Gucci 2

Member
Nov 8, 2017
31
95
Ndugu Watanzania,
Kila Raisi ana namna yake ya kufanya mambo( kuongoza) tusimlazimishe mama afanye mambo kama MH hayati Magufuri. Magufuri kaiongoza Tanzania kwa muda mchache tu, sasa tusimfanye yeye ndo akawa template ya uraisi wa JMT. Ni kweli kuna mambo tunaeza tukafanya reference kutoka katika uongozi wake. Na kuna vitu hatuhitaji reference kutoka kwake.

Watanzania mwacheni mama apige kazi, afufue huu uchumi ulokuwa unaenda shimoni, maswala ya uchumi huwa ni Kanuni na sio propaganda kama tulivyozoea.

Mama kanyaga twende, tuko nyuma yako.
 

This Day

Member
May 6, 2021
6
45
Kuna mtu amemzuia kufanya kazi?
Hakuna mtu anayemzuia kufanya kazi, shida ni pale watu wanapotaka atekeleze majukumu yake kwa namna na taratibu za mtangulizi wake, ndipo wanapokesea,Kila mtu ana stahili yake, ndiyo matatizo ya kuzoea,watu walishazoea,kukemewa na kugombezwa wandhani ndiyo njia pekee. Kuna mambo ya kurekebisha,kuna ya kuacha na kiasi kuna ya kufuata,atafanyaje??hiyo siyo lazima kufuata ya mtangulizi,
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
44,574
2,000
Hakuna mtu anayemzuia kufanya kazi, shida ni pale watu wanapotaka atekeleze majukumu ya kwa namna na taratibu za mtangulizi wake, ndipo wanapokesea,Kila mtu ana stahili yake, ndiyo matatizo ya kuzoea,watu walishazoea,kukemewa na kugombezwa wandhani ndiyo njia pekee. Kuna mambo ya kurekebisha,kuna ya kuacha na kiasi kuna ya kufuata,atafanyaje??hiyo siyo lazima kufuata ya mtangulizi,
Yeye ndiyo kasema yeye na mwendazake ni kitu kimoja
 

THE LOST

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
1,354
2,000
Mama naomba uiangalie hii idara. Ukanjanja na ujuaji wa hovyo mpaka kujifanya miungu watu (wanademka). Passport ni haki ya kila mtanzania ila sasa ukiritimba uliopo utafikiri unaenda mbinguni. Waangalie kwa umakini utendaji wao wa kazi. #kazi iendelee.
 

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
2,487
2,000
Kwanza nampongeza Rais wetu kwa kufanya ziara yenye mafanikio makubwa nchini Kenya, namuomba asiishie tu kenya sasa ni wakati wa kuonana na mataifa makubwa na kuwavutia wawekezaji.
 

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
13,448
2,000
Kwanini mnamwita mama Samia badala ya Rais Samia Suluhu? Au ana mtoto anaitwa Samia? Mbona Magufuli hamkuwa mnamwita baba John Magufuli? Mwiteni Rais kwa cheo chake hilo la mama ni nyumbani huko kwa mumewe na watoto.

Mtapata taabu saana maana Mama Samia is the 'iron lady'! Ukiingia anga zake tu kuvuruga serikali iliyoyaanzisha chini ya JPM, ambayo yy naye alikuwa sehemu ya serikali hiyo lazima apite na weye!

Hamtaamini huyu mama atakavyokuwa zaidi ya Magufuli kwa kutokucheka na nyani! Mama Samia atapandisha viwango vya uongozi kiasi kwamba tutatamani aendelee kutawala kwa muda mrefu!

Nafasi ya mwanamke kuchukua madaraka makubwa inaenda kuhakikishwa kwa utendani bora wa Mama Samia! Wezi mmeula wa chuya! Hamna chenu hapa!
 

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
268
1,000
NINAVYOMTAZAMA MHE SAMIA SULUHU HASSAN RAIS WA JMT.

Na Elius Ndabila
0768239284

Kama Mama, Ifahamike kuwa Mama akiwa na Watoto ndani basi KAZI yake ni kuhakikisha anawalea Watoto wake kwa viwango vinavyofanana. Hata kama Mama atakuwa anampenda mtoto mmoja zaidi ya wengine bado hawezi kuonyesha upendo huo hadharani. Mama Samia ni Mama kwa kuwa toka ameapishwa kuwa Rais anatulea Watanzania wote mazingira sawa. Amezingatia zaidi Utanzania na si ukada. Amevaa vizuri uhusika wa Mama.

Ametenganisha muda wa siasa na muda wakazi. Ni dhahiri kuwa Mama Samia kwa sasa anafanya KAZI na hafanyi Siasa. Anatambua kuwa kuna muda wa kazi na kuna muda wa siasa. Ukisikia hotuba zake hazungumzii kabisa juu ya Chama cha siasa, bali anazungumza zaidi juu ya mambo yanayowagusa watu wote bila kujali itikadi. Kutokana na mfumo wake huo wa kuendesha nchi amejipatia wafuasi wengi ndani ya Chama chake na kwenye vyama vingine. Hotuba zake zinaonyesha kutibu majeraha ya baadhi ya Watu ambao walikuwa na vidonda. Toka ameingia madarakani hotuba zake zimepokelewa vizuri na viongozi wakuu wa vyama vya siasa .

Ninamuona kama Mwanadipolomasia aliyebibea. Dunia ya sasa imejipambanua katika diplomasia ya kiuchumi. Yaani mahusiano ya nchi yamejikita zaidi kwenye mahusiano ya kiuchumi na si mahusiano tu ya urafiki. Mhe Samia alipoapishwa baada ya kumteua Mhe Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki alisema Tanzania haiwezi kujifungia na kutekeleza miradi mikubwa hii pekee yake. Alisema watu wana njaa ya mifukoni. Lakini Jana akiwa nchini Kenya amerudia kauli hiyo kwa lugha tofauti huku akisema anarudi Tanzania "ninaenda kufungua nchi, hakuna nchi ina develop pekee yake". Tafsiri yake ni kuwa Mhe SAMIA anaamini katika Uchumi wa kisasa ambao unajengwa katika misingi ya Mahusiano ya kiuchumi. Ameenda Kenya kutatua Mgogoro ambao ulikuwa unajengeka na kujaribu kuua Biashara ya muda mrefu ya Tanzania na Kenya.

Anaamini katika Umoja wa Kitaifa, Rais Samia alionyesha nia ya kutaka kuonana na viongozi wa vyama vya siasa nchini. Bila shaka nia yake hiyo ilikuwa ni kuendelea kutibu makovu na kujaribu kuwaambia nia yake ya kusahau yaliyopita na kuanza kujenga Taifa upya. Lakini hata wiki iliyopita akihutubia wajumbe wa Mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma alisema kuwa Chama kitaanza kutoa Elimu kwa viongozi wake ili waweze kuendana na siasa za sasa. Wadadisi wa mambo ya siasa wanasema inawezekana kwenye utawala wake ushindi wa CCM ukawa unajitenga na dola kubaki mahakamani. Anataka haki itakayo tokana na nguvu ya Chama na si nguvu ya dola kala alivyowahi kunukuliwa Katibu Mstaafu Bashiru.

Ni muumini wa Utawala wa Sheria ambao msingi wake mkubwa ni Demokrasia. Demokrasia inajengwa na misingi ya haki na wajibu. Hakuna haki bila wajibu, na kwenye utawala wa sheria ndiko unakoweza kuona tunda la haki na wajibu. Mhe SAMIA SULUHU alishatoa maelekezo kwa watu ambao wako magereza na Kesi zao hazina miguu wala kichwa waachiwe. Alishatoa maagizo pia kwa TRA ambayo imekuwa inachangia sana kuua Biashara za watu kwa sababu ya SHERIA kandamizi. Lakini Jana amepigilia msumari wa Mwisho kwa kusema hatuwezi kuwa watumwa kwenye sheria zetu wenyewe. Hivyo ninamuona SAMIA kama Rais anaye kuja kuhakikisha utawala wake mtu yeyote halii kwa kuonewa.

Zipo sifa nyingi ambazo ninaweza kumpa Mhe Samia. Duniani kote huwa viongozi wakubwa hupimwa baada ya siku mia Moja. Lakini kwa muda mfupi ambao Mama SAMIA ameliongoza Taifa inaweza kutoa taswira kuwa atatuongoza vizuri.

Ninaamini Mama huenda akaua kabisa sera ya Chama Cha CUF ambayo walikuwa wakitubagaza kuwa Watanzania kwa mjibu wa tafiti hawana furaha. Leo utafiti ungefanyika ninadhani watu wanafuraha.

Mimi si muumini wa msemo wa unapofika wakati wa kupokezana Madaraka yoyote kuwa hivi huyu kiatu cha mtangulizi kitamtosha? Mimi si muumini wa hili kwa kuwa ninajua wanaopokezana madaraka huwa si mapacha na hivyo miguu haifanani. Kila mtu ana mguu wake. Ninaamini kitu alichovaa Mama SAMIA Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinamtosha.
 

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
11,596
2,000
Nilipofungua huu Uzi tu na kukutana na namba ya simu.

Nikahitimisha tu hapa hamna kitu maono yako lazima yatakuwa biased tu - kwa kuwa kwa kuweka namba ya simu hapo maana yake unajioendekez.
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
41,285
2,000
Rais yeyote yule ajaye iwe ni kwa ghafla tu au kwa Mfumo wa Kisiasa ( Kupigiwa ) Kura akitawala kwa Kutoyarudia yale mabaya ( mapungufu ) ya Mtangulizi wake ( yaliyowachukiza Wananchi wengi ) ni 'obvious' tu atakubalika na hata kuanza Kupendwa na Watu wa nchi husika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom