MAONI: Students' Loans board ifutwe

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,293
12,593
Serikali ibane matumizi kwa kuzipa kazi benki za NMB na CRDB kazi ya kukopesha na kudai madeni madeni ya wanafunzi. Benki zina utaalam zaidi wa kukopesha na kudai madeni kwa wanafunzi kuliko watu wa HESLB. Kinachotakiwa ni mabenki kupewa fedha na vigezo vya kukopa.

Uzuri wake:
1. Wanafunzi wengi na baadae watakaokuwa wafanyakazi wengi wao wana account kwenye mabenk hayo.

2. Mabenki yana matawi mbalimbali nchi nzima kulinganisha na HESLB ambayo iko Mwenge - Dar es Salaam tu.

3. Itapunguza usumbufu kwa wanafunzi na msongamano pale Mwenge.

4. Serikali itaepuka gharama za kuajiri wafanyakazi na wajumbe wa mfuko.
 
nonsense.. unataka mkaandamane kwenye mabenki
benki ziko makini kuliko loans board, wanafunzi hawatakuwa na malalamiko ya kijinga kama waliyonayo sasa hivi kwa mfuko. Hata wakiwa na malalamiko hawatarundikana kwenye jengo moja kama ilivyo hivi sasa wote wanaenda Mwenge kudai na kuulizia uzembe uliofanywa na watendaji wa mfuko.
 
Haka kajamaa kameongea ukweli sana

Bank wanajua kudai aiseee kama unadaiwa na bank utaliopa tu

Au mifumo hiyo hiyo ya kibank ikatumika kudai wanufaika wa mkopo wa vyuo

Wapew muda baada ya kumaliza chuo ndan ya miaka miwili waanze kuleta marejesho yao kila nwezi

Utaona kama kutakuwa na msululu wa watu kudai mikipo au watu kukosa mikopo
 
kweli aisee kama ipo kweli hiyo loan's body(japo sijawahi kuisikia) ifutwe tuu ibaki hii hii tuliyo nayo loan's board
 
Serikali ibane matumizi kwa kuzipa kazi benki za NMB na CRDB kazi ya kukopesha na kudai madeni madeni ya wanafunzi. Benki zina utaalam zaidi wa kukopesha na kudai madeni kwa wanafunzi kuliko watu wa HESLB. Kinachotakiwa ni mabenki kupewa fedha na vigezo vya kukopa.

Uzuri wake:
1. wanafunzi wengi na baadae watakaokuwa wafanyakazi wengi wao wana account kwenye mabenk hayo.
2. Mabenki yana matawi mbalimbali nchi nzima kulinganisha na HESLB ambayo iko Mwenge - Dar es Salaam tu.
3. Itapunguza usumbufu kwa wanafunzi na msongamano pale Mwenge.
4. Serikali itaepuka gharama za kuajiri wafanyakazi na wajumbe wa mfuko.
serikali haifanyi biashara inatoa huduma.
 
Back
Top Bottom