri Mh Raisi juu ya kuanza na njia ya kupiga marufuku vitu wakati mlishaona hili lilianza kuleta matokeo hasi???
Kwenye sukari wasaidizi wa raisi mlipaswa kujifunza sana kwenye suala hili kwa sababu tangu Mh.Raisi apige marufuku uingizaji wa sukari bei ya sukari haijaweza kushuka kuwa kawaida hadi leo hii. Swali langu kwenu hamkujifunza kitu kwenye suala hili???? Hamjui kuwa bei ya sukari hadi leo haijawa kawaida na hili limepelekea nia nzuri ya Mh Raisi ishindwe kuonekana hapa???
Sio tu kwenye sukari, mlishindwa kumshauri Mh Raisi vizuri kwenye pesa kuondolewa kwenye benki za biashara na hadi leo hali ya kifedha imekuwa mbaya sana nchini hasa kwenye mzunguko na upatikanaji wa mikopo.
Kubwa zaidi mliloshindwa kumshauri Mh. Raisi ni hili la Acasia. Hivi ni nani aliwaambia kuwa wazungu unapambana nao kwa mabavu na sio akili? Hamjaona hili suala la Acasia linamuweka Raisi na nchi sehemu mbaya sana kiuchumi? Hivi hamkuona haja ya kumshauri Mh Raisi angeanza na kubadili sheria tena at least kwa kujifanya anawashirikisha hao wawekezaji wa madini alafu badae kunatokea maoni ya wadau ndo tunafikia kurekebisha sheria kwa muktadha tunaoona sie??? Hamkuona hi indo ilikuwa njia sahihi ya kudeal na suala la madini bila kucreate tension kwa dunia juu ya hali ya uwekezaji Tanzania???
Mmemuacha Mh Raisi ametumia nguvu kubwa kudeal na issue ya madini kwa kuzuia usafirishwaji wa makinikia kiasi ambacho kimeleta picha mbaya sana kiuwekezaji hapa kwetu. Kusema kweli mmeiweka Tanzania sehemu mbaya sana kiuwekezaji na pia hata hifadhi yetu ya pesa za kigeni itaathilika sana kwa kuwa kuondoka kwa Acasia msidhani itakuwa raisi kwa muwekezaji mwingine kuja Tanzania kama amefikiria vizuri kwenye kucalculate risk za kuinvest Tanzania. Kwa nchi yenye miaka mingi ya uhuru hii haikuwa approach tuliyotakiwa kuitumia kwenye kudeal na hawa ngozi nyeupe.
Mnamuacha raisi atamke juu ya vita vya uchumi hadharani. Hivi mmeshindwa kumshauri Mh Raisi juu ya madhara ya nchi kutangaza hadharani vita dhidi ya maslahi yao kiuchumi?? Au mnataka siku ya mwisho nchi itapata nini??? Mnadhani kama nchi itafaidika chochote kwenye vita dhidi ya maslahi ya kiuchumi ya wanamagharibi au wanamashariki??? Hamuoni Zimbabwe?? Hamuoni Venezuela??? Hamuoni Libya na Syria???? Mnataka Magufuli aje kukumbukwa kwa sifa mbaya zaidi????
KISIASA.
Mmeshindwa kumshauri Mh Raisi vizuri kiuchumi na mbaya zaidi hadi kisiasa mnaharibu kwenye kumshauri Mh. Raisi vizuri kiasi ambacho leo adui akitumia siasa kutuvuruga anatumaliza kesho asubuhi tu. Hivi kulikuwa na haja gani ya kumshauri raisi kuwafungulia mashtaka wapinzani kila wanapomsema??? Hamuoni hili linawatengenezea huruma kwa wananchi na siku ya mwisho wananchi kuwasikiliza na kuwaamini wao zaidi kuliko wanavyoiamini serikali au Raisi wao???? Mmeshindwa nini kumshauri Mh. Raisi kuimalisha kitengo cha propaganda na uenezi cha chama chake ili kiweze kujibu kila shutuma dhidi ya Mh.Raisi na siku ya mwisho kuanzia wananchi hadi wageni waone kuwa ni game za kisiasa tu????? Hamuoni kutumia vyombo vya dola kujibu hoja za kisiasa zinamuharibia raisi kimataifa n ahata kuharibu taswira ya nchi kimataifa????
Kwako Mh. Raisi, bado nakuamini sana, kama nilivokupigania kwenye uchaguzi sitaacha kukuigania kwa nia ya kutaka uongoze vizuri. Ila naomba uchague wasaidizi wa uhakika wanaojua dunia inavyoenda na figisu zake na mwisho wape uhuru wa kukushauri kwa weredi.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Hivi kitu gani kinamfanya magufuli yeye kutokukaa pembeni????
ILILIINGIZA, ANALIINGIZA NA ATALIINGIZA SN HASARA TAIFA
1. Alikamata kiholela samaki wa magufuli kesi tumeshingwa kwa ujinga wa mtu mmoja
2. Alivunja mkataba wa ujenzi kijingajinga kabisa tumeshindwa kesi
3. Alijiuzia nyumba za serikali
4. Anavunja katiba na sheria za nchi
5. Anavunja sheria za manunuzi na kujipangia matumizi ya raslimari za taifa mfano kujijengea uwanja wa ndege chato, kujinunulia bomberdier kwa maslahi yake binafsi...
MTU WA HIVI ANAFAIDA GANI KWA TAIFA? KWA NN ASIKAE PEMBENI YEYE KWANZA????
Acha ujinga usipende kuongea vitu ili mradi umeongea ,una uthibitisho na unachoongea?Kuna uwezekano wa 99% kwamba waliovamia clouds ndio waliofanya jaribio la kumuua Lissu. Siro alipewa u-IGP ili kikosi cha bashite kiweze kutekeleza matendo yake bila bugudha popote nchini. Amani ya nchi hii inaondolewa na bashite.
Uthibitisho ni kwamba waliovamia clouds bashite anawafahamu na hawajakamatwa.Acha ujinga usipende kuongea vitu ili mradi umeongea ,una uthibitisho na unachoongea?
Sent using Jamii Forums mobile app
Bashite umeishajulikana unajisikiaje?Kuna uwezekano wa 99% kwamba waliovamia clouds ndio waliofanya jaribio la kumuua Lissu. Siro alipewa u-IGP ili kikosi cha bashite kiweze kutekeleza matendo yake bila bugudha popote nchini. Amani ya nchi hii inaondolewa na bashite.