Maoni: Rais JK Tafadhali Hutubia Taifa Kabla Ya Sensa...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni: Rais JK Tafadhali Hutubia Taifa Kabla Ya Sensa...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PakaJimmy, Aug 23, 2012.

 1. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mwenendo wa nchi yetu kwa sasa ni alarming, kama ni geji ya fuel kwa sasa iko under Empty!.

  Zoezi la Sensa ya watu na makazi ambalo limebakiza siku mbili tu tokea leo limekumbwa na majaribu mengi, ambapo kwa mwenye umakini yeyote anatabiri waziwazi kuwa ufanisi wake utaathiriwa kwa kiasi kikubwa...Kwa Taifa makini na linalomaanisha maendeleo ya kweli kwa raia wake, huu ni msiba wa Kitaifa!
  Huku mitaani tunakoishi hali ni mbaya sana kuhusu zoezi hilo la sensa. Ni watu wengi mno wanaoapa kutohesabiwa, sio tu kwa sababu za dini na Posho, bali pia kwa kuona serikali yetu ni ya wachache wanaoifaidi!

  Sensa tokea zamani imekuwa ni moja kati ya nguzo zilizokuwa zinatuunganisha Watanzania wa makabila dini na rangi zote.

  Kuna matukio mengine mengi ya kitaifa km Zoezi la Katiba, vitambulisho, uchaguzi mkuu 2015, ambapo tusipokuwa makini yanaweza kutumiwa na wasioitakia mema nchi kama chanzo cha kusambaratisha nchi, na tukafutika kwenye ramani ya dunia.

  Ninachoweza kusema ni kwamba mambo yote haya yameletelezwa(gradual instil) na ukimya wa serikali ya JK kwenye matukio makubwa yanayoimaliza nchi yetu. Uzalendo wa wananchi umeporomoka, na hawaoni tena sababu ya kuheshimu Mamlaka.
  Kutochukua, au kuchelewesha mno hatua za kinidhamu(stern measures) ndiko kunakosababisha wananchi kufikia maamuzi ya kuingiza misimamo yao kuvuruga serikali kama hili la sensa.

  Rais angekuwa mkali kwenye mambo kama ya akina Jairo, Ngeleja, Mhando na wenzie, Mramba, Mzee wa vijisenti, mar.Balali, na kwenye skendo zote za ufisadi zilizoikumba nchi9ambazo ni nyingi mno), angalau kungekuwa na nidhamu(japo hata ya woga).

  Namwomba Rais wangu JK ahutubie Taifa haraka iwezekanavyo ili kuweka msimamo mkali wa kitaifa, akiongelea suala la sensa 'parse' bila kuingiza mambo mengine yoyote, wala kuwananga WAPINZANI...

  Hotuba hii haiwezi kuwabadilisha wenye misimamo hasi na sensa 'overnight', lakini inaweza kuwa stepping stone ya misimamo mingine itakayosaidia nchi hii huko mbele ya safari.

  Imagine nimesoma mahali, imefikia hata wenyeviti wa mitaa na vijiji wanawagomesha wananchi kuhesabiwa!!(My hairs)...tuko wapi kama Taifa?
  Wazee hakuna kwenye nchi yetu?...kwanini wana'underestimate hasara ya wrong data ya Population ya Watanzania?

  Taifa kwa mara nyingine linakula hasara ya ajabu kwa fedha zilizotengwa kwa zoezi hili kupotea bila kudeliver kile kilichotarajiwa.
  ..i can smell census-gate soon to be on pipe-line!
  Naamini wasaidizi wa Rais mnaosoma hapa mtamweleza na kumshauri Rais haraka.

  Mungu Ibariki Tanzania.
   
 2. m

  mamajack JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  yeye mwenyewe anampango wa kugoma kuhesabiwa ahutubie nini sasa??????????
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,858
  Trophy Points: 280
  PakaJimmy......are u serious?...........ingelikuwa hii kauli ni kweli mbona maovu yameshamiri hivyo dhidi ya raia wanyonge?........watu wamekuwa wakatili sana na ubinafsi ndiyo hazina ya viongoziu kama vila hawajui walikuja bila chapaa na wataondoka bila ya sumuni?

  Sensa hapa nchini wala haina uhusiano wowote ule na mipango ya maendeleo na ingelikuwa inajumuishwa kwenye mipango tajwa leo Dar isingelikuwa imefurika hivyo.........................na vijana wengi hawana shughuli ya kufanya............ukifuatilia sana kwa undani sensa ni njia ya kufuja mali ya umma kwa sababu wakishamaliza zoezi lao vitabu hufunikwa hadi miaka mitano mingine ije....................sasa inamnufaisha nani kama siyo waajiriwa kwenye hilo kapu?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,858
  Trophy Points: 280
  mamajack.................................ahesabiwe khalafu siri ifichuke ya kuwa....................kumbe..................ana.............
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  una akili sana wewe.:thumbup:
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Watachakachua tu hizo data kama kawaida yao. . . . .kwani huwajui. Watasema zoezi lilikuwa successful.
   
 7. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  zoezi la sensa linaonyesha ni kiasi gani Watanzania wamepoteza imani na serikari. Pia inaonyesha wazi udhaifu mkubwa uliopo na hasa mawakala kubishania posho hata kabla ya kazi kuanza kitu ambacho hikijawahi kushuhudiwa miaka ya nyuma. Mfano kitendo cha kinafiki cha kuwaondoa walimu kwa unafiki tuna kuwapa hiyo kazi ya kuhesabu vijana wa 'mitaani' inaweza kusababisha matokeo yaliyotarajiwa yasifikiwe.

  Pia fikiria pamoja na kampeini iliyopo ya watu wanaopinga hiyo sensa lakini inaonyesha zimetumika pesa nyingi sana kwenye kutoa elimu ambapo kulikuwa na utata mpaka UN ikaingilia kati process ya tender hizo!

  Lakini funga kazi ni pale serikali inapoamua 'kuwahonga' baadhi ya Watanzania kwa kuwapa nyama ya pundamilia ili wahesabiwe! Nashindwa kuelewa kama pesa za kutoa hao wanyama zilikuwamo kwenye bajeti na kama ni kweli basi hata wengine wanaweza kuomba 'privilege' kama hizo.
   
 8. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kiongozi umeongea 'pwenti' sana kwa kweli. Nchi yetu kwa sasa imefika pabaya sana, sijui ni kwa makusudi au bahati mbaya. Hili swala la kuogopana si zuri kabisa yaani, ni bora kuchukua hatua hata kama baadae itakuja julikana otherwise lakini wananchi watajua serekali yao huwa inajali na kuchukua hatua.
  Kuwaambia watu kuwa sakata la Jairo halina maamuzi hadi sasa ni kitu kisichovumilika kabisa yaani, kuacha watu wanajipangia wahesabiwe au wasihesabiwe ni kichekesho sana. Kunakuwa na Rais, waziri mkuu wa kazi gani sasa? Unatembea na mapikipiki 12 na mabenzi 8 sijui unashindwa kuchukua hatua? Ni urafiki au malezi tu?

  mkuu JK unapoona watu wanapinga chochote kinachoamriwa na serekali ni dalili mbaya sana, watu hawaangalii umuhimu wake au ulazima wake kwa sasa, wanachoangalia ni namna ya kuibana serekali, namna ya kuikatalia serekali, hii ni dalili mbaya mkuu, ni kuonesha watu wamechoka na wanatafuta sababu tu, kama unabisha amka kesho useme serekali imeamua kugawa kilo 2 za sukari kwa kila familia kwa jinsi watu walivyoichoka serekali yako wapo watakaopinga! na kukwamisha hilo zoezi.

  Mkuu, funguka sasa, anza kazi please........
   
 9. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu PJ, last weeek nililikuwa Mkuranga -few kms from Dar. Huko wananchi walikuwa wanahamasishana na viongozi kuwa wasihesabiwe simply because enumerators wametokea maeneo ya Dar badala ya watoto wao wenyewe kupewa kazi hizo.....tena wao walikuwa wanasema wamesikia wameshaaindikishwa ya nini wasumbuliwe...which means tunaweza kupata cooked data by the end of the day. Suala la kuhutubia ni muhimu, lakini nadhani level ya awareness (acha radio na tv) haijawa nzuri hasa kwenye ngazi za vijijini huku ambako ndo watu wengi tulipo!
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mkuu,
  Hapo kwenye red huenda nilipitwa na jambo hili....ni habari gani tena hii? Tafadhali ielezee kidogo!...Hivi kuna anayeweza kuniambia mtu anapokuhonga ili uhesabiwe anakuwa na maana gani!...Labda anakuwa ameshakamata fungu kubwa la fedha ambalo ahofia atashindwa kujustify matumizi yake asipohesabu watu, then njia inakuwa ni kuwahonga ili wahesabiwe!
  Otherwise, to be precise i cant connect the relationship!
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mnanikumbusha eneo fulani la uchaguzi ambapo mgombea wa Udiwani aliibuka na kura 0!...kwa maana kwamba hata yeye hakujichagua!
   
 12. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,072
  Trophy Points: 280
  sensa.jpg inabidi kuwa makini hapa maana tumesikia katika kipindi cha miaka mitano sheria zikipitishwa na Bunge Dodoma na kusiniwa na rais lakini baadae tunasikia zimechakachuliwa na kurudishwa bungeni kufanyiwa marekebisho. Beware na hii isije kuwa miongoni mwa hizo sheria!

   
 13. only83

  only83 JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mimi nasema kukaa kimya kwa serikali kwenye mambo mazito yanayogusa maslahi ya Taifa ni kudhihirisha udhaifu aliousema John Mnyika. Ukweli ni kuwa ni kwa mara ya kwanza nimesikia sensa yenye vitimbi, walimu kufutwa kusimamia sensa kwa hoja za kufitiniana, makarani kutokupewa posho zao, waislamu na wengine kupinga kuhesabiwa nk. Hii ni hali mbaya kwa Taifa...wazo lako mkuu PakaJimmy ni ukweli mtupu. Tunahitaji tamko la raisi, kama ambavyo alikadhana kusema wakati wa mgomo wa madaktari nk sasa aseme na kwa hili.
   
 14. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hii hapa mkuu usije kusema ni uzushi!
  https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/311506-vioja-vya-sensa-2012-wahazabe-wao-bila-nyama-ya-kima-nyani-na-gongo-hawatashiriki-sensa.html
  Hadzabes ask for monkey meat during census
  ·
  ·
  Tweet
  Details
  Published on Wednesday, 22 August 2012 03:48
  Written by MARC NKWAME in Karatu
  Hits: 142

  THE Hadzabe who live in some parts of Lake Eyasi basin, in Karatu District, Arusha Region are demanding monkey's meat and "gongo" as a condition for them to take part in the population and housing census.
  However, officials in the district say they were not ready to hunt monkeys or baboons and give to the Hadza people, but were willing to look for zebras instead.

  "We are prepared to send a hunting team to get them Zebra meat for their special census treat next Sunday," said the Karatu District Commissioner Mr Daudi Ntibenda. The DC added that the bushmen also demanded bhang and illicit liquor known as "gongo".

  "We also refused them their demand for eating monkeys because under hunting regulations there are some wildlife species that cannot be killed. These include monkeys," he said. But during a meeting between the bushmen and district officials in the Mang'ola ward of Karatu, members of the Hadzabe community maintained that being small scale subsistence hunters, monkeys have always been their main source of meat.

  They were, however, happy with the proposal to get zebra meat. "We have earmarked 12 counting stations in the area resided by the bushmen," stated Ms Margaret Martin, the Arusha Regional Chief Statistician and area Census coordinator.

  She said the only way to gather the bushmen at one location is to provide them with something interesting to eat and use the occasion to collect their data.

  Living deep in the forests, the Hadza Bushmen residing in (Lake Eyasi area of) Karatu and in the vast Yaeda Valley stretching between Mbulu District of Manyara Region and Singida Region, have for years been avoiding National Census exercises and only a few of them have been turning up to be counted in the past.

  In 1975 the number of Hadzabe people in Yaeda was estimated to be around 5,000 but in recent years, local researchers have been reporting that the Hadza population had dropped to hardly 1000.  Source: http://dailynews.co.tz/index.php/loc...-during-census
   
 15. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Mtatafuta pa kutokea mwaka huu, madaktari, walimu na sasa sensa. Mtajikuta 2015.
   
 16. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mkuu only83
  Kwavile zoezi hili litakuwa na backing-up ya wajumbe wa nyumba kumi, mi nadhani ni rahisi kujua familia zitakazogoma kuhesabiwa na hivyo kuweka rekodi mahali kuonyesha kupinga huko.
  Rais aweke wazi madhara yatakayoipata familia au mtu ambaye kwa makusudi atakwamisha zoezi hili...Bila mkuu huyo kutamka kitu, tusitegemee mabadiliko katika misimamo ya watu hao...wataendelea kuamini kuwa ni (BAU)Business As Usual, na kwamba kelele za chura hazimzuwii mteka maji kuendelea na zoezi lake!
  Rais wetu naamini ni MSIKIVU, na pia serikali yake NI SIKIVU!...Kama rais amekuwa makini kuongelea mambo mengine ya kitaifa kama tulivyoona siku za nyuma, basi na kwa hili la sensa aliwekee msimamo wa Ikulu ya Magogoni!
   
 17. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  PHP:
  "We are prepared  to send a hunting team to get them Zebra meat for their  special census  treat next Sunday," said the Karatu District  Commissioner Mr Daudi  Ntibenda.
  My hairs!...The Government Machinery sounds like is fallen apart!
   
 18. only83

  only83 JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mkuu PakaJimmy hapo kwenye red nakuwa na shaka kidogo...ni kweli yawezekana raisi anasikia ila ni mzito kuchukua hatua, na hata wasaidizi wake ni wazito sana. Na nilitegemea tamko hata la waziri mkuu akijiwekeza specifically kwenye tishio la baadhi ya watanzania kukataa kuhesabiwa, badala ya kutoa hotuba za jumlajumla zinazoelezea umuhimu wa sensa.
   
 19. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Shida yao mpaka sasa hawajaja na data ni vp Sensa ya 2002 illiisadia Tanzania kwenye maendeleo, mi nadhani wangeanzia hapa. Kikweli tungekua tunatumia Data za Sensa Dar isingekua hivi
   
 20. Kalashkano

  Kalashkano Senior Member

  #20
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 7, 2012
  Messages: 187
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  YAP, KUMBE SASA WATANZANIA MKO JUU KIFIKRA...ha ha haaaa!!
   
Loading...