Rais tunaomba ulipe madeni ya PSSSF kwa wastaafu ATCL. Kila siku watendaji wako wanasema suala liko hatua ya mwisho.

Wapo wasio watiifu wizara Ujenzi na Uchukuzi na wapo muda mrefu. Marehemu John Kijazi akiwa Katibu Mkuu Kiongozi aliwahi kukemee tabia hii ya dharau na kuitaka wizara hii kulipa na apewe mrejesho. Bahati mbaya hatunae tena na issue imekwama tena.

RAIS WASAIDIE WASTAAFU ATCL WALIPWE MADAI YAO YA PSSSF. Mwaka 2016 mahakama kuu iliamuru ATCL kwa maana serikali iwalipe wastaafu hawa lakini hadi leo hakuna kilicho lipwa.
 
Sikujua ni kwanini siku ile alipoapishwa kuwa Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassana aliamua kuvaa rangi nyekundu kama sehemu ya mavazi yake. Ni baadae nikajulishwa kuwa ile rangi nyekundu ni ya mamlaka, ni ya kiongozi wa juu wa Taifa.

Amekuwa Rais wetu kwa mwaka mmoja na miezi miwili, ni kipindi tosha kabisa cha kujipambanua urais wake unasimamia katika sera zipi. Na ameweza kujitofautisha na mtangulizi wake hayati JPM. Amefanana na jinsia yake kwa namna anavyoongoza Tanzania.

Kwa maana ya usikivu, ukarimu, kutojikweza na ile lugha ya kukaribisha watu, wawe ni wa humu humu ndani au wale wa jamii za kimataifa. Kwenda kwake huko nje na kujitambulisha kumeipa dunia picha halisi ya kiongozi tuliyenaye, kwamba hajitengi na mataifa mengine na ile mitazamo ya kiujumla ya kidunia.

Amekuwa ni Rais mkweli siku zote. Nyeupe ataiita nyeupe, nyeusi anaiita nyeusi. Wapo walioozoea kuona kiongozi wa juu wa nchi akitumia uongo kidiplomasia. Uchumi wetu umetetereka kwa sababu ya COVID19, amekuwa mkweli kwamba lipo tatizo. Watu kwa wingi walikuwa wakifa, akawa mkweli kwamba tunapoteza nguvu kazi yetu kwa sababu ya maradhi haya. Uchumi wa nchi uliyumba na ukadorora na ni kweli hiyo ndio hali halisi. Anaweza asieleweka kwa wanasiasa waliozoea kuambiwa uongo wa kidiplomasia wa siku zote lakini ni hali inayoliponya taifa. Alipoongeza kodi za simu watu walilalamika sana, akasema ni makusanyo ya muhimu kama kweli tunataka kwenda sambamba na ahadi za mwaka 2025.

Amekuwa mkweli siku zote, na anajitahidi kuujenga hoja ukweli huo ili watu waelewe malengo haswa ya kile kinachoamuliwa. Angeweza akatupelekesha puta kijeshi na hakuna ambaye angekuja kulalamika mbele ya waandishi wa habari. Anatambua upana wa demokrasia hivyo inakuwa rahisi kwake kuzijibu kila tuhuma zinazoelekezwa serikalini kwa uwazi. Hiyo ni faida ya kuwa karibu na mitandao ya habari siku zote, kujua nini kinaendelea midomoni mwa watu na kukifanyia kazi, ukichunguza kwa undani ni tabia ya kiungwana kuliko tabia ya uswahili kama wanavyosema baadhi ya watanzania.

Neno la Mungu linasema Ukweli utatuweka huru. Anapokwenda huko nje, huku ndani anajikuta akidhihakiwa, kwamba anaiuza nchi, kwamba ni kibaraka wa mataifa ya magharibi, kwamba anajikomba kwa Marekani na wakubwa wengine. Yanasemwa mengi na wale waumini kindakindaki wa sera za hayati JPM. Walitegemea kuwa angeiga kila kitu kutoka kwake. Wanapoona anajitegemea kifalsafa ni lazima waumie na kusema kuwa remote ya kinachofanyika ikulu ipo Chalinze.

Pesa alizokwenda kuzitafuta huko nje, ndio hizi zinazoongeza bajeti ya kilimo, ndio hizi zinazoimalizia miradi ya awamu iliyopita mmoja baada ya mwingine. Ndio hizi zinazoongeza mishahara, na hapo ukichanganya na makusanyo ya kodi ya ndani. Amerudisha mahusiano mema kimataifa akiachana na kiburi na majivuno mengi ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa hayaonyeshi kwamba nchi yetu inao msimamo wake, bali walikuwa wakitushangaa tu wakishindwa kutuelewa. Humility is the best weapon, linapokuja suala la nchi yetu kuingiliana na mataifa mengine.

Ninaliona suala moja na ni la kutazamwa kwa kina kama anataka kukubalika zaidi ya anavyokubalika sasa. Wapambe wapo wa aina nyingi, wengine wanamuita Mama, wengine wanakuja na majina mengine na namna nyingine za kumpamba. Ni rais wa jinsi ya kike, anao udhaifu ule ule wa watu wa jinsia hiyo. Anaonekana kuuingia huu mtego wa kupambwa.

Siku zote binadamu anachojaribu kukionyesha machoni pake sicho kilichopo rohoni mwake, watu wanaishi wakiwa na nia mbili siku zote. Awe mwangalifu na upambe wa zile risala au hotuba kabla hajasimama na kuhutubia watu katika matukio rasmi ya kiserikali. Asimamie pale pale katika utendaji wenye kujishusha na unaoamini katika ukweli na usio na majivuno yanayopofusha nafsi za watu wakajikuta wakidondokea mtaroni na kupotea kabisa.

Wapambe na mitandao yao, ni wanasiasa kama wengine wowote wale. Awe nao makini ili wasipunguze dhamira aliyonayo moyoni mwake kwa watanzania.
 
Nakazia, pia akae mbali na Chawa wabobezi.

Mama namkubali sana haswa baada kuushudia Utawala wa Shetani
 
Mkuu
Hongera KWA bandiko
Uchawa unatuharibia viongozi Sana.
Uchawa uliasisiwa ccm tangu 1995 kwenye mchujo wa kupata jina la mgombea
Ccm imetufikisha huku kubaya Sana ilikuwa ina nafasi ya kutengeneza siasa nzuri zaidi kuliko hizi!!
 
Sikujua ni kwanini siku ile alipoapishwa kuwa Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassana aliamua kuvaa rangi nyekundu kama sehemu ya mavazi yake. Ni baadae nikajulishwa kuwa ile rangi nyekundu ni ya mamlaka, ni ya kiongozi wa juu wa Taifa.

Amekuwa rais wetu kwa mwaka mmoja na miezi miwili, ni kipindi tosha kabisa cha kujipambanua urais wake unasimamia katika sera zipi. Na ameweza kujitofautisha na mtangulizi wake hayati JPM. Amefanana na jinsia yake kwa namna anavyoongoza Tanzania.

Kwa maana ya usikivu, ukarimu, kutojikweza na ile lugha ya kukaribisha watu, wawe ni wa humu humu ndani au wale wa jamii za kimataifa. Kwenda kwake huko nje na kujitambulisha kumeipa dunia picha halisi ya kiongozi tuliyenaye, kwamba hajitengi na mataifa mengine na ile mitazamo ya kiujumla ya kidunia.

Amekuwa ni rais mkweli siku zote. Nyeupe ataiita nyeupe, nyeusi anaiita nyeusi. Wapo walioozoea kuona kiongozi wa juu wa nchi akitumia uongo kidiplomasia. Uchumi wetu umetetereka kwa sababu ya COVID19, amekuwa mkweli kwamba lipo tatizo. Watu kwa wingi walikuwa wakifa, akawa mkweli kwamba tunapoteza nguvu kazi yetu kwa sababu ya maradhi haya. Uchumi wa nchi uliyumba na ukadorora na ni kweli hiyo ndio hali halisi. Anaweza asieleweka kwa wanasiasa waliozoea kuambiwa uongo wa kidiplomasia wa siku zote lakini ni hali inayoliponya taifa. Alipoongeza kodi za simu watu walilalamika sana, akasema ni makusanyo ya muhimu kama kweli tunataka kwenda sambamba na ahadi za mwaka 2025.

Amekuwa mkweli siku zote, na anajitahidi kuujenga hoja ukweli huo ili watu waelewe malengo haswa ya kile kinachoamuliwa. Angeweza akatupelekesha puta kijeshi na hakuna ambaye angekuja kulalamika mbele ya waandishi wa habari. Anatambua upana wa demokrasia hivyo inakuwa rahisi kwake kuzijibu kila tuhuma zinazoelekezwa serikalini kwa uwazi. Hiyo ni faida ya kuwa karibu na mitandao ya habari siku zote, kujua nini kinaendelea midomoni mwa watu na kukifanyia kazi, ukichunguza kwa undani ni tabia ya kiungwana kuliko tabia ya uswahili kama wanavyosema baadhi ya watanzania.

Neno la Mungu linasema Ukweli utatuweka huru. Anapokwenda huko nje, huku ndani anajikuta akidhihakiwa, kwamba anaiuza nchi, kwamba ni kibaraka wa mataifa ya magharibi, kwamba anajikomba kwa Marekani na wakubwa wengine. Yanasemwa mengi na wale waumini kindakindaki wa sera za hayati JPM. Walitegemea kuwa angeiga kila kitu kutoka kwake. Wanapoona anajitegemea kifalsafa ni lazima waumie na kusema kuwa remote ya kinachofanyika ikulu ipo Chalinze.

Pesa alizokwenda kuzitafuta huko nje, ndio hizi zinazoongeza bajeti ya kilimo, ndio hizi zinazoimalizia miradi ya awamu iliyopita mmoja baada ya mwingine. Ndio hizi zinazoongeza mishahara, na hapo ukichanganya na makusanyo ya kodi ya ndani. Amerudisha mahusiano mema kimataifa akiachana na kiburi na majivuno mengi ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa hayaonyeshi kwamba nchi yetu inao msimamo wake, bali walikuwa wakitushangaa tu wakishindwa kutuelewa. Humility is the best weapon, linapokuja suala la nchi yetu kuingiliana na mataifa mengine.

Ninaliona suala moja na ni la kutazamwa kwa kina kama anataka kukubalika zaidi ya anavyokubalika sasa. Wapambe wapo wa aina nyingi, wengine wanamuita Mama, wengine wanakuja na majina mengine na namna nyingine za kumpamba. Ni rais wa jinsi ya kike, anao udhaifu ule ule wa watu wa jinsia hiyo. Anaonekana kuuingia huu mtego wa kupambwa.

Siku zote binadamu anachojaribu kukionyesha machoni pake sicho kilichopo rohoni mwake, watu wanaishi wakiwa na nia mbili siku zote. Awe mwangalifu na upambe wa zile risala au hotuba kabla hajasimama na kuhutubia watu katika matukio rasmi ya kiserikali. Asimamie pale pale katika utendaji wenye kujishusha na unaoamini katika ukweli na usio na majivuno yanayopofusha nafsi za watu wakajikuta wakidondokea mtaroni na kupotea kabisa.

Wapambe na mitandao yao, ni wanasiasa kama wengine wowote wale. Awe nao makini ili wasipunguze dhamira aliyonayo moyoni mwake kwa watanzania.
Anawatambua Sana ndio maana huwa hababaiki na sifa za kijinga 👇

Screenshot_20220520-082641.png

Screenshot_20220520-082641.png
 
Kwa mtizamo wangu Mhe. RAIS ameanza vizuri kuboresha mahusiano baiana ya watanzania lakini Tanzania na mataifa ya nje.

Amefanya vizuri katika project financing lakini amefeli kwenye project management. Anatoa Fedha kwenda kwenye miradi lakini msururu WA Watumishi wa umma wanaodeclare kwenda kukagua miradi kwa lengo la kujustfy malipo na posho ni kubwa sana, so management cost ya miradi yake inaweza kuwa 30% ya project value huku akiwa ameajiri Watumishi Kila eneo na anawalipa mishahara.

Anafanya vyema kutoa Fedha za kuendesha serikali lakini natabiri kwamba Fedha nyongi za kuendesha ofisi (OC) zitakuwa zinaliwa na top management. Hii naitabiri Kwa sababu movement ya mashangingi barabara ya Dodoma Dar, Mwanza, Arusha na Moro ni kubwa sana inayotoa tafsiri kwamba kazi zilizopaswa kufanywa ofisini zinafanyika nje ya ofisi kujustfy malipo. Madhara yake ni kwamba 80% ya OC inaweza ishia mifukoni mwa wakubwa huku watendaji wa chini wakiwa wanalia nja; in long run kukosekana Kwa wasimamizi ofisini kinadhorotesha usimamizi na hivyo kufungua milango la kudhorota Kwa huduma na Rushwa .

Amefeli kuunda timu ya vetting kwenye utumishi wa umma na hivyo viongozi wengi alionao sidhani kama Wana sifa za kiutendaji Bali Wana sifa za kielimu na may be wanaofanya vetting wanapick among senior officers bila kujali uwezo wao wakuitumikia taasisi. Kwa miradi anayopokea, anapaswa kuwa na timu ya watu ambao watapita Kila taasisi na kumtafutia majina ya vijana ambao wanawika na wanamaono makubwa then awe anawapandisha na kuwapa nafasi. Kasi ya Fedha anazopokea na Kwa deni la Taifa lilivyo sidhani kama wazee wa umri wangu waliowengi Wana mindset za kufanya reform most of them wanawaza kuzunguka wapate perdiem za kustaafia. Akiomba majina ya watoto wanaofanya kazi vizuri kwenye idara, wizara,mashirika bila kuwashirikisha makatibu wakuu au wakuu wa taasisi atapata new generation ambayo nao uwezo wa kuwapa even mkataba wa Nini angependa kifanywe na after sometimes ataona umuhimu wa vijana katika kuleta mabadiliko. Salim Ahmed Salimu alipewa madaraka akiwa mdogo na matunda yalionekana. Dukua majalada mama achana na majina unayoletewa maana anayeleta mwenyewe Hana Vision so ni vigumu kukuletea MWENYE vision.

Nampongeza Kwa kuelewa umuhimu wa kuboresha mifumo kupitia ICT lakini analo jukumu sasa la kuondoa wale wote waliopandikizwa mentality za ICT kutumika kubambikia watu kesi awamu ya Tano aje na bongo zinazoamini kwamba lengo la ICT nikurahisisha utoaji huduma.

Mama anafanya vibaya sana kwenye siasa hasa Ndani ya Chama Cha mapinduzi,hapaswi kuruhusu kusifiwa sana Kwa Sasa anapaswa kulazimisha Wana CCM waonyeshe talent zao kwenye kudeliver Ili iwe rahisi kwake kutumia talent na brain atazoibua kupanga safu ya wagombea na kampeni 2025. Wananchi wanataka watu wachapa kazi siyo wapiga tumba. Ajitahidi aanze kuzalisha viongozi Ndani ya CCM kama ambavyo Chadema imekuwa ikifanya. Chadema inazalisha watu ambao CCM inatamani wawe wao lakini kwanini upinzani uzalishe watu huku CCM ikiua vipaji Kwa kusifu na kumwabudu shetani? Tuangalie what is happening in Kenya; peaple are struggling in politics siyo kusifia ukisubiri upitishwe uwe mzigo kwa chama Hadi ulazimishe chama kiwekee polisi na dola Ndo ushinde.

Mwisho ,nimpongeze Kwa kuachana na kundi la wale walionwaga damu. Kuendelea kuwakumbatia watu wakatili nikujiwekea mazingira magumu ya kufanya siasa wewe na watu wako. Hakuna mtu katili MWENYE akili,mtu katili siku zote utumia dola kuhalalisha maovu yake na kuwanyamazisha watu. Kwanini uwekeze kunyamazisha watu?

Tatizo la mwisho, nikuendelea kusimamia mfumo wa dola unaopambana na maskini huku matajiri wakifanya uhalifu nakuendelea kusota mtaani. Nimwombe Mhe. RAIS,kaa na Jaji Mkuu mshauriane namna yakusafisha magereza pamejaa watu wengi ambao walipaswa kuwa uraiani wanazalisha. Waachieni mahabusu wote wenye kesi zisizo na ushahidi, wape Uhuru wanyonge kama ulivyofanya Kwa matajiri waliokuwa wamebambikiwa kesi kubwa kubwa; tukisimamia mfumo wa haki magereza yetu yatakuwa na watu wachache Kama ilivyo Zanzibar. Sijawahi kwenda Gerezani ila nikisikiliza masimulizi ya wapinzani wanapotoka jela naumia Sana kwamba we live once, kwanini tunalipwa fedha kuwatesa wananchi tuliopewa kuwaongoza? Mawakili wengi wa serikali wamekalia kuarisha kesi siyo kufanya kesi zisikilizwe; mama this needs no coin to impliment; it requires word of mouth and political will.

Kwa mtizamo wangu haya ni mambo ya kuboresha na yakifanyika we will see value for money lakini furaha ya wananchi itaongezeka na ikiongezeka kura zitatoka. Muda wakutumia wazee kunadi sera umepitwa na wakati; action and projects should speek for themselves.
 
Haipaswi kusubiria bali tunapaswa tumsaidie kwenye reforms anazofanya sasa (4Rs) tukimuachia peke yake hata weza na atakuwa hajafeli yeye bali tume feli kama taifa.

Kila mtu atimize wajibu wake kikamilifu kusaidia mabadiliko haya chap tu tunatoboa.
 
Hakikishe hawa nyumbu wa Uvccm hawapati nafasi za sensa maana watapika Data na lengo litakufa Mtu kama jingalao hajui chochote kuhusu sensa
 
Sisi wafanyakazi wa SGR (kampuni ya mkandarasi mkuu _ yapi merkezi) ambao wenye professional na wenye experience tulio jenga reli kuanzia mwanzo mpaka ivi sasa imekamilika, tunaomba Raisi atusaidie tuweze kupata kazi katika shirika la reli nchi (TRC).
 
Kwa mtizamo wangu Mhe. RAIS ameanza vizuri kuboresha mahusiano baiana ya watanzania lakini Tanzania na mataifa ya nje.

Amefanya vizuri katika project financing lakini amefeli kwenye project management. Anatoa Fedha kwenda kwenye miradi lakini msururu WA Watumishi wa umma wanaodeclare kwenda kukagua miradi kwa lengo la kujustfy malipo na posho ni kubwa sana, so management cost ya miradi yake inaweza kuwa 30% ya project value huku akiwa ameajiri Watumishi Kila eneo na anawalipa mishahara.

Anafanya vyema kutoa Fedha za kuendesha serikali lakini natabiri kwamba Fedha nyongi za kuendesha ofisi (OC) zitakuwa zinaliwa na top management. Hii naitabiri Kwa sababu movement ya mashangingi barabara ya Dodoma Dar, Mwanza, Arusha na Moro ni kubwa sana inayotoa tafsiri kwamba kazi zilizopaswa kufanywa ofisini zinafanyika nje ya ofisi kujustfy malipo. Madhara yake ni kwamba 80% ya OC inaweza ishia mifukoni mwa wakubwa huku watendaji wa chini wakiwa wanalia nja; in long run kukosekana Kwa wasimamizi ofisini kinadhorotesha usimamizi na hivyo kufungua milango la kudhorota Kwa huduma na Rushwa .

Amefeli kuunda timu ya vetting kwenye utumishi wa umma na hivyo viongozi wengi alionao sidhani kama Wana sifa za kiutendaji Bali Wana sifa za kielimu na may be wanaofanya vetting wanapick among senior officers bila kujali uwezo wao wakuitumikia taasisi. Kwa miradi anayopokea, anapaswa kuwa na timu ya watu ambao watapita Kila taasisi na kumtafutia majina ya vijana ambao wanawika na wanamaono makubwa then awe anawapandisha na kuwapa nafasi. Kasi ya Fedha anazopokea na Kwa deni la Taifa lilivyo sidhani kama wazee wa umri wangu waliowengi Wana mindset za kufanya reform most of them wanawaza kuzunguka wapate perdiem za kustaafia. Akiomba majina ya watoto wanaofanya kazi vizuri kwenye idara, wizara,mashirika bila kuwashirikisha makatibu wakuu au wakuu wa taasisi atapata new generation ambayo nao uwezo wa kuwapa even mkataba wa Nini angependa kifanywe na after sometimes ataona umuhimu wa vijana katika kuleta mabadiliko. Salim Ahmed Salimu alipewa madaraka akiwa mdogo na matunda yalionekana. Dukua majalada mama achana na majina unayoletewa maana anayeleta mwenyewe Hana Vision so ni vigumu kukuletea MWENYE vision.

Nampongeza Kwa kuelewa umuhimu wa kuboresha mifumo kupitia ICT lakini analo jukumu sasa la kuondoa wale wote waliopandikizwa mentality za ICT kutumika kubambikia watu kesi awamu ya Tano aje na bongo zinazoamini kwamba lengo la ICT nikurahisisha utoaji huduma.

Mama anafanya vibaya sana kwenye siasa hasa Ndani ya Chama Cha mapinduzi,hapaswi kuruhusu kusifiwa sana Kwa Sasa anapaswa kulazimisha Wana CCM waonyeshe talent zao kwenye kudeliver Ili iwe rahisi kwake kutumia talent na brain atazoibua kupanga safu ya wagombea na kampeni 2025. Wananchi wanataka watu wachapa kazi siyo wapiga tumba. Ajitahidi aanze kuzalisha viongozi Ndani ya CCM kama ambavyo Chadema imekuwa ikifanya. Chadema inazalisha watu ambao CCM inatamani wawe wao lakini kwanini upinzani uzalishe watu huku CCM ikiua vipaji Kwa kusifu na kumwabudu shetani? Tuangalie what is happening in Kenya; peaple are struggling in politics siyo kusifia ukisubiri upitishwe uwe mzigo kwa chama Hadi ulazimishe chama kiwekee polisi na dola Ndo ushinde.

Mwisho ,nimpongeze Kwa kuachana na kundi la wale walionwaga damu. Kuendelea kuwakumbatia watu wakatili nikujiwekea mazingira magumu ya kufanya siasa wewe na watu wako. Hakuna mtu katili MWENYE akili,mtu katili siku zote utumia dola kuhalalisha maovu yake na kuwanyamazisha watu. Kwanini uwekeze kunyamazisha watu?

Tatizo la mwisho, nikuendelea kusimamia mfumo wa dola unaopambana na maskini huku matajiri wakifanya uhalifu nakuendelea kusota mtaani. Nimwombe Mhe. RAIS,kaa na Jaji Mkuu mshauriane namna yakusafisha magereza pamejaa watu wengi ambao walipaswa kuwa uraiani wanazalisha. Waachieni mahabusu wote wenye kesi zisizo na ushahidi, wape Uhuru wanyonge kama ulivyofanya Kwa matajiri waliokuwa wamebambikiwa kesi kubwa kubwa; tukisimamia mfumo wa haki magereza yetu yatakuwa na watu wachache Kama ilivyo Zanzibar. Sijawahi kwenda Gerezani ila nikisikiliza masimulizi ya wapinzani wanapotoka jela naumia Sana kwamba we live once, kwanini tunalipwa fedha kuwatesa wananchi tuliopewa kuwaongoza? Mawakili wengi wa serikali wamekalia kuarisha kesi siyo kufanya kesi zisikilizwe; mama this needs no coin to impliment; it requires word of mouth and political will.

Kwa mtizamo wangu haya ni mambo ya kuboresha na yakifanyika we will see value for money lakini furaha ya wananchi itaongezeka na ikiongezeka kura zitatoka. Muda wakutumia wazee kunadi sera umepitwa na wakati; action and projects should speek for themselves.
Aondoe tozo za miamala, maisha yameshakuwa magumu. Watafute njia nyingine ya kuongeza mapato.
Wananchi hali ni ngumu. Bidhaa bei ghali.

Gharama za usafiri ziko juu.
Kuendelea kukata tozo, ni kuongeza gharama kwa wananchi wenye kipato cha chini.
 
Mtaani hakuna pesa.

Tunaona mapicha yao tu wakitalii kila mahali ila kwakweli hali za Raia mtaani ni mbaya to be honest.
 
Back
Top Bottom