Maoni: Safu ya Baraza la Mawaziri haiakisi maendeleo, inaakisi nchi kumilikiwa na familia fulani zinazoamini bila wao hakuna Tanzania

Nimeona mkeka wa baraza jipya la Mawaziri, unajiuliza uchaguzi umeisha au bado tupo Kwenye kampeni? Watu waliopo Kwenye baraza la Mawaziri ni watoto wa familia zilezile zinazoelekea kustaafu au zilizostaafu.

Hakuna ufanisi, ubunifu wala mikakati ndani ya baraza bali wamewekwa watu wakumsaidia Mhe. Rais kupiga kampeni kuelekea uchaguzi ujao.

Baraza la Mawaziri kwa kipindi hiki halipaswi kujazwa watu wa propaganda, inahitaji watu wakufikiri kuhusu maendeleo ya nchi yetu.

Baraza la sasa limerejesha fadhila Kwa timu Jk baada ya miaka mitano ya mateso. Naiona Tanzania maskini huko tuendako
Watoto wa walala hoi wanalia ajira,watoto wa vigogo wanazidi kutesa kila leo, Kweli nimeamini nchi hii ina wenyewe ni mali ya familia za watu,Hta aibu hakuna,wanajazana kwenye nafasi,kwa upendeleo,kwani wengine hatuna elimu.Si mlidhike na ubunge?Vyeo vitatu vitatu wakati wasomi wengine Hawana ajira.
 
Hili baraza limeonyesha kiwango kikubwa sana cha insecurity, kiufupi jinsia inaathiri utendaji wa mama yenu.

Yes hakuna nchi yoyote iliyowahi kufanikiwa kwa kuongozwa na mwanamke kama kiongozi mkuu kabisa except Germany, ni swala la muda tu.
Magufuli alijaza ndugu kuanzia baraza,hazina hadi makatibu tawala akiwemo mwanaye wa kumzaa Ruth Magufuli ambaye ni katibu tawala wilaya ya Morogoro.

Hoffman Sanga mkwe wake Magufuli katibu tawala wilaya ya Mvomero.

Dotto James katibu mkuu hazina ili kurahisisha uchotaji wa fedha bila kuulizwa.

Haya mbona hukuhoji hadi ukae kuhoji leo?
 
Shida ni tishio kwa mzoga gang kwa kuwa alikuwa mfuasi wa Magu,waliondolewa wote ni wafuasi wa magu kindakindaki wao wamegoma kwenda na mama wa kaya, kaawacha akidhani ndio anaondoa kadhia kumbe kadhia ndio kwanza imeanza, hivi Kingu,Bulembo, Zungu pamoja na kuimba mapambio wee hawajapewa uwaziri ama kweli CCM ina wenyewe na wenyewe ni wenye baba zao, akina January,Nape,Ridhiwani( huyu ndio ajira ya kwanza rasmi kila kitu analetewa mezani kuanzia ubunge na sasa uwaziri)
Na wakwilima akina mchengerwa
 
Magufuli alijaza ndugu kuanzia baraza,hazina hadi makatibu tawala akiwemo mwanaye wa kumzaa Ruth Magufuli ambaye ni katibu tawala wilaya ya Morogoro.

Hoffman Sanga mkwe wake Magufuli katibu tawala wilaya ya Mvomero.

Dotto James katibu mkuu hazina ili kurahisisha uchotaji wa fedha bila kuulizwa.

Haya mbona hukuhoji hadi ukae kuhoji leo?
Barazani ndug yake alikuwa nan wewe msoga gang?
 
Baadhi ya watu humu ni unafiki tu unawasumbua.

Magufuli alijaza watu wake hadi ndugu na watoto kwenye serikali hakuna aliyekemea ama kushangazwa lakini sasahivi wanajifanya kushangaa uteuzi alioufanya mheshimiwa Rais Samia.

Ruth Magufuli huyu ni mtoto wa damu wa Magufuli alimteua kama katibu tawala wilaya ya Morogoro.

Hoffman Sanga ni mkwe wa Magufuli aliyemuoa Ruth Magufuli ni katibu tawala wilaya Mvomero.

Dotto James ni mpwa wa Magufuli alimuweka Hazina ili kurahisisha kazi ya uchotaji fedha pasipo kipangamizi.

Na wengine wengi siwezi kuwaandika hapa ila wanajifanya kushangazwa na uteuzi alioufanya Mheshimiwa Rais.
 
Tulia wewe!! Mbona jiwe alikuwa anajaza warafiki na wanaukoo mkatulia, Mama Wala Hana hiana angekuwa na akili unayoisema hao kina Biteko,jafo,mbarawa ,Gwajima,ndalichako wote wangekuwa chali sahzi.
Ila Mama Turudishie Mchengerwa utumishi,au mpeleke hata Tamisemi,michezo na utamaduni Ni kumunderuse
 
Acha unafiki hao walioteuliwa wana tatizo gani? Nipe kashfa za hao wateuliwa ambazo zimethibitika kuliko kubwabwaja tu.

Kila Rais ana watu wake anaoamini watamsaidia sasa shida iko wapi hapo?

Hadi ateuliwe ndugu yako ndo uone Rais kafanya jambo la maana?
Hivi hata hauoni aibu kuongea hizi pumba??
 
Yana mwisho, hakuna lililo la milele,sisi watoto tuliokulia mlo mmoja wa kulamangia nasi ipo siku yetu inakuja soon, kwa sasa wacha wenye keki mzoga timu wakenue meno 32 baada ya kuminywa makende kwa miaka 5
Nyie hamna lenu nchi ina wenyewe hii🐒
 
Hili baraza limeonyesha kiwango kikubwa sana cha insecurity, kiufupi jinsia inaathiri utendaji wa mama yenu.

Yes hakuna nchi yoyote iliyowahi kufanikiwa kwa kuongozwa na mwanamke kama kiongozi mkuu kabisa except Germany, ni swala la muda tu.
Nilijua utaitaja Ujerumani na ni kwa sababu inaipa misaada CHADEMA kwa ajili ya kufanyia uchochezi na kutukana mitandaoni.
 
On my view:

Magufuli alifanikiwa sana kwenye uchaguzi kutokana na ufanisi kila kona kutokana na mawaziri aliokuwa nao.

Ushindi wa CCM 2025 utakuwa determined sana na perfomance ya hili baraza.
Jidanganye mwenyew,tegemeo la chama chakavu ni katiba chakavu tu hakuna lingne
 
69 Reactions
Reply
Back
Top Bottom