Muhimu airejeshe nchi kwenye utawala wa kikatiba, sheria na taratibu zinazoeleweka sio mihemuko na matamko yanayokinzana. Nchi inahitaji TAASISI IMARA sio UTAWALA WA KIIMLA
 
Mh Rais katka mambo ya kufanya hakikisha unafanya yafuatayo:

1.Futa wilaya ya Chato ibaki kata
2.Futa Mpango wa kuipa Chato Mkoa
3.Futa Mpango wa kujenga Daraja la Mwanza la ziwani
4.Ondo miradi ya Maendeleo ya maji chato
5.Ondoa makao makuu Dodoma, na turudi Dar
6. Futa strogiers gourge..tuendeleze gas na tuwape makampuni binadsi kuzalisha umeme ili tupate ajira zaidi
7.Futa SGR ili hera ziendele kwenye maendeleo ya watu na siyo ya vitu
8.Fut mambo ya EFD kwani yanasababisha biashara kusinyaa.
Mama Wafute watanzania Machozi. Magufuli alipeleka vilio kwa Watanzania wengi. Leo sisi Tunamlilia yeye kwa Uchungu, maana si dhani kama aliona kuwa aliyotufanyiani makosa mbele za Mungu. Huenda Hakutubu, sas msaidie Mpendwa wetu kwa kumtakasa.

Alipe fidia kwanza ya wahanga wa Kuvunjiwa majumba Kimara kibamba.
Awalipe fidia wafanyakazi waliofukuzwa kwa vyeti hewa bila ya kupewa mafao yao. Kwani na wao ni watanzania na wanayohaki ya kuajiriwa ,na kama walitimiza wajibu wao ,ni lazima walipwe.
Huenda kilio chao kikageuka Laana kwa Watawala,
 
Hongera Mama,

Tafadhari angalia sana kilimo:- masoko, pembejeo, mbegu, vifaa vya irrigation

TRA:- Kodi rafiki, fair za magari, pikipiki, vifaa vya ujenzi nk.

Criminal Justice system:- kesi zisicheleshwe, watu wasidhulumiwe hasa maskini, wajane, yatima.

Bima ya Afya:- gharama na coverage.

Kuna mengi lakini ni hayo tu kwa sasa.
 
Wengi wa waliokuwa that close to Magufuli, huyu Mama akiendelea kuwa-maintain kwenye system watamsumbua na wanaweza kumyumbisha. She need to come up with a good mix since kuna baadhi ya watu wachache wa Magufuli ni wazuri tu!

Kina viongozi kama Mwigulu, Bashiru, Kabudi sioni wakimsaidia Mama. Ni watu wanapenda radicalization ya watu! Nchi yetu inahitaji kuwa pamoja! Maridhiano na Umoja! Sioni watu wa aina nilizotaja kama watamsaidia Mama. Nisingependa kuona mama akikwama!

Pia Tukianza kumkosoa Rais mpya msituletee mambo ya jinsia hapa.
 
Wengi wa waliokuwa that close to Magufuli, huyu Mama akiendelea kuwa-maintain kwenye system watamsumbua na wanaweza kumyumbisha. She need to come up with a good mix since kuna baadhi ya watu wachache wa Magufuli ni wazuri tu!...
Anaanzaje kuwchana na kina bashiru kisha aungane na majizi na matetezi ya MIGA?
 
Tutajie wanaofaaa
Kundi la magufuli linajulikana sana na pia sio kama kauli za mama hazipo zenye utata

Kwa mfano kwenye kampeni mama alisema "Hata msipotupigia kura sisi ndio tutakaounda Serikali"

Lakini nilitaka kumwambia kuwa njia za magufuli zilikuwa sio nzuri.

Ndani ya ccm wapo sahihi
 
Enyi TISS, sisi raia wema huku mitaani tuna imani Sana na nyinyi,kusema kweli tunawapenda Sana,Sasa Mimi Lee kwa niaba ya Watanzania wema,tunawaomba mumshauri na mhakikishe amepokea ushauri huu mheshimiwa Samiha.
Nawe mama Samiha Rais wetu nakuomba upokee ushauri huu Ili kufanya Tanzania iwe na amani upendo raha furaha na haki,kwani haki huinua Taifa.

Ushauri wangu
Naomba TISS chombo chetu Watanzania,mshaurini Rais Samiha atengeneze taasisi imara ili zilete haki.
Baadhi ya taasisi imara Ni
Mahakama huru,
Bunge huru,
Polisi huru,


TISS huru,
Takukuru huru,
NEC huru,
N.k
Faida ya taassisi huru itamfanya atawale kwa haki,kwa urahisi,kwa raha na bila lawama.
Taasisi huru itawafanya TISS wawe na kazi nyepesi bila lawama kutoka upande wowote.
Polisi hawata onea raia,
Mahakama itaamua kwa Haki,
Bunge litafanya kazi kwa weledi,
Takukuru hawata mwonea mtu,
NEC haitalaumiwa,
TISS haita laumiwa,
Hivyo Mama ataongoza kwa raha bila lawama,yeye atasimamia kuleta maendeleo tu.

Mbali na hayo yote tunaomba Rais Samiha uruhusu katiba pendekezwa ya Jaji Warioba, ambayo wewe Rais ulikua Spika wa Bunge la katiba,tunaomba haya kwa Mustakabali wa Taifa.

Ukiruhusu hayo utatawala ka amani Sana.

Tunaomba Taasisi Imara.
 
Wakuacha kabisa ni

Polepole
Mwigulu
Kabudi
Kalemani
Bashiru
Ndalichako

List goes on
Yeah. Wa kuambatana nao wawe ni Lissu, Zitto, Kigogo, Fatma K, Mange, Lema, Mdude...natumai nchi itasonga mbele kwa kasi ya ajabu
 
Back
Top Bottom