Maoni: TAMISEMI fanyeni haya kuboresha Mfumo wa Kuajiri Walimu

msovero

JF-Expert Member
Jun 30, 2019
839
1,472
Kwa mtazamo wangu naona haya ni maeneo ya muhimu yanayopaswa kufanyiwa marekebisho ili kuepusha changamoto zinazojitokeza wakati wa kutoa ajira.

1. Unganisheni mfumo wenu na database ya NECTA kwakuwa wao ndio wenye taarifa zote za kielimu za waombaji basi hii itasaidia pale ambapo mwombaji atagushi namba ya kidato cha nne wakati wa kuomba ajira mfumo kumkatalia moja kwa moja.

2. Kwakuwa waombaji wa hizi ajira ni wengi basi kuna haja ya kuongezea server zenu ili iwe rahisi kupokea maombi ya waombaji wengi kwa muda mfupi na hivyo kuwapunguzia hadha na usumbufu wa kimtandao wanaopata waombaji wakati wa kutuma maombi.

3. Unganisheni mfumo wenu wa ajira na database ya NIDA ili kuzuia udanganyifu wa waombaji wanaogushi au kutumia NIN za ndugu zao kuomba ajira.

4. Rekebisheni kipengele cha kujaza majina maana mfumo unahitaji majina matatu ilihali waombaji wengine wanatumia majina mawili kwenye vyeti vyao vya kitaaluma.

5. Wekeni mfumo wa kuweza kutambua (detect) masomo ya waombaji kwenye vyeti au au hati zao za matokeo(transcript). Hii itasaidia kuzuia udanganyifu wa masomo unaofanywa na waombaji. Mfano mtu kujaza Economics badala ya somo lake la kiingereza alilobobea.

Mwisho, hakuna umuhimu tena wa kuendelea kutumia kanzi data (database) ya maombi yaliyopita kwa sababu tayari imegubikwa na dosari nyingi kama zilivyo bainishwa na kuibuliwa na wadau mbali mbali. Ni vyema kuufanyia mfumo maboresho kwanza kisha kufungua upya dirisha la kutuma maombi ili kukamilisha ajira 5000 zilizosalia kama ilivyokuwa ahadi ya mheshimiwa Rais ya kuajiri walimu 13,526.

Mengine yataongezewa na wadau
 
Zile ajira zilikuwa purposively.
Unajiuliza wanatumia nini kuchagua watu wanaowataka??
Km n vyeti, mbona vinaonesha mwaka wa kumaliza, na kam n masomo, mbona yapo kweny transcript.
Lakini kwanin watu waombe tena wakati walishaomba
 
Hivi kama kuna waombaji wamepitia mafunzo ya ualimu na wana uwezo wa kumudu kazi hiyo lakini hawakupata vyeti vya NECTA wanaweza kupata ajira hiyo? Ikiwezekana wapitishwe kwenye usaili mkali kama kweli wanaimudu kazi hiyo na wako tayari kupangiwa kituo cha kazi popote katika jamhuri ya muungano wa Tanzania,mradi elimu ya muombaji ijulikane aliipata wapi na ana elimu gani ya nyongeza kuweza kutekeleza mitaala iliyopangwa kufundishwa
 
Kuhusu uchaguzi wa waombaji katibu mkuu alisema ulitumika mfumo wenyewe kwa 100% kuchagua wenye sifa na kupangiwa vituo japo sina uhakika na hili. Kuhusu kuomba upya inasadia kutambua wahitaji maana wengine kadri ya wanavyokaa mtaani hata ndoto za kuwa walimu zinapotea na mwingine anaweza kuwa ameomba katika awamu iliyopita lakini kwa bahati mbaya akafariki hivyo serikali ikampangia kazi mtu ambaye hayupo.
 
Hivi kama kuna waombaji wamepitia mafunzo ya ualimu na wana uwezo wa kumudu kazi hiyo lakini hawakupata vyeti vya NECTA wanaweza kupata ajira hiyo? Ikiwezekana wapitishwe kwenye usaili mkali kama kweli wanaimudu kazi hiyo na wako tayari kupangiwa kituo cha kazi popote katika jamhuri ya muungano wa Tanzania,mradi elimu ya muombaji ijulikane aliipata wapi na ana elimu gani ya nyongeza kuweza kutekeleza mitaala iliyopangwa kufundishwa
Ebu fafanua kidogo hapa

Mtu anawezaje kupata mafunzo ya ulimu bila kupitia NECTA? huyo mtu ina maana hata mtihani wa kidato cha nne hakufanya?
 
Ebu fafanua kidogo hapa

Mtu anawezaje kupata mafunzo ya ulimu bila kupitia NECTA? huyo mtu ina maana hata mtihani wa kidato cha nne hakufanya?
Ndugu kuna uthibitisho toka NECTA unafanyika wewe weka vyeti wakuthibitishie kama namba zipo na matokeo yk wanayaona si tu toka kwenye vyeti vyako ili ukichauliwa umepitia michujo haswa
 
Tamisemi na utumishi zingatieni huu ushauri msije mkaturudisha kwenye enzi za jiwe kuajiri walimu hewa
 
Back
Top Bottom