JFK wabongo
JF-Expert Member
- Aug 11, 2015
- 3,887
- 3,187
Wadau naamini wote tunafahamu umuhimu wa salaamu. Salamu ni kiashiria cha umoja na uungwana. Ni kawaida kusikia watu wenye vinyongo kugoma kusalimiana au watu kugoma kumsaidia mtu asiye na kawaida ya kusalimia. Salamu hujenga udugu na urafiki. Hata tuwapo kwenye hafla za kitaifa pia tunahitaji kusalimiana.
Changamoto inayotukabili kama taifa ni kuwa lugha ya kiswahili haina salamu moja kwa makundi yote. Utasikia mtu anajikanyanga kwa kusema 'wakubwa shikamoni, vijana wenzangu mambo vipi, wale ninaowazidi umri marahaba. Ni kawaida pia kusikia mtu anatumia maakizi/ salaamu kama 'Tumsifu Yesu Kristu, Bwana Asifiwe, Salama Aleyekum, CCM Oyee, Chadema Vema, Haki sawa n.k. Maamkizi haya siyo jumuishi kwani kuna watu hawana vyama wala salamu za dini zao hazisikiki popote kwenye hafla hizi. Watu hawa huhisi wanasahaulika au hawapewi umuhimu.
Kwa mtazamo wangu salamu za vikundi vikundi hazitujengei uzalendo wala umoja wa kitaifa. Hivyo basi napendekeza tuwe na maamkizi ya kitaifa. Hii itasaidia kuimarisha uzalendo na utambulisho wetu. Naomba JF tuwe wakwanza kujenga uzalendo. Tujadiliane kuhusu maamkio/salamu ya kitaifa. Je, tuendelee na salamu hizi za vikundi vikundi? Au tupate salamu ya taifa ambayo itatumika kwa watu wa vyama vyote, dini zote na makabila yote tuwapo kwenye hafla za kitaifa?
Kwa mantiki hiyo ni salamu gani (miongoni mwa zilizopo au Mpya) ambayo unafikir itawatuunganisha watanzania wote tuwapo kwenye shughuli za kitaifa? Maoni yenu tafadhali!