Status
Not open for further replies.
Kwa utafiti mdogo nilio ufanya, Nimefahamu kuwa wanao lichelewesha taifa hili kusonga mbele kwa haraka ni wazee walioko kwenye taasisi na mashirika ya umma. Wengi wao wanafanya kazi kwa mazoea na kutoweza endana na kasi ya serikali yako..hivyo basi fukuza wote ikiwezekana umri wa kustafu kazi uwe miaka 45.

Ajiri vijana wengi uwezavyo..hawa wana nguvu na ari ya kufanya kazi kwa bidii..na wana uwezo wa kwenda na kasi ya serikali yako. Hivyo basi hata dhana ya viwanda itafanikiwa kwa kiasi kikubwa. Nawasilisha
asha sema fomu alichukuwa mwenyewe,wee tulia hataki ushauri
 
Kazi aliyojipa Rais ni kubwa na ya hatari, hebu tumpe nafasi na muda wa kuikamilisha kisha tuje tumpime na kumhoji mwaka 2020 wakati atakaporudi kwetu kutuomba ridhaa tena ya kuendelea. Kule kwetu kuleeeee kuna misemo 2 maarufu inayosema, "Miluzi mingi inamchanganya mbwa" na "usimchambishe mtoto kabla hajamaliza kujisaidia ili usije ukapata shida ya kumchambisha tena". Unapowimuwinda simba unahitaji macho, pua, masikio na viungo vyote viwe timamu ili uweze kuona, kusikia, kunusa na hata kukimbia ikitakapobidi. Kelele na vurugu za vitu vingine sio nzuri kwa mwindaji wa Simba. Hakuna ubishi kuwa mambo anayoyafanya Rais sio mambo yanayohitaji uwepo wa vurugu, kelele na mavumbi yatakayomuondolea umakini kwenye vita dhidi ya wauza dawa, wakwepa kodi, mafisadi na wezi wa mali za watanzania. Na bahati mbaya watangulizi wake kwa kujua au kutokujua ni wahusika wakuu kwenye mfumo uliosababisha mambo hayo anayopambana nayo hivi leo ya wafanyakazi hewa, vyeti feki, kuuzwa kwa migodi, mikata mibovu, wizi wa EPA/Escrow, n.k. Nadhani nadhani nadhani tumsubiri kwanza amalize kipindi chake halafu tuje tumfanyie tathimini.
 
Huu ndio wakati rasmi tunamuhitaji Rais wa watanzania wote. Nchi inahitaji Raisi mwenye uwezo mkubwa wa kuhimili mikiki ya kisiasa ya vyama vingi na demokrasia.

Tunamuhitaji rais mwenye Exposure ya kimataifa na weledi wa uchumi wa kidiplomasia ili tuipate Tanzania ya neema.

Tunamuhitaji Rais wa watanzania wote , makabila yote, dini zote, rika zote, makundi yote ya kisiasa, kiuchumi na kibiashara , kitaaluma na hata makundi ya wasiojiweza.

Tunahitaji Rais mweledi wa utawala na mwenye kufuata misingi ya kisheria katika nchi na anayeweza kubadilika kwa kadiri ya mahitaji ( Flexible President).


Naam Tunaiihitaji Tanzania yetu , tunamuhitaji Rais wa watanzania wote.





Kishada.
 
Wanajamvi tumeona kila sehemu anapoenda suala Kubwa ni wapiga dili, vyeti feki, kila sehemu hewa hewa! Tumechezewa vya kutosha!, barabara n.k ila suala la maslahi ya watumishi wa umma ni mwoga mno kuligusia hivi kwa nini?

Mnyerede
 
Ningekuwa Rais Magufuli, Ninge.......

Kwanza kabisa, ningehakikisha wafanyakazi wote wanaoacha kazi wenyewe (resignation), na wanaofukuzwa kazi, wanapewa fedha zao au FAO LA KUJITOA toka mifuko ya jamii bila ukiritimba na mizengwe yoyote. Hii ingesaidia sana kujiimarisha kisiasa, kwa sababu waathirika wa hizi fedha zilizozuiwa na hii mifuko ya jamii bila maelezo yanayoingia kwenye bongo, wengi ni vijana. Kadhalika uchumi ungepaa sana kwa sababu vijana wengi wangefanya kilimo na biashara, tofauti na sasa ambapo kijana akifukuzwa kazi, hana pa kuanzia kutokana na kutokuwa na kianzio (capital) kwa ajili ya biashara na kilimo.

Pili, ningemteua Tundu Antiphas Lissu awe Waziri wa sheria, au attorney general. Hii ingesaidia sana katika masuala yote ya kisheria, nina hakika serikali ingeshinda kesi zake kirahisi inazoshitaki au kushitakiwa.

Tatu, ningeruhusu mikutano ya kisiasa kwa sababu naamini siasa ni kazi na ndiyo maana vyuoni kuna kozi za kisiasa.

Nne, ningehakikisha kila Mtanzania anapata bima ya afya, kwa sababu maendeleo ya taifa lolote duniani, iwe kielimu, kuchumi, na hata kiteknolojia yanategemea afya imara ya watu wake.
 
My respectful readers, I beg you to forgive me by writing the longest letter. For the past two years I have never written such long articles as this. It was written for the purpose of reaching our President or his assistants through various instruments especially in the newspapers. I sent the article to editors three weeks ago but most of them when I contacted them, they told me they are still editing, the last thing I saw it would lose real meaning and my goal. I decided to write it here on blog. I urge you to read deeply and see if what I am trying to tell Mr. President is logical.

Your comments are important after reading to improve my next articles.

For advice and comments abdulnoor3@gmail.com

AN OPEN LETTER TO HIS EXCELLENCY PRESIDENT MAGUFULI
 
Mtawala ni slave master while mtawaliwa ni slave i hate nikiskiaga hilo neno " katika utawala wangu......sjui anajitoa fahamu ......watch it .....
 
Rais Magufuli mtetezi wa wanyonge,shikamoo

Wanyonge tumekuzoea mara kwa mara umekuwa ukitusemea mambo mbalimbali. Lakini toka urejee kutoka Tanga kwenye uzinduzi wa bomba la mafuta umekuwa kimya sana.

Tunatambua kwamba upo nchini badala ya kuwa South Africa kwenye vikao vya Umoja wa Afrika.Umeamua kubakia nchini kwa kuogopa wale mawaziri wapumbavu kufanya uzembe. Pia kuzuia na kubana mianya ya wapigaji kupiga! Safi sana Rais,lakini mbona kimya sana.

Lakini kubwa ni hili la ndege yetu kutekwa na kuzuiwa kwa sababu ya deni la kampuni ya kigeni. Wanyonge tumepatwa na taharuki,ndege ile umetununulia wanyonge

Wewe kama mnyonge mkuu tunaomba useme neno moja tu roho zetu zitulie
 
Tanzania ni nchi iliyojawa na rasilimali nyingi kama madini, gesi na wanyama pori/utalii

Ili Tanzania ipate maendeleo kodi ni muhimu

Maeneo muhimu ya nchi kupata maendeleo ni rasilimali na Kodi

Sasa inapofikia wana wa nchi wapata shida kwenye mfumuko wa bei kama Sukari na gesi ya ,kupikia, ujue hizo bidhaa zinapigwa kodi kubwa sana

Mafuta ya kupikia, sukari, mafuta taa..ni bidhaa za wanyonge

Je, wanyonge wanafurahia bei ya sukari kupanda kutoka 1800 hadi 3000?

bei ya gesi kupikia juu, je misitu itapona?
 
Hello JF,

Sijui wenzangu mnaonaje,ila naona kama Rais anapotea njia,

Kuwateua maproffesor ,

Taaluma zao ni za zamani,lol

Nadhani hata projects walizozifanya ni za zamani,

Mkuu angeteua fresh graduates,

waliosoma current time,current climate

tena kama salad,ateue kote,

waliosoma ndani na nje,

ningependa pia kuona kuna CONTINOUS PROFESSIONAL DEVELOPMENT kwa hao utakaowateua,namaanisha kuwe na appraisal na training inapobidi,......
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom